Nilivyopata Upofu na Uziwi Shuleni A -level pasipo kujua chanzo na kuwaambukiza Marafiki zangu wa karibu

singanojr

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
1,452
8,104
Habarini wanajamvi wa Jf

Natumaini wote wazima na ni wenye furaha, sitaki kuongea mengi Zaidi na kama uzi unavyojieleza na mimi leo nimeamua kuleta kwenu kisa changu hiki ambacho naamini kwa namna moja ama nyingine kinaweza kuwa na msaada mkubwa kwa baadhi ya watu, lakini pia huenda ushauri wenu hapa ukasaidia baadhi ya watu ambao huenda wanapitia hali kama niliopitia mimi.

Nitatumia muda wangu kuandika kisa hiki mpaka kiishe majina yote nitakayotumia sio ya ya kweli na nitasimulia mpaka mwisho kadri akili yangu itakavyoweza kuniruhusu kuendelea kuandika.

NB :Hii sio chai bali ni maji ya uhai.

Mwaka 2014 ndio mwaka ambao nilimaliza kidato cha nne ndani ya shule moja ya serikali inayopatikana mkoani Tanga Wilaya ya Lushoto..

Baada ya kufanya mtihani wa kidato cha nne na kumaliza salama nilikuwa nikijiamini sana kwamba nitafaulu na kwenda kidato cha tano , moja ya sababu ilionifanya nijiamini ni kutokana na kuwa na matokeo mazuri tokea nikiwa kidato cha kwanza , lakini pia namna mtihani nilivyoufanya.

Basi baada ya kukaa nyumbani miezi kadhaa hatimae matokeo yalitoka na kama nilivyotegemea niliweza kufaulu kwa ufaulu wa ‘Dinstiction’ Gpa ya 4.1 first class, kwa wale ambao mnakumbuka mwaka wetu wa 2014 matokeo yalikuwa yakipangwa kwa mfumo wa GPA.

Ilikuwa ni furaha kwangu kufaulu kwenda kidato cha tano na kwa wakati huu niliona ndoto zangu za kuwa Daktari zinakwenda kutimia.

Wakati wote wa masomo ya O-level nilikuwa nikiishi kwa Shangazi yangu aliekuwa akiishi Lushoto mjini kwani shule niliokuwa nikisomea ilikuwa ya Day na hata nilipomaliza kidato cha nne nilibakia hapo hapo kwa shangazi mpaka matokeo yalivyotoka , basi nilipongezwa hapa na pale na Baba shangazi na Shangazi mwenyewe kwa kufaulu , huku ndugu kutoka kijijini akiwemo mama yangu pia walinipongeza kwa kufaulu , Mzee alitutoka miaka kadhaa nyuma nikiwa Darasala nne hivyo nilikuwa na mzazi mmoja tu.

Basi baada ya miezi michache kupita hatimae selection zilitoka na nikachaguliwa kwenda shule moja iliokuwa ikiitwa Kantalamba , kusema ukweli sikujua kwanini nilichaguliwa hii shule kwani sikua nimeichagua , kombi niliochaguliwa ilikuwa ni PCM , shule ilikuwa huko Sumbawanga mkoa wa Rukwa .

Ndugu zangu akiwemo Shangazi Mkubwa Anaesimamia Mirathi yetu baada ya kuona nimetupwa mbali huko waligoma mimi kwenda shule hio kwani kulikuwa ni mbali sana , Baba Shangazi yeye alikuwa anakomalia niende huko huko, huku akifanya mpango wa kunihamishia shule za karibu, Baba shangazi yangu yeye alikuwa mwalimu mkuu wa shule flani hapo hapo Lushoto mjini na alikuwa na koneksheni ndio maana alitaka niende huko huko Kantalamba , lakini shangazi zangu wao walikomaa wakasema ni mbali na isitoshe kombi sio niliokuwa nikiitaka maana nilikuwa nnikitaka PCB.

Basi baada ya mazungumzo ya ndugu kuisha hatimae maamuzi yakawa niende Dar kwa baba mdogo yeye atanitafutia shule ya Private ,Ada haikuwa tatizo kutokana na kwamba mzee alikuwa mwalimu na mirathi yake ilitoka kipindi nikianza form one kwa hio pesa ilikuwepo .
Baba mdogo aliweza kupata shule kabla hata ya mimi kuanza safari ya kwenda Dar, shule aliopata ilikuwa ni ya jeshi maeneo flani hivi ya Mwenge

Nilipitia changamoto kubwa sana nikiwa ndani ya hii shule na hapa ndipo misukosuko ya kukatisha tamaa ilipoanzia ….. Inaendelea Baada ya dakika tano

Bonyeza kiungo kusoma kipande kinachofata

Sehemu ya Pili

Sehemu ya tatu
Sehemu ya nne
Sehemu ya tano
Sehemu ya sita
Sehemu ya saba
 
INAENDELEA
Basi baada ya maandalizi ya hapa na pale safari ya kwenda Dar ilianza , haikuwa mara yangu ya kwanza kufika Dar , siku nilioanza safari ilikuwa ni siku ya Alhamisi so baada ya kupanda basi kutoka Lushoto kwenda Dar na baba mdogo alitakiwa kunipokea Ubungo kwani sikuwa nikipafahamu kwake , yeye alikuwa akiishi Bagamoyo .

Muda wa saa Tisa ndio muda niliongia Dar na nikakutana na baba mdogo .

Tulifika Shuleni pale mida ya saa kumi na moja kasoro hivi tukaingia ofisini pale , ofisi yao iko poa tu ya kisasa , basi tukapokelewa pale vizuri tukachukua ‘joining instruction’ baba mdogo akaweka begi begani tukasepa , siku ya kuripoti ilikuwa kesho yake.

Basi tukafika kituo cha Shuleni pale kusubiria daladala zinazokwenda Bagamoyo gari zilikuwa zimejaa kweli maana ilikuwa ni Peak hours, watu wanarudi majumbani , wakati tukisubiria bahati nzuri kuna rafiki yake Baba mdogo alikuwa akitoka kazini na alituona pale kituoni na akasimamisha gari yake aina ya Spacio ya Deeb Blue kutupa Lift, muda ulikuwa umeenda ilikuwa ni saa kumi na mbili kama na nusu hivi za jioni nimechoka balaa na njaa inauma maana sikula njiani.
Baada ya dakika kadhaa tulikuja kufika sehemu ambayo nilikuja kujua inaitwa Mapinga , Rafiki yake baba mdogo alisimamisha Gari na kisha tukavuka upande wa kulia barabara ambayo inaelekea zahanati ya Mapinga na hapa ndio kulikuwa na shule ya msingi ,Baba mdogo aliokuwa akifundishia na yeye alikuwa mkuu wa shule hio ,hakunifikisha nyumbani kwake bali alinielekeza kwa kunionyesha kwamba niende nyumba inayowaka taa ndio nyumbani na kisha akaingia kwenye gari wakasepa , walikuwa wakienda Bar kula bata sikumind nilienda nikapokewa vizuri , uzuri ni kwamba nilikuwa nikifahamiana na watoto wa baba mdogo , kesho yake nikaenda Tegeta tukanunua mahitaji , tukalipia Ada CRDB tawi Kipo Complex tukatembea tena mpaka n upande wa kulie tukalipa Ada ya Hostel NBC pale na safari ya kwenda Shuleni ikaanza.

Baada ya kufika nilifata taratibu zote za usajili pale , baada ya kumaliza usaili baba mdogo akasepa , msajili akaniambia ni mtafute Afande Juma(sio jina halisi) mwalimu anaehusika na Hosteli anipe utaratibu , muda ulikuwa ni saa nane hivi , niliulizia baadhi ya wanafunzi na nikaambiwa Afande Juma yupo Mwembeni(Ni kaeneo hapo hapo Shuleni walimu wanapenda kurest hapo) , nilienda mpaka Mwembeni hii sehemu ilikuwa na vimbweta na walimu walikuwa wengi na wote walikuwa wanajeshi , nilivyofika pale nikasalimia kiupole kwa heshima ya hali ya juu maana nilikuwa na nidhamu ya woga hasa kwa wajeda.

“Namtafuta Afande Juma“

“Dogo wewe ni mgeni?”Aliuliza moja ya mwalimu licha ya kuniona na ‘Trunker’ na godoro.

“Ndio nahitaji kwenda Hosteli”

“Mwalimu Juma hapa hayupo mpaka ukanyoe kwanza hizo nywele”Aliongea na kunielekeza saluni ilipo nje ya geti, nikaacha vitu vyangu pale pale na kwenda kupiga kipara nikarudi naAfande Juma akajitokeza (Mwalimu Juma muda wote alikuwepo hapo) alimwita dogo flani hivi wa O- level anipeleke hosteli.

Hosteli ilikuwa ikijitegemea na shule ilikuwa ikijitegemea , yaani kama mwalimu hahusiki na Hosteli hajishughulishi nako , ukienda hosteli unavuka geti , kule hosteli kuna ukuta ambao unaanzia mwanzo wa eneo la shule unakuja kupakana na ukuta wa Kambi ya jeshi.

Hosteli za wavulana pale zimetenganishwa na Kota za wanajeshi pale , Mazingira ya pale yalikuwa Bomba kabisa , ndani ya eneo la Hosteli kuna kiwanja cha Mpira kikubwa tu ,Vollebal Pitch,Basketball Pitch ,Netball Pitch .Eneo La hostel lilikubwa kubwa tu.

Hosteli za wasichana nazo pia zilikuwa Bomba tu Mazingira safi in short Accomodation ilikuwa safi japo sio sana ila afadhari.

Basi nikapewa Room pale , kiongozi akanikabidhi kwa Jamaa mmoja hivi aliekuwepo hapo ndani ya Chumba alikuwa peke yake na chumba kilikuwa na jumla ya watu wawili tu wanaolala,Nikasalimiana na mshikaji pale nikamuuliza vipi mambo ya simu , maana nilimkuta jamaa anachat , jamaa akaniambia simu wanatumia kibabe ,Huyu mshikaji yeye alikuwa alikuwa akisoma kombi ya KLF ni kidato cha tano kama mimi ila yeye aliwahi kufika na ana miezi Zaidi ya mine hapo shuleni.

Basi baada ya kuweka Godoro langu na kutandika kitanda kengere iligonga na jamaa akaniambia ni kengele ya usafi hio , hivyo nikaongozana nae na kwenda , tulikuwa tumechelewa kiasi kufika eneo la Assemble so nilikuta pale kiongozi anawapigisha wanafunzi wa Form Six PushUp , nilishangaa maana lilikuwa swala geni kwangu kuona kiongozi wa O-Level kuwapa adhabu Advance.
Basi baada ya kupigishwa kwata pale za kulia kushoto na kurukaruka kiongozi alitoa maagizo ya watu kufanya usafi , lakini wakati akiendelea kutoa maagizo alikuja mwalimu pale ,ambae nilikuja kumjua ni Mwanajeshi pia mwenye nyota Tatu(Captain).

Baada ya kuja pale alitoa simu yake ya Smart pale na kisha kutembea upande wa wanafunzi wa O-level na kuwakagua na ndani ya dakika alianza kuchomoa wanafunzi na kuwaambia wapige magoti mbele ,Tension ilikuwa kubwa na mimi kwakuwa ni mgeni sikuelewa kinachoendelea .

Baada ya kumaliza kukagua alisogea mbele na kuanza kutoa matangazo na akasema wanafunzi waliokuwa mbele alikutana nao Ambiance Sinza(kwa wale wasiojua Ambiance ni sehemu ambayo madada poa yanapatikana) akasema kwamba baada ya kuwaona akapiga nao Selfie kuweka kumbukumbu vizuri.
Wajamaa walichezea kibano sio poa , ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ndani ya hii shule lakini kwa pigo nilizoona hapo nilianza kujutia maamuzi yangu ya kuja kusomea hapa.

Msosi wa pale kusema ukweli wajeda walikuwa wanajitahidi sana , chakula kisafi na kitamu .

Siku iliofata nikakutana na jamaa ambae anakaa kwenye chumba hiki nilichopangiwa maana tokea niingie sikumuona , jamaa baada ya kusalimiana nae ile asubuhi jamaa akaanza kunitishia kuhusu fimbo na mimi niliyachukulia maneno yake siriasi kutokana jana yake tu nilishuhudia , lakinii sikuogopa sana, nilijiapiza kwamba nitatii sheria kadri ya uwezo wangu ili kuepuka vibano.
Basi wakati jamaa anaendelea kunipump na upepo wa woga pale walikuja na marafiki zake wengine kuendelea kunijaza woga , ila mimi nikawaambia kuwa nitakuwa mtiifu na niliwaambia walimu wanatoa adhabu kwa watu wenye makosa, hivyo nikawaambia mimi siwezi chapwa kizembe maana nitakuwa mtiifu , wakacheka na wakaniambia wewe huelewi na mbishi kama Kunguni na kweli nilikuwa sielewi mpaka lisaa limoja mbele haha..
Kengere ya kuhesabiwa iligongwa , hapa ilikuwa ni Jumamosi asubuhi , baada ya kuhesabiwa pale tukapewa maelekezo wa kwenda kumwagilia maua nje ya Shule, haya ni maua ya pale Bagamoyo Road ukipita hata saivi utayaona sasa hivi yamekuwa makubwa na pamendeza , sasa wakati naanza kidato cha tano yalikuwa ndio yanapandwa na tuliyamwagilia sana maji .

Tulibeba ndoo zetu , maji tulikuwa tukichukulia shuleni kule na kuvuka barabara na kunyweshea, sasa mimi na wajamaa flani tulikuwa wa mwisho kwenda kuchota maji , wakati tunafika eneo la kuchota maji mimi nikiwa mtu wa mwisho kuchota , mara kuna gari aina ya X-trail pale iliingia, sasa hatukusubiri gari ile isimame sisi tukasepa , lakini ile tunataka kukata kona tukaitwa, alikuwa ni Afande pia wa Nyota tatu tena alikuwa na Gwanda kabisa na alionekana anatoka Shift huyu alikuwa ni afande anaehusika na kuwasimamia wanafunzi wa O-level.
Akatuuliza kwanini hatujasimama na kumsalimia , hakuwa na majibu kati yetu , tukaambiwa kunja ngumi na kuna jamaa akaagizwa fimbo pale , fimbo ikaja nikapewa zangu sita safii nikakumbushwa kuwa nipo shule ya jeshi.

Wajamaa baada ya kuniona nimelambwa Sita tena siku ya pili baada ya kuripoti walicheka na wakaniambia hayo ndio tuliokuwa tukikwambia , nilicheka na kuwaambia wameshinda.

Eniwei mambo hayo ya fimbo hayahusiani sana na kisa hiki ila nimejaribu kuonogesha .

Wakati nafika hapa hapa shuleni nilikuwa mzima wa Afya kabisa sikuwa na shida yoyote ile , nitajaribu kufupisha ili twende sawa.
Itaendelea

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
INAENDELEA
Basi nilianza masomo , licha ya kwamba nilikuwa nimechelewa kuripoti kwani wenzangu walikuwa wamefika tokea mwezi wa tatu na mimi ndio kwanza mwezi wa Saba ndiio niliripoti , kitabu kilikuwa kigumu kwa kiasi chake , na maisha ya shule nilianza kuyazoea na kuona mazingira ya kawaida tu , isitoshe pia shule ilikuwa na mambo mengi ya kuvutia pale maana Ni shule iliokuwa ikithamini sana vipaji so Event zilikuwa nyingi sana na hili lili cheer up sana wanafunzi na kuzoea mazingira haraka.

Ni baada ya semista ya kwanza kuisha tulifunga shule vyema , mitihani yangu ya kwanza nilikuwa nimefanya vyema tu licha ya kwamba nilichelewa kuripoti ,nakumbuka nilikuwa mtu wa kumi baada ya matokeo kutoka , semista ya pili ilianza kwa spidi kubwa , maana tulikuwa na mtihani wa mchujo wa kuingia Six na ile shule ukishindwa kufikisha wastani wao hawana huruma , unahama shule au unakuwa Private Candidate

Hivyo along na wanafunzi wenzangu tulikomaa sana , japo masomo yalikuwa magumu lakini hakukuwa na namna Zaidi ya kukomaa , nilipima ufaulu wangu kupita Test na niliona nafanya vizuri na nitatoboa kwenye mchujo

Ilikuwa ni mwezi wa nne hivi katikati ndio mambo yalipoanza kunibadilikia , ilikuwa ni siku ya jumatatu niliamka asubuhi nikiwa mgonjwa sana , joto lilikuwa juu , kichwa kilikuwa kinauma hatari nilishindwa hata kuhudhuria vipindi na kwenda moja kwenye Zahanati ya shule kwa ajjili ya matibabu na nikagundulika na Maralia , so nikapewa ALU na kurudi hosteli kupumzika, baada ya siku mbili hali ilitulia na nikarudi darasani na hapa ndipo niliposhangaa mabadiliko niliokuwa nayo.
Ilikuwa ni kipindi cha Physics asubuhi hio wakati naingia Class lakini cha kushangaza ni kwamba mwalimu alikuwa anafundisha lakini alichokiandika ubaoni nilikuwa sikioni , niliona labda ni swala la kawaida kwakua nilikuwa nimekaa nyuma so nikachukiua kiti na kusogea mbele , lakini hali ilikuwa vile vile sikuwa nikiona ubaoni, nilikuwa ‘ghastly pale’ kwa mabadiliko yangu kwenye upande wa macho , kipindi kilianza mpaka kikaisha sikuwa nimeelewa hata na sikuona ubaoni .

Nikapotezea nikasema labda ni swala la kawaida , lakini ukweli halikuwa la kawaida kwani siku nzima sikuona chochote ubaoni na sikuelewa kilichofundishwa , kesho yake ikawa hivyo hivyo na sasa haikuwa kutokuona ubaoni tu ni kwamba nilishindwa hata kutambua watu waliokuwa mbali na mimi , yaani nilikuwa na uwezo wa kumuona mtu kwa mbali lakini kumtambua kwa sura nilikuwa nikishindwa , nikamwambia moja ya marafiki zangu kuwa sioni ubaoni akaniambia labda ni ishu ya kawaida tu itapita nikakaa wiki , ikawa hivyohivyo na hapa nikawa agitated na kuona hili sio swala la kawaida and I need to be serious to solve the situation maana sikuwa sasa nikisoma na hili swala linaingilia masomo yangu na mtihani wa mchujo wa mwisho wa muhula ulikuwa near around the corner..

Nilikuwa na simu , nilirudi nayo likizo so mtu wa kwanza niliewaza kumpigia simu na kumueleza swala langu ni Aunt wangu wa Lushoto, nilimfikiria yeye maana nilikuwa nimemzoea sana na alikuwa kama mzazi kwangu licha ya kwamba shuleni hapa nililetwa baba mdogo.

Nilimweleza na akasikitika , ila akaniambia niende Kijichi kwa Aunt yangu mwingine atanisaidia ,so nikaaga shuleni nikasepa kwa Aunt , hii siku ya kwenda kijichi ilinisumbua sana maana hata magari nilishindwa kusoma pale mbele kwamba gari lilikuwa likienda wapi , so nilitegemea masikio tu.

Nilifika kwa Aunt nikamweleza shida yangu ,Aunt yangu ni Daktari mstaafu na alikuwa akifahamiana na moja wa madaktari wa macho Zakiem , so baada ya kuwasiliana nae akaambiwa niende kesho , so siku iliofata Aunti akanipeleka asubuhi nikapigwa pale na kisha akanichongea miwani ya Macho pale tukalipia palepale tukasepa , sasa jambo la kushangaza nimevaa miwani lakini sikuwa nikiona vilevile , nikaona huu ujinga kesho narudi pale maana niliona dokta ni kama amekula pesa yetu bure licha ya kwamba hela hio ilikuwa ikienda kwenye mapato ya serikali lakini sikutaka kukubali hela ipotee bure.

Kichekesho ni kwamba tulitumia kila aina ya miwani pale sikupata afadhali , ila akanipima tena na akanipa vidonge vya Vitamin pale na kuniambia nirudi baada ya mwezi kwa ajili ya Follow up .

Nilirudi shule maana niliona na Slack off sana na sikuwa serious na masomo so nikarudi shuleni na sasa hapa sikuwa nikienda class Zaidi ya kwenda Library kila asubuhi kujisomea maana nikienda class sikuwa nikiona , nilikuwa anikienda kipindi cha Bios tu maana kusikiliza tu ilikuwa inatosha na afande aliekuwa anafundisha somo la Bios alikuwa vyema sana , japo nilipata shida kwenye michoro kwani bado nilikuwa sioni.

Baada ya wiki kuisha hali , hali yangu kutoona ikaisha ghafla tu , nikafurahi , lakini wiki nyingine tatizo likarudi nikawa sioni karibu , yaani nashindwa hata kuelezea lakini ilikuwa hivi , nilikuwa nikishika daftari nikianza kusoma ghafla maandishi yanakuwa ‘Blurr’ na baada ya dakika kadhaa hivi unaona maandishi kwenye kitabu yanacheza cheza halafu yanapotea , nilikuwa Frustrated maana nilishindwa kusoma kabisa na mbaya Zaidi muda unaenda halafu Physics ninatopic ambazo sijapitia bado masmo mengine kama BAM ambayo nilikuwa nikisolve wiki za mwisho mwisho , nakumbuka hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba nikaenda kutafuta simu niwasiliane na Aunt tena, lakini jambo la kuhudhunisha ni kwamba nilishindwa kuweka vocha , lakini sio hivyo tu hata simu ilinishinda kutumia maana sikuwa nikiona hata Menu ya simu wala majina ,nilijishangaa mpaka nikajisema kwamba bora kutokuona ubaoni kuliko kutokuona maandishi , mbaya Zaidi tulikuwa na wiki mbili tu ya kuingia kwenye mtihani wa mwisho wa muhula.

Nilifanikiwa kuwasiliana na Aunt na yeye akawa hana cha kufanya , alichonishauri tu ni kwamba niende hospitali huku yeye anafanya maombi maana alikuwa mlokole,Yeye alikuwa anaamini nachezewa , lakini kwa upande wangu akili ilikuwa nzito na sikuwa nikiamini kabisa katika maswala ya kichawi na niliona tatizo langu ni la kibailojia tu.

Soon Itaendelea

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
INAENDELEA
Basi baada ya wiki moja kupita Mungu akasaidia hali yangu ya kutokuona karibu ikapita na hata pia mbali nilikuwa nikiona vizuri japo sio sana lakini nilishukuru.
Basi nilianza kula pindi kwa spidi zote maana nina wiki chache tu za kujiandaa na mtihani wa mwisho wa mwezi wa Tano kukamilisha muhula.

Basi baada ya kama siku tano hivi zilipita , ilikuwa ni siku ya ijumaa nikiwa zangu Library napiga msuli na rafiki yangu mmoja hivi msukuma,Mida kama ya jioni hivi saa kumi na moja kama na nusu hivi , alikuja dogo flani wa O-level , alionekana alikuwa akitutafuta na mazungumzo yake baada ya kutufikia yalikuwa hivi.

“Braza kuna wadada Flani hivi wageni wanamtafuta Deusi Mathayo”

Rafiki yangu huyu alikuwa akiitwa Deus Steven(sio jina lake halisi), hivyo huyu dogo kuja kwetu ni kutokana na kwamba alikuwa amemkosa mtu anaeitwa Deus Mathayo.

“Mimi naitwa Deusi Steven sio Deusi Mathayo”Aliongea rafiki yangu.

“Braza hao wadada wanasema wanaemtafuta ndio Deusi Mathayo na kwa maelezo yao wanasema Deusi anaishi hosteli , lakini nimuelizia bwenini hakuna mtu anaeitwa Deus Mathayo hivyo washikaji wakaniambia labda itakuwa ni wewe hao wadada wamechanganya majina ndio maana nimekuja labda ukawa unawajua , au kama vipi ukaonane nao”.

“Hao wadada wakoje?” Jamaa yangu akauliza .

“Mmoja ni rangi mchanganyiko kama muarabu hivi na mwingine ni mweupe mrefu , hawajaniambia majina yao”.

“Ni Warembo?”Aliuliza Msukuma haha.. alikuwa akipenda warembo sana huyu jamaa na moja ya kitu kinachonichekesha nikiwa nae ni lafudhi yake iliojaa usukuma.

“Ndio broo huyo shombeshombe ni mzuri hatari”.

“Basi ngoja nikaonane nao”Msukuma akaniambia nimsindikize tukawaone hao wadada , akaniambia kama ni wabovu tunaachana nao hata siwasogelei nikamwambia poa.

Dogo akaongoza njia ya kwenda hosteli maana muda huu tulikuwa shuleni huku madarasani , baada ya kufika hosteli , wadada wenyewe walikuwa wamejificha upande wa kota za wanajeshi , walikuwa na aibu hatari maana eneo walilokuwepo lilikuwa ni hosteli za wavulana.

Basi baada ya kuwafikia pale na kuwaona aisee walikuwa wazuri balaa hasa huyu shombeshombe,kusema ukweli mimi sikuwa nikijiamini sana mbele ya wanawake so kazi niliacha kwa Msukuma maana alikuwa akijiamini sana , jamaa alikuwa thick skinned , hakuwa na aibu.
Jamaa akaniambia Mwanangu Jr hawa watoto ni wazuri hatari siwaachi hata kama mimi sio mtu wanaemtafuta nikamwambia itakuwa vyema.

“Naitwa Deusi Mathayo nimepata taarifa mnanitafuta”Nilitamani kucheka , msukuma alikuwa na mambo ya ajabu kweli maana alichofanya ni kubadilisha jina lake kutoka Deusi Steven kwenda Deusi Mathayo,Tatizo ni kwamba wale wadada hawakuwa wakimjua wanaemtafuta kwa sura.

Basi wale wadada wakacheka pale maana Jamaa yangu alikuwa mcheshi balaa , lakini mwishowe wakasema sio yeye wanaemtafuta , tukawauliza mnamtafutaje jamaa msiemjua ndio Shombeshombe akatuambia kuwa rafiki yake katongozwa na huyo Deusi lakini hawajawahi kuonana , lakini pia maelekezo yake akasema kuwa Deusi alijitambulisha kuwa anasoma hapo Shuleni na pia anakaa Tabata Segerea na Kwa maelezo ya Deusi ni kwamba wao ni majirani hivyo wamekuja hapo ili kumfahamu. Kifupi ilionekana wanahamu sana ya kumuona Deusi , lakini Deusi hakuonekana na haraka haraka tulijua lazima hawa wadada wamedanganywa jina.

Tuliongea nao mpaka Kengele ya Msosi ,saa kumi na mbili na nusu ilipogonga so tukataka kuachana nao.
Hawa wadada in short walikuwa ni wanafunzi kutoka shule moja ya Islamic iliokuwa maneo ya Ubungo na muda huo pia walikuwa wamevaa Uniform za rangi flani hivi ya Zamabarau(wote walikuwa wamevaa juba).

Huyu ShombeShombe baada ya kutuona tunaondoka akaniita …

“Kaka unaitwa nan?”

“Naitwa Jr”.

“Ijumaa nitakuja kukusalimia”

Nikashangaa lakini nikamjibu kuwa hakuna noma akija atanikuta , ila kwangu nilichukulia labda anafanya utani tu hakuwa akimaanisha kwa hio nikapotezea pale pale na kusahau lile swala , lakini sikusahau uzuri wake yule mdada.

Basi siku hio ikapita , zikaisha siku kama saba hivi , siku hio kulikuwa na mechi kati ya Shuleni kwetu na Kibiti , ilikuwa ni siku ya ijumaa , hii mechi ilikuwa ya moto sana na hii ni kutokana na aina ya ushangiliaji wa wanafunzi wa Kibiti licha ya kuwafunga bao nyingi mno , nakumbuka tuliwafunga kumi na mbili , lakini spirit yao ya kushangilia haikukoma.

Sasa wakati nikiwa nimenogewa na Gemu licha ya kwamba sikuwa nikiona vizuri , alikuja jamaa flani hivi wa A-Level wa Day Sikujuia hata kombi yake maana wanafunzi pale ni wengi sana akaniambia Bro kuna mdada anaitwa Naira(sio jina lake halisi) anakutaita , nikashangaa maana sikuwahi kusikia hilo jina kabla so nikamuuliza jamaa una uhakika ni mimi ninaeitwa , akaniambia wewe sio ndio Jr nikamwambia ndio, akaniambia basi ni wewe unaeitwa.

Nikaona niongozane na jamaa tu , japo nilikuwa na uhakika kwamba jamaa kakosea , nilidhania hivyo kutokana mimi nimoja ya wanafunzi ambao hatukuwa tukitembelewa.

Basi baada ya kutembea mpaka nyuma ya Mesi barabarani ndipo nilipomuona mwanafunzi aievalia Juba , Aisee sikuamini na nilikuwa nimesahau kabisa yaani kwamba nina miadi , na kilichofanya nisahau ni kwamba hawa wadada siku ile tunaonana nao licha ya kuniambia atakuja sikuchukulia siriasi kama atakuja kweli.
Siku hio alikuwa peke yake hakuwa na yule rafiki yake aliekuja nae wiki iliopita, baada ya kumsogelea nikamuuliza kumbe unaitwa Naira , akatabasamu akasema ndio , ile siku wakati tunakutana nao hata hatukuwaliza majina.

Basi tukatafuta eneo la kukaa tukakaa huku nikimwambia kuwa nilijua siku ile anaongea utani , akaniambia huwa hatoagi ahadi za uongo, anaspeaking Scent hivi ya kiarabu lakini mara nyingi alikuwa akichanganya maneno na kingereza

Ukweli siku hii sikuwa hata nikijua nisema nini maana nilikuwa moja ya wanafunzi madomo Zege,Kwakuwa muda umeenda nikamwambia tutembee kuelekea kituoni ili asichelewe , maana ilikuwa saa kumi na mbili hivi halafu alikuwa akikaa Tabata Bima.

Katika stori za kufahamiana nae nilijua kwanza baba yake alikuwa hayupo hapa nchini aalikuwa akiishi nchi moja ya Afrika ambayo haikuwahi kutawaliwa na baba yake ni Arabs Pure na hapa Bongo alikuwa akiishi na mama yake tu mwenyeji wa Handeni Tanga ,pia nilikuja kujua kwamba na yeye yupo kidato cha tano HGE.

Huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana na Naira shombeshombe, alitokea kunipenda balaa , kila ijumaa alikuwa akija kunitembelea na zawadi mbali mbali , washikaji walikuwa wakiona wivu balaa, Ubaya tu ni kwamba hakuwa na simu so hatukuwa na mawasiliano na kama ijumaa haji basi lazima anitumie kimemo kutoka kwa washikaji wa Day.

Huyu dada ni mhanga wa kwanza kupata tatizo la kuona na kutokusikia

Sasa siku za mtihani zikiwa zinakaribia , macho yangu yalikuwa angalau yalikuwa yanaona vizuri lakini sasa tatizo lingine likaibuka , washikaji walikuwa wakinilaumu sana kwamba nina dharau , kwani walikuwa wakiniita nilikuwa nikawakaushia na moja ya watu waliokuwa wakinipa tuhuma hizo ni Msukuma , lakini mimi nilijitahidi kujitetea kwamba sikuwasikia waliponiita.

Sasa ikawa kero sasa kwani ilikuwa ni Zaidi ya wiki Napata hizi lawama na hapa ndipo nilipokuja kugundua kuwa uwezo wangu wa kusikia umeshuka sana kwa kiasi kikubwa , na kilichonifanya nifahamu hivyo ni kwamba siku moja mwalimu wa Physics aliingia kufundisha , huyu mwalimu sauti yake ina base so sikuweza kumsikia kipindi chote.

Nilijaribu kuziba sikio moja na kidole likawa linasikia japo sio sana , nikaziba sikio lingine likawa limeniziba kabisa , nilishangaa sana na kuogopa nini kinanitokea, kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndio hali ilizidi kuwa mbaya nikawa sisikii kabisa , yaani sauti ikawa inakuja kwa mbaali sana, lakini pia tatizo langu la kutokuona mbali likarudi upya.

Ukweli nilitamani kulia , ila nilijikaza kibabe huku nikijjipa matumaini kuwa huenda ni tatizo la kawaida tu na nikienda hospitalini litaisha , hivyo kwakuwa muda uliokuwa ulikuwa ni kama wiki moja hivi niliona nikomae kwanza na mtihani na swala la afya yangu nitalishughulikia baada ya pepa.
Itaendelea Soon

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
INAENDELEA
Basi baada ya maandalizi ya hapa na pale safari ya kwenda Dar ilianza , haikuwa mara yangu ya kwanza kufika Dar , siku nilioanza safari ilikuwa ni siku ya Alhamisi so baada ya kupanda basi kutoka Lushoto kwenda Dar na baba mdogo alitakiwa kunipokea Ubungo kwani sikuwa nikipafahamu kwake , yeye alikuwa akiishi Bagamoyo .

Muda wa saa Tisa ndio muda niliongia Dar na nikakutana na baba mdogo ,Baba mdogo alikuwa mwalimu wa shule ya msingi na sifa yake kubwa ilikuwa ni ubahili , alikuwa mpare halisi , tulipokutana hapo Ubungo akanambia kwamba hana hela ya nauli kwa hio yeye atabeba Begi na tutapiga Raba kwenda kupandia gari kutuo cha Shuleni(Shule sitaitaja jina lake halisi lakini nitaiita Shuleni)

Hii shule sikuwa nikiijua ilipo so nilisema poa maana sikuwa nimechoka sana , lakini tulivyoanza safari ndio niliona umbali wake maana tulitembea si mchezo mpaka tunakuja kufika Mwenge ni kama lisaa hivi tumetumia , lakini kutokana na kwamba nilikuwa nimezoea kutembea sikuwa na shida na sikuchoka kiviile .

Tulifika Shuleni pale mida ya saa kumi na moja kasoro hivi tukaingia ofisini pale , ofisi yao iko poa tu ya kisasa , basi tukapokelewa pale vizuri tukachukua ‘joining instruction’ baba mdogo akaweka begi begani tukasepa , siku ya kuripoti ilikuwa kesho yake.

Basi tukafika kituo cha Shuleni pale kusubiria daladala zinazokwenda Bagamoyo gari zilikuwa zimejaa kweli maana ilikuwa ni Peak hours, watu wanarudi majumbani , wakati tukisubiria bahati nzuri kuna rafiki yake Baba mdogo alikuwa akitoka kazini na alituona pale kituoni na akasimamisha gari yake aina ya Spacio ya Deeb Blue kutupa Lift, muda ulikuwa umeenda ilikuwa ni saa kumi na mbili kama na nusu hivi za jioni nimechoka balaa na njaa inauma maana sikula njiani.
Baada ya dakika kadhaa tulikuja kufika sehemu ambayo nilikuja kujua inaitwa Mapinga , Rafiki yake baba mdogo alisimamisha Gari na kisha tukavuka upande wa kulia barabara ambayo inaelekea zahanati ya Mapinga na hapa ndio kulikuwa na shule ya msingi ,Baba mdogo aliokuwa akifundishia na yeye alikuwa mkuu wa shule hio ,hakunifikisha nyumbani kwake bali alinielekeza kwa kunionyesha kwamba niende nyumba inayowaka taa ndio nyumbani na kisha akaingia kwenye gari wakasepa , walikuwa wakienda Bar kula bata sikumind nilienda nikapokewa vizuri , uzuri ni kwamba nilikuwa nikifahamiana na watoto wa baba mdogo , kesho yake nikaenda Tegeta tukanunua mahitaji , tukalipia Ada CRDB tawi Kipo Complex tukatembea tena mpaka n upande wa kulie tukalipa Ada ya Hostel NBC pale na safari ya kwenda Shuleni ikaanza.

Baada ya kufika nilifata taratibu zote za usajili pale , baada ya kumaliza usaili baba mdogo akasepa , msajili akaniambia ni mtafute Afande Juma(sio jina halisi) mwalimu anaehusika na Hosteli anipe utaratibu , muda ulikuwa ni saa nane hivi , niliulizia baadhi ya wanafunzi na nikaambiwa Afande Juma yupo Mwembeni(Ni kaeneo hapo hapo Shuleni walimu wanapenda kurest hapo) , nilienda mpaka Mwembeni hii sehemu ilikuwa na vimbweta na walimu walikuwa wengi na wote walikuwa wanajeshi , nilivyofika pale nikasalimia kiupole kwa heshima ya hali ya juu maana nilikuwa na nidhamu ya woga hasa kwa wajeda.

“Namtafuta Afande Juma“

“Dogo wewe ni mgeni?”Aliuliza moja ya mwalimu licha ya kuniona na ‘Trunker’ na godoro.

“Ndio nahitaji kwenda Hosteli”

“Mwalimu Juma hapa hayupo mpaka ukanyoe kwanza hizo nywele”Aliongea na kunielekeza saluni ilipo nje ya geti, nikaacha vitu vyangu pale pale na kwenda kupiga kipara nikarudi naAfande Juma akajitokeza (Mwalimu Juma muda wote alikuwepo hapo) alimwita dogo flani hivi wa O- level anipeleke hosteli.

Hosteli ilikuwa ikijitegemea na shule ilikuwa ikijitegemea , yaani kama mwalimu hahusiki na Hosteli hajishughulishi nako , ukienda hosteli unavuka geti , kule hosteli kuna ukuta ambao unaanzia mwanzo wa eneo la shule unakuja kupakana na ukuta wa Kambi ya jeshi.

Hosteli za wavulana pale zimetenganishwa na Kota za wanajeshi pale , Mazingira ya pale yalikuwa Bomba kabisa , ndani ya eneo la Hosteli kuna kiwanja cha Mpira kikubwa tu ,Vollebal Pitch,Basketball Pitch ,Netball Pitch .Eneo La hostel lilikubwa kubwa tu.

Hosteli za wasichana nazo pia zilikuwa Bomba tu Mazingira safi in short Accomodation ilikuwa safi japo sio sana ila afadhari.

Basi nikapewa Room pale , kiongozi akanikabidhi kwa Jamaa mmoja hivi aliekuwepo hapo ndani ya Chumba alikuwa peke yake na chumba kilikuwa na jumla ya watu wawili tu wanaolala,Nikasalimiana na mshikaji pale nikamuuliza vipi mambo ya simu , maana nilimkuta jamaa anachat , jamaa akaniambia simu wanatumia kibabe ,Huyu mshikaji yeye alikuwa alikuwa akisoma kombi ya KLF ni kidato cha tano kama mimi ila yeye aliwahi kufika na ana miezi Zaidi ya mine hapo shuleni.

Basi baada ya kuweka Godoro langu na kutandika kitanda kengere iligonga na jamaa akaniambia ni kengele ya usafi hio , hivyo nikaongozana nae na kwenda , tulikuwa tumechelewa kiasi kufika eneo la Assemble so nilikuta pale kiongozi anawapigisha wanafunzi wa Form Six PushUp , nilishangaa maana lilikuwa swala geni kwangu kuona kiongozi wa O-Level kuwapa adhabu Advance.
Basi baada ya kupigishwa kwata pale za kulia kushoto na kurukaruka kiongozi alitoa maagizo ya watu kufanya usafi , lakini wakati akiendelea kutoa maagizo alikuja mwalimu pale ,ambae nilikuja kumjua ni Mwanajeshi pia mwenye nyota Tatu(Captain).

Baada ya kuja pale alitoa simu yake ya Smart pale na kisha kutembea upande wa wanafunzi wa O-level na kuwakagua na ndani ya dakika alianza kuchomoa wanafunzi na kuwaambia wapige magoti mbele ,Tension ilikuwa kubwa na mimi kwakuwa ni mgeni sikuelewa kinachoendelea .

Baada ya kumaliza kukagua alisogea mbele na kuanza kutoa matangazo na akasema wanafunzi waliokuwa mbele alikutana nao Ambiance Sinza(kwa wale wasiojua Ambiance ni sehemu ambayo madada poa yanapatikana) akasema kwamba baada ya kuwaona akapiga nao Selfie kuweka kumbukumbu vizuri.
Wajamaa walichezea kibano sio poa , ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika ndani ya hii shule lakini kwa pigo nilizoona hapo nilianza kujutia maamuzi yangu ya kuja kusomea hapa.

Msosi wa pale kusema ukweli wajeda walikuwa wanajitahidi sana , chakula kisafi na kitamu .

Siku iliofata nikakutana na jamaa ambae anakaa kwenye chumba hiki nilichopangiwa maana tokea niingie sikumuona , jamaa baada ya kusalimiana nae ile asubuhi jamaa akaanza kunitishia kuhusu fimbo na mimi niliyachukulia maneno yake siriasi kutokana jana yake tu nilishuhudia , lakinii sikuogopa sana, nilijiapiza kwamba nitatii sheria kadri ya uwezo wangu ili kuepuka vibano.
Basi wakati jamaa anaendelea kunipump na upepo wa woga pale walikuja na marafiki zake wengine kuendelea kunijaza woga , ila mimi nikawaambia kuwa nitakuwa mtiifu na niliwaambia walimu wanatoa adhabu kwa watu wenye makosa, hivyo nikawaambia mimi siwezi chapwa kizembe maana nitakuwa mtiifu , wakacheka na wakaniambia wewe huelewi na mbishi kama Kunguni na kweli nilikuwa sielewi mpaka lisaa limoja mbele haha..
Kengere ya kuhesabiwa iligongwa , hapa ilikuwa ni Jumamosi asubuhi , baada ya kuhesabiwa pale tukapewa maelekezo wa kwenda kumwagilia maua nje ya Shule, haya ni maua ya pale Bagamoyo Road ukipita hata saivi utayaona sasa hivi yamekuwa makubwa na pamendeza , sasa wakati naanza kidato cha tano yalikuwa ndio yanapandwa na tuliyamwagilia sana maji .

Tulibeba ndoo zetu , maji tulikuwa tukichukulia shuleni kule na kuvuka barabara na kunyweshea, sasa mimi na wajamaa flani tulikuwa wa mwisho kwenda kuchota maji , wakati tunafika eneo la kuchota maji mimi nikiwa mtu wa mwisho kuchota , mara kuna gari aina ya X-trail pale iliingia, sasa hatukusubiri gari ile isimame sisi tukasepa , lakini ile tunataka kukata kona tukaitwa, alikuwa ni Afande pia wa Nyota tatu tena alikuwa na Gwanda kabisa na alionekana anatoka Shift huyu alikuwa ni afande anaehusika na kuwasimamia wanafunzi wa O-level.
Akatuuliza kwanini hatujasimama na kumsalimia , hakuwa na majibu kati yetu , tukaambiwa kunja ngumi na kuna jamaa akaagizwa fimbo pale , fimbo ikaja nikapewa zangu sita safii nikakumbushwa kuwa nipo shule ya jeshi.

Wajamaa baada ya kuniona nimelambwa Sita tena siku ya pili baada ya kuripoti walicheka na wakaniambia hayo ndio tuliokuwa tukikwambia , nilicheka na kuwaambia wameshinda.

Eniwei mambo hayo ya fimbo hayahusiani sana na kisa hiki ila nimejaribu kuonogesha .

Wakati nafika hapa hapa shuleni nilikuwa mzima wa Afya kabisa sikuwa na shida yoyote ile , nitajaribu kufupisha ili twende sawa.
Itaendelea

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Kijana nilikuona 2014 kipindi mkimwagilia maua kwenye hiyo barabara nitatuma picha yako soon
 
INAENDELEA
Basi baada ya wiki moja kupita Mungu akasaidia hali yangu ya kutokuona karibu ikapita na hata pia mbali nilikuwa nikiona vizuri japo sio sana lakini nilishukuru.
Basi nilianza kula pindi kwa spidi zote maana nina wiki chache tu za kujiandaa na mtihani wa mwisho wa mwezi wa Tano kukamilisha muhula.

Basi baada ya kama siku tano hivi zilipita , ilikuwa ni siku ya ijumaa nikiwa zangu Library napiga msuli na rafiki yangu mmoja hivi msukuma,Mida kama ya jioni hivi saa kumi na moja kama na nusu hivi , alikuja dogo flani wa O-level , alionekana alikuwa akitutafuta na mazungumzo yake baada ya kutufikia yalikuwa hivi.

“Braza kuna wadada Flani hivi wageni wanamtafuta Deusi Mathayo”

Rafiki yangu huyu alikuwa akiitwa Deus Steven(sio jina lake halisi), hivyo huyu dogo kuja kwetu ni kutokana na kwamba alikuwa amemkosa mtu anaeitwa Deus Mathayo.

“Mimi naitwa Deusi Steven sio Deusi Mathayo”Aliongea rafiki yangu.

“Braza hao wadada wanasema wanaemtafuta ndio Deusi Mathayo na kwa maelezo yao wanasema Deusi anaishi hosteli , lakini nimuelizia bwenini hakuna mtu anaeitwa Deus Mathayo hivyo washikaji wakaniambia labda itakuwa ni wewe hao wadada wamechanganya majina ndio maana nimekuja labda ukawa unawajua , au kama vipi ukaonane nao”.

“Hao wadada wakoje?” Jamaa yangu akauliza .

“Mmoja ni rangi mchanganyiko kama muarabu hivi na mwingine ni mweupe mrefu , hawajaniambia majina yao”.

“Ni Warembo?”Aliuliza Msukuma haha.. alikuwa akipenda warembo sana huyu jamaa na moja ya kitu kinachonichekesha nikiwa nae ni lafudhi yake iliojaa usukuma.

“Ndio broo huyo shombeshombe ni mzuri hatari”.

“Basi ngoja nikaonane nao”Msukuma akaniambia nimsindikize tukawaone hao wadada , akaniambia kama ni wabovu tunaachana nao hata siwasogelei nikamwambia poa.

Dogo akaongoza njia ya kwenda hosteli maana muda huu tulikuwa shuleni huku madarasani , baada ya kufika hosteli , wadada wenyewe walikuwa wamejificha upande wa kota za wanajeshi , walikuwa na aibu hatari maana eneo walilokuwepo lilikuwa ni hosteli za wavulana.

Basi baada ya kuwafikia pale na kuwaona aisee walikuwa wazuri balaa hasa huyu shombeshombe,kusema ukweli mimi sikuwa nikijiamini sana mbele ya wanawake so kazi niliacha kwa Msukuma maana alikuwa akijiamini sana , jamaa alikuwa thick skinned , hakuwa na aibu.
Jamaa akaniambia Mwanangu Jr hawa watoto ni wazuri hatari siwaachi hata kama mimi sio mtu wanaemtafuta nikamwambia itakuwa vyema.

“Naitwa Deusi Mathayo nimepata taarifa mnanitafuta”Nilitamani kucheka , msukuma alikuwa na mambo ya ajabu kweli maana alichofanya ni kubadilisha jina lake kutoka Deusi Steven kwenda Deusi Mathayo,Tatizo ni kwamba wale wadada hawakuwa wakimjua wanaemtafuta kwa sura.

Basi wale wadada wakacheka pale maana Jamaa yangu alikuwa mcheshi balaa , lakini mwishowe wakasema sio yeye wanaemtafuta , tukawauliza mnamtafutaje jamaa msiemjua ndio Shombeshombe akatuambia kuwa rafiki yake katongozwa na huyo Deusi lakini hawajawahi kuonana , lakini pia maelekezo yake akasema kuwa Deusi alijitambulisha kuwa anasoma hapo Shuleni na pia anakaa Tabata Segerea na Kwa maelezo ya Deusi ni kwamba wao ni majirani hivyo wamekuja hapo ili kumfahamu. Kifupi ilionekana wanahamu sana ya kumuona Deusi , lakini Deusi hakuonekana na haraka haraka tulijua lazima hawa wadada wamedanganywa jina.

Tuliongea nao mpaka Kengele ya Msosi ,saa kumi na mbili na nusu ilipogonga so tukataka kuachana nao.
Hawa wadada in short walikuwa ni wanafunzi kutoka shule moja ya Islamic iliokuwa maneo ya Ubungo na muda huo pia walikuwa wamevaa Uniform za rangi flani hivi ya Zamabarau(wote walikuwa wamevaa juba).

Huyu ShombeShombe baada ya kutuona tunaondoka akaniita …

“Kaka unaitwa nan?”

“Naitwa Jr”.

“Ijumaa nitakuja kukusalimia”

Nikashangaa lakini nikamjibu kuwa hakuna noma akija atanikuta , ila kwangu nilichukulia labda anafanya utani tu hakuwa akimaanisha kwa hio nikapotezea pale pale na kusahau lile swala , lakini sikusahau uzuri wake yule mdada.

Basi siku hio ikapita , zikaisha siku kama saba hivi , siku hio kulikuwa na mechi kati ya Shuleni kwetu na Kibiti , ilikuwa ni siku ya ijumaa , hii mechi ilikuwa ya moto sana na hii ni kutokana na aina ya ushangiliaji wa wanafunzi wa Kibiti licha ya kuwafunga bao nyingi mno , nakumbuka tuliwafunga kumi na mbili , lakini spirit yao ya kushangilia haikukoma.

Sasa wakati nikiwa nimenogewa na Gemu licha ya kwamba sikuwa nikiona vizuri , alikuja jamaa flani hivi wa A-Level wa Day Sikujuia hata kombi yake maana wanafunzi pale ni wengi sana akaniambia Bro kuna mdada anaitwa Naira(sio jina lake halisi) anakutaita , nikashangaa maana sikuwahi kusikia hilo jina kabla so nikamuuliza jamaa una uhakika ni mimi ninaeitwa , akaniambia wewe sio ndio Jr nikamwambia ndio, akaniambia basi ni wewe unaeitwa.

Nikaona niongozane na jamaa tu , japo nilikuwa na uhakika kwamba jamaa kakosea , nilidhania hivyo kutokana mimi nimoja ya wanafunzi ambao hatukuwa tukitembelewa.

Basi baada ya kutembea mpaka nyuma ya Mesi barabarani ndipo nilipomuona mwanafunzi aievalia Juba , Aisee sikuamini na nilikuwa nimesahau kabisa yaani kwamba nina miadi , na kilichofanya nisahau ni kwamba hawa wadada siku ile tunaonana nao licha ya kuniambia atakuja sikuchukulia siriasi kama atakuja kweli.
Siku hio alikuwa peke yake hakuwa na yule rafiki yake aliekuja nae wiki iliopita, baada ya kumsogelea nikamuuliza kumbe unaitwa Naira , akatabasamu akasema ndio , ile siku wakati tunakutana nao hata hatukuwaliza majina.

Basi tukatafuta eneo la kukaa tukakaa huku nikimwambia kuwa nilijua siku ile anaongea utani , akaniambia huwa hatoagi ahadi za uongo, anaspeaking Scent hivi ya kiarabu lakini mara nyingi alikuwa akichanganya maneno na kingereza

Ukweli siku hii sikuwa hata nikijua nisema nini maana nilikuwa moja ya wanafunzi madomo Zege,Kwakuwa muda umeenda nikamwambia tutembee kuelekea kituoni ili asichelewe , maana ilikuwa saa kumi na mbili hivi halafu alikuwa akikaa Tabata Bima.

Katika stori za kufahamiana nae nilijua kwanza baba yake alikuwa hayupo hapa nchini aalikuwa akiishi nchi moja ya Afrika ambayo haikuwahi kutawaliwa na baba yake ni Arabs Pure na hapa Bongo alikuwa akiishi na mama yake tu mwenyeji wa Handeni Tanga ,pia nilikuja kujua kwamba na yeye yupo kidato cha tano HGE.

Huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana na Naira shombeshombe, alitokea kunipenda balaa , kila ijumaa alikuwa akija kunitembelea na zawadi mbali mbali , washikaji walikuwa wakiona wivu balaa, Ubaya tu ni kwamba hakuwa na simu so hatukuwa na mawasiliano na kama ijumaa haji basi lazima anitumie kimemo kutoka kwa washikaji wa Day.

Huyu dada ni mhanga wa kwanza kupata tatizo la kuona na kutokusikia

Sasa siku za mtihani zikiwa zinakaribia , macho yangu yalikuwa angalau yalikuwa yanaona vizuri lakini sasa tatizo lingine likaibuka , washikaji walikuwa wakinilaumu sana kwamba nina dharau , kwani walikuwa wakiniita nilikuwa nikawakaushia na moja ya watu waliokuwa wakinipa tuhuma hizo ni Msukuma , lakini mimi nilijitahidi kujitetea kwamba sikuwasikia waliponiita.

Sasa ikawa kero sasa kwani ilikuwa ni Zaidi ya wiki Napata hizi lawama na hapa ndipo nilipokuja kugundua kuwa uwezo wangu wa kusikia umeshuka sana kwa kiasi kikubwa , na kilichonifanya nifahamu hivyo ni kwamba siku moja mwalimu wa Physics aliingia kufundisha , huyu mwalimu sauti yake ina base so sikuweza kumsikia kipindi chote.

Nilijaribu kuziba sikio moja na kidole likawa linasikia japo sio sana , nikaziba sikio lingine likawa limeniziba kabisa , nilishangaa sana na kuogopa nini kinanitokea, kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndio hali ilizidi kuwa mbaya nikawa sisikii kabisa , yaani sauti ikawa inakuja kwa mbaali sana, lakini pia tatizo langu la kutokuona mbali likarudi upya.

Ukweli nilitamani kulia , ila nilijikaza kibabe huku nikijjipa matumaini kuwa huenda ni tatizo la kawaida tu na nikienda hospitalini litaisha , hivyo kwakuwa muda uliokuwa ulikuwa ni kama wiki moja hivi niliona nikomae kwanza na mtihani na swala la afya yangu nitalishughulikia baada ya pepa.
Itaendelea Soon

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Haya mambo yapo sana kuna mshikaji wangu aliachia kidato cha pili kila akiingia class giza akitoka fresh kaangaika mwisho akapiga chini shule,kuna madogo wengine kama watatu nawajua wame-hustle sana na hizo mambo
 
Basi siku ya pepa ilifika , nikafanya vizuri tu mtihani ,tena pepa ni kama nimeiotea vile maana ilikuwa nyepesi mno ,siku ya mwisho ya kumaliza pepa kuna msela mmoja hivi anachukua kozi ya PCM alinifata na kuniambia ana kibarua changu , alinikabidhi na kuniambia kapewa na mdada flani hivi kwenye daladala.
Niliangalia kile kikaratasi na alikuwa ni Naira alikuwa akiniambia kuwa atakuja Ijumaa, kifupi ni kwamba hatukuwa tumeonana kwa muda mrefu kidogo Zaidi ya wiki tatu.

Licha ya kupata ujumbe ule sikuwa na mudi kabisa ya kubaki shuleni , nilikuwa nikiwaza nirudi home tu nikashughulike na swala la masikio na macho , lakini pia niliona huyu bidada akinikuta kwenye hali niliokuwa nayo itakuwa sio poa , so nilikosa ujasiri wa kumsubiri , baada ya kumaliza pepa nikaenda Kimara kwa Aunt yangu mwingine na hapa ni baada ya kupewa maagizo na Aunt wa Lushoto niende Kimara, ili akanisaidie swala langu .
Inshort ni kwamba bi mkubwa hakuwa akijua kinachoendelea shuleni na ndugu zangu waliniambia nisimwambie, bi mkubwa anatatizo flani la kisaikolojjia ambalo lilimwathiri baada ya kaka zangu wawili wote walionitangulia kufariki kwa mazingira ya kutatanisha, so ni kama tukio hilo lilimwathiri sana kisaikolojia.

Kuna siku sister alikuwa akisafiri kwenda shuleni Advance Bukoba huko tukapoteza mawasiliano nae wakati akiwa yupo njiani ,Bi mkubwa alizimia mara kibao.
So hakukuwa na haja ya kumwambia kuhusu hali yangu ilionipata shuleni.

Basi nilienda kimara pale kwa Aunt , nilakaa siku chache tu akaniambia kuwa kanisani kwao wameandaa kongamano la vijana ambalo linafanyikia kanisa la City Center kwa Askofu Katunzi ,Mtoni mtongani,nikamwambia nataka kwanza kwenda Muhimbili kucheki shida nini , ila akakomaa akaniambia niende huko kwanza , so nikatii na kwenda kwenye hilo kongamano la kuombewa la walokole.
Kongamano lenyewe lilikuwa ni siku saba tunalala hukohuko ,Nilipigwa maombi kwa sana tu , lakini sikupata nafuu yoyote , na imanii yangu ilikuwa ndogo mno , kwani moyo wangu ulikuwa ukiniambia suruhisho la tatizo langu ni kwenda Hospitali tu.

So baada ya Kongamano kuisha sikupata nafuu kabisa ,nikasema ngoja niende hospital , lakini hospitali niliochagua sio Muhimbili nilichagua kwenda hospitali flani hivi ipo Tegeta kibaoni inaitwa Rabbynisia kama sikosei , nilifika pale mida ya asubuhi nikakata bima , ila manesi wale wa mapokezi pale wakaniambia Dokta wa ENT anakuja saa saba hivyo kama nitaweza kusubiri nisubiri, nikawaambia nitakuja huo muda na hapo nilipanga niende kwanza Mapinga kwa Baba mdogo nikachukue Pc yangu nilirudi nayo Kimara nikaangalie Season kupoteza mawazo.

Muda wa Saa saba nikarudi pale , na kwakuwa nilikuwa na Appointment nikawa mgonjwa wa pili kuonana na Daktari gorofanni kabisa kule.

Dokta akaniuliza maswali , maswali pale , kama natumia Earphone nikamwmabia natumia ila mara chache sana , akaniuliza nilikuwa na mafua tatizo lilipoanza nikamwambia hapana , akaniuliza limeanzaje anzaje nikamweleza kuwa mwenyewe sijui lilianza vipi ila watu ndio walioanza kujua kuwa sisikii freshi.

Basi akanipima pima pale , akanimulika masikioni na tochi yake na kisha akaniambia kuwa Jumatano wiki ijayo niende Muhimbili pale nikaonane nae ili nipime kipimo cha Audiometry , akanipa namba yake ya simu na chumba anachofanyia matibabu na muda ,nikasepa, hapa malengo yangu kwanza ni kushughulika na swala la Masikio kwanza halafu nifanye mpango wa swala la macho.

Basi baada ya Jumatano kufika nikaenda pale asubuhi , watu walikuwa wengi mno kule Bima nakumbuka nilipewa namba 301 , yaani nilikuwa mtu wa Mia tatu na moja mpaka zamu yangu ifike kuandikiwa karatasi ya Bima ,Nilisubiri Zaidi ya masaa manne pale yaani mpaka saa sita na nusu sikuwa nimepata huduma.

Basi baada ya kupata karatasi zile nikaenda kwa huyo dokta sasa , nikaulizia kwa jina lake pale nikaambiwa kuwa ashaondoka , nikaona haina noma ngoja nitibiwe na dokta yoyote , nikafanya taratibu pale na zamu yangu ikafika ,taratibu zilikuwa kama zile zile za kule Rabynsia , ila hapa mwishoni Dokta akaniambia niende chumba namba sitni na tano kupima kipimo cha Audiometry , nikaenda pale nikaambiwa kuwa mashine ina hitilafu nirudi Jumatatu wiki ijayo , Nilimind maana naona kama wananihangaisha, nikarudi kwa Dokta akaniandikia dawa Flani hivi ambazo sikuzisoma hata jina Plus vidonge vya Vitamin B nikasepa.

Next week ilivyoingia nikarudi mikafata taratibu zilezile ila nikaambiwa mashine haijafaa bado nirudi wiki ijayo , niliona miyeyusho , baada ya kuona muda upo wa kutosha nikaenda kitengo cha macho pale , nikakutana na mzee mmoja pale akanicheki macho pale, akaniambia nenda chumba kingine , hiki chumba ni kwa ajili ya kupima uwezo wangu wa kuona mbali na karibu kwa kutumia Chart, baada ya kumaliza nikarudi kwa yule dokta , ila sikumkuta alikuwa ashasepa na kapokewa na mdada flani hivi Shombeshombe , basi na yeye akanipima pale akaniambia itakuwa Nerve za macho zimelegea , nikamuuliza lakini pia nina shida kwenye masikio vipi nako shida itakuwa hio hio , akashangaa , ila akaniambia niende ENT , akaniandikia vidonge pale vvya Vitamin nikasepa.

Baada ya kutumia tumia vidonge vile , hali kidogo ikawa imeimarika kwa kiasi flani , nikawa nasikia japo sio sana, Basi tokeo likatoka baada ya siku chache na nikawa nimefaulu vizuri tu , nilikuwa na division 1.

Siku ambayo natoka kuangalia matokeo , ilikuwa asubuhi nipo daraja la Mwenge pale simu yangu ikaita namba mpya nikapokea pale na hapo ndipo nilipojua mpigaji alikuwa ni Naira, akaniuliza niko wapi , nikamtajia nipo Mwenge , akaniambia nisubiri , nikamsubiri baada kama ya nusu saa huyu hapa , ilikuwa ni muda wa saa nne hivi kwenda saa tano, alikuwa amependeza mno , mpaka nimemsahau kwani mara zote nilikuwa nikimuona na Uniform , ila siku hio alikuwa amekuja amevaa suruali ya jeans na kiblazia , na shungi , alikuwa ananukia kama jini.

Basi akaniambia kuna sehemu anataka twende wote nikamwabia poa , huyu msichana licha ya kuwa na mazoea naye ya karibu sana na kuonesha dalili za kunipenda ila sikumtongoza , kwanza nilikuwa Domo Zege naanzaje , pia nilikuwa mpole mno na hio ilikuwa sifa yangu , ila yeye alikuwa mjanja sana na muongeaji, nilikuwa nikipenda sana sati yake na Speaking Scent yake.

Basi tukapanda bajaji na ndani ya muda flani tulifika mbele ya Ghorofa flani maneo flani hivi ,ni nyumba ya makazi ya watu na akaniambia hapo anakaa mama mdogo wake , nikamwambia sawa lakini mimi siingii, akanilazimisha na kuniambia Mama mdogo wake hayupo , niligoma ila baada ya ushawishi wake nikaingia na kupanda ngazi mpaka floor ya nne na hapo ndio Apartment ya mama yake mdogo ndipo ilipo , niliingia ndani, palikuwa pazuri balaa , ni Apartment ya vyumba vitatu.

Basi baada ya kupiga piga stori pale , huku akinilalamikia kuondoka shuleni licha ya kuniambia anakuja , nilijitetea yakaisha , basi bwana akaniambia twende kwenye chumba chake, nikashangaa ma kugoma I was so nervous this Time , Nilitamani kuondoka tu , na ubaya ni kwamba mapozi aliokuwa akinifanyia , yalinifanya kuona leo naliwa kimasikhara.

Niligoma goma , pale lakini katika kubembelezana tukajikuta tukianza michezo ya kikubwa, mwishoni hata sikujua nilifikaje chumbani.. yaliondelea hapa Mungu anisamehe, ila ni kwamba Naira alikuwa ndio mara yake ya kwanza , ila kwangu haikuwa mara ya kwanza.. nitaeleza baadae maana nisehemu ya kisa hiki.

Basi baada ya tukio la mimi na Naira kufanyika hatukuahi kuonana wala kuwasiliana mpaka nafungua shule na Mizi kadhaa ikapita , siku aliokuja kuniona nilimuonea huruma mno na kujilaumu kwa wakati mmoja.
ITAENDELEA

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
INAENDELEA
Basi baada ya wiki moja kupita Mungu akasaidia hali yangu ya kutokuona karibu ikapita na hata pia mbali nilikuwa nikiona vizuri japo sio sana lakini nilishukuru.
Basi nilianza kula pindi kwa spidi zote maana nina wiki chache tu za kujiandaa na mtihani wa mwisho wa mwezi wa Tano kukamilisha muhula.

Basi baada ya kama siku tano hivi zilipita , ilikuwa ni siku ya ijumaa nikiwa zangu Library napiga msuli na rafiki yangu mmoja hivi msukuma,Mida kama ya jioni hivi saa kumi na moja kama na nusu hivi , alikuja dogo flani wa O-level , alionekana alikuwa akitutafuta na mazungumzo yake baada ya kutufikia yalikuwa hivi.

“Braza kuna wadada Flani hivi wageni wanamtafuta Deusi Mathayo”

Rafiki yangu huyu alikuwa akiitwa Deus Steven(sio jina lake halisi), hivyo huyu dogo kuja kwetu ni kutokana na kwamba alikuwa amemkosa mtu anaeitwa Deus Mathayo.

“Mimi naitwa Deusi Steven sio Deusi Mathayo”Aliongea rafiki yangu.

“Braza hao wadada wanasema wanaemtafuta ndio Deusi Mathayo na kwa maelezo yao wanasema Deusi anaishi hosteli , lakini nimuelizia bwenini hakuna mtu anaeitwa Deus Mathayo hivyo washikaji wakaniambia labda itakuwa ni wewe hao wadada wamechanganya majina ndio maana nimekuja labda ukawa unawajua , au kama vipi ukaonane nao”.

“Hao wadada wakoje?” Jamaa yangu akauliza .

“Mmoja ni rangi mchanganyiko kama muarabu hivi na mwingine ni mweupe mrefu , hawajaniambia majina yao”.

“Ni Warembo?”Aliuliza Msukuma haha.. alikuwa akipenda warembo sana huyu jamaa na moja ya kitu kinachonichekesha nikiwa nae ni lafudhi yake iliojaa usukuma.

“Ndio broo huyo shombeshombe ni mzuri hatari”.

“Basi ngoja nikaonane nao”Msukuma akaniambia nimsindikize tukawaone hao wadada , akaniambia kama ni wabovu tunaachana nao hata siwasogelei nikamwambia poa.

Dogo akaongoza njia ya kwenda hosteli maana muda huu tulikuwa shuleni huku madarasani , baada ya kufika hosteli , wadada wenyewe walikuwa wamejificha upande wa kota za wanajeshi , walikuwa na aibu hatari maana eneo walilokuwepo lilikuwa ni hosteli za wavulana.

Basi baada ya kuwafikia pale na kuwaona aisee walikuwa wazuri balaa hasa huyu shombeshombe,kusema ukweli mimi sikuwa nikijiamini sana mbele ya wanawake so kazi niliacha kwa Msukuma maana alikuwa akijiamini sana , jamaa alikuwa thick skinned , hakuwa na aibu.
Jamaa akaniambia Mwanangu Jr hawa watoto ni wazuri hatari siwaachi hata kama mimi sio mtu wanaemtafuta nikamwambia itakuwa vyema.

“Naitwa Deusi Mathayo nimepata taarifa mnanitafuta”Nilitamani kucheka , msukuma alikuwa na mambo ya ajabu kweli maana alichofanya ni kubadilisha jina lake kutoka Deusi Steven kwenda Deusi Mathayo,Tatizo ni kwamba wale wadada hawakuwa wakimjua wanaemtafuta kwa sura.

Basi wale wadada wakacheka pale maana Jamaa yangu alikuwa mcheshi balaa , lakini mwishowe wakasema sio yeye wanaemtafuta , tukawauliza mnamtafutaje jamaa msiemjua ndio Shombeshombe akatuambia kuwa rafiki yake katongozwa na huyo Deusi lakini hawajawahi kuonana , lakini pia maelekezo yake akasema kuwa Deusi alijitambulisha kuwa anasoma hapo Shuleni na pia anakaa Tabata Segerea na Kwa maelezo ya Deusi ni kwamba wao ni majirani hivyo wamekuja hapo ili kumfahamu. Kifupi ilionekana wanahamu sana ya kumuona Deusi , lakini Deusi hakuonekana na haraka haraka tulijua lazima hawa wadada wamedanganywa jina.

Tuliongea nao mpaka Kengele ya Msosi ,saa kumi na mbili na nusu ilipogonga so tukataka kuachana nao.
Hawa wadada in short walikuwa ni wanafunzi kutoka shule moja ya Islamic iliokuwa maneo ya Ubungo na muda huo pia walikuwa wamevaa Uniform za rangi flani hivi ya Zamabarau(wote walikuwa wamevaa juba).

Huyu ShombeShombe baada ya kutuona tunaondoka akaniita …

“Kaka unaitwa nan?”

“Naitwa Jr”.

“Ijumaa nitakuja kukusalimia”

Nikashangaa lakini nikamjibu kuwa hakuna noma akija atanikuta , ila kwangu nilichukulia labda anafanya utani tu hakuwa akimaanisha kwa hio nikapotezea pale pale na kusahau lile swala , lakini sikusahau uzuri wake yule mdada.

Basi siku hio ikapita , zikaisha siku kama saba hivi , siku hio kulikuwa na mechi kati ya Shuleni kwetu na Kibiti , ilikuwa ni siku ya ijumaa , hii mechi ilikuwa ya moto sana na hii ni kutokana na aina ya ushangiliaji wa wanafunzi wa Kibiti licha ya kuwafunga bao nyingi mno , nakumbuka tuliwafunga kumi na mbili , lakini spirit yao ya kushangilia haikukoma.

Sasa wakati nikiwa nimenogewa na Gemu licha ya kwamba sikuwa nikiona vizuri , alikuja jamaa flani hivi wa A-Level wa Day Sikujuia hata kombi yake maana wanafunzi pale ni wengi sana akaniambia Bro kuna mdada anaitwa Naira(sio jina lake halisi) anakutaita , nikashangaa maana sikuwahi kusikia hilo jina kabla so nikamuuliza jamaa una uhakika ni mimi ninaeitwa , akaniambia wewe sio ndio Jr nikamwambia ndio, akaniambia basi ni wewe unaeitwa.

Nikaona niongozane na jamaa tu , japo nilikuwa na uhakika kwamba jamaa kakosea , nilidhania hivyo kutokana mimi nimoja ya wanafunzi ambao hatukuwa tukitembelewa.

Basi baada ya kutembea mpaka nyuma ya Mesi barabarani ndipo nilipomuona mwanafunzi aievalia Juba , Aisee sikuamini na nilikuwa nimesahau kabisa yaani kwamba nina miadi , na kilichofanya nisahau ni kwamba hawa wadada siku ile tunaonana nao licha ya kuniambia atakuja sikuchukulia siriasi kama atakuja kweli.
Siku hio alikuwa peke yake hakuwa na yule rafiki yake aliekuja nae wiki iliopita, baada ya kumsogelea nikamuuliza kumbe unaitwa Naira , akatabasamu akasema ndio , ile siku wakati tunakutana nao hata hatukuwaliza majina.

Basi tukatafuta eneo la kukaa tukakaa huku nikimwambia kuwa nilijua siku ile anaongea utani , akaniambia huwa hatoagi ahadi za uongo, anaspeaking Scent hivi ya kiarabu lakini mara nyingi alikuwa akichanganya maneno na kingereza

Ukweli siku hii sikuwa hata nikijua nisema nini maana nilikuwa moja ya wanafunzi madomo Zege,Kwakuwa muda umeenda nikamwambia tutembee kuelekea kituoni ili asichelewe , maana ilikuwa saa kumi na mbili hivi halafu alikuwa akikaa Tabata Bima.

Katika stori za kufahamiana nae nilijua kwanza baba yake alikuwa hayupo hapa nchini aalikuwa akiishi nchi moja ya Afrika ambayo haikuwahi kutawaliwa na baba yake ni Arabs Pure na hapa Bongo alikuwa akiishi na mama yake tu mwenyeji wa Handeni Tanga ,pia nilikuja kujua kwamba na yeye yupo kidato cha tano HGE.

Huo ndio ukawa mwanzo wa kufahamiana na Naira shombeshombe, alitokea kunipenda balaa , kila ijumaa alikuwa akija kunitembelea na zawadi mbali mbali , washikaji walikuwa wakiona wivu balaa, Ubaya tu ni kwamba hakuwa na simu so hatukuwa na mawasiliano na kama ijumaa haji basi lazima anitumie kimemo kutoka kwa washikaji wa Day.

Huyu dada ni mhanga wa kwanza kupata tatizo la kuona na kutokusikia

Sasa siku za mtihani zikiwa zinakaribia , macho yangu yalikuwa angalau yalikuwa yanaona vizuri lakini sasa tatizo lingine likaibuka , washikaji walikuwa wakinilaumu sana kwamba nina dharau , kwani walikuwa wakiniita nilikuwa nikawakaushia na moja ya watu waliokuwa wakinipa tuhuma hizo ni Msukuma , lakini mimi nilijitahidi kujitetea kwamba sikuwasikia waliponiita.

Sasa ikawa kero sasa kwani ilikuwa ni Zaidi ya wiki Napata hizi lawama na hapa ndipo nilipokuja kugundua kuwa uwezo wangu wa kusikia umeshuka sana kwa kiasi kikubwa , na kilichonifanya nifahamu hivyo ni kwamba siku moja mwalimu wa Physics aliingia kufundisha , huyu mwalimu sauti yake ina base so sikuweza kumsikia kipindi chote.

Nilijaribu kuziba sikio moja na kidole likawa linasikia japo sio sana , nikaziba sikio lingine likawa limeniziba kabisa , nilishangaa sana na kuogopa nini kinanitokea, kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndio hali ilizidi kuwa mbaya nikawa sisikii kabisa , yaani sauti ikawa inakuja kwa mbaali sana, lakini pia tatizo langu la kutokuona mbali likarudi upya.

Ukweli nilitamani kulia , ila nilijikaza kibabe huku nikijjipa matumaini kuwa huenda ni tatizo la kawaida tu na nikienda hospitalini litaisha , hivyo kwakuwa muda uliokuwa ulikuwa ni kama wiki moja hivi niliona nikomae kwanza na mtihani na swala la afya yangu nitalishughulikia baada ya pepa.
Itaendelea Soon

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Nukuu:

....washikaji walikuwa wakinilaumu sana kwamba nina dharau , kwani walikuwa wakiniita nilikuwa nikawakaushia na moja ya watu waliokuwa wakinipa tuhuma hizo ni Msukuma , lakini mimi nilijitahidi kujitetea kwamba sikuwasikia waliponiita.

Inauma sana!
 
Back
Top Bottom