Picha: Hospitali ya Rufaa ya Chato iliyowekwa jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi. Kuhudumia takriban watu milioni 18 mikoa ya Kanda ya Ziwa

Ninaamini hivyo mkuu,

Hatuwezi kuwa na miji michache ambapo watu wanajazana na kuzaliwa kila siku.

Tena kama angekuwa na mda zaidi natumaini angefanya mazuri zaidi.

Kwa kweli ana uthubutu na vision pia.

Huo mji ni wetu wote.

Hao wakuu wa mikoa wangekuwa na maono wangetafuta nao wawekezaji wa kuwekeza mikoani ili miji iendelee kukua na kuleta ajira kwa local people.

Ila jamaa anapambana
Bado inakuja Chato international stedium!
Itachukua muda mpaka akili zije ziwakae sawa!
 
Hakika.....

Mbona Dodoma imechangamshwa?!!

Mperampera huu wa kuzichangamsha wilaya na mikoa ungali unaendelea.......

Awamu ya 5 inathubutu kwa kubadilisha STATUS QUO iliyotuchelewesha......
Kila Rais akiingia akafanya hivi, sijui tutakuwa taifa gani?
Kama waliotangalulia wangefanya hivi basi tungekuwa na miradi mikubwa kama viwanja vya ndege vya kimataifa vijijini!
 
Chato ni muhimu kuliko Tanzania wewe!! Mbona kama huelewi?
Binafsi nafikiri na nashauri Serikali itoe idadi ya watumishi wanaohitajika hapo, halafu waajiriwe wapya wote. Ndipo uanze uhamisho wa kubadilishana na wazoefu/wakongwe. Lkn tukihamishia tu kutoka kwenye hoslitali zilizopo tutatengeneza upungufu mkubwa sana kwenye hoslitali nyingine bila ulazima huo.
 
Ni Nani asiyejua kuwa BUGANDO HOSPITALI ilizidiwa kwa kukosekana HOSPITALI KUBWA ZA RUFAA kule Mara na Shinyanga?!!!

1.JPM amewajengea wanaMARA ambao waliteseka toka UHURU....
2.JPM amewaongezea wanakanda hapo CHATO GEITA......
3.Kule Mtwara amejenga HOSPITALI KUBWA YA RUFAA itakayowahudumia wanaKusini....

👆👆👆👆👆
HAKIKA NI HATUA KUBWA MNO...TENA MNO!!!
Sisi watu wa Kigoma, Rukwa na Kagera twende wapi? Kwanini hospitali hiyo isingejengwa hata Nyakanazi ili tukapate huduma huko?
 
Hii ni hatari sana kwa ustawi wa utawala.. kuna Rais atakuja afanye kufuru miaka ijayo kama upendeleo huu utaachwa.

Mtu atoke Simiyu au Shinyanga eti aende Chato wakati Bugando ipo?

Nadhani hii ji project ya kupendezesha kijiji cha Chato.
 
Maendeleo hayana chama ila maendeleo yana ukanda, hapa nimemkumbuka mzee Butiku aliyesema hakuna wa kumfananisha na Nyerere kweli ni hakika.
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom