PICHA: Mafuriko yalikumba jiji la Dar es Salaam

20111221_121034.jpg


Picha za Moja kwa moja kutoka Eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuzingirwa na maji/Mafuriko kutokana an mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam Muda Huu na kufanya eneo lote la Jangwa Kuonekama Kama Ziwa.Picha Hizi za Moja kwa Moja Kutoka Jangwani Zimepigwa na Mdau Bilal Ahme
Mkuu figganigga, hivi hapa si ndio kuna hiyo njia mpya inayounganisha barabara ya Kigogo!?
Kwa mbele kidogo hiyo barabara imejengewa ukuta wa kuitenganisha na mto Mszimbazi kwa mawazo kwamba ukijaa maji 'yapite juu na barabara ibaki chini'. Alafu upande wake wa kuelekea barabara ya Morogoro si ndio kuna majengo mapya ya TANRODS/DART!?
Nauliza maswali haya kwa sababu watu wote wanaopajua hata wasio na elimu ya ujenzi na uinjinia wanajua kuwa maji miaka yote yanajaa hapa tena kwa kiwango hiki hiki, sana walidesign vipi barabara ambayo ipo chini ya kina cha maji! ...kwamba mvua ikinyesha inabidi watumiaji wa barabara wasubiri maji yaishe ndio waitumie!?
Ni wazi hizi ni natural disasters lakini hapa kwenye hili kuna uzembe. Huwezi kufanya feasibility ya mradi kama huu bila kuhusisha wataalamu wa mazingira au ndio yale ya siasa kuingilia kila kitu!?

 
Back
Top Bottom