(PICHA) Mwakyembe: Mjadala wa AFYA yangu UMEFUNGWA 'FULL STOP'

Ila ki2 kingin hata kama polisi walisema tofauti au wamekataa kusema vile inavyotatikana kwann asijitokeze mwenyewe hadharani kama alivyofanya mwanzo wakati anataka huruma ya uma na maombi ye2 ku2juza exactly kipi ni kipi na lipi ni lipi 2elewe kweli huyu jamaa mnafiki sana na ngoja aumwe tena ......
 
  1. Kuna jamaa alitangaza dunia nzima kuwa ndugu X ndiye aliyempa mimba mke wake, siku alipogundua kuwa mkewe kapewa mimba na kaka yake mwenyewe alianza kutembea mtaani na kusema hataki tena watu wazungumze hiyo habari, wakati yeye in the first place ndo aliimwaga hadharani..........
  2. Inakuwaje unapofikiria unaumwa Malaria baadaye unagundua kumbe una Typhoid?
 
Kama POLISI hawataki kuongea ukweli,ulitaka Mwakyembe aseme nini?Au ukienda MAHAKAMANI wakasema ushahidi wako hautoshelezi utafanya nini?

Yeye ametoa ukweli upi wa kiundani/ wenye ushahidi zaidi ya kuwakosoa polisi na kuwaita polisi wanafiki huku akitoa ahadi za kuweka wazi kila kitu akirejea??
Unafiki wake/wao haujaanza leo,wanaparuana na kuchokonoana huku wakijitokeza na kulialia wanapozidiwa lakini wakipoa hasemi ukweli kwani wote ni wachafu!! Kweli unahitaji akili za mfu kuitetea ccm&co,na awamu ya nne ni kama yote na watu wake wamelaaniwa!!
 
Afya inaendelea vizuri, kwanini anavaa kofia ofisini na joto lote hili? Hii kitu ikishaingia kwenye bone marrow ni mgogoro sana! Hata hivyo nakutakia kila kheri, damu asimame nawe.

Huyo ana ukosefu wa kinga mwilini ambao umeshambulia "bone marrow" na hana cha kupewa sumu wala nini. Sasa mnataka awaambieni kuwa ana ngwengwe ya ngozi na mifupa?
 
KYELA hatuna mbunge.Tuitishe uchaguzi wa mbunge kwa kigezo cha kuto
mwamini mbunge wetu,hajakuwepo jimboni kwake muda mrefu na ki afya pia.
 
Siamini kama ameongea kwa ufupi kiasi hicho, kwani watanzania siku zote wamekuwa wakisononeka juu yake na kumuombea kila siku, leo aje atoe matamshi ya kuwakatisha tamaa kiasi hicho! mimi siamini hadi nipate taarifa kamili!
 
Nilijua tu atatuzuga kama alivyotuzuga kwenye Richmond
Next time Magamba mkimnanii msikosee tena..
 
Nadhani wana jamvi hamjamwelewa Dr Mwakyembe

yeye anasema,kwa kuwa serikali imeunda tume ya kuchunguza ugonjwa wake,basi tuache tume imalize kazi yake na itatoa ripoti kwa wananchi.

nadhani anacho ogopa yeye ni kutoa taarifa ambayo labda itaweza kuilazimisha tume iseme kile alicho sema yeye.labda kama tume itakuja na majibu kinyume na Dr aonavyo,basi anaweza sasa kutueleza alicho nacho
 
Siamini kama ameongea kwa ufupi kiasi hicho, kwani watanzania siku zote wamekuwa wakisononeka juu yake na kumuombea kila siku, leo aje atoe matamshi ya kuwakatisha tamaa kiasi hicho! mimi siamini hadi nipate taarifa kamili!

mleta mada amechukua tu vichwa vya habari na picha toka michuzi blog na kutubandikia hapa
 
jembe limepiga kutu halwezi lima tena hilo!!
"kweli jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza"
yaani nilitegemea jamaa ndio angetumalizia lile wimbi la "Kolimbalization" sasa limekubali kufa kifo cha kondoo.'I'm dissappointed"
 
...jamaa kwisha habari yake.

it will be interesting kuona sasa watu wa kyela wanasemaje juu ya huyu "shujaa" wao maslahi!
 
Hakika huyu jamaa sasa ndo twaweza kumjua vyema, nasafiri boti moja sasa na Mwalimu mkuu wa watu mzee Mayega! Aliyokuwa akiandika juu ya huyu bwana pamoja na gamba mwenzake sitta nilidhani ni chuki binafsi ila kumbe yeye aliwafahamu kabla yetu, wajue hawatopata nafasi tena ya kutudanganya.
 
Ameonywa huyo...akafie mbele. Kimya kimya utasikia alishavuta huyu. Mpiganaji ndani ya magamba, wapi bwana. ndiyo...kwisha, full stop!

Ukitaka ukweli soma hii kwenye MWANAHALISI.
Na Saed Kubenea - Imechapwa 22 February 2012

UGONJWA wa Dk. Harrison Mwakyembe, mbunge wa kyela (CCM) umeivuruga serikali.
Wakati Waziri wa Afya, Dk Hadji Mponda anadai kwamba hajaona ripoti ya ugonjwa huo, taarifa zinasema Rais Jakaya Kikwete alishatoa taarifa juu ya ugonjwa wa Mwakyembe ndani ya Baraza la Mawaziri.
Chanzo cha habari hii kinasema pamoja na kukana kupata taarifa za ugonjwa wa Mwakyembe, Waziri Mponda ameelezwa kuwepo ndani ya kikao cha baraza la mawaziri ambacho Rais Kikwete alifafanulia ugonjwa wa Mwakyembe.
Kwa miezi sita sasa, Dk Mwakyembe amekumbwa na ugonjwa wa mnyauko unaopukutisha ngozi yake hadi kufanya sura yake ya awali ipotee.
Mvurugano kuhusiana na ugonjwa wa mbunge wa Kyela ulikuzwa na taarifa ya polisi wiki iliyopita, iliyokanusha kauli za baadhi ya viongozi serikalini kwamba kinachomsibu Mwakyembe kinatokana na kulishwa sumu.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es salaam wiki iliyopita kwamba polisi ina uhakika kuwa ugonjwa wa Mwakyembe hautokani na kulishwa sumu.
Kauli ya Manumba ililenga moja kwa moja kukanusha madai ya Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta kwamba ugonjwa wa Mwakyembe unatokana na kulishwa sumu; madai ambayo ameshikia bango kwa miezi mitatu sasa.
Mtoa taarifa kutoka ndani ya serikali ambaye hakutaka jina lake kuwekwa hadharani, ameliambia MwanaHALISI kwamba ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe iko mikononi mwa serikali na kwamba wao wameipata kutoka wizara ya afya, ambayo waziri wake anakana kuiona.
Mbunge Mwakyembe tayari amerejea India kuendelea na matibabu. Wakati anaondoka Dar es Salaam Mwakyembe alikandia polisi kwa alichoita kuingilia matibabu yake, huku ikiwa bado kuthibitishwa ni kitu gani kinamsibu.
Hivi karibuni Mwakyembe alisema tatizo lake liko katika mchuzi wa mfupa na bado halijathibitishwa kiini chake. Hivyo kuingilia kwa polisi na kudai sio sumu ni upotoshaji wa kiwango cha juu.
Mtoa taarifa amesema, “Ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe ipo. Serikali inayo. Wizara ya afya wanayo. Jeshi la polisi wanayo. Hilo halina ubishi.”
Amesema, “Nakuhakikishia ripoti ipo na nakwambia imewahi kufikishwa hadi kwenye kikao kimoja cha baraza la mawaziri. Katika kikao kile, Rais Kikwete alisoma ripoti yote na alifafanua kwa mapana kinachomsibu waziri wake.”
Hata hivyo, haijafahamika iwapo taarifa iliyoko mikononi mwa serikali inataja waziwazi kwamba Mwakyembe alipewa, alilishwa au alishikishwa sumu.
Kumekuwa na madai kwamba chanzo cha ugonjwa wa mbunge wa Kyela ni maji aliyonawa ofisini kwake na baadaye kujipanguza kwenye kitambaa kilichokuwa maliwatoni.
Haijafahamika pia, iwapo taarifa ambayo serikali inadai kuwa nayo imetokana na juhudi zake za kuulizia moja kwa moja kutoka kwa uongozi wa Hospitali ya Apollo, iliyopo Hyderabad nchini India ambako anatibiwa.
Wachunguzi wa mambo wanasema pamoja na kwamba hospitali hutoa taarifa kwa serikali, juu ya watumishi wake (serikali) waliokwenda kutibiwa nje, sio rahisi kuweka waziwazi chanzo cha ugonjwa wa mhusika.
“Nina wasiwasi. Kama serikali itasema kwamba imepewa taarifa na watalaam wa hospitali juu ya siri ya mgonjwa wao, ili linaweza kuharibu hadhi ya hospitali ndani ya nchi husika na kimataifa,” ameeleza mchunguzi mmoja.
Amesema uchunguzi unaoweza kuthibitisha chanzo cha ugonjwa wa aina hiyo, ni ama ule wa uandishi wa uchunguzi au ulioamriwa moja kwa moja na chombo cha haki kama mahakama, hasa baada ya kutokea utata ambao chombo hicho kinaona utahatarisha maslahi ya taifa.
Mvurugano huu umefikia hatua hii mwaka mmoja tangu Mwakyembe amwandikie barua ya kurasa saba, Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, Said Mwema kulalamikia tishio la kuondoa maisha yake.
Katika barua hiyo, Mwakyembe alisema tukio analolalamikia ni sehemu ya mlolongo wa matukio ambayo alikwishayalalamikia kwa jeshi hilo.
Aliwataja walengwa wa tishio lama lake kuwa ni pamoja na kiongozi mkuu wa upinzani nchini, Dk. Willibrod Slaa, Mfanyabiashara Reginald Mengi, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kabla ya kuondoka kwenda India wiki iliyopita, Mwakyembe alimshtumu Manumba kwa alichoita kupotosha ripoti ya ugonjwa wake.
Alisema, “Napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yangu au walisoma taarifa nyingine…kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au walisomewa.”
Alisema, “Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa waandishi wa habari, hakifanani kabisa na picha iliyoko kwenye taarifa halisi ya Hospitali ya Apollo, inayotamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaika kukijua, kukidhibiti au kukiondoa...”
Akijadili uwezekano wa sumu, Mwakyembe alisema, “siyo lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu.”
Mwishoni mwa mwezi uliyopita, Mwakyembe alinukuliwa akisema kuwa waliomsababishia hali aliyomo, “Wameshindwa. Watashindwa na watalegea kwa jina la bwana – Amin.”
Alikuwa kwenye mahubili katika Kanisa la Ufufuo na Uzima la Kawe jiji Dar es Salaam.
Mahubili hayo yalikuwa maalum kwa ajili ya kumuombea Dk. Mwakyembe kupitia kile kilichoitwa, “Neno la Hekima kutoka kwa kiongozi.”
MwanaHALISI lilipomuuliza Sitta juu ya uthibitisho wa madai yake kwamba Dk. Mwakyembe alisema, “Ushahidi nilionao ni wa kimazingira. Ripoti yenyewe aulizwe Waziri wa Afya na Dk Mwakyembe mwenyewe.”
 
Back
Top Bottom