Picha itakayomsuta JK na wabunge wake mamilionea.....

hii ndio hali halisi kule mbagala ..na ndio tanzania ya 2009

enough with mijadala ya ufisadi...hali halisi on the ground ni hii...
maendeleo.jpg

wanafunzi wa darasa la saba kutoka mbagala kuu jijini dar es salaam wakiwa katika mitihani yao ya kila mwezi.


-spika wa bunge letu bwana samuel sitta anasema kuwa wabinge wanastahili kulipwa zaidi ya milioni 7 kwa mwezi apart from marupu rupu

-pesa za kupigana vita comoro tunazo

-pesa za mabilioni kwa ajili ya id cards pia tunazo

-pesa za kumpa mattaka na wajumbe wake kule nic tunazo

this picture shows how out of touch tumekuwa na majority on the ground. Its been 2 years hakuna kinachojadiliwa zaidi ya ufisadi, ile ilani yetu ya uchaguzi imetupwa kapuni na mbaya zaidi wapinzani kama chadema nao wako more out of touch kuliko wote on the ground kwani wao bora kukodi helicopter ili kuwakimbia wananchi wakati wa kampeni...

Pesa ya helicopter si wangewanunulia madawati hawa wanafunzi?

Anyway nawasilisha.

thank you belinda-huwezi jua watoto wote hawa utakuwa umewapatia madawati
 
thank you belinda-huwezi jua watoto wote hawa utakuwa umewapatia madawati

Nguli...
Na iwe mkuu, natumaini mtawasaidia na muhimu pia msimamie/mhakikishe hiyo misaada iwafikie hawa watoto. Mbarikiwe sana!!
 
Maskini Tanzania, Maskini Tanzania...........!!! Maskini kura yangu......nliyompa JK kama ningejua mambo yangekuwa hivi ni bora ule muda wa kwenda kupiga kura ningejilaza jamvini kwangu nimpumzike kwenye kivuli chetu cha Mwarobaini.......!!! Sijui kama ntapiga kura tena....sijui !
Anayeniona mjinga na nliyekata tamaa hiyo ni shauri yake.......!! Ukitaka kuona hii nchi inapepesuka jiulize ni kwanini Afande Shimbo anafuga Ndevu !
 
Sidhani kuna ubaya chadema kutumia helikopta infact tunahitaji kutumia more resources kuwaamsha raia kwani usingizi wa watanzania wenzetu ni fofo, busanda imedhihirisha hilo.hakuna mtu angeamini ccm ingepata kura zote with all empty promises za kina komba. Katika utafiti wa afrobarometa unafanya ktk nchi za kiafrica kila mika miwili, yule editor kutoka ghana alishindwa kutoa tittle kwa repoti ya tanzania mishoni akaamua kuipa tittle hi..."uncritical citzenry" watafiti pamoja na maswali mengine waliuza kwenye madodoso yao hivi...je mna maji..jibu...hatuna...huduma za affya?...hatuna...barabara?...mbovu......umeme? Hatuna...rushwa? Ipo juu....kiongozi wako ni wa chama gani? Ccm...je mwakani utamchagua nani? Ccm. Jamma akaamua aipe title uncritical citzenry...so tunahitaji more civic education programme kuiamsha jamii yetu..heko kanisa katoliki kwa kufungua pazia ..wengine fuateni. Je mnayakumbuka mapokezi ya kina chenge kule bariadi? Je misururu ya magari kule arusha kumpokea lowasa, je kingmaker ra anavyoabudiwa kule igunga? Twendeni vijijini tukaelimishe.
 
Hili si tatizo la Kikwete na CCM, hili ni tatizo la watz kujitia umasikini wa makusudi kwa kuwachagua wezi hawa

asante saan... halafu unakuta mtu kasoma na anasema haoni sbb ya kupiga kura as CCM wataziiba tuu.. hicho hasa ndo wakitakacho CCM.. msiende kupiga kura wapate mwanya wa kuiba.. ni sawasawa ulale mlango wazi ukisema hata ukifunga wataiba tuu.. hata kama hawataki kuiba sasa mnawashawishi waibe

GO VOTE PPL!!!
 
Sasa picha kama hii ndio tunatakiwa kuwatumia wasifu wa jk nje ya nchi kama obama.mbona nchi zingine viongozi wao wakija dc wanaandamana na kuonesha maovu ya hio serikali? Tutumeni hio picha white house na kuwaambia matatizo yote mpaka ya ufisadi.
 
Maisha bora kwa kila mtanzani ndio hayo! sasa tuseme nini na ndio kauli mbiu?? heri kuwalinda mafisadi wasibughudhiwe kuliko kuwapa huduma bora wanafunzi wa maskini? kwani ni mbunge yupi au waziri gani mwenye mtoto anaye soma kwenye shule kama hii?

kama jibu ni hapana basi tuwe wapole tu, they already have enough milk, why keep a cow?
 
Alafu rahisi JK anataka stimulus package ya kuinua uchumi over $250 million hivi inachukua hata $50,000 kujenga shule Tanzania. Yaani kwa kweli vitu kama hivi vinakera mno sijui mna interpret vipi. Hii ni shule tu bado watu wanaokosa madawa. mme muona huyo mtoto wa kwanza kwenye picha hata viatu ana anavaa ndala, ndala zenyewe sole ishaanza kwenda chini mpaka rangi inaonekana.

hiyo hela uliyo taja hapo juu ya sehemu moja pekee serikali ilikuwa na uwezo wa kununua zaidi ya mabasi mia moja ya second hand, kuajiri madereva 250 kwa shift, kuajiri makondakta 300, 50 admin operative, 20 mechanics na kurudisha their investment within 10yrs kama kutakuwa na usimamizi mzuri hawataki kumfikia "Aloyce wa Buguruni" katika ajenda zao na awapo dunia yetu. Wao shule Private, Hospital Private, HE abroad ndio maana mshahala wa wabunge hauwatoshi.

Mungu Ibariki Tanznania
 
Inauma sana ila tusikae tu nakulalamika tufanye kitu labda mioyo yao migumu itafunguka kwa kuanza tu nimetuma picha kwa directorate nzima, endapo hili ombi mungu atasimama watatoa usd 2000 na mungu akibariki ziko directorate 9 zote zikitoa ina maana ni 2000x9 imagine! Tusichoke kupiga kelele...tukinyamaza hata mawe yatazungumza, kazi ni kutafuta jina la hio shule ili hela zisiishie mikononi mwa watu wenye roho ngumu.
 
LAKINI HII NDIYO ILANI YETU (ccm)YA UCHAGUZI 2005 KUUA OR SORRY KUINUA KIWANGO CHA ELIMU KWA ASILIMIA ......

By the way kuna mtu anajua watoto wa hawa wakuu wanasoma wapi?
mkulu JK
Makamba
RA
Sita
EL
Karamagi
Vijisenti
Pinda
mawaziri wate ktk wizara ya elimu
 
Sijawahi kusikia uchungu kama huu katika moyo wangu kuhusu usifadi Tanzania. Kwanini wanafunzi wanakaa njini na wakati watu wanaiba hela za taifa? Hii picha inaset reality ya maisha ya more tha 80% of Tanzanians.
 
Katika utafiti wa afrobarometa unafanya ktk nchi za kiafrica kila mika miwili, yule editor kutoka ghana alishindwa kutoa tittle kwa repoti ya tanzania mishoni akaamua kuipa tittle hi..."uncritical citzenry" watafiti pamoja na maswali mengine waliuza kwenye madodoso yao hivi...je mna maji..jibu...hatuna...huduma za affya?...hatuna...barabara?...mbovu......umeme? Hatuna...rushwa? Ipo juu....kiongozi wako ni wa chama gani? Ccm...je mwakani utamchagua nani? Ccm. Jamma akaamua aipe title uncritical citzenry.

African huyu jamaa kwa kuwa alitokea Ghana alikuwa very fair. Nilikwenda Ghana b4 uchaguzi wao mwaka jana. Yaani hiyo serikali ambayo walisema wataiondoa madarakani tungeipata sisi mbona tungeringa? Serikali ya Kuffor yaani ilifanya mambo makubwa kwa kweli nilitembelea mpaka vijijini kwa kweli you could see waliyofanya waziwazi lakini still wananchi walisema wataipiga chini na kweli wakaipiga chini. So huyu jamaa alikuwa hatuelewi kabisa kutuita uncritical citizenry I would say it was our fair share.
 
Jamani shida za watoto wetu kusomea katika mazingira ya ovyo hayako Mbagala tu, bali hata kule Muleba mkoani Kagera niliwakuta watoto wanasomea katika mazingira haya hapa chini. Muulizeni Masilingi yule mbunge wa Muleba kama anajua hali hii. Kwani haya ni mazingira mazuri katika karne hii ya sayansi na teknolojia? Twategemea kupata madaktari bingwa na wanasayansi mahahiri hapa? twategemea kupata wachumi hapa? au twategemea kupata mafisadi watakaotaka kufanya vijiji vyao kuwa na villas?

_IGP9731.JPG

Darasa la 5.jpg

MF
 
woman of substance umenena kweli hapo..lijamaa linalohusisha mambo ya chedema na picha hiyo sijui linawaza nin...
lkn pia sisi kama wananchi ambao tunateseka na hali hii pamoja na watoto wetu nadhan we are to blame...hawa watoto watatulaani sana..maana tunatakiwa sasa kutumia kura zetu mwakani hapo kuitoa ccm..pengine atakayekuja ataleta hali nzuri zaidi...ccm jamani imeshindwa...sidhan wanahitaji muda zaidi..kila siku hali ni mbaya kuliko jana yake..angalia sasa hapo watoto hawana viti wala meza...this is very bad.
 
Kwa mazingira haya alafu wanasimama bungeni milioni 7 wanazo pata eti hazitoshi jamani jamani muwe mnaona hata aibu alafu mnawadanganya watu tutahakikisha kila mtoto ana pata nafasi ya kusoma yaani asome kwenye shule ya nyasi akae chini Mungu atawahukumu endeleeni kutembelea mashangingi hayo.
 
ww unayesema mambo ya kukodi helikopta,mjadala wa ufisadi uko out of touch,kumbuka ni kwa sababu ya ufisadi unaoppigiwa kelele na chadema ndio uliosababisha matokeo ya picha hiyo hapo.

Hata ungechukua hela ya kukodi helicopta ukainunulia madawati je kwa uelewa wako ingetosha shule ngapi??jiulize msafara wa mtu kama pinda(pm)anapoenda mikoani unaigarimu nchi kiasi gani????????????kokotoa then uje na longolongo zako za helopta
 
Back
Top Bottom