PICHA: Chuki ya Dola dhidi ya wananchi inatoka wapi?

PICHA: Chuki ya Dola dhidi ya wananchi inatoka wapi?

Ilaa kusambaza picha za wachochezi sio uchochezi zaidi[emoji53][emoji53]?????
 
Ama kweli turtaona mengi mwaka huu... duh.. kosa "kudai utawala wa sheria" mbona kesi zingine vituko..
Mbona kujidhalilisha kumekuwa kwingi
 
Ninaomba ccm iache kutumia polisi kupambana na wananchi kwa jinsi isivyo halali.

Halii hii inamadhara mapana na maerfu kuliko yanavyoweza kudhaniwa na wapiga debe wa ccm mtandaoni.

Polisi wanawajibu wa kulinda watu na mali zao. Wanapashwa wawe rafiki wa watu wema ili wawe chombo kimoja.

Ninasikitishwa na baadhi ya wasemaji wa jeshi la polisi kuongea masuala mazito kwa wepesi usiomithilika. Wanasema suala la ulinzi ni kazi ya polisi hviyo raia hawahitaji kufanya ulinzi, bila kukukmbuka kwamba jeshi la polisi linaaskari wasiotosha kulinda kila raia ama kuwa katika sehemu zote Tanzania kwa wakti mmoja. Inavunja moyo na kuwaweka raia mbali na polisi.

Kitendo cha polisi kujibainisha kama kikundi cha utetezi wa ccm, kinaongeza kutokuaminiwa na kubaguliwa kwa jeshi katika jamii. Ninanomba uongozi wa jeshi letu, utathimini kama ni halali kulinda maslahi ya ccm na kuacha kusimamia ualama wa raia na mali zao.

Ninasikitishwa sana na mauji ya Askari wetu ambao hawana hatia. Wako katika kazi lakini wanashambuliwa na watu wenye nia ovu.

Ninaomba jeshi la polisi lisifanye maamuzi na tathimini za kisiasa kwamba eti vyama vya siasa ndiyo vinafanya haya. Huu ni udhaifu wa kulenga shabaha.

Historia ya Iraq, Syria, Libya, na kwinginevyo kote kulikovamiwa na makundi ya kigaidi, kulianza kwa kutumia fursa za serikali kupambana na wananchi wake.

Ni vizuri sana intelijensia ya polisi ikalitazama hili kwa umakini. Tumesikia na kuona clips kadhaa ambazo si za kudharau za watu kujiumba kigaidi. Hawa atu bila shaka wanaweza kutumia mwanya huu ambapo serikali imeelekeza nguvu kubwa katika kupambana na raia wasio kuwa na madhara yoyote kwa srikali, wakafanikisha malengo yao ya kigaidi kama ilivyokuw akwa nchi za wenzetu.

Hakuna uchochezi katiak kukumbushana kuheshimu katiba ambayo ndiyo kiongozi cha maisha ya Watanzania katika nchi yao. Ninadhani kama tunaona katiba iliyopo imepunguza madaraka ya maamuzi ya viongozi, ipekelwe miswada bungeni ili sheria zirekebishwe na zijumulishe maamuzi yote yanayotolewa na viongozi ni halali na hayatakiwi kuhojiwa.

Lakini pia, bado tunaweza kukubaliana kwa njia salama kwamba kuanzia sasa nchi hii itakuwa ni ya utawala wa kifalme na haitakuwa na raisi tena. Watu watajua na wataishi kwa mfumo huo.

Sasa tuna katiba, inapokosewa hairuhusiwi kuhojiwa, mwisho wake ni kujichanganya na kupoteza mwelekeo.

Ninaomba serikali isiendelee kuchukia raia na kuingia vitani na wananchi wasiokuwa na hata wembe mkononi. Kwa kufanya hivyo wanachochea chuki kati ya serikali na wananchi.

Ccm iache kutumia polisi kama jeshi la kulinda uhai wa chama. Kwa kufanya hivho ccm na polisi kwa umoja wao wanachochea chuki kati ya makundi ya kisiasa nchini. Na hii ni hatari kwa sababu, kunakuwa na tensions na kutuhumu wale wasiopendelewa na jeshi la polisi kuwa ndiyo wanaendesha uharifu.

Sasa tunasubiri kanusho la serikali juu ya mikutano ya siasa kutengeneza uhalifu baada ya hao waliokamatwa mbagala.

Lingine, ninaomba Jeshi letu la polisi liache kufanya kazi za ccm. Ccm ina makada wake kama vilivyo vyama vingine vya siasa. Waachwe ccm wajisimamie wenyewe polisi wasimame kama wlainzi wa usalama wa watu na mali zao. Ninawasiwasi mkubwa maadui wa taifa wanasoma nyendo zenu. Mnapokuwa mnajikita kufanya kazi za ccm, waharifu wanatumia huo mwanya kutekeleza uharifu kwa kuwa wanaona sasa mko busy kupigana na wapinzani wa ccm.

Ninaomba Jeshi la polisi liwahurumie vijana wetu wanaothirika na uharifu. Lirudi kwenye mstari, mjipange kupambana na uharifu ili kuziba mianya ya waharibu wanayoitumia pengine kwa kuona mnaeleekza nguvu kupigana na raia kwa maslahi ya ccm.

Jeshi la polisi liache kauli za kuwavunja mioyo raia kwamba ulinzi ni kazi ya polisi raia hawatakiwi wakati siyo kweli. Raia ndio wanaoishi na waharifu. Rudisheni utaratibu wa awali uliokuwa unamotivate raia kushirikiana na jeshi l apolisi katika kupambana na uharifu.
 
Huyo jesca mbona hajaweka kazi, au anafanya kazi zisizoruhusiwa kisheria..

Nawaza tu kwa sauti.
 
Amendika Comrade Malisa GJ

Anaandika Malisa GJ

Jeshi la Polisi wilayani Mbozi leo limemkamata Afisa wa Teknolojia ya Habari wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Nyasa) Mdude Nyagali kwa madai ya kuandika uchochezi katika ukurasa wake wa Facebook, kuhusiana na tukio la kuuawa kwa askari polisi wanne huko Mbande jijini Dar.

Mbali ya kumkamata Polisi wamempiga sana na kumvunja miguu yote miwili. Licha ya kumvunja miguu Polisi wamekataa kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu. Viongozi wa Chadema waliokusanyika katika kituo cha Polisi Vwawa aliposhikiliwa Afisa huyo wamekataliwa kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu.

Tangu asubuhi Polisi walipomkamata, wamekua wakimpiga na kumshinikiza kutoa maelezo juu ya taarifa za uchochezi anazodaiwa kuandika. Lakini Ndugu Mdude amekataa kufanya hivyo kwa madai kuwa hawezi kutoa maelezo yoyote hadi Mwanasheria wake afike. Kwa sasa Mwanasheria wa Chadema kanda ya Kusini anaelekea mjini Vwawa akitokea Mbeya ili kumsaidia Mdude kutoa maelezo.

Licha ya kumvuja miguu Polisi pia wamempiga sehemu nyingine za mwili na kumsababishia majeraha kadhaa, pia wamemchania nguo zake kitendo ambacho ni cha udhalilishaji.

#MyTake:
Nalaani vikali kitendo alichofanyiwa ndugu Mdude. Sio kwa sababu ni kada mwenzangu wa Chadema, ila ni kwa sababu nae ni binadamu. Ana haki ya kuheshimiwa na kulindiwa utu wake hata kama angekua CCM. Ukatili aliofanyiwa Mdude unapaswa kupingwa na kulaaniwa na kila binadamu mwenye utashi na akili timamu.

Pia nashauri Polisi waliohusika na ukatili huu wachukuliwe hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi kisha kushtakiwa. Hivi Polisi hawajui mtuhumiwa ana haki? Hivi Polisi hawajui maana ya "presumption of inocense" kwa mtuhumiwa? Kuna sababu gani ya kumpiga mtuhumiwa ambaye hajaonesha reaction yoyote?

Taarifa niliyopata ni kuwa Polisi walipofika nyumbani kwa Mdude walianza kumpiga kabla hata ya kumfikisha kituoni. Na walipomfikisha kituoni wakashirikiana kumpiga na hatimaye kumvunja miguu yote miwili. Uongozi wa CHADEMA wilayani Mbozi umeomba kumpeleka hospitali lakini umekataliwa. Pia baadhi ya viongozi wamepeleka magongo ktk kituo cha Polisi Vwawa angalau yamsaidie kusimama lakini polisi wamekataa kupokea magongo hayo.

Natoa wito wabunge wote wa Chadema mkoa wa Mbeya waungane kupinga unyama huu aliofanyiwa mwenzetu. Joseph Mbilinyi, Sophia Hebron, Silinde Ernest David, Pascal Haonga na Frank Mwakajoka najua mnanisoma hapa. Tafadhali chukueni hatua ya haraka dhidi ya ukatili huu. Hatuwezi kuendelea kuvumilia watu wetu wakifanyiwa uhuni wa kiwango hiki.

Ameuawa Kamanda Mawazo tukakaa kimya, wamekamatwa makamanda wengi na kubambikiziwa kesi tupo kimya, sasa wameanza kutuvunja miguu na kutufanyia unyama na ukatili usiovumilika. Hii si sawa hata kidogo. Tukinyamaza hata Mungu atatuhesabia dhambi.

Polisi wanapaswa kuheshimu sheria. Kama hawataki kuheshimu sheria kwa hiyari yao, tutawalazimisha kuziheshimu. Kazi ya polisi si kupiga na kuua. Kazi ya Polisi ni kulinda usalama wa raia na kuzuia uhalifu. Polisi haruhusiwi kutumia nguvu bila sababu. Hata ikifikia mahali pa kutumia nguvu sheria inasema iwe nguvu ya kawaida (reasonable force).

Lakini nguvu iliyotumika kwa Mdude sio reasonable. Wameenda nyumbani kwa Mdude wakiwa na silaha, wakamkuta hana hata fimbo lakini bado wakampiga. Huu ni upumbavu. Kwanini mtumie nguvu mahali pasipohitaji nguvu? Mlipaswa kumkamata na kumfikisha kituoni akiwa salama, kisha mumfungulie mashtaka mnayoona yanamfaa then mumfikishe majakamani.

Kwanini mumpige? Kwanini mnahukumu kabla ya mahakama? Kuanzia lini kazi ya Jeshi la Polisi imekuwa ni kuhukumu? Kwanini mnatumia mabavu kutesa raia? Kwanini hayo mabavu msiyatumie kupambana na wahalifu? Ona sasa mmemsababishia kamanda wetu ulemavu wa kudumu.

Hata kama atapona na kutembea tena lakini Mdude atakuwa mlemavu wa miguu kwa maisha yake yote. Kwahiyo hata ikitokea Mahakama ikimkuta hana hatia tayari atakuwa mlemavu. Hii si sawa kabisa....

Seriakali ya CCM isipoacha upuuzi huu wa kuona wapinzani ni magaidi itaangamiza hili taifa. Narudia kusema serikali ya CCM na vyombo vyenu vya dola acheni upumbavu. Takwimu za Umoja wa mataifa za mwaka huu zimeonesha wastani wa polisi kwa raia nchini ni 1:15000 yani askari mmoja anahudumia raia 15000. Hivi raia wakiamua kureact ni polisi gani atapona. Ni askari gani anaweza kusurvive kwenye nguvu ya raia 15000?? Hata awe na silaha za kivita hawezi kupona? Kwahiyo acheni ujinga. Hii nchi ni yetu sote. Msijione nyie mna haki kuliko wengine. Tumieni sheria kutekeleza kazi yenu sio kufanya kazi kwa mihemko ya kisiasa.!

Malisa G.J
 
..hapa Raisi amekosea.

..tatizo ni hawa wanaomhimiza aongeze UBABE na UKATILI dhidi ya vyama vya upinzani...
Nina wasi wasi sana. Mtuhumiwa anabaki na haki na heshima yake hadi atakapothibishwa na mahakama vinginevyo

Hata wenye hatia haki zao za msingi kama binadamu zinapaswa kulindwa

Hiki kinachofanyika ni katika kuwadhalilisha na kuwatia hofu wananchi

Nikijiuliza sana kwanini yatokee mauaji watu wengine wasikitishwe?
Kwa mwendo huu, peace and harmony ipo?

Sina tatizo na kukamatwa, nina tatizo na jinsi ubabe unavyovuka mipaka

Hili ni baya the least to say
 
Tanzania imelaaniwa, kudai demokrasia au rule of the law ni kosa?
 
hivi waziri wa sheria na katiba ana fanya kazi gani? kwa mtazamo wangu alipaswa kufukuzwa kazi mara moja...
 
Hawa polisi naona kuna UMUHIMU wa kuwapima akili..... Nini lengo la hizi picha??


LENGO LA MWANASIASA NI KUPATA PUBLICITY... HAWA POLISI WANASAIDIA KUWATANGAZA.
 
Back
Top Bottom