Picha hii ya Lema imenifikirisha sana!

Picha hii ya Lema imenifikirisha sana!

Lema anaonekana yupo imara sana.
Hili ni pigo kubwa kwa watesi wake.. Gambo and the alikes..!!
Kesi iliyokuwa isikilizwe leo 21 disemba 2016 inayomkabili mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema ya kumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya lema kuwa mbaya gerezani.

Taarifa za Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai leo asubuhi kwa hakimu mfawidhi katika mahakama ya hakimu mkazi Augustino Rwezile ,alisema alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza mshatakiwa Lema anumwa hivyo siku ya leo alipewa mapumziko pamoja na hayo taarifa hizo hazijaeleza kwa undani ni tatizo gani linamsumbua mbunge huyo.

Pia alisema alipewa cheti cha mgonjwa cha zahanati ambacho kilionyesha mahudhurio ya mgonjwa kwenye zahanati hiyo kutokana na kuwepo na taarifa za kuumwa za mbunge huyo na kushindwa kufika mahakamani,aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine .

Leo ilikuwa ni siku ya kusomewa hoja za awali kwa mbunge huyo na mkewe Neema Lema , ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka jamhuri alikuwa Georgr Katabazi alikuwa anatoa ushahidi.

Hata hivyo hakimu mfawidhi Augustino Rwezile amesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Januari 2017

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema na mkewe Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya mkumtukana mkuu wa mkoa Mrisho Gambo.
 
Mkuu pamoja na kusema yote hayo lakini bado hakupunguzi adha za Binadamu kuwa Rumande au Gerezani. Nakuhakikishia kuwa Wewe unaweza labda ukawa unamwona Mheshimiwa Lema yupo ngangari ila nikuambie tu kuna uwezekano mkubwa tu moyoni mwake anaumia mno tena kwa mengi ila anajikaza tu kwa nadharia yao ya Ukamanda.

Kama Wewe unaona Mheshimiwa Lema huko alipo sijui rumande au gerezani anapata raha inayompelekea kutokuwa na hofu basi kaombe kubadilishana nae yeye atoke halafu Wewe ukae huko hata kwa siku tatu ( 3 ) kisha uje utupe mrejesho wako humu.

Namkubali sana Mbunge Lema ila akae akijua kuwa Siku zote sikio halizidi Kichwa na kama ile Kauli tunayoambiwa aliongea jana Mbunge mwenzie Kiukamanda Nassari kuwa yoyote anayepinga yanayofanywa na Serikali ya Rais Dkt. Magufuli ni taahira na akapimwe akili ni ya kweli basi Mheshimiwa Mbunge Lema amejitakia mwenyewe na inabidi tu sasa awe mpole.

Awamu hii ya Mr. Sulphuric Acid siyo ya Ki sport sport jamani Wanasiasa wa Upinzani hivyo nendeni nae kwa akili mno na mahesabu makali otherwise you will all be doomed.
kama ni sulphuric acid basi ni ile conc. na sio dilute. Ukiijaribu inakulamba hadi mfupa. Hapa kazi tu.
 
Back
Top Bottom