Kuna siku tulienda kuangalia kiwanja na mshikaji maeneo ya makonde mbezi ya kimara...kiwanja kilikuwa kikuuubwa afu bei ndogo ukilinganisha na uzuri wa kile kiwanja ...
Tuakkubaliana kabisa kuwa tunaleta ela siku inayofuata...Mungu mkubwa...mvua si ikanyesha...aisee gari ilikuwa na four wheel lakini tulishuka na kuanza kutembea kwa miguu maana ilikuwa inateleza hakuna maelezo...dongo la mfinyazi haswa...
Tulivyofika tukamwambia yule mama tutakuja tena siku nyingine...nahisi aligundua tumeshtuka...akaanza ooh mtashirikiana na wenzenu majirani kutengeneza hii barabara...hahahaha...tutengeneze barabara sie tanroads...
Yani tulishukuru mmno...from that day ikawa formula...kiwanja kizuri utakijua wakati wa masika