Picha na maelezo: Kikao cha Marafiki Wa Regia BC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha na maelezo: Kikao cha Marafiki Wa Regia BC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sanctus Mtsimbe, Feb 6, 2012.

 1. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #1
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kumbumbukumbu za Kikao

  Kikao Cha Marafiki wa Marehemu Mh. Regia Mtema – January 2012

  Mada Kuu: "Kumtambua Regia na Alichosimamia na Nini Kifanyike Baada ya Kututoka"

  Kikao cha Marafiki wa Marehemu Mh. Regia Mtema (Mb) Waishio Ndani na Nje ya Nchi Kupitia Skype uliitishwa baada ya baadhi ya Wanajamii waliokutana katika Ibada ya Kumwombea Marehemu Mh. Regia Mtema Kanisa katoliki Segerea kupendekeza hivyo. Wanajamii hawa walipendekeza kuwa ipangwe siku maalumu hivi karibuni ambayo Marafiki wa Marehemu Regia na Wadau mbalimbali watakutana British Council na kujadili yale yote aliyosimamia Regia na nini cha kujifunza kutoka kwake na kukifanya ikiwa ni njia mojawapo ya kumuenzi marehemu.

  Ilipendekezwa kuwa Kiitishwe Kikao katika Ukumbi wa British Council siku ya Ijumaa Tarehe 27-01-2012 kuanzia saa 11jioni hadi saa 2 Usiku ili kuweza kulijadili masuala husika. Wazo hili liliwakilishwa kwa Wanajamii wengine kupitia mtandao wa Jamiiforums (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...an-2012-a.html) ambapo Wanajamii wengi wapatao 70 waliunga mkno wazo hili na kusthibitisha kushiri ama kwa kufika British Council, ama Kushiriki kwa njia ya Skype kupitia ID maalumu ya: jamiiforums.

  Hatimaye Kikao kilithibitishwa kupitia Jamiiforums (https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...01-2012-a.html) na kufanyika kama ulivyopangwa. Jumla ya Wanajamii 25 Walihudhuria British Council wakiwemo Wazazi wa Regia na Pacha wa Regia na wengine wapatao 60 walishiriki kupitia Skype Video Conferencing ambapo baadhi pia walipata nafasi ya kuchangia maoni yao. Baadhi walifuatilia kupitia Mtandao wa Jamiiforums ambapo jumla ya mabandiko 273 yaliwekwa siku hiyo na maangalizo (views) zaidi ya 6000.

  Majadiliano katika Kikao hiki yaliendeshwa kwa utaratibu wa kuchangia hoja/mada kuu, huku mchangiaji akielezea suala / hoja husika, anavyomtambua Marehemu Mh. Regia, Mchango wake na nini kifanyike baada ya Regia kututoka, mapendekezo na mikakati ya utekelezaji. Washiriki wa Skype waliweza kupiga Voice au Video Call British Council na wakasikika katika vipaza sauti huku na wengine wakifuatilia mjadala kwa kuangalia internet kupitia: Friends of JF on USTREAM: . Baada ya hapo washiriki walipitia hoja mbalimbali na kukubaliana juu ya namna gani Marehemu Regia atambuliwe, Maazimio na Mikakati ya Utekelezaji. Yote haya yalifanyika kwa kuzingatia nafasi ya Regia katika jamii bila kujali itikadi yake kisiasa.

  Mmoja wa Waanzilish wa Jamiiforums pia alipata fursa za kuwakilisha rambirambi za wanachama wa JF. Kiasi kilichowakilishwa ni TZS 1.5 Millions.

  Zifuatazo ni Kumbukumbu, Maazimio na Mikakati kama ilivyokubalika katika Kikao hicho:


  1. Kuhusu Kumtambua Regia: Kikao Kilichambua na kukubaliana Regia atambuliwe rasmi kama ifuatavyo:

  1. Kwamba wote walioshiriki katika hicho Kikao wanamtambua Regia kama Rafiki yao katika harakati za Kijamii bila kujali itikadi, imani au jinsia yake.

  2. Regia alikuwa ni Mwanaharakati wa Kijamii na Kisiasa aliyekuwa Mlemavu wa kiungo lakini ambaye ulemavu wake haumkumzuia kufanya jambo lolote alililiamini na kulisimamia. Kwa hili Regia amekuwa mfano wa kuigwa kuwa kuwa na ulemavu si sababu ya kushindwa kutenda jambo unalokusudia kulitenda.

  3. Regia alikuwa ni Mwanamke shujaa ambaye hakuikumbatia dhana ya "Wanawake tukipewa nafasi au tukiwezeshwa tunaweza". Alikuwa mwanamke jasiri anayejiamini kwa uwezo wake bila kujali jinsia yake. Hilo alilidhihirisha pia pale alipoamua kugombea ubunge wa jimbo la Kilombero na kuchuana vikali na mgombea wa jinsia ya kiume na huku akitoa changamoto kubwa sana. Hata alipoashindwa aliweza kuteuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalumu huku akiwa Waziri Kivuli wa Wizara ya kazi na Ajira. Kwa hili Regia amekuwa ni mfano wa Kuigwa na Wanawake wote.

  4. Regia alikuwa ni mtu mwenye mapenzi makubwa na Nchi yake na Jamii kwa ujumla. Regia amekuwa mara nyingi akiwahimiza Wananchi wampelekee kero zao ili aweze kuzisemea Bungeni na Kuziwasilisha katika vyombo husika.

  5. Regia alikuwa ni Mtu mwenye Upendo na Huruma na Msaada kwa Wahitaji. Kwa hili aliwasaidia yeye binafsi wale ambao walitaka msaada wa namna mbalimbali kutoka kwake kama Wasiojiweza na Yatima n.k. Hili ni jambo la kuigwa maana kuna wenye uwezo zaidi ya Regia na wasio na Ulemavu wowote ambao hawajaweza kufanya kama Regia alivyofanya.

  6. Regia katika nia njema ya kuwatumikia Wananchi wa jimbo analotoka la Kilombero kwa karibu, alikuwa katika harakati ya kuanzisha taasisi itakayosaidia kuboresha maisha ya Wana Kilombero aliyokusudia kuipa jina la Kilombero For Change (K4C).

  2. Maazimio ya Kikao Kutokana na hoja zilizotajwa hapo juu; Kikao Kimeazimia yafuatayo:

  1. Ili kumuenzi Marehemu Regia Mtema, ianzishwe Taasisi maalumu itakayoendeleza yale aliyoyaamini na kuyasimamia kwa faida ya Watanzania wote. Mchakato wa Kuianzisha ufanywe na kisha kuisajili huku ikiwahusisha Wadau mbalimbali ambao wangependa kuona harakati za Regia zinaendelea.

  2. Kiandikwe kitabu cha Maisha ya Regia "Biography" ambacho mbali la historia yake ya maisha na harakati za kijamii, kitakusanya maandiko na matamko yake mbalimbali pamoja na picha zake.

  3. Kero zote ambazo Mh. Regia aliandikiwa na wananchi ili aweze kuzisemea Bungeni na kuziwasilisha kunakohusika zikusanywe na kuwekwa katika Kijarida au Kitabu kidogo ambacho kitawakilishwa kwa Spika wa Bunge ali afikishe kwa wahusika na pia kuwapa nakala kila Mbunge ili waweze kuyasemea Bungeni kama alivyokusudia.

  4. Ili kumuenzi Regia na pia kuhamasisha Wanawake na hasa wale wasiojiweza, itaandaliwa tuzo maalumu kila Mwaka ambayo itapewa jina la Regia. Tuzo hii itatolewa kwa mtu yeyote mwenye ulemavu kwa viungo ambaye ulemavu wake haujaweza kuwa kikwazo hasa katika kufanikisha utendaji wake katika jamii huko akizingatia maadili.

  5. Taasisi itakayoundwa ianzishe pia Programu maalumu ambayo itaendeleza baadhi ya mambo ya kimsingi ambayo Regia alipanga kuyaendeleza.

  6. Kwa kuwa Regia alikuwa anawasaidia Yatima na Wasiojiweza na kuwasomesha baadhi yao, itaanzishwa Programu maalumu ya kuendeleza na kuyasimamia hayo pamoja na Scholarship ambayo itachangiwa na Marafiki wa Regia na wale wote wenye mapenzi mema na suala husika.

  7. Kuomba kibali cha Kujenga Mnara wa Kumbukumbu sehemu aliyopatia ajali ikiwa ni ishara ya

  a) Kuwakumbusha Watanzania kuwa hata Mwanamke Anaweza bila Kuwezeshwa.
  b) Hata Mlemavu anaweza akafanya jambo lolote kama asiye mlemavu
  c) Kwamba watumiaji wa barabara hiyo ambayo inaongoza kwa ajali, wawe makini pale wanapoitumia na hasa kwa kuzingatia vema sharia za barabarani
  d) Sheria za barabarani ziboreshwe na barabara kupanuliwa ili kuondoa kabisa au kupunguza ajali.
  e) Kumbukumbu ya Regia kuwa hata kama hayupo lakini aliyoyaamini na kuyasimamia yataendelezwa.

  3. Kuhusu Mikakati ya Utekeleza ya Maazimio na Hoja Zilizotolewa: Kikao kiliafikiana Mikakati ifuatayo kwa ajili ya Utekelezaji:

  a) Kamati ya Muda ilichaguliwa ili kufanya uchambuzi yakinifu wa nini kifanyike ili yale yote ya msingi yatekelezwe ikiwa ni pamoja na Kuisajili Taasisi husika katika kipindi kisichozidi miezi mitatu. Hadidu rejea zilizotolewa zilikuwa ni:

  1) Kufanya utafiti na tathmini ya je Taasisi isajiliwe kwa jina gani na kwa mfumo gani wa kisheria ikiwa ni pamoja na kuangalia mambo ya kiofisi.
  2) Kutafute mtu ambaye kwa haraka atakusanya kero zote ambazo Regia alifikishiwa na kasha kuzichapisha na kuzifikisha kunakohusika.
  3) Kutafuta mtu atakayeandika Biography ya Regia katika kipindi kifupi kabla ya kututoka kwa kusahaulika.
  4) Kushirikiana na Wanafamilia na Wadau mbalimbali ili kupata orodha ya Wahitaji wote ambao Regia alikuwa akiwasaidia na kisha kufanya tathmini ya nini cha kufanya.

  b) Wafuatao walichaguliwa kama Wanakamati kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa awali:

  1) Sanctus Mtsimbe Mwenyekiti
  2) Michael Dalali Katibu
  3) Maxence Melo Mweka Hazina
  4) Martha Noah Mjumbe
  5) John Mnyika Mjumbe
  6) Remijia Mtema Mjumbe
  7) Mary Mniwasa Mjumbe
  8) Josephine Mshumbusi Mjumbe
  9) Yericko Nyerere Mjumbe  c) Ili kuwezesha utekelezaji wa awali, michango ifuatayo ilitolewa:

  Jina Ahadi ktk TZS Mengineyo:

  1) A 500,000 Pia atachangia 100,000 Kila Mwezi
  2) B 100,000
  3) C 400,000 Ametoa cash na Kila Mwezi atachangia
  TZS 50,000
  4) D 50,000 Ataichangia Kila Mwezi
  5) E 100,000 Ametoa Cash TZS 100,000
  6) F 50,000
  7) G 1,000,000
  8) H 500,000
  9) I 100,000
  10) J 100,000
  11) K 100,000
  12) L 50,000 Ametoa Cash TZS 20,000
  13) M 50,000
  14) N 500,000
  15) O 50,000
  16) P 50,000
  17) Q 100,000 Pia atatoa TZS 1,000,000 kila Mwaka
  kwa ajili ya Regia Award
  18) R 100,000 Ametoa Cash
  19) S 80,000 Ametoa Cash
  20) T 200,000 Ametoa Cash

  Kikao kilikubaliana kuwa ahadi zote zitimizwe ndani ya miezi mitatu.

  ------------------------------------------------------------------------------------------

  NB:

  Kwa niaba ya Marafiki wa Regia waliokutana, napenda kuchukua fursa hii kuwaalika wadau wote ambao wangependa kuweka nia yao ya kuwa Wanachama wa Taasisi itakayoanzishwa kama ilivyo ainishwa hapo juu. Pia wale wote ambao wangependa kuchangia kwa hali na mali wanakaribishwa.

  Unaweza kumwandikia Maxence au Sanctus (PM).

  Wasalaam

  Sanctus Mtsimbe
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu nijisemee kwanza mie mwenyewe.

  Nashukuru kwa hizo picha ingawa kidogo maelezo yamepungua hasa kujulisha nani ni nani.

  Ila kuna dada anafanana sana na Merehemu, sijui atakuwa ndiye pacha wake?

  Mbarikiwe kwa zoezi zima kuanzia kufikiri, kuanza na kumaliza.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hongereni kwa hilo mlilolifanya
  Ila naomba nitofautiane na mtoa mada hapo juu ingependeza zaidi picha zikabakia kama zilivyo bila utambulisho. May be kwa ridhaa ya wahusika unaweza kusema huyu ni nani na yule ni nani
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "Hivi hao watu hawana majina"?
   
 5. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Seen but far from being convincing with that handful of just a few people scattered on the floor - the much advertising notwithstanding. Why did things have to take this long before coming back to air after all?

  If not enough, we long to see itemised set of resolutions to the effect that is intended to be undertaken outside Regia's known formal political outfit in the country.

  Hongereni hata hivo.
   
 6. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mkuu ka unapicha yangu pia niweke.
   
 7. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Majina yamepotea!
   
 8. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Skype Voice Calls:

  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 9. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  safiiiiiii na hongereni sana
   
 10. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Good work please keep it up, it is one step towards the correct direction

  VIVA JF
   
 11. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru wakuu kwa kutuwakalisha
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hongereni sana
   
 13. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #13
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  More photos:

  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]
   

  Attached Files:

 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks wakuu

  i hope kutakua na muendelezo na haya hayataishia hapa
   
 15. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,422
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  tumefurahi sana....kwa uwakilishi huo...

  tunaomba mleta uzi ungetuhabarisha yaliyosemwa na wahusika wakuu....eg mama yetu Josephine...JJ nk..

  ila mnyika namkubali!!!! ona anavyotulia na bic yake.....kama OBAMA VILE....

  mnyika tulia mdogo wangu...naamini kabla sijafa nitakuwa nimeishakupigia kura ya kuingia ikulu!!!! wala uciwe na papara.....baada ya slaa unaonekana kuwa ni NEXT presidential material......UNACHOHITAJI SASA NI KUJIFUNZA KWA BIDII SYSTEMS ZINAVYOFANYA KAZI......NA KUJUA JINSI YA KUFANYA KAZI NAZO ILI UPATE UUNGWAJI MORORO MKONO....PIA UNAHITAJI KUFANYA MASTERS HARAKA HARAKA..........HUNA MUDA TENA....fanya mpango uoe pia sasa....usisahau kujirusha rusha kidogo kidogo..ukiingia kwenye lile jumba usiwe unatoroka uciku kwenda viwanja kama mukulu jk

  YOU MIGHT BE THE NEXT SOKOINE.......KWENYE SEREKALI YAKO MAKE SURE ZITO NI vp AU PRIMEIR! SO FAR KWA STARS WETU CHADEMA WEWE NA ZITO MNAPASWA MTULIE SANA...... MNATUONGOZA WENGI SANA PIA.....
   
 16. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wewe picha yako ipo wapi?tuiandike jina..
   
 17. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #17
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  More Pictures:

  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]
   

  Attached Files:

 18. K

  Kanyigo JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 959
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kila nikimuona mnyika roho yangu mwemele..sijui kwanini mimi nimpiga kura wa nshomile area najuta sana.
   
 19. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kwani hunioni hapo?
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  thanks mkuu, nilichelewa kufika siku hiyo, ila wakati mnatoka nilikuwepo nje najiburuza chini, (kama uliona kizee kilichochoka sana nje na nguo kuukuu ndo nilikuwa mimi, getini walikataa kuniruhusu kuingia kutokana na uchafu nilokuwanao)
   
Loading...