Huyu Mtani wangu hapa alikuwa analia nini? Ni ile wanasema Machozi ya Mamba sijui?
Nina uhakika alikuwa anatania tu kwani juzijuzi tu alikuwa akiboronga upupu na huwezi amini kuwa ana uchungu na Watanzania.
Makinda, acha kujifanya una uchungu na Watanzania.
Badala ya kujilimbikizia Posho, jumba lako kudai liwe na swiming Poool na kuikataa nyumba aliyokuwa akiishi Sita na ukataka nyumba mpya. Ubadhirifu wote mnaofanya badala ya kujenga njia bora za maji machafu, matokeo yake ni haya.
Namsifu sana huyu dada wa Kizungu (Samahani kutumia neno Mzungu) anayeonaka kwenye picha nyingi akiokoa watu.
Yaani hata Mitumbwi ya kuokolea watu ya kujaza upepo wanayotumia askari wa majini hamna. haya mamitumbwi bei yake ni ndogo sana na kwa mashangingi wanayonunua, zingelinunuliwa kwenye mikoa kadhaa na kuwa tayari kutumia kila inapohitajika.
Wee mtani wee, acha zako bana. Heri ya Kikwete ambaye tunajua huwa hajali kabisa watu wanavyosema na tunamfahamu kwa hilo kuliko WANAFIKI wanaojifanya wana uchungu lakini hamna kitu. Juzi kulikuwa na Mabomu mara mbili, mwaka 2009 mafuriko na leo mafuriko na msijifanye mlikuwa hamjui hilo linakuja.
<!-- google_ad_section_end -->