Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,478
- 34,363
..Chadema wasijaribu hata siku moja kumfukuza Shibuda.
..wanapaswa kujifunza makosa waliyoyafanya kwa Kafulila.
Sikubaliani wewe mkuu, mi nadhani Chama kiongozwe na 'policy''. Chadema wakianza kumuogopa mtu ndio mwanzo wa matatizo. Angalia CCM sasa hivi wanamatatizo makubwa sababu tu wanamuogopa Chenge/RA/EL.
Hapa simaanishi kuwa wamfukuze tu Shibuda, hapana nina maana wafuate taratibu hadi itakapofika wakati wa kumfukuza.
Kuhusu Kafulila mimi nadhani uamuzi wa kumfukuza ulikuwa sahihi kabisa. Huwezi kuwa na watu wawili watatu wanaotaka kuvuruga chama kwa masilahi yao binafsi. Alipoondoka Chadema akasema ni chama cha ukoo na ukabila, lakini ni huyo huyo alikua kiongozi CDM masaa 24 kabla hajaondoka. Angalia Kafulila ndiye ameungana na CCM kuyumbisha kanuni za bunge in favor of CCM ili apate uwaziri kivuli.
Ni kutokana na vurugu za akina Kafulila na Hamad Rashid Makinda akapata mwanya wa kuchagua akina Lowasa na January huku wapinzani wakipigana wao kwa wao. The bottomline ni upuuzi wa Kafulila na hisia za kulipa kisasi. Uzembe huu wa Kafulila unadhihiirisha maamuzi sahihi ya CDM.
Maelezo yangu hapo juu ni mifano ya viongozi wanaodhani wao ni Chama. Chama kijengwe kama taasisi na si watu. Alikuwepo Mtei, akaja Bob Makani, sasa Mbowe na atakuja mwingine n.k ndio taasisi inavyokuwa si kuogopa fulani akiondoka chama kitakufa.