Picha: Hali ya Muhimbili kwa sasa inatisha

Picha: Hali ya Muhimbili kwa sasa inatisha

eeeh hatuna namna tumechoka...tunasububiri muda tu tuondoke madarakani acha walale chini tu kwa kipindi hiki.
 
Wenyewe wanasema Padre Slaa na watendaji wake akina Lema, Sugu, Vincent Nyerere,Mbowe etc wataibadilisha hiyo hali hiyo. Hao niliokutajia ndio mawaziri vivuri kwa sasa . Means wakichukua nchi ndio watakuwa mawaziri wetu . Yaani mawaziri wa nchi yetu.

Utakuwa mchezo wehu hao kujiongoza wenyewe hawawezi wataweza kuongoza nchi?
 
Nasikia Chadema wakichukua nchi mambo yatakuwa kama mbinguni. mtu ukihitaji sindano unabofya tu kitufe kwwenye face book yako sindano inaingia

Hii misekule ya Bavicha ni kuyaombea Mungu hakuna jinsi!
 
Hii nchi sasa hakuna anaetujali kila mtu anaangalia tumbo lake...Mhimbili sio sehemu ya kukimbilia kama unaumwa na unataka kupona...
 
Kama mmimi najiita Profesa wa Muhimbili,basi uprofesa wangu ni fake!

Can you imagine Profesa wa Kizungu,atibu mgonjwa analala chini?

Wangegoma kutibu hawa wagonjwa kuishinikiza serikali ifanye la maana

ndugu yangu watanzania hawabebeki, madaktari walipogoma mliwabeza sana, asiefunzwa na mama yake hufunzwa na ulimwengu, tuuache ulimwengu utufunze ili akili zikae sawa.
 
makene, wiki mbili hivi zilizopita nimepata msukumo mpya wa kutamani nchi inaondoka kwenye makucha hatari ya serikali ya namna hii, inayoongozwa na ccm. Wewe unasema matumaini ya kupona yanaweza kufifishwa ukifika muhimbili, sasa mimi mwenyewe yamenikuta, maana nimempoteza colleague wangu ofisini kwa style hii hii.

Alipata ajali ya pikipiki, kavunjika chini ya goti, kapelekwa muhimbili (ana bima yake ya afya kwa miaka zaidi ya tano), madaktari pale muhimbili walipoona ile bima wakaanza kupuuza hivi. Akalazwa pale sewahaji kwenye vigodoro hivyo vya mauti. Siku mbili bila kuhudumiwa eti wanaprocess bima yake mguu ukaanza kutoka funza. Baadae sana kapelekwa moi, infections zimeshasambaa hadi kwenye vital organs, mguu wakaukata, too little too late, ndugu yangu kaondoka hivi hivi.

Now, nimejifunza jambo moja kuu kuhusu serikali hii:
- katika tanzania hii ya sasa chini ya utawala huu wa sasa, kila raia ajielewe this is survival of the fittest. Kama wewe ni raia wa kawaida, kitakachokuokoa ni mungu wako tu. Usitegemee vyombo vyetu vya sasa vya huduma popote pale. Vipo pale kama ushahidi kwamba kuna ardhi fulani pale afrika mashariki na ni taifa huru likiwa na mtu pale ikulu na vyombo vyote vya serikali. Lakini utendaji wake zero. Polisi ndo haohao majambazi na majangiri, hospitali ndo hizo hizo kama concetration camps za hitler au death chambers magerezani, shule na vyuo vyetu vipo pale kama kutengeneza bongo low grade kama bidhaa za kichina, wabunge wetu ndo hao hao wachawi na waganga wa kienyeji. Kila kitu muhimu hovyo hovyo. Taifa gani hili?

a very big like .
 
Mara zote madaktari wamekuwa wakiyapigania haya , wamepuuzwa na kudhalilishwa ! Hii yote ni kwa vile viongozi wenu hawatibiwi Muhimbili , naona aibu sana !
 
Madaktari kama wamesema,''you all sick people just go to hell'' baada ya serikali ikishirikiana na watanzania ambao ni mentally retarded kusema madaktari wanataka mishahara mikubwa na kusema watawashtaki madaktari.Ukipata ajali Dar sehemu stahiki ya kufika ni hapo and when you come out alive ukatoe shukrani kwa Mungu maana inavyoonekana ''death is inevitable'' kwenye hayo mazingira.
 
Hii mbona ni hali nzuri tu, nendeni vijijini ndo mtabubujikwa na machozi,

Majuzi nilienda Bukoba Goverment hospital, ni majanga,

Kwa sasa hospitali mkombozi kwa wakazi wa kagera ni Mugana Hospital iliyoko jimbo la Nkenge, hospitali hiyo iko chini ya kanisa la RC,
 
Unazunumza kutoka rohoni?!

Hebu jiweke katika nafasi ya huyo mgonjwa aliyelala chini na shuka zimetapakaa damu! Ungeona kwamba huduma zimeboreka?

Huwezi kuzuwia kuona damu hospitali, unajuwa hiyo ni wodi ipi?

Kulala chini hakujaanza leo, sema leo kumepunguwa sana. Au hilo nalo ni tatizo kwako kuelewa?
 
Kwahiyo kabla ya Kikwete serekali ilikuwa ya CCM na sasa ni ya MACCM ?
Mbona unapenda/mnapenda kutofautisha hawamu ya Nyerere, mwinyi, mkapa na Kikwete?
sisi tunazungumzia Miaka 50 ya Uhuru ndipo uwezo wenu ulipofikia?

Hizi no awamu tofauti nauongozi tofauti, Tanzania hatuchaguwi chama tunachaguwa kiongozi. Kumbuka hilo, na fani mzuri ni Slaa, alibwagwa CCM kwenye kura za maoni akacha kiuchaguliwa chadema. Mwingine ni Shibuda. Ni kipi kinachokupa taabu kuelewa hapo?
 
kama una roho nyepesi unaweza ukatoa machozi, kwa jinsi mwanadamu mwenzio amelazwa chini pasipo kupata huduma kama vile wapo somalia. Ikiwa madini yetu na wanyama wetu wanapanda ndege na kwenda kunufaisha mataifa mengine. Hii ni wadi ya sewahaji.

Je kwa staili hii tutafika?

------------------------------

attachment.php



attachment.php

haya ndo maisha bora tuliyoahidiwa mwaka 2005 na mgombea aliyeshinda uchaguzi wa mwaka huo ambaye ndo kiongozi wetu hadi sasa. Ila jina lake nimelisau, hivi ni nani vile wadau???????
 
Huwezi kuzuwia kuona damu hospitali, unajuwa hiyo ni wodi ipi?

Kulala chini hakujaanza leo, sema leo kumepunguwa sana. Au hilo nalo ni tatizo kwako kuelewa?

Sasa mbona yeye na watu wake wakiumwa hawaendi hapo? Nijibu Hilo. Uwe na huruma bi dada, likimfika mwenzako ulione kama lako
 
Tatizo serikali yetu inadili na vitu vingi sana,mara Malawi,sasa Rwanda tena,we need to stay focused
 
hapo ni mnh(rufaa) hujaenda kwenye hospitali zetu walalahoi huko madongo kuinama ukutane na maisha bora kwa kila mTz.
 
Kama mmimi najiita Profesa wa Muhimbili,basi uprofesa wangu ni fake!

Can you imagine Profesa wa Kizungu,atibu mgonjwa analala chini?

Wangegoma kutibu hawa wagonjwa kuishinikiza serikali ifanye la maana

Watanzania hatuchelewi kusahau.Hayo si ndicho Dr Ulimboka na Madokta wenzake walichojaribu kukipigania wakati ule mpaka akaumizwa?Na kuna baadhi ya mazezeta ya Lumumba yakaanza kumkejeli Ulimboka na wenzake kuwa ni wauaji sababu wagonjwa hawakuwa wakipata huduma wakati wa ule mgomo.Leo msiwalaumu Madokta kutokana na hali mbaya ya huduma Muhimbili kwasababu tulishindwa kuwaunga mkono kuishinikiza Serikali kutekeleza matakwa ya hawa Wataalam ambayo mengi ya hayo matakwa hayakuwa ya Madokta binafsi bali yalihusu zaidi huduma duni zitolewazo katika hospitali nyingi Nchini kwasababu ya uwepo wa nyenzo duni au kukosekana kabisa kwa baadhi ya vifaa muhimu na vya kisasa kwaajili ya vipimo na tiba.
 
Back
Top Bottom