Picha: Mpenzi mwingine wa lulu Michael anaswa na "UNGA" Nigeria

warumi

R I P
May 6, 2013
16,273
18,382
Jamaa ambaye inasemekana ni rafiki wa karibu wa staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu' aitwaye Morris Sekwao ‘Junior' inadaiwa amepata msala ‘hevi' baada ya kutiwa mbaroni nchini Nigeria akituhumiwa kunaswa na madawa ya kulevya ‘unga'.Habari kutoka kwa mtu wa karibu wa familia ya Junior zilidai kuwa, jamaa huyo alipatwa na mkasa huo hivi karibuni nchini humo ambapo alikuwa akitokea Bongo na mzigo huo.

AKAMATWA UWANJA WA NDEGE NA KILO 25
Chanzo hicho kilidai kwamba Junior alikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Murtala Muhammed (MMIA) uliopo Ikeja, Lagos nchini Nigeria, akiwa na madawa hayo aina ya Ephedrine yenye uzito wa kilo 25.Ilidaiwa kwamba Junior ambaye ni rafiki wa mastaa mbalimbali Bongo, alidakwa na polisi wa uhamiaji uwanjani hapo baada ya kutilia shaka begi kubwa alilokuwa amelibeba.

NI BEGI ZIMA
Ilidaiwa kwamba, baada ya ukaguzi alikutwa na begi zima la unga wenye ujazo huo wa kilo 25 ambao thamani yake haikuwekwa wazi mara moja.

KAMA MASOGANGE

Chanzo hicho kilizidi kumwaga ‘ubuyu' kwamba aina ya madawa aliyokamatwa nayo ni kama yale aliyokamatwa nayo video queen wa Bongo, Agness Gerald ‘Masogange' nchini Afrika Kusini ‘Sauzi' mwaka 2013.

BOSI YULEYULE
Madai mazito yalishushwa kwamba ‘doni' aliyembebesha mzigo (aliyemfanya punda) Junior ndiye yuleyule aliyedaiwa kumbebesha Masogange.Ilisemekana kuwa baada ya kukamatwa, uchunguzi wa kipolisi unaendelea nchini humo ambapo kwa sheria za Nigeria, jamaa huyo akikutwa na hatia anaweza kwenda jela miaka kadhaa.

NDUGU WAHAHA
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba kukamatwa kwa Junior kumewashtua baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki zake kwa kuwa hawakuwa wanajua kama ndugu yao huyo anafanya kazi hiyo.

KUHUSU JUNIOR
Habari zilizo kwenye makabrasha ya gazeti hili zinaeleza kuwa Junior ni mtoto wa mjini ambaye mara nyingi hupenda kuambatana na wasanii mbalimbali Bongo ambapo mara nyingine husafiri nao nje ya nchi bila kujulikana anapiga dili gani.

NDIYE ALIYEMKIMBIZA LULU USIKU WA KIFO CHA KANUMBA?
Ilidaiwa kwamba usiku wa kuamkia Aprili 7, 2012 ambapo ndiyo siku kilitokea kifo cha aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Steven Kanumba, Junior ndiye aliyedaiwa kumkimbiza Lulu kutoka nyumbani kwa Kanumba na kwenda naye kwenye Ufukwe wa Coco kabla ya kukamatwa alfajiri yake maeneo ya Bamaga-Mwenge jijini Dar.

attachment.php


Chanzo: GPL
 

Attachments

  • 1429859093901.jpg
    1429859093901.jpg
    38.3 KB · Views: 2,956
  • Screenshot from 2015-04-24 13:41:15.png
    Screenshot from 2015-04-24 13:41:15.png
    84.2 KB · Views: 2,174
Duuh!.Sembe Imekua Habari Ya Mujini Kwa Vijana Wanaotamani Kuishi GudLife.Ila Wengi Wao Wataozea Jela.
 
Husingeongeza Na Uzushi Thread Yako Ingekua Na Maana Sana.

Lakini Umeipunguzia Credibility Thread Yako Katika Heading Yako Kumuhusisha Moja Kwa Moja Huyu Bwana Kama Mpenzi Wa Lulu Without Any Vivid Proof.Wakati Content Ya Thread Inaonesha Alikua Ni Rafiki Tu Wa Karibu.

JF Kuna Watu Makini Ambao Wanauwezo Mkubwa Wa Kufanya Reasoning.Na Wanapenda Kudeal Na Realfacts Badala Ya PersonalUzushi.Kwahiyo Hakuna Haja Ya Kuongeza Chumvi Kama Haina Mashiko Au Ushahidi Wowote.

Mpenzi Ni Mpenzi Na Rafiki Ni Rafiki.Kupiga Picha Pamoja Wanakunywa Au Wanacheka Sio Sababu Inayojitosheleza Ya Kuhalalisha Mahusiano Yao.

Kwahiyo Tuwe Makini Katika Kustick Kwenye Facts.This Is A Home Of Great Thinkers!
 
Huyu jamaa hata asingekamatwa na Unga maisha yake hapa duniani ni mafupi sana, hana muda mrefu wa kuishi.

RIP Kanumba, Capt. Komba na Secky wa Mirerani!
 

Attachments

  • 1429867065224.jpg
    1429867065224.jpg
    172.3 KB · Views: 932
Last edited by a moderator:
Hii sasa sio fair kumuhusisha Lulu kwa matukio mabaya hata asiyohusika ili kuuza habari, heading ni tofauti na content
 
Huyu jamaa hata asingekamatwa na Unga maisha yake hapa duniani ni mafupi sana, hana muda mrefu wa kuishi.

Asingekamatwa angepata kama Milioni 60 hivi Tsh za hizo ephedrine. 6,000,000/=

Lakini kama zingekua ni cocaine angepata kama bilioni moja na milioni 165 hivi kama angeuzia mitaa ya marekani. 1165,000,000/=

Angeishi kwa starehe tu.
 
snipa sasa yeye ni punda tu angepewa kdg kisha akakutana na lulu then ikifika between February na April the next year angedondoka na kufa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom