Picha na maelezo: Kikao cha Marafiki Wa Regia BC

Muhtasari wenu ni dhaifu na unanishawishi niwaulize kwamba lengo lenu hasa lilikuwa ni nini?

Hii ndiyo shida ya Mods kuunganisha threads bila mpangilio. Wameshachanganya thread ya Picha na Muhtasari . . . .

Anyway . . . kamata hii Mkuu:
Kumbumbukumbu za Kikao

Kikao Cha Marafiki wa Marehemu Mh. Regia Mtema – January 2012

Mada Kuu: "Kumtambua Regia na Alichosimamia na Nini Kifanyike Baada ya Kututoka"
Kikao cha Marafiki wa Marehemu Mh. Regia Mtema (Mb) Waishio Ndani na Nje ya Nchi Kupitia Skype uliitishwa baada ya baadhi ya Wanajamii waliokutana katika Ibada ya Kumwombea Marehemu Mh. Regia Mtema Kanisa katoliki Segerea kupendekeza hivyo. Wanajamii hawa walipendekeza kuwa ipangwe siku maalumu hivi karibuni ambayo Marafiki wa Marehemu Regia na Wadau mbalimbali watakutana British Council na kujadili yale yote aliyosimamia Regia na nini cha kujifunza kutoka kwake na kukifanya ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi marehemu.

Ilipendekezwa kuwa Kiitishwe Kikao katika Ukumbi wa British Council siku ya Ijumaa Tarehe 27-01-2012 kuanzia saa 11jioni hadi saa 2 Usiku ili kuweza kulijadili masuala husika. Wazo hili liliwakilishwa kwa Wanajamii wengine kupitia mtandao wa Jamiiforums (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ukutana-dsm-kumuenzi-regia-27-jan-2012-a.html) ambapo Wanajamii wengi wapatao 70 waliunga mkno wazo hili na kusthibitisha kushiri ama kwa kufika British Council, ama Kushiriki kwa njia ya Skype kupitia ID maalumu ya: jamiiforums.

Hatimaye Kikao kilithibitishwa kupitia Jamiiforums (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...d-regia-kukutana-ijumaa-hii-27-01-2012-a.html) na kufanyika kama ulivyopangwa. Jumla ya Wanajamii 25 Walihudhuria British Council wakiwemo Wazazi wa Regia na Pacha wa Regia na wengine wapatao 60 walishiriki kupitia Skype Video Conferencing ambapo baadhi pia walipata nafasi ya kuchangia maoni yao. Baadhi walifuatilia kupitia Mtandao wa Jamiiforums ambapo jumla ya mabandiko 273 yaliwekwa siku hiyo na maangalizo (views) zaidi ya 6000.

Majadiliano katika Kikao hiki yaliendeshwa kwa utaratibu wa kuchangia hoja/mada kuu, huku mchangiaji akielezea suala / hoja husika, anavyomtambua Marehemu Mh. Regia, Mchango wake na nini kifanyike baada ya Regia kututoka, mapendekezo na mikakati ya utekelezaji. Washiriki wa Skype waliweza kupiga Voice au Video Call British Council na wakasikika katika vipaza sauti huku na wengine wakifuatilia mjadala kwa kuangalia internet kupitia: Friends of JF on USTREAM: . Baada ya hapo washiriki walipitia hoja mbalimbali na kukubaliana juu ya namna gani Marehemu Regia atambuliwe, Maazimio na Mikakati ya Utekelezaji. Yote haya yalifanyika kwa kuzingatia nafasi ya Regia katika jamii bila kujali itikadi yake kisiasa.

Mmoja wa Waanzilish wa Jamiiforums pia alipata fursa za kuwakilisha rambirambi za wanachama wa JF. Kiasi kilichowakilishwa ni TZS 1.5 Millions.

Zifuatazo ni Kumbukumbu, Maazimio na Mikakati kama ilivyokubalika katika Kikao hicho:

1. Kuhusu Kumtambua Regia: Kikao Kilichambua na kukubaliana Regia atambuliwe rasmi kama ifuatavyo:

1. Kwamba wote walioshiriki katika hicho Kikao wanamtambua Regia kama Rafiki yao katika harakati za Kijamii bila kujali itikadi, imani au jinsia yake.

2. Regia alikuwa ni Mwanaharakati wa Kijamii na Kisiasa aliyekuwa Mlemavu wa kiungo lakini ambaye ulemavu wake haumkumzuia kufanya jambo lolote alililiamini na kulisimamia. Kwa hili Regia amekuwa mfano wa kuigwa kuwa kuwa na ulemavu si sababu ya kushindwa kutenda jambo unalokusudia kulitenda.

3. Regia alikuwa ni Mwanamke shujaa ambaye hakuikumbatia dhana ya "Wanawake tukipewa nafasi au tukiwezeshwa tunaweza". Alikuwa mwanamke jasiri anayejiamini kwa uwezo wake bila kujali jinsia yake. Hilo alilidhihirisha pia pale alipoamua kugombea ubunge wa jimbo la Kilombero na kuchuana vikali na mgombea wa jinsia ya kiume na huku akitoa changamoto kubwa sana. Hata alipoashindwa aliweza kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu huku akiwa Waziri Kivuli wa Wizara ya kazi na Ajira. Kwa hili Regia amekuwa ni mfano wa Kuigwa na Wanawake wote.

4. Regia alikuwa ni mtu mwenye mapenzi makubwa na Nchi yake na Jamii kwa ujumla. Regia amekuwa mara nyingi akiwahimiza Wananchi wampelekee kero zao ili aweze kuzisemea Bungeni na Kuziwasilisha katika vyombo husika.

5. Regia alikuwa ni Mtu mwenye Upendo na Huruma na Msaada kwa Wahitaji. Kwa hili aliwasaidia yeye binafsi wale ambao walitaka msaada wa namna mbalimbali kutoka kwake kama Wasiojiweza na Yatima n.k. Hili ni jambo la kuigwa maana kuna wenye uwezo zaidi ya Regia na wasio na Ulemavu wowote ambao hawajaweza kufanya kama Regia alivyofanya.

6. Regia katika nia njema ya kuwatumikia Wananchi wa jimbo analotoka la Kilombero kwa karibu, alikuwa katika harakati ya kuanzisha taasisi itakayosaidia kuboresha maisha ya Wana Kilombero aliyokusudia kuipa jina la Kilombero For Change (K4C).

2. Maazimio ya Kikao Kutokana na hoja zilizotajwa hapo juu; Kikao Kimeazimia yafuatayo:

1. Ili kumuenzi Marehemu Regia Mtema, ianzishwe Taasisi maalumu itakayoendeleza yale aliyoyaamini na kuyasimamia kwa faida ya Watanzania wote. Mchakato wa Kuianzisha ufanywe na kisha kuisajili huku ikiwahusisha Wadau mbalimbali ambao wangependa kuona harakati za Regia zinaendelea.

2. Kiandikwe kitabu cha Maisha ya Regia "Biography" ambacho mbali la historia yake ya maisha na harakati za kijamii, kitakusanya maandiko na matamko yake mbalimbali pamoja na picha zake.

3. Kero zote ambazo Mh. Regia aliandikiwa na wananchi ili aweze kuzisemea Bungeni na kuziwasilisha kunakohusika zikusanywe na kuwekwa katika Kijarida au Kitabu kidogo ambacho kitawakilishwa kwa Spika wa Bunge ali afikishe kwa wahusika na pia kuwapa nakala kila Mbunge ili waweze kuyasemea Bungeni kama alivyokusudia.

4. Ili kumuenzi Regia na pia kuhamasisha Wanawake na hasa wale wasiojiweza, itaandaliwa tuzo maalumu kila Mwaka ambayo itapewa jina la Regia. Tuzo hii itatolewa kwa mtu yeyote mwenye ulemavu kwa viungo ambaye ulemavu wake haujaweza kuwa kikwazo hasa katika kufanikisha utendaji wake katika jamii huko akizingatia maadili.

5. Taasisi itakayoundwa ianzishe pia Programu maalumu ambayo itaendeleza baadhi ya mambo ya kimsingi ambayo Regia alipanga kuyaendeleza.

6. Kwa kuwa Regia alikuwa anawasaidia Yatima na Wasiojiweza na kuwasomesha baadhi yao, itaanzishwa Programu maalumu ya kuendeleza na kuyasimamia hayo pamoja na Scholarship ambayo itachangiwa na Marafiki wa Regia na wale wote wenye mapenzi mema na suala husika.

7. Kuomba kibali cha Kujenga Mnara wa Kumbukumbu sehemu aliyopatia ajali ikiwa ni ishara ya

a) Kuwakumbusha Watanzania kuwa hata Mwanamke Anaweza bila Kuwezeshwa.
b) Hata Mlemavu anaweza akafanya jambo lolote kama asiye mlemavu
c) Kwamba watumiaji wa barabara hiyo ambayo inaongoza kwa ajali, wawe makini pale wanapoitumia na hasa kwa kuzingatia vema sharia za barabarani
d) Sheria za barabarani ziboreshwe na barabara kupanuliwa ili kuondoa kabisa au kupunguza ajali.
e) Kumbukumbu ya Regia kuwa hata kama hayupo lakini aliyoyaamini na kuyasimamia yataendelezwa.

3. Kuhusu Mikakati ya Utekeleza ya Maazimio na Hoja Zilizotolewa: Kikao kiliafikiana Mikakati ifuatayo kwa ajili ya Utekelezaji:

a) Kamati ya Muda ilichaguliwa ili kufanya uchambuzi yakinifu wa nini kifanyike ili yale yote ya msingi yatekelezwe ikiwa ni pamoja na Kuisajili Taasisi husika katika kipindi kisichozidi miezi mitatu. Hadidu rejea zilizotolewa zilikuwa ni:

1) Kufanya utafiti na tathmini ya je Taasisi isajiliwe kwa jina gani na kwa mfumo gani wa kisheria ikiwa ni pamoja na kuangalia mambo ya kiofisi.
2) Kutafute mtu ambaye kwa haraka atakusanya kero zote ambazo Regia alifikishiwa na kasha kuzichapisha na kuzifikisha kunakohusika.
3) Kutafuta mtu atakayeandika Biography ya Regia katika kipindi kifupi kabla ya kututoka kwa kusahaulika.
4) Kushirikiana na Wanafamilia na Wadau mbalimbali ili kupata orodha ya Wahitaji wote ambao Regia alikuwa akiwasaidia na kisha kufanya tathmini ya nini cha kufanya.

b) Wafuatao walichaguliwa kama Wanakamati kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa awali:

1) Sanctus Mtsimbe Mwenyekiti
2) Michael Dalali Katibu
3) Maxence Melo Mweka Hazina
4) Martha Noah Mjumbe
5) John Mnyika Mjumbe
6) Remijia Mtema Mjumbe
7) Mary Mniwasa Mjumbe
8) Josephine Mshumbusi Mjumbe
9) Yericko Nyerere Mjumbe

c) Ili kuwezesha utekelezaji wa awali, michango ifuatayo ilitolewa:

Jina Ahadi ktk TZS Mengineyo:

1) A 500,000 Pia atachangia 100,000 Kila Mwezi
2) B 100,000
3) C 400,000 Ametoa cash na Kila Mwezi atachangia
TZS 50,000
4) D 50,000 Ataichangia Kila Mwezi
5) E 100,000 Ametoa Cash TZS 100,000
6) F 50,000
7) G 1,000,000
8) H 500,000
9) I 100,000
10)J 100,000
11)K 100,000
12)L 50,000 Ametoa Cash TZS 20,000
13)M 50,000
14)N 500,000
15)O 50,000
16)P 50,000
17)Q 100,000 Pia atatoa TZS 1,000,000 kila Mwaka
kwa ajili ya Regia Award
18)R 100,000 Ametoa Cash
19)S 80,000 Ametoa Cash
20)T 200,000 Ametoa Cash

Kikao kilikubaliana kuwa ahadi zote zitimizwe ndani ya miezi mitatu.
 
Naona mmegeuka kujadili watu namuonekano wao dah hii hatari sasa, msimtukane mama Rwakatare kwa kusema ukweli, ushaidi ni uzi huu

nawee uncle bana kabla ya ridandaziiiiiiii ulikuwa na kitumbo tofauti na sasa uko mtaani

kwelli wamefanana hadi rasta . kuhusu uwepo wake hapa JF sijui ila 70% atakuwa hayupo hapa JF ...

aliuliza mnaziweka jf wakati akipigwa picha akaambiwa hapana akasema pls...sasa msije mkakuta mke wa m tu kwenye uongozi mkaaribu ndoa za watu jamani..wake wengi wa viongozi ni member wa jf..sema wanaogpa kuwa open against waume zao sababu ya kazi ni kazi
 
"Hivi hao watu hawana majina"?

Angalia vizuri picha hii ndio utapata jina/majina yao

attachment.php
 
Pdiddy na wenzio msiharibu thread hii kwa kunyambua watu kihivyo bwana....
We huo "uzuri" wako ulilipia sh ngapi hadi uwacheke wenzio?
Hivyo vitu vya kuchekacheka watu nakumbuka tulifanya utotoni sana.
Shame on You.

Utoto na umbumbu wa watu utauona! What physical appearance ya mtu has to do with the mind content.
Nina wasiwasi na uwezo wa kufikiri wa watu wanaojadili physical appearance.
Kwa nini tusijadili hoja zilizotolewa na maazimio yaliyofikiwa? Au ndo janja ya kututoa kwenye hoja baada ya kuona inamshiko na kujikita kwenye kujadili upupu?!!!!
 
aliuliza mnaziweka jf wakati akipigwa picha akaambiwa hapana akasema pls...sasa msije mkakuta mke wa m tu kwenye uongozi mkaaribu ndoa za watu jamani..wake wengi wa viongozi ni member wa jf..sema wanaogpa kuwa open against waume zao sababu ya kazi ni kazi
ndio wanawafukuza member hivyo kuhudhuria vikao
 
wakuu mbona picha yangu siioni? au mchango wangu haukuthaminiwa mpaka nisitoke kwenye picha?
 
Tanzania ziadi ya uijuavyo . . .

Pamoja na posts zoote, sijaona hata moja inayozungumzia kutoa mchango au msaada wa namna yoyote to support the good cause.

Tumeongelea mengi saaaana hapa jamvini juu ya dada yetu Regia (RIP), matumaini ya wengi yalikuwa ni kweli tutamuenzi kwa vitendo. Ni mwana JF moja tu ameweza kutoa pledge yake na nini angependa kussaport, wengine wote tumezama kwenye Cht-Chat za picha tu.

Tubadilike wakuu!
 
Don't judge others. God likes variety and we've all got our own little brand of "strangeness.".
 
Of course not. Sidhani kama umem-judge mtu. Would you not like the fact to take its own course? Wacha ukweli uwe ukweli.

Palipo na simple facts sidhani kama kuna haja ya kuanza kumsingizia Mungu. Another reasons why we are where we are! Si, ufisadi tu, ila tuna matatizo mengi sana!
 
Tanzania ziadi ya uijuavyo . . .

Pamoja na posts zoote, sijaona hata moja inayozungumzia kutoa mchango au msaada wa namna yoyote to support the good cause.

Tumeongelea mengi saaaana hapa jamvini juu ya dada yetu Regia (RIP), matumaini ya wengi yalikuwa ni kweli tutamuenzi kwa vitendo. Ni mwana JF moja tu ameweza kutoa pledge yake na nini angependa kussaport, wengine wote tumezama kwenye Cht-Chat za picha tu.

Tubadilike wakuu!

Distractions na digressions ungeweza kabisa kuziepuka kama usingebandika picha. Kulikuwa hakuna umuhimu wowote wa kubandika picha.

Sasa picha umebandika, watu wamezijadili halafu mnalalamika. If you didn't want people to talk about what is in the pictures then you should not have posted them in the first place.

What did you expect when you decided to post them? That people weren't gonna talk about them? Come on...y'all need to get really real now...
 
hizi ni picha za baadhi tu ya wana jf ambao ni marafiki wa regia na walihudhuria kikao, mleta mada amebandika picha kwa niaba yao, pilipili usiyoila vipi ikuwashe?

Mama lwakatare na issue za regia wapi na wapi, potezea tu, mfano wako hauna mantiki hapa rukus.
mushi na wewe hata kanisani wapo hawa uoni kila siku tunapambana na matumizi mpaka wengine wanataka sasa tra waje kuanza kula chao ...samehe mara sababa sadidy
 
Kumbumbukumbu za Kikao

Kikao Cha Marafiki wa Marehemu Mh. Regia Mtema – January 2012

Mada Kuu: "Kumtambua Regia na Alichosimamia na Nini Kifanyike Baada ya Kututoka"

Kikao cha Marafiki wa Marehemu Mh. Regia Mtema (Mb) Waishio Ndani na Nje ya Nchi Kupitia Skype uliitishwa baada ya baadhi ya Wanajamii waliokutana katika Ibada ya Kumwombea Marehemu Mh. Regia Mtema Kanisa katoliki Segerea kupendekeza hivyo. Wanajamii hawa walipendekeza kuwa ipangwe siku maalumu hivi karibuni ambayo Marafiki wa Marehemu Regia na Wadau mbalimbali watakutana British Council na kujadili yale yote aliyosimamia Regia na nini cha kujifunza kutoka kwake na kukifanya ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi marehemu.

Ilipendekezwa kuwa Kiitishwe Kikao katika Ukumbi wa British Council siku ya Ijumaa Tarehe 27-01-2012 kuanzia saa 11jioni hadi saa 2 Usiku ili kuweza kulijadili masuala husika. Wazo hili liliwakilishwa kwa Wanajamii wengine kupitia mtandao wa Jamiiforums (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...an-2012-a.html) ambapo Wanajamii wengi wapatao 70 waliunga mkno wazo hili na kusthibitisha kushiri ama kwa kufika British Council, ama Kushiriki kwa njia ya Skype kupitia ID maalumu ya: jamiiforums.

Hatimaye Kikao kilithibitishwa kupitia Jamiiforums (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...01-2012-a.html) na kufanyika kama ulivyopangwa. Jumla ya Wanajamii 25 Walihudhuria British Council wakiwemo Wazazi wa Regia na Pacha wa Regia na wengine wapatao 60 walishiriki kupitia Skype Video Conferencing ambapo baadhi pia walipata nafasi ya kuchangia maoni yao. Baadhi walifuatilia kupitia Mtandao wa Jamiiforums ambapo jumla ya mabandiko 273 yaliwekwa siku hiyo na maangalizo (views) zaidi ya 6000.

Majadiliano katika Kikao hiki yaliendeshwa kwa utaratibu wa kuchangia hoja/mada kuu, huku mchangiaji akielezea suala / hoja husika, anavyomtambua Marehemu Mh. Regia, Mchango wake na nini kifanyike baada ya Regia kututoka, mapendekezo na mikakati ya utekelezaji. Washiriki wa Skype waliweza kupiga Voice au Video Call British Council na wakasikika katika vipaza sauti huku na wengine wakifuatilia mjadala kwa kuangalia internet kupitia: Friends of JF on USTREAM: . Baada ya hapo washiriki walipitia hoja mbalimbali na kukubaliana juu ya namna gani Marehemu Regia atambuliwe, Maazimio na Mikakati ya Utekelezaji. Yote haya yalifanyika kwa kuzingatia nafasi ya Regia katika jamii bila kujali itikadi yake kisiasa.

Mmoja wa Waanzilish wa Jamiiforums pia alipata fursa za kuwakilisha rambirambi za wanachama wa JF. Kiasi kilichowakilishwa ni TZS 1.5 Millions.

Zifuatazo ni Kumbukumbu, Maazimio na Mikakati kama ilivyokubalika katika Kikao hicho:

1. Kuhusu Kumtambua Regia: Kikao Kilichambua na kukubaliana Regia atambuliwe rasmi kama ifuatavyo:

1. Kwamba wote walioshiriki katika hicho Kikao wanamtambua Regia kama Rafiki yao katika harakati za Kijamii bila kujali itikadi, imani au jinsia yake.

2. Regia alikuwa ni Mwanaharakati wa Kijamii na Kisiasa aliyekuwa Mlemavu wa kiungo lakini ambaye ulemavu wake haumkumzuia kufanya jambo lolote alililiamini na kulisimamia. Kwa hili Regia amekuwa mfano wa kuigwa kuwa kuwa na ulemavu si sababu ya kushindwa kutenda jambo unalokusudia kulitenda.

3. Regia alikuwa ni Mwanamke shujaa ambaye hakuikumbatia dhana ya "Wanawake tukipewa nafasi au tukiwezeshwa tunaweza". Alikuwa mwanamke jasiri anayejiamini kwa uwezo wake bila kujali jinsia yake. Hilo alilidhihirisha pia pale alipoamua kugombea ubunge wa jimbo la Kilombero na kuchuana vikali na mgombea wa jinsia ya kiume na huku akitoa changamoto kubwa sana. Hata alipoashindwa aliweza kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu huku akiwa Waziri Kivuli wa Wizara ya kazi na Ajira. Kwa hili Regia amekuwa ni mfano wa Kuigwa na Wanawake wote.

4. Regia alikuwa ni mtu mwenye mapenzi makubwa na Nchi yake na Jamii kwa ujumla. Regia amekuwa mara nyingi akiwahimiza Wananchi wampelekee kero zao ili aweze kuzisemea Bungeni na Kuziwasilisha katika vyombo husika.

5. Regia alikuwa ni Mtu mwenye Upendo na Huruma na Msaada kwa Wahitaji. Kwa hili aliwasaidia yeye binafsi wale ambao walitaka msaada wa namna mbalimbali kutoka kwake kama Wasiojiweza na Yatima n.k. Hili ni jambo la kuigwa maana kuna wenye uwezo zaidi ya Regia na wasio na Ulemavu wowote ambao hawajaweza kufanya kama Regia alivyofanya.

6. Regia katika nia njema ya kuwatumikia Wananchi wa jimbo analotoka la Kilombero kwa karibu, alikuwa katika harakati ya kuanzisha taasisi itakayosaidia kuboresha maisha ya Wana Kilombero aliyokusudia kuipa jina la Kilombero For Change (K4C).

2. Maazimio ya Kikao Kutokana na hoja zilizotajwa hapo juu; Kikao Kimeazimia yafuatayo:

1. Ili kumuenzi Marehemu Regia Mtema, ianzishwe Taasisi maalumu itakayoendeleza yale aliyoyaamini na kuyasimamia kwa faida ya Watanzania wote. Mchakato wa Kuianzisha ufanywe na kisha kuisajili huku ikiwahusisha Wadau mbalimbali ambao wangependa kuona harakati za Regia zinaendelea.

2. Kiandikwe kitabu cha Maisha ya Regia "Biography" ambacho mbali la historia yake ya maisha na harakati za kijamii, kitakusanya maandiko na matamko yake mbalimbali pamoja na picha zake.

3. Kero zote ambazo Mh. Regia aliandikiwa na wananchi ili aweze kuzisemea Bungeni na kuziwasilisha kunakohusika zikusanywe na kuwekwa katika Kijarida au Kitabu kidogo ambacho kitawakilishwa kwa Spika wa Bunge ali afikishe kwa wahusika na pia kuwapa nakala kila Mbunge ili waweze kuyasemea Bungeni kama alivyokusudia.

4. Ili kumuenzi Regia na pia kuhamasisha Wanawake na hasa wale wasiojiweza, itaandaliwa tuzo maalumu kila Mwaka ambayo itapewa jina la Regia. Tuzo hii itatolewa kwa mtu yeyote mwenye ulemavu kwa viungo ambaye ulemavu wake haujaweza kuwa kikwazo hasa katika kufanikisha utendaji wake katika jamii huko akizingatia maadili.

5. Taasisi itakayoundwa ianzishe pia Programu maalumu ambayo itaendeleza baadhi ya mambo ya kimsingi ambayo Regia alipanga kuyaendeleza.

6. Kwa kuwa Regia alikuwa anawasaidia Yatima na Wasiojiweza na kuwasomesha baadhi yao, itaanzishwa Programu maalumu ya kuendeleza na kuyasimamia hayo pamoja na Scholarship ambayo itachangiwa na Marafiki wa Regia na wale wote wenye mapenzi mema na suala husika.

7. Kuomba kibali cha Kujenga Mnara wa Kumbukumbu sehemu aliyopatia ajali ikiwa ni ishara ya

a) Kuwakumbusha Watanzania kuwa hata Mwanamke Anaweza bila Kuwezeshwa.
b) Hata Mlemavu anaweza akafanya jambo lolote kama asiye mlemavu
c) Kwamba watumiaji wa barabara hiyo ambayo inaongoza kwa ajali, wawe makini pale wanapoitumia na hasa kwa kuzingatia vema sharia za barabarani
d) Sheria za barabarani ziboreshwe na barabara kupanuliwa ili kuondoa kabisa au kupunguza ajali.
e) Kumbukumbu ya Regia kuwa hata kama hayupo lakini aliyoyaamini na kuyasimamia yataendelezwa.

3. Kuhusu Mikakati ya Utekeleza ya Maazimio na Hoja Zilizotolewa: Kikao kiliafikiana Mikakati ifuatayo kwa ajili ya Utekelezaji:

a) Kamati ya Muda ilichaguliwa ili kufanya uchambuzi yakinifu wa nini kifanyike ili yale yote ya msingi yatekelezwe ikiwa ni pamoja na Kuisajili Taasisi husika katika kipindi kisichozidi miezi mitatu. Hadidu rejea zilizotolewa zilikuwa ni:

1) Kufanya utafiti na tathmini ya je Taasisi isajiliwe kwa jina gani na kwa mfumo gani wa kisheria ikiwa ni pamoja na kuangalia mambo ya kiofisi.
2) Kutafute mtu ambaye kwa haraka atakusanya kero zote ambazo Regia alifikishiwa na kasha kuzichapisha na kuzifikisha kunakohusika.
3) Kutafuta mtu atakayeandika Biography ya Regia katika kipindi kifupi kabla ya kututoka kwa kusahaulika.
4) Kushirikiana na Wanafamilia na Wadau mbalimbali ili kupata orodha ya Wahitaji wote ambao Regia alikuwa akiwasaidia na kisha kufanya tathmini ya nini cha kufanya.

b) Wafuatao walichaguliwa kama Wanakamati kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa awali:

1) Sanctus Mtsimbe Mwenyekiti
2) Michael Dalali Katibu
3) Maxence Melo Mweka Hazina
4) Martha Noah Mjumbe
5) John Mnyika Mjumbe
6) Remijia Mtema Mjumbe
7) Mary Mniwasa Mjumbe
8) Josephine Mshumbusi Mjumbe
9) Yericko Nyerere Mjumbe

c) Ili kuwezesha utekelezaji wa awali, michango ifuatayo ilitolewa:

Jina Ahadi ktk TZS Mengineyo:

1) A 500,000 Pia atachangia 100,000 Kila Mwezi
2) B 100,000
3) C 400,000 Ametoa cash na Kila Mwezi atachangia
TZS 50,000
4) D 50,000 Ataichangia Kila Mwezi
5) E 100,000 Ametoa Cash TZS 100,000
6) F 50,000
7) G 1,000,000
8) H 500,000
9) I 100,000
10) J 100,000
11) K 100,000
12) L 50,000 Ametoa Cash TZS 20,000
13) M 50,000
14) N 500,000
15) O 50,000
16) P 50,000
17) Q 100,000 Pia atatoa TZS 1,000,000 kila Mwaka
kwa ajili ya Regia Award
18) R 100,000 Ametoa Cash
19) S 80,000 Ametoa Cash
20) T 200,000 Ametoa Cash

Kikao kilikubaliana kuwa ahadi zote zitimizwe ndani ya miezi mitatu.

------------------------------------------------------------------------------------------

NB:

Kwa niaba ya Marafiki wa Regia waliokutana, napenda kuchukua fursa hii kuwaalika wadau wote ambao wangependa kuweka nia yao ya kuwa Wanachama wa Taasisi itakayoanzishwa kama ilivyo ainishwa hapo juu. Pia wale wote ambao wangependa kuchangia kwa hali na mali wanakaribishwa.

Unaweza kumwandikia Maxence au Sanctus (PM).

Wasalaam

Sanctus Mtsimbe
------------------------------------------------------------------------------

Zifuatazo ni baadhi ya kumbukumbu za Picha katika Kikao hicho:

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

attachment.php

Shikamooni wakuu Nilistuka nikasema whoopi naye alikuwemo...
 
Back
Top Bottom