Picha hii ya Lema imenifikirisha sana!

Picha hii ya Lema imenifikirisha sana!

Umetumia kipimo gani kujua yuko imara? THEMOMETER,BAROMETER,Kipimo cha kupimia ukimwi,kuharisha au umetumia nini kilichokuhakikishia yuko imara?
Kuna maswali mengine hufanya watu badala ya kujibu swali huishia kuuliza hivi muuliza swali yukoje!?
 
Mkuu pamoja na kusema yote hayo lakini bado hakupunguzi adha za Binadamu kuwa Rumande au Gerezani. Nakuhakikishia kuwa Wewe unaweza labda ukawa unamwona Mheshimiwa Lema yupo ngangari ila nikuambie tu kuna uwezekano mkubwa tu moyoni mwake anaumia mno tena kwa mengi ila anajikaza tu kwa nadharia yao ya Ukamanda.

Kama Wewe unaona Mheshimiwa Lema huko alipo sijui rumande au gerezani anapata raha inayompelekea kutokuwa na hofu basi kaombe kubadilishana nae yeye atoke halafu Wewe ukae huko hata kwa siku tatu ( 3 ) kisha uje utupe mrejesho wako humu.

Namkubali sana Mbunge Lema ila akae akijua kuwa Siku zote sikio halizidi Kichwa na kama ile Kauli tunayoambiwa aliongea jana Mbunge mwenzie Kiukamanda Nassari kuwa yoyote anayepinga yanayofanywa na Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ni taahira na akapimwe akili ni ya kweli basi Mheshimiwa Mbunge Lema amejitakia mwenyewe na inabidi tu sasa awe mpole.

Awamu hii ya Mr. Sulphuric Acid siyo ya Ki sport sport jamani Wanasiasa wa Upinzani hivyo nendeni nae kwa akili mno na mahesabu makali otherwise you will all be doomed.
Lema ni wazi anaonekana mchovu,mwenye mawazo mengi! Ila ushabiki tu unawadanganya wengi !
 
Unasifia ujinga kwa mapenzi yaliyopitiiza.Lema hana heshma yoyote kwa sababu yeye mwenyewe hajiheshimu.

View attachment 448558
Ule msemo maarufu duniani kwamba "Picha huongea maneno elfu"`umenifanya niiangalie picha ya Lema huku nikifikiria Propaganda za kisiasa zinazopigwa dhidi yake na wanaomchukia. Kwanza kwenye picha hii Lema anaonekana yupo Imara zaidi tofauti kabisa na kabla ya kuingia Mahabusu.Ukimwangalia kwa makini kama wapinzani wake walidhania kumweka mahabusu wanaweza kumjaza hofu basi watakuwa walikosea sana. Lema anaonekana hana hofu kabisa na ana utimamu wa akili.

Jambo jingine nimejiuliza kama washtakiwa huwa wana faragha ama hawana wanapoongea na Mawakili wao wakiwa Kizimbani. Maana kwa namna yoyote hii picha inaonesha kwamba Askari huyo anasikiliza kwa makini sana kinachoongelewa kati ya Lema na wakili wake. Ili iweje?

Lakini pia Lema anaheshimiwa hata na watesi wake. Pamoja na kumsema vibaya na kujaribu kumdhalilisha. Lema analindwa na Askari Magereza mwenye cha Nyota moja. Maana yake hata hao wanaomchukia Lema wanaijua hadhi yake! Lakini siye akina yakhe huwa tukiingizwa Mahabusu ni lazima siku hiyo hiyo tunyolewa nywele. Walisahau kumnyoa nywele Lema ama ni heshima waliyo nayo kwake?
 
Lema yuko Fit kwa sababu Tanania ni nchi inayofuata sheria, haitesi mahabusu, inawapa haki mahabusu kuona wanasheria wao na hata ndugu! Unadhani angekuwa anateswa angekuwa hivyo Subutuuuu! Kwa nini haya hamuyaoni. Yeye akae tu mahabusu kwa kosa alilolitenda! nanyi mnatakiwa mumshauri vizuri sio ninyi mnaenjoy uhuru wenu na mnamshabikia mwenzenu anaetamani huru mlio nao!
 
sasa kama yuko fit dhamana anataka ya nini?
si aendelee kukaa huko huko tu!

yuko fit lakini haki ya uhuru wake iko palepale fikiri kwa kina zaidi acha kushabikia mateso ya wenzio.
 
Hakunaga faragha ukiwa mtuhumiwa.
Hata huko kwa wenzetu mfungwa hapaswi kunong'ona iwapo anaongea na ndugu yake aliyekuja mtembelea.
 
Allen Kilewela inaonekana huna ufahamu Zaidi ya uropokaji ,,,ni mfungwa tu ndio anyolewaye nywele sio mtu aliye mahabusu.

Ila ukitaka kujua tamu na chungu ya lupango basi kamuulize Lissu
 
Lema Mungu yu pamoja na ww kama yusuph ktk biblia nimebahatika kusoma mwanzo hadi sasa naona ushindi uliotukuka nimemsoma snowden nakutabiria/nakuombea uyapite yote pole sanaaaa
 
Nywele unanyolewa ukiingia jela au mahabusu?
Nenda kwenye Gereza lolote utapata jibu la hili swali lako. Na inaonekana mtu anayebisha kwamba mahabusu ambao huingizwa Gerezani hunyolewa hajui lolote kuhusu mahabusu na wafungwa likifika jambo la Kunyolewa au kutonyolewa!
 
Back
Top Bottom