PICHA: Mererani mwanajeshi ajitoa mhanga

Msimshabikie mwenzenu akifanyiwa court martial na kuondolewa jeshini muwe tayari kumpa ajira! Wanajeshi wakitaka siasa watoke jeshini kwanza ndio kanuni ilivyo.
 
vp kuwaita wakurugenzi wa tanesco na tanroad kunadi sera za ccm ni dunia gani inaruhusu ichi kitu,
 

What if Angepiga picha na Nepi, Chichidodo, Jangili, Nyoka wa Mdimu, Vijicent, Prince...wangemtimua?
 
Siyo siasa sema upinzani!

Jiulize ilikuwaje jenerali Mboma aligombea ubunge kwa ticketi ya CCM soon baada ya kustaafu.
Tena akijifia kuwa ni kada wa CCM wa siku nyingi toka enzi za TANU.
 
Ukada wako sisi hatuhusu,mbona mnatumia viongozi na watumishi wengi tu wasiostahili,Tuambie akina Tibaigana wakati wanagombea ubunge huko Muleba baada ya kustafu Polisi lini alikuwa mwana CCM,Je na James Kombe kamanda wa Polisi huyu kila cheo cha ccm anakitaka japo wanaflush,Je na huyu Jenerali Mboma?,na MADC,MARC ?.kafie mbali
 
Siku njema huoneka asubuhi! na mwenye macho huwa haambiwi tazama! Ushauri wangu Hebu Chama kisome alama za nyakati ugumu wa maisha sio tuu kwa raia hata Wanajeshi wanalalamika sana! huyo ni mmoja tuu wapo wengine wengi tuu ambao bado hawajalipuka sipati picha siku wakilipuka sijui mtawaeleza nini zangu mnao wadanganya wananchi kwa kuleta hoja uchwara za kadi ya Dr kuwa ziwe za kitaifa. Safi sana kamanda kwa kuwa muwazi na kueleza hisia zako kwa taifa Hiyo ndio M4C LAZIMA KIELEWEKE...........
 
Mkuu Moshe Dayan

Kama jeshi letu linaamini na kusimamia hili, akina Shimbo wasingekuja na matamko kama yale mwaka 2010. That was too bad. Tamko lile, lilimpotezea credibility sana na , no woder, mkuu wake Mwamunyange kwa nafasi yake kama CDF hakutoka hadharani na kuyaongea yale.

Tusubiri; Tuone. Kuna mengi yatasemwa juu ya askari huyu:

1. Anatoka Kambi/Kikosi gani pale Monduli? SOFA, Mbuni au TMA?
2. Ilikuwaje akatoka kituo chake cha kazi, hadi kwenda Simanjiro? Mkoa (Arusha) na mkoa mwingine(Manyara)
3. Si mzoefu na mambo ya majeshi, sare za rangi zile tunazo au ni zile zenye kijani hivi? Au ni rangi ya tu ya kamera?
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwa maisha haya ukilipwa 300,000 utajiita unamaisha mazuri...
Sio kweli wanajeshi wana maisha mazuri sana kulinganisha na kada nyingine,, mikopo ,,mshahara,, hela ya chakula ,, wanaoishi nje ya kambi umeme maji bure,,achani unazi huyu. Kanyea debe tayari
 
Mwanachama wa CDM kavalishwa gwanda. Kwenye mitumba utapata kila kitu
 
Msimshabikie mwenzenu akifanyiwa court martial na kuondolewa jeshini muwe tayari kumpa ajira! Wanajeshi wakitaka siasa watoke jeshini kwanza ndio kanuni ilivyo.

Mbona Shimbo hakutoka? Mbona Kamuhanda hajatoka? Andengenya? Jack Zoka? Mahita?...Hizo sheria taratibu plus kanuni haziwahusu Viongozi?Wakufunzi wa Siasa Jeshini JK akiwa mmoja wao mbona hawakutimuliwa? Marekebisho ya kanuni taratibu na sheria yalifanyika lini jeshini?...
 
jibu swali...kosa lake litakuwa ni lipi?

kwanza nasikitika kwa tukio hili, mimi nilikuwa kwenye huu mkutano jana huyu mwanajeshi huwa anafundisha mgambo mjini mererani, jana wakati chadema wakifanya mkutano wa hadhara mwanajeshi huyo aliwaamuru mgambo wote waende kwenye mkutano kuwasikiliza wabunge wa chadema, kabla mwanajeshi huyu haja fikia uwamuzi huo, kuna haice moja ilikuja na makamanda kadhaa wa Chadema, akiwepo mpambe mmoja wa Millya, Oleleshwa alikwenda kuongea na huyu mwanajeshi huyo na ndo migambo wakapewa amri ya kwenda kwenye mkutano, bado niko hapa Mererani nafanya uchunguzi wa kina na nimesha gundua kuwa, Lema, Nassari, Heche wakishirikiana na Millya wanatengeneza Jeshi na watatumia msitu wa Komolo wilayani simanjiro, mtu anayeratibu mafunzo ya wa wanajeshi hao wanafundishwa kwa mwamvuli wa mgambo ni mzee mmoja anaitwa Peter Peshut akishirikiana na Oleleshwa, kwa ufadhili wa kamanda Ndesamburo na Mbowe, naendelea na ufafiti na kuna taarifa kuwa gideon Sanago naye yuko hapa Mererani akiendelea kuwashawishi Apolo wajiunge na jeshi la kina Lema.
 
ukweli gani unataka ni mwanajeshi kutoka monduli sasa unataka nini tena kutoka jwtz mbona yule polisi alietaka kugombea unec magamba hamkufatilia details zake kwa IGP MWEMA mwacheni yeye na maisha yake na huu ni mfano tu kwanza unatakiwa kujua kua maaskari wengi hasa jwtz na polisi wanatoka ktk mikoa ambayo ccm mara nyingi haifui dafu mf MBEYA, MARA, ARUSHA, KILIMANJARO, MANYARA n.k fanya utafiti na utakubaliana mimi kwaio sishangai ,pia jiulize kwann afanye hivo ktk kipindi hiki cha awamu ya nne FREEDOM IS COMING IN BONGO LAND AND LET IT RINGS IN EVERY WHERE.
 

sijui unazijua vizuri sale za jwtz au unaongea tu...kwa cc tunaojua hiyo sio sale ya jwtz.... Na siasa na ukombozi wa kweli hauji hivyo kwa kutafuta watu kuwavalisha kombati kutimiza maelngo ya kiasiasa ,....ukombozi w akweli uko moyoni na mapenzi na chama yako moyoni....
 
Ndugu si kweli kabisa unachokisema, kwa mfano
1/Kuna nchi nyingi sana wanasiasa karibu wote ni wanajeshi(eg.Iraq, Afghanstan, Syria, DRC, Somalia, Sudan, Cuba, Iran, Rwanda nk)

2/Sheria za Tanzania haziruhusu kuvaa mavazi ya jeshi la Tanzania tu kwa raia na wala sio za majeshi ya nchi zingine.

3/Kama askari wetu wa JWTZ wanajitokeza na sare za jeshi kwenye vilabu vya gongo, mitaani kupiga raia, Bar wakilewa na kuchukua malaya kwa nguvu, madangulo kufanya ngono, sembuse kupiga picha na wabunge wa Tanzania.

Try to think big!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…