Nigeria: Gavana wa Jimbo la Borno Amewataka Raia Wake Waanze Mfungo wa Kumuomba Mungu Awatatulie Shida za Gharama Kubwa za Chakula na Usalama Mdogo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,785
Gavana wa Jimbo la Borno Nchini Nigeria amewataka Raia Wake kuingia kwenye Mfungo Kwa kile ameita Kumuomba Mungu Ili Awatatulie Shida ya bei kubwa ya chakula na usalama mdogo ambapo karibia Kila siku mabomi hulipuka kwenye Barabara za Jimbo Hilo.

Rais wa Nigeria ameitisha Mkutano wa magavana Ili kutafuta suluhu ya kupanda Kwa gharama kubwa za maisha na Hali mbaya ya Uchumi kwenye Taifa Hilo kubwa la Afrika.
---

Rai Yangu Kwa Chadema.

Chadema acheni mzaha wa kuandamana eti Tanzania Kuna maisha magumu wakati wali maharage ni buku jero.

Ni vyema mkatunia mda huo kuhamasisha watu wazalishe zaidi na kuwauzia Nigeria na Ethiopia ambao Wana Hali mbaya za kiuchumi kuliko kutatiza shughuli za wananchi Kwa maigizo ya kijinga.
---

Raia kadhaa wa Nigeria katika jimbo la kaskazini mashariki la Borno wanajinyima chakula baada ya gavana wao kutoa wito wa "kuingilia kati kwa Mungu" juu ya hali mbaya ya kiuchumi na usalama ya nchi.

Siku ya Ijumaa, Gavana Babagana Zulum aliwataka wakaazi kushiriki mfungo wa siku moja katika jimbo lote siku ya Jumatatu ili kukabiliana na kupanda kwa gharama ya chakula na misururu ya milipuko ya mabomu ya ardhini katika barabara zake kuu.

Bello Zabarmari, mkazi wa jimbo la Borno, aliambia BBC kwamba yeye na wengine wengi wanafunga na kumwomba Mungu kutatua matatizo yao.

"Tumeamka na mfungo leo na tunatumai maombi yetu yote yatajibiwa hivi karibuni, mkuu wa jimbo alifanya jambo sahihi kwa kuwaita watu kufunga," alisema.

Umar Shehu, mkazi anayefanya kazi na idara ya zima moto serikalini, alisema yeye na wenzake pia wanafunga kama alivyoagizwa na mkuu wa Jimbo.

Raia wa Nigeria wanapitia moja ya kipindi kigumu zaidi cha uchumi katika historia - bei ya vyakula na bidhaa muhimu imepanda katika miezi ya hivi karibuni.

BBC SWAHILI

My Take
Aliyewaroga Waafrika alifaulu.Kwamba badala muende shambani kulima eti mnafunga ndio itakimbiza njaa? 😁😁😁😁
 
Jimbo la borno ni moja ya majimbo yanayoandamwa na waislamu wenye msimamo mkali ambao wameharibu amani kabisa kwa kufanya mauaji na utekaji wa mara kwa mara,kubali kata najua wewe ni muislamu ila nikuambie dini yenu imefanya dunia kuwa sio sehemu salama ya kuishi.
Maisha ni hovyo Nigeria nzima sio Borno tuu.

Harafu inakuaje Nchi ishindwe kufanya oparesheni ya kuwasaka hao watu?
 
Maisha ni hovyo Nigeria nzima sio Borno tuu.

Harafu inakuaje Nchi ishindwe kufanya oparesheni ya kuwasaka hao watu?
Hakuna kazi ngumu kama kuondoa magaidi yanayofichiwa siri na wenyeji,maana yake wakiwa hawana mask ni watu poa lakini wakivaa tu mask ni wanyama na ndio maana serikali ya somalia inahangaika kuwasafisha Al shabab mpaka kesho bila mafanikio,wamepiga marufuku niqab lakini wapi,haya sasa hata barakoa zimepigwa marufuku lakini hakuna matokeo watapata.
 
Back
Top Bottom