Elections 2010 PICHA NA VIDEO: Kampeni za Slaa jimboni Kawe leo

CCM wamemaliza kila silaha kuanzia ya kujaribu kuwafungia chumbani kwa Dr. Slaa, ukabila, udini, tishio la amani na sasa wanapayukapayuka kama vile wanaamkakwenye usingizi wa dawa iitwayo "Ketalar". Wametujeruhi, wametuua kwa kutumia genge lao la wahuni Green Guards na sasa wamembambikia kesi mpiganaji wetu Shibuda.
Kisasi chetu watakiona Jumapili Oktoba 31 ambapo ule usemi wa kilichoingia kwa kishindo huondoka kwa kishindo utadhihirika.
Labda wafanye kama kule jirani kwa Kibaka ambako msanii wetu huyu alipata PhD kiulaini kwa kuwapatanisha. Nadhani safari hii itakuwa zamu ya mwingine kujiokotea PhD ya kupatanisha.
Haya yatakuwa matokeo ya Chama kuongozwa na watu wasio na vision ambapo walishindwa kusoma alama za nyakati na kushindwa kukinusuru chama kwa kumsimamisha mgombea competent. Kosa moja goli nne. Mi bado naamini CCM inao baadhi ya watu waadilifu (Lakini wanaopigwa vita na sijui kwa nini wameendelea kung'ang'ania huko) ambao wangesimamishwa wangeweza kutoa changamoto kwa upinzani lakini si huyu mtalii na msanii Kikwete.
Dr. Ongeza spidi tunakaribia mwisho CHADEMA
 
kwakweli silaa ni kama anawasha moto moyoni ivi tumejipanga vipi na kura zetu hawa wenzetu nahisi watacheza michezo yao kama kawa tukapige kura tafadhali
 
Jamani geograph ya Dar nimeisahau, Kawe iko upande upi? Msinicheke, I left Dar about 18 years ago,and even though i visited Tanzania so ma
ny times but i dont know WHERE IS WHERE?

Kawe inapakana na kambi ya jeshi ya Lugalo na makao makuu ya JKT.
 
Kwa siku zilizobakia nitasali kwa dhati ya moyo wangu kwa Mungu wetu ili tu aliongoze taifa hili katika makabidhiano ya madaraka kwa haki na amani. Slaa na awe Baba mdogo wa Taifa
 
kwakweli silaa ni kama anawasha moto moyoni ivi tumejipanga vipi na kura zetu hawa wenzetu nahisi watacheza michezo yao kama kawa tukapige kura tafadhali


Ona wananchi walivyotulia na kumsikiliza kwa makini. Nakumbuka habari ya Dilunga na mama muuza ndizi, aliyesahau kuuza ndizi akimsikiliza Dr Slaa. Watu wametulia tulii kama maji ya mtingini. CCM kiama chao kimefika. Rais ni Slaa, na wabunge wao kibao.
 
Change is inavitable huwezi kuzuia mabadiliko,tuombe Mwenyezi Mungu wananchi kwa ujumla wapige kura kwa usalama wasuburi matokeo kwa amani.Mambo yako wazi mshindi anaonekana bila kuweka kachumbari.Ili kuepusha vurugu na ghasia vyombo vya usalama,majeshi ya ulinzi,na NEC ni LAZIMA vitende haki sio kujaribu kutenda haki,HAKI ni muhimu wakati huo kuliko wakati wowote toka tupate uhuru,kwani bila ya kutenda haki taifa litatumbukia kwenye vurugu kubwa kuliko ambazo hatujapata kuziona katika taifa letu.Tukubali Daudi amemwangusha Goliati.
 
watanzania hofu yangu ipo kwenye uchakachuaji wa kura zetu hapo ndo mashaka yangu makubwa yalipo kama tulichopiga kitatoka kwa usahihi si unasikia mwenyewe zile mita zetu zilishaondolewa wote turudi majumbani baada ya kupiga kura
 
qpijye.jpg

2emcsas.jpg

xcnmh3.jpg

108af07.jpg

2hrlx0w.jpg


VIDEO:



Kama Chadema wangekuwa wanatumia mbinu kama ya CCM kuwakodia wananchi usafiri wa kwenda na kutoka kwenye mikutano ya kampeni ingekuwaje? Slaa sasa hivi angekuwa Segerea, wangemchomekea kama walivyomfanyia Shibuda kule Maswa maana watu wangekufa kwa kukosa hewa ingawa mikutano hiyo inafanyikia maeneo ya wazi.....teteh tetehe ahaha.
 
Last edited by a moderator:
Kwa siku zilizobakia nitasali kwa dhati ya moyo wangu kwa Mungu wetu ili tu aliongoze taifa hili katika makabidhiano ya madaraka kwa haki na amani. Slaa na awe Baba mdogo wa Taifa

Kumlilia Mungu ni kitu cha muhimu sana kwani yeye ndiye muweza wa yote. Mungu wetu ambaye sisi ni watoto wake tunamlilia na kumuomba atuondolee CCM na viongozi wote wabovu. Baada ya kumuomba twende tukapige kura, tulinde kura na tuhakikishe kuwa kila msimamizi wa kituo anatangaza na kutuma matokeo sahihi. Vilevile ni lazima kuhakikisha kuwa Kiravu na Makame wanatangaza matokeo ya kweli na si yale ambayo IKULU imeshayatunga na inataka kuwa ndiyo yatangazwe.
 
mimi ndio mwana ccm wa kufa mtu, ila kura yangu nampa
dr. Rev. Peter slaa mkombozi wa tanzania
wana ccm wengine wote
msitupe kura zenu ******,
mkimpa kikwete kura ni kumpa
rostam aziz
lowassa
kikwte na familia yake
makamba na familia yake nchi
mpeni dr. Slaa kura ili watoto wetu wapate elimu wanayao stahili. Kura kwa dr. Slaa wana ccm wote

dr. Slaaa hoyeeeeeeeeeeeeeee
hoyeeeeeeeeeeeeeeeee
Duh kweli watu wameamka Tanzania mwaka huu, mungu akubariki kwa hili. Natumaini kuna wenzako wengi ambao watapiga kura kwa Slaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom