Mkuu advance nimesoma PCB so physics naielewa vizuri...mathematics na physics ni formula tu na derivations zake...ukielewa hivyo haikusumbui hata kidogoUmesoma kweli phys ya advance ww?
Phys ya advance unapoanza lazima uchezee 30,30 za kutosha halafu huko mbeleni ndo utaanza kupata A kama utajibidiisha maana topics za mbele ni nyepesi sana
Halafu kingine phys usiposoma kama ndo umeingia form five ukifundishwa kitu halafu usipitie ukija kusoma tena utaona as if mambo ni mapya kabisa na hujawahi kukutana nayo .
Sawa engineerBasi inaonekana ulikuwa mbovu sana kwenye phys
Yani hata electrostatic ilikuwa inakushinda??
Aisee ,am sorry to say but ulivamia kombi
Hizo wave,electrostatic na heat ni topics nyanya sana
At least hiyo electromagnetism ingawaje nayo ni nyepesi sana ila ina formula nyingi sana.
Kwenye ku prove lazima calculus na Trig uzijue inside out ndo utakuwa unapata pata maswali yake bila hivyo utasumbuka sanaMkuu maswal yanayonisumbua sana ni ya kuprove
Phys unapoanza form five lazima ikutese sana huo ndio ukweliDogo,
Watu watakwambia hiyo subtopic ni rahisi, But trust me Mechanics inahitaji Nguvu ya Ziada. Hiyo kitu hata Mimi ilinisumbua mwanzoni.. Badae nikaipatia.
Tafuta aliyeielewa akupumzikie hiyo utaiona rahisi tu..
Labda nikutoe wasiwasi
Hiyo projectile ina kaswali ka marks 5-10 kwenye paper 1,
Na huenda lisiwepo pia,
Kuwa focused,
Kuna topics rahisi (RAHISI MNO) form six kama Modern Physics, Umeme, Wave, Heat, Electronics ambazo ukizimaster Vizuri zitakupa 60% na hiyo mechanics ikakupa hata 20% basi ushatoboa.
Mechanics ni Pana sana na hupoteza Muda kwa wengi.
Nakushauri, unatakiwa kufauru pepa ya Form six, No matter what.
Hivyo basi Kuanzia LEO somea NECTA,
ikitokea unapata namba za Viatu kwenye pepa za Ndani hilo lisikukatishe Tamaa, ni Kawaida kwa hizi kombi zetu.
Narudia, Somea NECTA kuanzia leo, ndio elimu yetu ilivyo.
Mimi nlitoka NECTA na mitihani ya ndani sikuwahi pata 50%
Nlikuja kuwaacha midomo wazi raia kwenye Mock.
Dogo Chapa kazi.
Lastly, Discussions ni kila kitu. Chagua marafiki mnaofanana malengo,
Sisi tulikuwa na group la mtu tano,,tulikuwa tunafanya discussion kila siku kuanzia saa tisa usiku hadi saa moja Asubuhi, na wote tulitoboa.(wote kwa ufaulu wa One na two)
Phys unapokutana na swali kwa mara probability ya kulipata hilo swali ni ndogo sanaPhysics ya advance haitaki mihemko, unaweza maliza kusoma subtopic na ukafanya maswali 15 yote ukakosa, lakini kama uko makini, kila swali unalokosa lazima utambue wapi ulikosea, eventually mambo huenda sawa, usikate tamaa, kwa ufupi projectile motion ndio mteremko, vilima vinakuja
Sio kila kitu utakiweza kwenye maisha ya kujifunza...mfano mimi nilipomaliza mtihani wa tahosa nikalala mbele kisa ilikuwa Organic tu kwenye chemistry...lakini leo hii Fundi viatu maridadi sana hapa mitaa ya Posta.

Ni kitabu kizuri sana yaniRespicius kiiza???? over my dead body, nilikua sikipendi hiki kitabu na sikuwahi kitumia kabisaa
Habari wanajamvi ??
Wanajamvi mimi ni mwanafunzi niliyemaliza kidato cha nne mwaka jana(2016), ufaulu wangu katika masomo ya sayansi ni mzuri hivyo nina mipango ya kwenda Advanced level comb PCB au PCM
Lakini tangu nilipo anza kusoma physics yaani nakata tamaa maana kuna ki subtopic kinaitwa PROJECTILE MOTION yaana kila nikifanya swali lake nakosa. Please wanajamvi naombeni ushauri wenu katika somo hili.
Maana kubadilisha comb siwez sababu nilisoma TECHNICAL SCHOOL hivyo siwez soma comb za art wala CBG.
hata kuprove lazima uchore kwanza ndo yanakuwa mteremko... yaan kufanya bila kuchora ujue unajua sana.. ila kwa anayeelewa lazima aanze kwa kuchora..!Mkuu maswal yanayonisumbua sana ni ya kuprove