mfereji maringo
JF-Expert Member
- Nov 19, 2010
- 1,037
- 250
Wakuu Salaam!!!
Yale maandamano ya Kanda ya Ziwa leo yanahamia Mkoa wa Mara baada ya jana kuingia Geita, Sengerema, Misungwi, Kwimba na Ukerewe. Maandamano yatakuwa Musoma kuanzia Viwanja vya Bweri mpaka Uwanja Mkendo Musoma Mjini. Msafara wa Vikosi toka Mwanza mjini unatarajiwa kupokelewa na Mbunge wa Musoma Mijini Vincent Nyerere.
Dalili zinaonesha kuwa na leo CHADEMA itaiteka Musoma kwa jinsi ambavyo watu wamejipanga na kujiandaa kwa hamu maandamano haya. Maandamano yanatarajiwa kuanza saa 7 mchana.
Aluta Continua.
Kutoka Kitangiri Mwanza
Regia E Mtema
Waziri Kivuli-Kazi na Ajira
=====================
KATIKA PICHA
asante
endelea kutupasha,
waambie makamanda wengine watupe habari humu jamvini,
tunataka tuwasikie na wao pia.