Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Niache kwenda Bugando nifunge safari kwenda CHATO?
Inawezekana nyie wanachama wa CCM mmefanya Chato imekuwa Maka hata wa Dar es Salaam wataacha Muhimbili wakatibiwe huko maana ikishindikana kupona watafukizwa mpaka wapone.
 
Bado inakuja Chato international stedium!
Itachukua muda mpaka akili zije ziwakae sawa!
 
Hakika.....

Mbona Dodoma imechangamshwa?!!

Mperampera huu wa kuzichangamsha wilaya na mikoa ungali unaendelea.......

Awamu ya 5 inathubutu kwa kubadilisha STATUS QUO iliyotuchelewesha......
Kila Rais akiingia akafanya hivi, sijui tutakuwa taifa gani?
Kama waliotangalulia wangefanya hivi basi tungekuwa na miradi mikubwa kama viwanja vya ndege vya kimataifa vijijini!
 
Chato ni muhimu kuliko Tanzania wewe!! Mbona kama huelewi?
 
Sisi watu wa Kigoma, Rukwa na Kagera twende wapi? Kwanini hospitali hiyo isingejengwa hata Nyakanazi ili tukapate huduma huko?
 
Hii ni hatari sana kwa ustawi wa utawala.. kuna Rais atakuja afanye kufuru miaka ijayo kama upendeleo huu utaachwa.

Mtu atoke Simiyu au Shinyanga eti aende Chato wakati Bugando ipo?

Nadhani hii ji project ya kupendezesha kijiji cha Chato.
 
Maendeleo hayana chama ila maendeleo yana ukanda, hapa nimemkumbuka mzee Butiku aliyesema hakuna wa kumfananisha na Nyerere kweli ni hakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…