Picha: Hali ya Muhimbili kwa sasa inatisha

Picha: Hali ya Muhimbili kwa sasa inatisha

halafu kuna majitu huwa nayaheshimu leo yanakuja kutupa lecture eti tushikamane rais wetu katukanwa! STOP IT!

CC.Manyerere
Ben
 
Kama mmimi najiita Profesa wa Muhimbili,basi uprofesa wangu ni fake!

Can you imagine Profesa wa Kizungu,atibu mgonjwa analala chini?

Wangegoma kutibu hawa wagonjwa kuishinikiza serikali ifanye la maana
Walipogoma ulifanya nini kama mwananchi
 
Ukiona vita inatokea nchi fulani ujue uvumilivu umeshindikana
Tz tumegeuzwa kama watu wasiojua lolote
haiwezekani mambo makubwa hivi watu wanashabikia eti madaktari walitaka mishahara mikubwa
kumbe walikuwa na haki 100
Tuamke tuchukue hatua uvumilivu


Uko sawa 10009%..
Kilichonishangaza toka kwa Baba MwanaAsha ni,kuomba wafadhili ktk jambo ambalo umuhim wake ni mdogo kuliko vingi vinavyohitaji misaada..
1,Afya
2,Elimu bora
Chenji ya Rada walisema itaenda kusaidia usambazwaji wa Vitabi na Madawati,
Lakini hadi leo takwimu sahihi ni wapi vimepelekwa vitabu,hamna hata Madawati hamna.. Mkuu kalala tu White House..
Hovyo kabisa
 
Hiyo picha imepigwa wakati kuna unafuu! Kuna wakati wgonjwa wanaolala chini wanajazana hadi inabidi ufanye sarakasi kuyapita magodoro kumwona mgonjwa aliye upande mwingine wa wodi.
Na bado! hujasema wakati wa mvua inaponyesha nje, halafu watu wanaingia hospitalini na ndara na makubasi wakikanyaga chini sakafuni na maji machafu!! NI adhabu ya kifo tuu ndio itajenga nchi na siyo midomo ya wana siasa! wenzetu Kenya hivi sasa hospitali zao zina video na na pressing button za kuita nurse, sisi ndio kwanza wagonjwa wana lala sakafuni!
 
Hivi jamani zile seating allowances za wabunge kwa siku 20 tu zinaweza kutengeneza vitanda vingapi?
Zile shangingi wanazotumia wabunge na mawaziri gharama ya shangingi moja inaweza kutupatia vitanda vingapi?
Hivi zile gharama za kumsafirisha jk kutimiza malengo yake ya kutembelea nchi zote duniani na misafara yake inaweza tupatia vitanda vingapi?
Hivi...................
Naomba nisiendelee nisije haribu siku yangu bure bora na mimi nisogeze kilago changu nilale
 
ndio maana wao wanatibiwa nje ya nchi , na hata wakirudi wamepoa , hawana haja ya kuleta technology mpya za jinsi vitanda vya kisasa vya wagonjwa vinavyotakiwa!
 
Kikwete anataja mibarabara tuuuuuuuuu hapa kwenye hotuba yake,anamsifia obama lakini hospitalini wagonjwa wanalala chini tena mzungu wa nne...aibu gani hii jamani?
 
Hiyo ndo hospitali kuu ya taifa. Walipogoma madaktari na kutaka mazingira ya kazi yao na vifaa viboreshwe muliwaona kama majuha vile wanaotaka kupewa mishahara mizuri tu. Serikali hii imekwishalaaniwa na Mungu anatuonesha haya ili watanzania tuamue wenyewe.
Wao hawajari kwasababu wanatibiwa nje ya nchi tena kwa kodi zetu, mazingira ya hospitali zetu hawayajui hadi pale kuwe na kongamano au warsha fulani ndio viongozi wanakanyaga mazingira ya hospitali zetu zikiwa zimeshapakwa rangi siku mbili zilizopita.
I wish waandishi wa habari wa kimataifa wangekuwa wanareport haya mambo katika nchi rafiki na donors wa budget zetu ili wajue michango wanayotupatiaga haiwanufaishi watanzania wote bali viongozi na familia zao huku watanzania wanalala chini mawodini na mama wajawazito kufariki njiani juu ya baiskeli wakiwahishwa hospitali.
 
Post nyingi za humu zinaonesha watu wasivyo tembelea Mahospitalini kuona na kuwatia moyo na kuwaombea Wagonjwa... kuona wagonjwa na masikini ni sehemu ya ibada...
Ritz umeona barabara za Muhimbili!
 
Last edited by a moderator:
My God!

Aisee! Matumaini ya kupona yanaweza kufifishwa zaidi ukifika hospitali, hasa ukikutana na mazingira ya namna hii!

Ndiyo dalili za serikali kuchoka, kama alivyokiri Waziri Mkuu?

Maana kama haiwezi kutoa huduma za msingi kama afya, elimu, ulinzi, usalama (wa mipaka, raia na mali zao), maji, n.k...

poor you. Mkurugenzi wa uchochezi na chuki
 
Buku Saba Lumumba Project fame..
 
Dah,
Inasikitisha sana,hapo wamelala chini huku kodi ya sh elfu moja ya simcard ingali inawasubiri,

Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi??

Au kuwaleta wakuu wa dunia ndizo zilikuwa ahadi zake kwa watanzania??
 
Vita waliyopigana madaktari wakitarajia wananchi na serikali iwasikie,
Maumivu na damu ya ulimboka,
Vifo vya wahanga ambavyo pamoja na vifo vyao jamii haikuona umuhimu

Ndo mwangwi wake umeanza.........................................
Mpaka akili ije
 
My God!

Aisee! Matumaini ya kupona yanaweza kufifishwa zaidi ukifika hospitali, hasa ukikutana na mazingira ya namna hii!

Ndiyo dalili za serikali kuchoka, kama alivyokiri Waziri Mkuu?

Maana kama haiwezi kutoa huduma za msingi kama afya, elimu, ulinzi, usalama (wa mipaka, raia na mali zao), maji, n.k...

Makene, wiki mbili hivi zilizopita nimepata msukumo mpya wa kutamani nchi inaondoka kwenye makucha hatari ya serikali ya namna hii, inayoongozwa na CCM. Wewe unasema matumaini ya kupona yanaweza kufifishwa ukifika Muhimbili, sasa mimi mwenyewe yamenikuta, maana nimempoteza colleague wangu ofisini kwa style hii hii.

Alipata ajali ya pikipiki, kavunjika chini ya goti, kapelekwa Muhimbili (ana bima yake ya afya kwa miaka zaidi ya tano), madaktari pale Muhimbili walipoona ile bima wakaanza kupuuza hivi. Akalazwa pale Sewahaji kwenye vigodoro hivyo vya mauti. Siku mbili bila kuhudumiwa eti wanaprocess bima yake mguu ukaanza kutoka funza. Baadae sana kapelekwa Moi, infections zimeshasambaa hadi kwenye vital organs, mguu wakaukata, too little too late, ndugu yangu kaondoka hivi hivi.

Now, nimejifunza jambo moja kuu kuhusu serikali hii:
- Katika Tanzania hii ya sasa chini ya utawala huu wa sasa, kila raia ajielewe this is survival of the fittest. Kama wewe ni raia wa kawaida, kitakachokuokoa ni Mungu wako tu. Usitegemee vyombo vyetu vya sasa vya huduma popote pale. Vipo pale kama ushahidi kwamba kuna ardhi fulani pale Afrika Mashariki na ni taifa huru likiwa na mtu pale Ikulu na vyombo vyote vya serikali. Lakini utendaji wake zero. Polisi ndo haohao majambazi na majangiri, hospitali ndo hizo hizo kama concetration camps za Hitler au death chambers magerezani, shule na vyuo vyetu vipo pale kama kutengeneza bongo low grade kama bidhaa za kichina, wabunge wetu ndo hao hao wachawi na waganga wa kienyeji. Kila kitu muhimu hovyo hovyo. Taifa gani hili?
 
Back
Top Bottom