Mwakyembe aitwa na NaCoNGO kueleza kwa kina madai aliyoibua kuhusu baadhi ya ngo kuhusika kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Mwanasiasa aliyewai kuwa Waziri kwenye Wizara tofauti, ikiwemo Wizara ya Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe ameitwa na Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) kueleza kwa kina kile alichoeleza mbele ya Umma kuhusu madai ya baadhi ya mashirika (NGOs) kuhusika kueneza mapenzi ya jinsia moja nchini, ambapo ametumia masaa zaidi ya matatu kujieleza.

Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 2, 2023, Mwenyekiti wa NaCoNGO, Dr. Lilian Badi, amesema Kamati Tendaji kwa kushirikiana na Kamati Ndogo ya Maadili ya Baraza hilo, imeanza kumuhoji Dr mwakyembe na kuzihoji NGO's hizo zinazotuhumiwa ili kubaini uhalisia.

"Tupo hapa Leo Kamati Tendaji ya NaCoNGO tukishirikiana na kamati ndogo ya maadili kujadili tuhuma za uwepo wa NGO's zinazoendesha masuala ya ushoga kama ilivyoelezwa na Dk. Mwakyembe. Dk. Mwakyembe atatueleza alifanyaje tafiti, amegundua nini, kwa nini aliamha kutoa taarifa. Hivyo anatoa maelezo yake yakikamilika NaCoNGO itatoa taarifa kwa umma kinaga ubaga," amesema Dk. Badi.

Aidha Dr. Lilian Badi amesema baada ya kamati hizo kumaliza kuwahoji wahusika, ikiwemo mashirika yanayotuhumiwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mashirika yatakayobainika kuhusika na vitendo hivyo, lakini pia ameweka wazi kuwa jitihada zimefanyika kuyaita mshairika yaliyotajwa kuleta taarifa ya shughuli wanazofanaya.

"Kumefanyika mawasiliano na mashirika yote yaliyoorodheshwa kwenye taarifa ya Dk. Mwakyembe, tumeomba watuletee taarifa ya shughuli wanazofanya miaka mitano iliyopita. Tumewaita kuwasikiliza na kuanza kuwahoji na kuanza uchunguzi"-M/Kiti NACoNGO, Dk. Lilian Badi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa NaCoNGO, ameitaka sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali kuwa watulivu katika kipindi ambacho Baraza hilo linafanyia kazi tuhuma zinazoibuliwa na Mwakyembe, ambapo amesisitiza kuwa NaCoNGO itaendelea kuzingatia taratibu ambazo hazikiuki sheria za Nchi sambamba na maadili.

"Kama NaCoNGO tunataka kuilinda jamii yetu na kubaki salama katika suala hili lililokinyumr na maadili. Ni vyema kuungana kuwa pamoja kuliko kunyoosheana vidole," amesema Dk. Badi.

Ikumbukwe Dk. Mwakyembe hivi karibuni mbele ya Umma alinukuliwa akitaja baadhi ya NGOs (29) akidai kuwa zihusika kueneza ushoga nchini, ambapo alidai kuwa anayo orodha na majina ya waratibu wa masuala hayo, kufuatia kauli hiyo iliibua mjadala mseto huku baadhi ya wadau wakionekana kumuunga mkono na wengine kupingana nae.

IMG_20230402_182946_383.jpg
 
Mwenyekiti wa baraza la NGO's Tanzania, Lilian Badi amesema wameyaita mashirika yote yaliyotuhumiwa na Dk Harrison Mwakyembe kwamba yapo hapa kwa ajili ya kueneza ushoga nchini.

Mwenyekiti huyo ameyataka mashirika hayo kuja na taarifa ya miaka 5 iliyopita wakielezea shughuli walizokuwa wakifanya hapa nchi ikiwemo hela wanafadhiliwa na nani.
 
Kukaa kimya ndiyo kutatua tatizo?
Hata akiongea akiwaita.. hana la kuwafanya... labda for the sake of public moody... bora aache wasijetibua kila kitu, wanufaika ni wengi kama mchanga wa bahari... she will lose every single time.
 
Hata akiongea akiwaita.. hana la kuwafanya... labda for the sake of public moody... bora aache wasijetibua kila kitu, wanufaika ni wengi kama mchanga wa bahari... she will lose every single time.
Are you threatening her?
 
Mwenyekiti wa baraza la NGO's Tanzania, Lilian Badi amesema wameyaita mashirika yote yaliyotuhumiwa na Dk Harrison Mwakyembe kwamba yapo hapa kwa ajili ya kueneza ushoga nchini.
Mwenyekiti huyo ameyataka mashirika hayo kuja na taarifa ya miaka 5 iliyopita wakielezea shughuli walizokuwa wakifanya hapa nchi ikiwemo hela wanafadhiliwa na nani.


Viva Mwakyembe, sasa serikali imeamka usingizi wa pono.
 
Tanzania bila ushoga inawezekana.... serikali ifanye mahamuzi magumu
20230320_210438.jpg
 
Back
Top Bottom