Picha na maelezo: Kikao cha Marafiki Wa Regia BC

Naona mmegeuka kujadili watu namuonekano wao dah hii hatari sasa, msimtukane mama Rwakatare kwa kusema ukweli, ushaidi ni uzi huu
Hizi ni picha za baadhi tu ya wana JF ambao ni marafiki wa Regia na walihudhuria kikao, mleta mada amebandika picha kwa niaba yao, pilipili usiyoila vipi ikuwashe?

Mama Lwakatare na issue za Regia wapi na wapi, potezea tu, mfano wako hauna mantiki hapa Rukus.
 
Kuna mtu alimfananisha huyo na avatar yako.

Nasikia huyo ndio PAW kwa mujibu wa posts za kwenye nyuzi hii, naogopa ku comment kuja kula ban ambazo sikutegemea. Kama kweli ni Paw, na kwa kui analyze hiyo sura yake, sasa najuwa kwanini ban zake zinakuwa sana baada ya saa sita usiku.
Lol...ROTFL..nimecheka sana!! Ngoja nijilalie tu!
 
aisee tuna madada wazuri kweliiiiiiii JF LAKINI WAKO SIRIAZI SIJUI LIZZY HUYU!!!NINGEKUWEPO KARIBU NINGEDONDOSHA SHILLINGI NIHAKIKISHE


attachment.php

haaah haaah Lizy upooo?!
 
Poa kaka,

Soma tu PM sasa hivi utakuta maelezo zaidi,

Naomba sana tujitahidi walau kwenye hili jambo...Watanzania tumekuwa mabingwa sana wa kulalamika pale ambapo wenzetu wanashindwa kutekeleza mambo fulani...Hiyo tuifanye hii iwe changamoto kwetu ili tupate uhalali wa kuwalaumu wazembe....

Just motiviating myself and wadau wengine wanaounga mkono jitihada zenu!!

Babu DC!!


Mkuu nimekusoma kwenye PM. Mambo yako ni makubwa sana na yanatisha. Hakika wewe ni mtu wa vitendo and I wish wadau wengine waige mfano wako.

Who knows, inaweza ukawa ndo mwanzo mzuri wa kufanya mambo makubwa.

Pamoja sana Mkuu.
 
Mijitu mingine bana, badala ya kujadili hoja inakimbilia kwenye kujadili picha. Hongera kwa kubandika andiko hili hapa hata kama limekuja kwa kucheklewa na wote waliohudhuria, hasa toka JF mlifanya kitu sahihi, wanaojadili uzuri au ubaya wa picha nakosa neno baya lenye uzri unaowastahili, ngoja nitizame avatar yangu nipoze hasira
 
Poa kaka,

Soma tu PM sasa hivi utakuta maelezo zaidi,

Naomba sana tujitahidi walau kwenye hili jambo...Watanzania tumekuwa mabingwa sana wa kulalamika pale ambapo wenzetu wanashindwa kutekeleza mambo fulani...Hiyo tuifanye hii iwe changamoto kwetu ili tupate uhalali wa kuwalaumu wazembe....

Just motiviating myself and wadau wengine wanaounga mkono jitihada zenu!!

Babu DC!!

Asante sana Babu CD. Tumekusoma na tutajitahidi katika utekelezaji.
 
Waama kuwasema watu waliojumuika kwa jambo la heri msibani si jambo la maana.

Isitoshe muungwana hujua "hujafa hujaumbika" na kutoa maneno ya kashfa kwa sababu ya majaliwa ya maisha, majaliwa ambayo hata huyajui mwanzo mwisho wake, majaliwa yanayoweza kukukuta hata wewe, ni kukosa taadhima na busara za utu wa kawaida tu.

Mie nitawapigia heko wote waliojumuika katika jambo hili la heri na kumuenzi bibie.

Habari za kuleta matani katika mambo yaso masikhara sintoweza.
 
Kama hamkutaka watu wazijadili hizo picha basi msingeziweka! Mngeweka hoja kwa maandishi tu pasipo na picha na watu wakajikita kwenye hoja.

Zaidi ya hapo mtu unapoweka picha kwenye jamvi la hadhara kama hili basi ujue yote yatajadiliwa. Hutaki watu wajadili picha, usiweke picha. Sasa mtu unabandika picha halafu unategemea watu tusitie maneno yetu kwenye tunachokiona? Mnacheza nyinyi!

Kuweka picha na kutegemea watu wasijadili picha na badala yake wajadili mengine ni sawa na kupaka rangi upepo!
 
Kafanana na whoopy Goldberg Yule actress wa kimerekani. Na inawezekana kuwa yupo JF vile vile, unajuwaje kama hayupo?
kwelli wamefanana hadi rasta . kuhusu uwepo wake hapa JF sijui ila 70% atakuwa hayupo hapa JF ...
 
Mkuu nijisemee kwanza mie mwenyewe.

Nashukuru kwa hizo picha ingawa kidogo maelezo yamepungua hasa kujulisha nani ni nani.

Ila kuna dada anafanana sana na Merehemu, sijui atakuwa ndiye pacha wake?

Mbarikiwe kwa zoezi zima kuanzia kufikiri, kuanza na kumaliza.

Brother Sikonge Bwana

Mie nahitaji jina la mama wa Kwanza mwenye Suti,
SM do the needful please
 

attachment.php


Alijitambulisha kama Mama J. Member wa JF na alijivunia sana kuwa Member. Alitufurahisha alipoelezea historia ya yeye alivyoingia JF.

attachment.php


Mohamed Shossy - Hata hapa JF anatumia jina hilo hilo.




attachment.php


Remijia Mtema - Pacha wa Rejia - Aliwaacha Wadau hoi alipoweka wazi kuwa Gaijin alikuwa anawapa changamoto sana kiasi kuwa yeye na Rejia walikuwa wanajipanga kujibu mashambulizi. Anasema hakupenda kuona pacha wake anashambuliwa hivyo ilibidi naye aanze kupenda jukwaa la siasa ingawa lake lilikuwa MMU.




attachment.php


Mh. John Mnyika - akichangia jambo


attachment.php


JF Founde Maxence Melo - Akimkabidhi Cheque ya Rambirambi Mzee Mtema - Baba yake Rejia​
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom