Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,838
- 50,543
Ule msemo maarufu duniani kwamba "Picha huongea maneno elfu"`umenifanya niiangalie picha ya Lema huku nikifikiria Propaganda za kisiasa zinazopigwa dhidi yake na wanaomchukia. Kwanza kwenye picha hii Lema anaonekana yupo Imara zaidi tofauti kabisa na kabla ya kuingia Mahabusu.Ukimwangalia kwa makini kama wapinzani wake walidhania kumweka mahabusu wanaweza kumjaza hofu basi watakuwa walikosea sana. Lema anaonekana hana hofu kabisa na ana utimamu wa akili.
Jambo jingine nimejiuliza kama washtakiwa huwa wana faragha ama hawana wanapoongea na Mawakili wao wakiwa Kizimbani. Maana kwa namna yoyote hii picha inaonesha kwamba Askari huyo anasikiliza kwa makini sana kinachoongelewa kati ya Lema na wakili wake. Ili iweje?
Lakini pia Lema anaheshimiwa hata na watesi wake. Pamoja na kumsema vibaya na kujaribu kumdhalilisha. Lema analindwa na Askari Magereza mwenye Nyota moja. Maana yake hata hao wanaomchukia Lema wanaijua hadhi yake! Lakini siye akina yakhe huwa tukiingizwa Mahabusu ni lazima siku hiyo hiyo tunyolewa nywele. Walisahau kumnyoa nywele Lema ama ni heshima waliyo nayo kwake?