Namuunga mkono BEN SAANANE AWE MBUNGE WE2 WA ROMBO KWA NGUVU ZOTE
Magesi,
-Mkuu usitake kuua watu presha
Pia kuna mtu anadai hapo juu kwamba anajua nina nia ya kugombea ubunge Rombo.Hii ni ramli kwani siku zote naamini katika taasisi.Nimekua nikisizitiza umuhimu wa kukijenga chama badala ya kujijenga.Hatuhitaji watu imara bali taasisi imara zenye uhakika wa kutoa watu imara siku zote
Sioni mantiki ya kujijenga kwa ajili ya kukimbilia bungeni kudai nyongeza ya posho badala ya kushiriki katika harakati nchini katika ujenzi wa Chadema imara kitakachoshinikiza mabadiliko ya kisheria na kisera ili kuleta maendeleo kwa watu wote na kwa mfumo halali bila kulazimika ku-accomodate hoja za ovyo za watu kudai nyongeza ya posho ili wawagawie wananchi.
-Pia ni kweli sikubaliani na kitendo cha kutamani kuibatiza Barabara kwa jina la Rais 'Jakaya Kikwete Road'.Fikra za aina hii ndizo zinazorudisha harakati za mabadiliko ya fikra nyuma kwa kuwa wananchi wanawexa kudhani ni hisani na sii huduma ya msingi na si wajibu wa serikali kufanya hivyo.Dhana ya kumpongeza ni motisha lakini tusifikie hatua tukawa tunafanya mambo ya ajabu
Barabara ni vipaumbele na ni utekelezaji wa mkakati wa kisera kuliko haiba ya kujitukuza kama wafanyavyo madikteta wengi wa Afrika kwa kujijengea minara na kujibatiza majina katika viunga.Rais kufungua au kutenga bajeti kwa ajili ya kujitukuza na kukosa umakini
Nasizitiza kwamba barabara ya Rombo ni haki yao na si hisani.Ni barabara ya kimkati na CCM na serikali yake walikosea vipaumbele kwani ni strategic road.Kama waliweza kukwapua bilioni 152 za EPA ni kwa nini wakose fedha za kujenga ile barabara?
Pia huyo anayeuliza nimefabya nini Rombo,jibu analo.Anajua mchango wangu wangu katika kuhakikisha Chadema inashinda Ubunge Rombo,Ubungo,Kawe na Kilombero katika uchaguzi mkuu uliopita.Naendelea kutoa mchango wangu kwa chama bila hofu.
Sitaki kuwa opportunist kama wale wanaojiunga na harakati dakika za mwisho na wengine wakitokea vyama vingine kwa ajili ya kuwaza ubunge tu.Sitaki kuwa mtu wa kufuata upepo wa kisiasa tu.Watu wa aina hii mara nyingi wana matatizo
Siasa za propaganda bila mikakati hazitatusaidia.Matokeo yake tutafikiria kusolve matatizo kwa falsafa ya dharura kwa njia ya kufikiria kuwagawia fedha.Wananchi wanahitaji migomba,vijana wanahitaji migomba na sio ndizi
Nasizitiza kua tuendelee kuijenga CHADEMA ili tusukume harakati hizi bila kufikiria POSHO.Mbunge sio father xmass.Ni wajibu wa serikali kutoa huduma muhimu na si wabunge kuwagawia fedha,ni wajibu wa serikali kujenga barabara kwa kuzingatia vipaumbele vya kisera kama public expenditure according to national priorities other than self glorification under unguided principles!