Billionaire kutoka Abu Dhabi aongozana na watu 680 kufanya utalii. Je, Tanzania tunaweza kuvutia utalii huu?

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,317
24,209
Bhisho Bulembu
Eastern Cape, Republic of South Africa

REKODI HII YA RAIS WA UAE MTAWALA WA ABU DHABI

Katika mwezi Aprili mwaka 2023 mji mdogo wa Bhisho Bulembu jimbo la mashariki la Cape ambapo kulikuwa na uwanja wa ndege pekee wa,nchi ya Bantustan nchini Afrika ya Kusini uliotelekezwa na serikali ya chama cha ANC habari zilitapakaa kuwa billionaire mmoja ameamua kukarabati uwanja huo kwa pesa yake kiasi cha randi za Afrika ya Kusini 20 milioni ili aweze kuja kwa likizo akiongozana na kundi la watu 680
1696551090985.png

Picha ya mji wa Bhisho mwaka 2016.

Watu hao 680 wanatokea mataifa zaidi ya 32 yakiwemo UAE, Palestine, nchi kadhaa za ulaya, Marekani ya Kaskazini, Asia na Kenya iliyojumuisha wasanii, watumbuizaji, wapishi, mayaya, walinzi, marafiki, ndugu na jamaa wa ukoo wa mtawala wa Abu Dhabi.

View: https://m.youtube.com/watch?v=ZRwTXAK7SNE

Jambo hilo lilipokelewa vizuri na wenyeji wa mji wa mdogo wa Bhisho uliopo uwanja wa ndege wa Bulembu lakini likizua gumzo kubwa lenye hisia hasi kwa wakaazi wa mbali walio miji mikubwa ya Johannesburg, Pretoria, Durban n.k nchini Afrika ya Kusini ambapo wengi hujiona ni wajuvi wa mambo makubwa kuliko wale washamba wa miji midogo.

Wakaazi wa Bhisho Bulembu waliona ujio huo ni neema na fursa baada ya serikali kuu iliyopo Pretoria kuwatelekeza. Ujio wa bilionea huyo kutoka UAE ungeleta ajira na fedha ktk uchumi mdogo wa mji huo wa shamba.

Wajanja wa miji mikubwa wao walijivika uzalendo kuwa iweje bilionea apewe uwanja auendeleze na kuutumia kwa ndege zake na helicopter kadhaa kutua na kuruka wakati hakuna ofisi ya idara ya uhamiaji, forodha wala Polisi wa uwanja wa ndege kukagua silaha n.k

Kelele za wajanja wa mujini Johannesburg, Pretoria n.k miji mikubwa ikapelekea gumzo hilo litue bungeni kujadili hilo kadhia huku vyombo vya habari vikubwa kadhaa tajwa Afrika ya Kusini kuendesha mjadala wa hadhi ya kitimoto kuhusu "bilionea kupendelewa" kinyume na sheria za uhamiaji wazijuazo watu wa miji mikubwa.

Waziri wa mambo ya ndani Dr. Aaron Motsoaledi, ikabidi ahojiwe bungeni na pia sawia katika vyombo tajwa vikubwa vya media Afrika ya Kusini.

Katika ripoti yake kwa bunge na mahojiano kupitia vyombo vya habari waziri Dr. Aaron Motsoaledi alilieleza bunge na umma kupitia media kuwa hakuna sheria iliyovunjwa na kuwa protokali zote zilifuatwa kwa majina ya wageni hao 680 kuwasilishwa kwa mkono siku kadhaa kabla ugeni huo haujatua shamba na maofisa wa uhamiaji walikwenda huko Bhisho Bulembu shamba kutekeleza wajibu wa kuhakikisha taratibu zote zimefuatwa.

Je kwa Tanzania na kampeni za Tanzania: The Royal Tour na Amazing Tanzania tunaweza kumpatia bilionea uwanja Ruaha National park, Saadani National Park akatengeneza runway ya uwanja wa ndege atue huko shamba kuja kutumbua Holiday na kutuketea madolari kibao sekta ya utalii Tanzania ishindane na ya South Afrika ? Au tukakuwa wazalendo kama wake wajanja wa Johannesburg kupinga aina hii ya utalii .

View: https://m.youtube.com/watch?v=YytHBvborfg&t=1s

Minister briefing on Landing of UAE President and 500 entourage at the Bulembu Airport​

05 May 2023​

Chairperson: Mr M Chabane (ANC)​


The Portfolio Committee on Home Affairs met on a virtual platform to receive a briefing from the Minister and the Department of Home Affairs on the landing of the United Arab Emirates (UAE) President and his entourage of 500 at the Bulembu Airport in the Eastern Cape.

The Minister insisted that everything had been above board and all laws had been complied with. He pointed out the various economic benefits this private visit brought with it, as the UAE President promised to invest more than $10 billion (R185 billion) in energy, oil, economic infrastructure, tourism, agriculture and other sectors of the economy. He further assured the Committee that the Office of the Public Protector was investigating the matter following a complaint lodged by a Member of Parliament (MP) on the matter.

After hearing the Department’s explanation on the issue, some Members were happy to defer their oversight responsibilities to the Public Protector, but others wanted more documentary proof and demanded that the Minister provide it to the Committee.

Three types of documents were requested by some Members. The first was the note verbale, the second was the original application that the DHA had received from the Premier of the Eastern Cape, and the last was the visa and passport information of those who had accompanied the President to the Republic. A Member publicly stated on the platform that he suspected there had been “shenanigans” around the visa process.

Among other concerns which some Members raised were the interpretation of the Border Management Authority(BMA) Act, the distinction between a state and a private visit, and whether a private visit made by a head of state should warrant that he should receive all the protocols and privileges that would normally be accorded to during a state visit. Other issues raised were the types of visas given to the entourage staff, and the rationale behind using Bulembu Airport instead of the airport in Port Elizabeth, which was much closer to the President’s intended destination.

Those Members who preferred to let the investigation process unfold expressed confidence in the Public Protector’s Office, and warned their colleagues of potential overreaching in intervening in the administrative affairs of the executive. Some of them also suggested that the Committee should rather engage with the Department and other involved departments in a closed meeting, as some information, such as people’s visa information, passport numbers, etc. should not be released to the public.

Some Members were uncertain of the investment benefits, as the President had brought everything from overseas to the country and thus had not benefited the South African tourism sector. There was a suggestion that this trip might have been for the personal enrichment of the UAE ruler and the Premier of the Eastern Cape. There was also a complaint about the lack of a government notice on this matter, with a view that the matter should have been published in the Government Gazette and be available for public comments for a period of no less than 30 days.

Meeting report​

The Chairperson said this was a special Portfolio Committee meeting for Members to interact with the ministry on the issues surrounding the landing of the President of the United Arab Emirates and the entourage. The Committee would be interacting with the Department of Home Affairs (DHA) and the Border Management Authority (BMA).

Minister's briefing
Dr Aaron Motsoaledi, Minister of Home Affairs, read the given explanation provided by the Department of Home Affairs. The document had been provided to the Committee.

The Minister received an application on 7 April from the Premier of the Eastern Cape, with all supporting documentation, including diplomatic communications between South Africa and the United Arab Emirates.

Following due consideration and taking due regard to Section 9 (a) of the Immigration Act, read with regulation 8 of the immigration regulations; he had designated Bulembu Airport as a place of entry and exit.

Source : Minister briefing on Landing of UAE President and 500 entourage at the Bulembu Airport | PMG
 
East African Airways! ngozi nyeusi bladibastard iliiua tunu hii! sasa tunatamani Emirates to Land in EA!
 
Tz janja janja kila deal viongozi wanataka wawe shareholder
 
Back
Top Bottom