sixgates
JF-Expert Member
- Mar 19, 2011
- 3,979
- 1,673
Lema:
ndugu zangu juzi nilikuwa muleba, nikapigiwa simu kuwa hukumu yangu ni tar 21. nikajiuliza mbona imekuwa ghafla.
nikamweleza katibu mkuu kuwa nimepata taarifa ya hukumu, katibu akamiambia naye amepata taarifa.
katibu akanimbia kwakuwa uko mbali we piga kazi tutakupokelea hukumu yako.
nikamwambia sawa.
Lakini mke wangu akaniambia amesoma kwenye mitandao ya jamii kuwa hukumu yako ni ijumaa unaenda? nikwambia mke wangu siendi kama ni mbaya au nzuri tutapokea tukiwa huku tunapiga kazi.
mke wangu akaniambia nenda kwa maana Mungu anakwenda kufuta machozi ya Arusha.
Nikamwuliza Tundu hiyo hukumu imekaaje?
Tundu akaniambia bana mi sipigi ramli we twende mahakamani.
Nikamwuliza Mawazo niliyekuwanaye Muleba aniambie mawazo yake...... Mawazo akaniambia bwana tupige kazi hukumu itukute huku. nikampigia mke wangu kuwa siendi. mke wangu akaniambia kwa hili naomba nisikilize nenda mahakamani.
Tulipokuwa mahakamani hukumu ikaanza kusomwa. Golugwa akanikonyeza, nami nikamkonyeza katibu mkuu, tundu naye akanikonyeza maana ngoma ilikuwa kwa chadema.
sasa kakake Tundu akawa ameshika kichwa.
mkanga na wenzake wakawa wanasikiliza tu hawajui kinachoendelea maana hata kiingereza hawajui. hata mary chatanda sidhani kama anajua neno ofcourse!
hukumu ikasomwa Lema nikawa mbunge.
sasa tumeshinda kesi hawa watu watalipa pesa.
Nyumba ya mkanga mteja wake tayari yupo hapa, nimemwambia anilipe advance kabisa.
Mahakamani wamesema wanatakiwa kulipa milioni mia tatu na hamsini....... hiyo si kweli kwasababu wamepiga haraka haraka!
Lengo la hawa jamaa kufungua kesi ilikuwa kuni frustrate ili nisifanye kazi.
watalipa pesa zote bila huruma!
ninarudi bungeni mtindo ni uleule...... nimeamua die or live
MUNGI unajitahidi sana