Boramaisha
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 820
- 18
Hii ndio hali halisi kule MBAGALA ..na ndio Tanzania ya 2009
enough with mijadala ya ufisadi...hali halisi on the ground ni hii...
Wanafunzi wa darasa la saba kutoka Mbagala Kuu jijini Dar es salaam wakiwa katika mitihani yao ya kila mwezi.
-Spika wa bunge letu bwana Samuel Sitta anasema kuwa wabinge wanastahili kulipwa zaidi ya milioni 7 kwa mwezi apart from marupu rupu
-Pesa za kupigana vita Comoro tunazo
-Pesa za mabilioni kwa ajili ya ID cards pia tunazo
-Pesa za kumpa Mattaka na wajumbe wake kule NIC tunazo
This picture shows how out of touch tumekuwa na majority on the ground. Its been 2 years hakuna kinachojadiliwa zaidi ya UFISADI, ile ilani yetu ya UCHAGUZI imetupwa kapuni na mbaya zaidi wapinzani kama CHADEMA nao wako more out of touch kuliko wote on the ground kwani wao bora kukodi helicopter ili kuwakimbia wananchi wakati wa kampeni...
Pesa ya helicopter si wangewanunulia madawati hawa wanafunzi?
anyway nawasilisha.
Tatizo ni kwamba viongozi hawajali na wamesahau kabisa kwamba uongozi ni dhamana na kazi yao ni kutumikia WATU waliowapa dhamana ya kuongoza. Nchi maskini kama yetu inahitaji viongozi waadilifu wanaojua na kujali wajibu wao kwa wananchi. Viongozi wanapaswa kuwa 'watumwa' wenye kukosa usingizi wakiwaza wafanye nini kuwatumikia na kuwanufaisha waliowachagua badala ya kuwaza kujinufaisha wao wenyewe. Matokeo ya hali iliyopo ya viongozi kukengeuka ndio inapofika kwenye Budget matatizo ya wananchi hayakumbukwi na kushughulikiwa kwa kina.
Nchi yenye asilimia 60 ya wananchi wasio na uhakika wa maisha yao ya kila siku; yenye wanafunzi mijini na vijijini wasio na madawati wanaoketi chini wakifanya mitihani yao kama hawa tulioonyeshwa n.k., n.k.; Budget ya mwaka kwa ajili ya maendeleo ya wananchi hao wasio na matumaini, inasheheni kasma za mabilioni ya fedha kwa ajili mambo yasiyo ya lazima kama CHAI maofisini. Wabunge wawakilishi wa watu hao wasio na matumaini, wanaipitisha Budget hiyo kirahisi bila matatizo yoyote. Ndiko tulikofika, hakuna anayeguswa kwa dhati wala anayejali mustakabali wa walalahoi na watoto wao wanaoketi chini darasani! Kila anayepata nafasi ya uongozi ya ngazi yoyote ile anawaza 'pangu pakavu, nitieje mchuzi nifaidi!'