Kwa hiyo wale walio vunjiwa walionewa si ndio ukweli huo? Suala ni miundo mbini si kuvunja baadhi ya nyumba na kuacha nyingine wakati adha ni ileile, lile eneo laweza kuwa linahitajika kwa matumizi mengine mvua ilikuwa kisingizio tu, ndio maana nimesema Dar nzima avunje basi ishu si mafuriko?Ndugu mwanachama wa JF, unafatilia habari za nchi vizuri? Msimu huu wa mvua mafuriko yako karibu mikoa mingi na inaharibu makazi ya watu. Hivyo ukisema watu wahame Dar na kwenda mikoa mingine ili wakaishi kwenye mito na maziwa yaliyofurika?
Pia mafuriko haya sio Dar tuu juzi juzi tuu Houston palifurika na makazi ya watu yalijaa maji na huko ni USA ambayo miundombinu yake iko superb bin perfect bin kurekebishwa mara kwa mara.
Tofauti tuu mafuriko kwetu ni kila inyeshapo mvua wakati wao ni pale inapotokea disaster kuwa mvua imenyesha kubwa mno.