PICHA: Mbowe ampongeza rais Kikwete...

PICHA: Mbowe ampongeza rais Kikwete...

nimeipenda hiii..umoja kwenye mambo kimaendeleo kwenye ya kijinga tunapingana...
 
Huyo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kuna siku ataumeza huo mkoa. Anajilia tu hata hafanyi mazoezi. Naona ndoa ya Selasini na Kikwete kama inanukia. Yangu macho na masikio baba yenu.
 
Kwenye kufungua barabara wa kwanza, leo hii kuna hospitali hazina hata gloves achilia mbali asprin. Akisikia watu wanagoma kuhusu ubovu wa administration yake huyooo anapanda ndege.
Ebu jiulize bila miundombinu bora ya barabara utaweza kufika hospitali kirahisi? usambazwaji wa dawa na vifaa utafika vipi kwenye zahanati,vituo vya afya na hospitali? Je madaktari na wauguzi wanapenda kukaa sehemu ambazo hazifikiki kwa barabara? kama mpaka hapo haujautambua umuhimu wa barabara kiuchumi na kijamii ni maombi pekee yatakayokusaidia.
 
Huyo mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama kuna siku ataumeza huo mkoa. Anajilia tu hata hafanyi mazoezi. Naona ndoa ya Selasini na Kikwete kama inanukia. Yangu macho na masikio baba yenu.

Hata mkuu wa wilaya ya Hai anatakiwa ashtuke mapema. Naona anaelekea hukohuko kwa mkuu wa mkoa. Shavu linaanza kung'aa! Mchemsho mtamu jamani. Fanyeni mazoezi wakuu!
 
Kwenye picha ya kwanza, inaonekana 'kwa tafsiri yangu' kuna infiriority complex kwa mmoja.
 
Watanzani ni unbearable, angekuwa mh.mrema au mbatia au zitto mngesema ni vibaraka. Kwan mbowe ni nani?
 
Watanzania ni unbearable, angekuwa mh.mrema au mbatia au zitto mngesema ni vibaraka. Kwan mbowe ni nani?
 
Ukweli husemwa:

Hotuba ya hivi majuzi aliyoitoa Mh Freeman Mbowe Mbele ya Rais Jakaya Kikwete katika ufunguzi wa Barabara ya Sadala - Masama, Wilayani Hai pamoja na kuwa ilikuwa ni hotuba fupi, lakini imetoa ujumbe mzito kwa jamii ya Kitanzania ambayo bado imegubikwa na wingu la chuki za kisiasa zinazochagizwa na tofauti za kiitikadi. katika lugha nyingine, Mh Freeman Mbowe anaiasa jamii ifunguke na itambue kuwa;
1) Taifa linajengwa na wenye moyo wa uzalendo
2) Tofauti za Kiitikadi siyo msingi wa chuki katika jamii kama wanasiasa uchwara (fake) wanavyotaka kuiaminisha jamii, bali ni catalyst katika maendeleo.
3) Kukomaa katika siasa ni pale pia unapotambua na kupongeza mchango chanya wa serikali au mpinzani wako kisiasa.
4) Serikali ya awamu ya nne inaendelea kutimiza ahadi zake za uchaguzi.
5) Serikali haina ajenda ya 'ideological discrimination' among region.
6) Rais Jakaya Kikwete ni msikivu pamoja na 'udhaifu' wake katika utendaji ndani ya serikali.

Mh Freeman Mbowe, Umeonyesha ukomavu wa kisiasa nchini. Pongezi kwa hilo.

[video=youtube_share;vlH-YG_Kmnw]http://youtu.be/vlH-YG_Kmnw[/video]

video kwa hisani ya michuziblog
 
Mbowe ni mwanasiasa aliekomaa bt angekua yule mdini silaaa duh angeponda tuu 2005 nilimwambia james mbowe wakati tulipokua chuo nilimwambia baba yako he's fit as tanzania presdnt eventhough mm ni ccm bt mbowe namkubali tena sanaaaaa ww ndie kamanda na jemedari kuliko huyo mdini slaa
 
Hapa hutawaona hata kwa fimbo kwa ushahidi huo aaaaaaaaaaaah....
 
nawagoja magamba watoe comment zao nitarudi......
 
SIERA,

..Mbowe alikuwa na ombi lake la kuongezewa km 3 ktk mradi wa barabara.

..kwa msingi huo ilikuwa ni lazima amsifie JK na Magufuli. It worked, manaake Magufuli alikuwa anakenua kama hana akili nzuri.

..hapo Mbowe alikuwa ni sawa na wale wazee wa Kichaga ambao wakiwa na shida zao huwaamkia hata vijana wadogo, "Shikamoo mwanangu."
 
Last edited by a moderator:
wamewaulisha bure vijana wa watu pale arusha eti ukombozi? mchagga mpe biashara hiyo ndio sehemu yake, ndio maana mimi huwa siungi mkono chama chochote kinachoongozwa na mchagga.
 
Naona safari ya mbowe inaelekea , kama alivyosema yupo tayari kuondoka CHADEMA
 
Siku za karibuni tumeshuhudia pongezi zikimwagwa na viongozi wa Chadema kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete kutokana na uongozi wake uliotukuta katika kutekeleza ahadi kwa wananchi pasipo kujali itikadi za kisiasa.
Mheshimiwa Freeman Mbowe, Mheshimiwa Joseph Selasini na Mheshimiwa Rose Kamili kwa wakati na mahala tofauti wamesikika wakitoa ushuhuda wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ulioenda sambaba na utekelezaji wa ahadi zilizotolewa na Rais kipenzi cha watanzania, Dr. Jakaya Kikwete.
Tangu zimetolewa pongezi hatuzikia mwanachama yeyote wa Chadema kupinga ama kulaumu matamshi ya viongozi wao.

Lakini huku nyuma tulihushudia Mheshimiwa Zito na Shibuda wakilaumiwa kwa vitendo vyao vya kutoa pongezi kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete.

Matukio haya mawili yanatufundisha kuwa ndani ya Chadema kuna wenyewe (watokao Arusha, Kilimanjaro na Manyara) na wakuja (watokao nje ya mikoa hiyo miwili). Asanteni Chadema kwa kutudhihirishia watz kuwa ndani ya chama chenu; UKANDA unaangaliwa zaidi kabla ya kutoa kasoro kwa jambo lolote linalofanywa na viongozi na wanachama wenu.
 
Back
Top Bottom