PICHA: Mbowe ampongeza rais Kikwete...

Mbowe ni kijana wa JK humu JF Pro-Chadema povu linawatoka ovyo mwenye chama Mbowe yupo katulia kwa JK anawachora tu.
 
-Kuwa mkweli na you should quote him right

-Acha kupotosha.Maendeleo yaliyopo hayalingani na miaka 50 ya uhuru.

Sijui kwanini mtafute faraja kwa nguvu kiasi hiki
 
Congrats Mbowe, mbunge makini aliyepata kutokea ktk jimbo la hai, amepambana na JK ameridhia barabara korofi kupita zote inayotoka Kwasadala mpaka Kalali inawekwa lami, this is great!!
 
Kamanda ndani ya Kombati.

Hiyo picha angekuwa Zitto, ungesema yote lakini umemuona Mbowe umeamua kusifia Kombati, ha haa ha! JK bana anawapatia sana hawa watu.
 
Last edited by a moderator:
mikelele mengiii, wakikutana nae ovyoooooooooo

hao wote ni viongozi wa watanzania na maendeleo huja kwa kufundishana sio kupigana ndio maana kuna mawaziri vivuli sasa kama wewe ulitaka mbowe asiongee na jk unamatatizo binafsi na watu sample yako ni wakuogopwa kama fistura....
 
Hapo ni wapi mkuu? sio unatuletea picha alf hatupi maelezo yanijitosheleza sisi wengine tutajuaje walikuwa kwenye tukio gani?
KIkwete yuko ziarani katika mkoa wa Kiklimanjaro na leo alikuwa anazindua barabara katika wilaya ya Hai ambako Mbowe ni mBunge wake. ... KUna picha nyingine tena akiwa huko Rombo ambako Selasini naye alikuwepo
 
Siku zote nimekua nikisema mbowe anahekima sana ktk viongozi wote wa magwanda ngalia siku wanachangisha pesa dar lema alikurupuka kulaani makampuni ya simu baada ya kuona wanaotuma hawapati mtandao mbowe kwa hekima kubwa alijua wingi wa subscribers alisimama na kutoa ufafanuzi wakati lema alianza kutukana na kulaani ,mbowe anahekima sana kuliko hata padri
 
Katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo...Mheshimiwa mbowe amemsifu Raisi Kikwete Kwa juhudi zake za kuboresha miundo mbinu nchini.

My Take.
Siasa si uadui...Kwa hiyo hata sisi tunaweza kijadiliana hapa bila ya kukashifiana au kutukanana
Siasa si Kutukanana..
Siasa ni kuambiana Ukweli.
Siasa ni Kusema Ukweli...Kama alivyosema Mheshimiwa Mbowe leo.."Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni"View attachment 69922

View attachment 69923
View attachment 69924
View attachment 69925

PICHA ZOTE KWA HISANI YA Global Publishers
Kwa habari na picha zaidi Bonyeza
 
JK ni ''dhaifu'' lakini anawajali saana wapinzani wake kisiasa.Sisi mashabiki huku ndio utasikia ''kachomwa mshale'', ''meno yang'ooka'' ama vifo.Yote haya ni kwa sababu tu eti tunawafia wanasiasa ''Rais wetu wa Moyoni'' teeeeh...teeeh.

Mtazame Seif Sharif Hamad, watu walikufa leo anacheka na Shein, Raila na Kibaki,Mugabe na Chengelai/Cvangilai-Hii ndio siasa jamani, wafuasi tusiuane wala kuchomeana nyumba kwa sababu ya ''wanasiasa'' hawa.
 
Heko kwako ZZK, naona viongozi wenzako waCDM wameanza kuelewa falsafa zako hakika wewe ni mwalimu big up.
 
-Kuwa mkweli na you should quote him right

-Acha kupotosha.Maendeleo yaliyopo hayalingani na miaka 50 ya uhuru.

Sijui kwanini mtafute faraja kwa nguvu kiasi hiki

Ben maendeleo ya miaka 50 yanafananaje? nadhani kwa mawazo yako tungekuwa tunatengeneza ndege sasa!

Naamini wewe ni mfuasi wa Mwalimu Nyerere na hujawahi kumkosoa hata siku moja.Katika hiyo miaka 50 unayolilia, Mwalimu ametumia karibu nusu akiwa Madarakani.Swali langu ni je!Nyerere anapaswa kutupiwa lawama????
Ama tutaendelea kuishi kwa ''imagination'' through out!

Tuwe tunasoma historia vizuri kabla ya kukosoa ama kuhukumu.Unaambiwa nchi imeanza kujijenga miaka ya 80 baada ya ukombozi wa Afrika angalau kueleke tamati, mbona hili ulisemi?

Hii ni principle tu hata katika maisha kwawaida, mara nyingi maendeleo ya mtu anaesaidia ndugu zake saana huchelewa tofauti na yule mwenye mkono wa birika.
 
Leo kupitia Itv nimeona juhudi zako kwa kuwa umeweza kumleta rais Kikwete na Magufuli wakazindua barabara ya kwasadala -masama kwa kiwango cha lami na huenda ikaunganishwa tokea MASAMA,SONU,BWANI hadi KALALI.
Nimekupongeza wewe kwa kuwa niliona juhudi zako toka bunge la bajeti ulivyoifuatilia hii barabara.
Ombi langu kwako vijiji vya USWAA,SHARI,KYERI havina huduma ya mwochwari wala zahanati ya uhakika ujitahidi uwabane hao magamba watumie hizo kodi zetu watuletee hiyo huduma.
Naomba kuwasilisha
 
hivi Kamanda Mbowe hana e-mail address?
 
Waache wampongeze tu, sasa angepongezwa na nani? maana jana kule Rombo alipongezwa tena na Selasini, na hii inatokana na kuwa majimbo mengi ya uchagani ni Upinzani isipokuwa mawili tu moshi vijijni na siha. Sasa nani angempongeza ilihali barabara zimetengenezwa?
 
hivi ndio ile jk alitoa hotuba ya kejeli kwamba ninyi upinzani mnapinga kila kitu,
Poor president
 
Ben maendeleo ya miaka 50 yanafananaje? nadhani kwa mawazo yako tungekuwa tunatengeneza ndege sasa!

Naamini wewe ni mfuasi wa Mwalimu Nyerere na hujawahi kumkosoa hata siku moja.Katika hiyo miaka 50 unayolilia, Mwalimu ametumia karibu nusu akiwa Madarakani.Swali langu ni je!Nyerere anapaswa kutupiwa lawama????
Ama tutaendelea kuishi kwa ''imagination'' through out!

Tuwe tunasoma historia vizuri kabla ya kukosoa ama kuhukumu.Unaambiwa nchi imeanza kujijenga miaka ya 80 baada ya ukombozi wa Afrika angalau kueleke tamati, mbona hili ulisemi?

Hii ni principle tu hata katika maisha kwawaida, mara nyingi maendeleo ya mtu anaesaidia ndugu zake saana huchelewa tofauti na yule mwenye mkono wa birika.

Umeandika kama vile una uhakika kwamba sijawahi kumkosoa Nyerere hata siku moja.Kaka hebu pitia post zangu mkuu
 
Back
Top Bottom