Kitu kimoja Angola maisha yako juu sana,hata Tokyo ni nafuu chakula cha hovyo tu Usd 50 na kuendelea,umasikini pia ni mkubwa hadi unatisha,ukitoka nje kidogo tu ya jiji la Luanda utashangaa kuona hali ya maisha ilivyo duni,utajiri wa mafuta umewatajirisha ruling elite &Co.
Nilichokipenda ni kuwa majengo mengi utakuta ofisi zipo chini juu utakuta makazi,yale mambo ya kutoka Kibaha kwenda kufanya kazi Temeke na kuongeza misururu ya magari barabarani ni kama haipo.
Mwisho kupata visa ya Angola ni kama unaenda kuomba visa ya Marekani au Uingereza ,hata Marekani na Uingereza uwezekano wa kupata viza zao ni mkubwa kuliko wa Angola,na bahati mbaya sana ukiwa na haya majina ya akina Omar,Hassan ,Abdulah ndio balaa.Ila Wareno walijenga bana haya majiji ya Luanda na Lorenco Maquis.