bado hawajatambua kuwa Luanda inamilikiwa na wafanyabiashara kutoka portugal na spain wakishilikiana na rais wa nchi hiyo, wananchi wa kawaida hawanufaika na chochote japokuwa ni nchi ya madini, gesi na mafuta..
Exactly mkuu. Ni kikundi tu cha watu kinaendeleza Luanda kwa maslahi ya wachache. Ndo maana kote wanakoonyesha huoni watu hata kwenye makazi. Na wachache walioonekana sio 'watamu'.
Dar, japo haivutii kama huko Luanda, picha chache tu zilizowekwa unaona mishemishe kibao.
Ni bahati mbaya waTz wengi wanashobokea nje bila kujua wao hasa wanataka nini. Hivi Dar leo hii ikijaa mabarabara na maghorofa makubwa, wangapi kati yetu watayatumia?
Kuliko kufocus kwenye majumba na barabara za Dar pekee, kuna ya msingi kama vile ubora wa elimu, tija kwenye utumishi wa umma, madaraja mengi zaidi kuvusha mazao, tiba bora hospitali za umma, etc.
WaTz tuchukue fursa kwenye uchumi na rasilimali zetu. Sawa ccmscrow wanabana, basi na tuwatoe. Binafsi nawatoa Oktoba. Na nilianza tangu serikali za mitaa.
Tunavyozidi kukamata fursa na kuzitumia, hayo maghorofa na mabarabara ni derived demand.
Sasa hivi hapo Dar, wamatumbi wamekimbilia segerea, mabwepande, mbezi, yombo, mbagala mwisho, n.k. then haohao wanasifia maghorofa kwa wengine. Dar ya nini wakati watu hawayawezi?
Tung'ang'anie vipaumbele sahihi. Sio kila king'aacho dhahabu, na sio kila kizuri tunakihitaji sasa.
Btw, kimfaacho mtu chake.