Ushauri kwa Serikali, TAMISEMI na Wizara ya Elimu

Cyn

Member
Jul 19, 2022
76
138
Kwanza naishukuru sana serikali na wizara ya elimu kwa kujitahidi kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata nafasi ya kufikia walau elimu ya sekondari bila malipo.

Nikiwa nimefundisha shule za umma kwa miaka 15+ na kujua na kuona changamoto za mashuleni nimeona niandike kile ambacho katika miaka hii 15 nadhani kitaweza kusaidia sana wanafunzi wengi.

Kwa mtu asiye mwalimu au ambaye hajakaa sana na kusoma tabia za wanafunzi na kujaribu kuwaza kitu gani kinaweza kusaidia wanafunzi anaweza asinielewe. Lakini ushauri wangu ukitiliwa maanani utasaidia sana wanafunzi wengi sana mashuleni.

Andiko langu ni kuishauri wizara kubadilisha mfumo wa elimu ili wanafunzi wengi waweze kujitegemea, kufaulu na kupata ujuzi zaidi katika nyanja ya masomo yao lakini pia kupanua vipaji vyao.

Ili kufanikisha haya nashauri yafuatayo.

1. WANAFUNZI SEKONDARI (O-LEVEL )WAPUNGUZIWE MASOMO
Nasema hili kwa sababu wanafunzi wengi wamekuwa na utitiri wa masomo ambayo mpaka mwisho wanajikuta wamekuwa na uelewa kidogo kwa kila somo na kuishia kufeli masomo yote,wakati ambapo kama mtoto angepewa masomo 4 ambayo ndani yake ataweza kuchagua combination 2 tu ataweza kuyamudu vizuri sana na kufaulu.

Halafu ili waweze kupata general knowledge ya vitu kama lugha,current issues, common issue na hesabu za kumsaidia kimaisha; Liwepo somo la GENERAL STUDIES/KNOWLEDGE ambalo ndani yake asome hesabu kidogo, political issues, common issues pamoja na lugha ya kiswahili na kiingereza.

Kwa Mfano; akisoma PHYSICS, BIOLOGY, MATHS & CHEMISTRY ataweza kusomea either PCB ama PCM au akisoma BIOLOGY, PHYSICS, GEOGRAPHY, MATHS& CHEMISTRY ataweza kusomea CBG/PGM/EGM.

Akisoma KISWAHILI, HISTORY, ENGLISH, GEOGRAPHY ataweza kusoma HGE, HKL, HGL, HGK. Na michepuo tofauti tofauti itawezekana kulingana na alichosoma mtoto ila waruhusiwe kuanzia masomo 3 hadi 5 maximum ili kuepusha ile kushindwa kumudu masomo yote kabisa.

Tuamue kwamba mtoto ajue masomo 3 tu kwa uhakika au ajue asilimia 2 ya kila somo afeli yote. Kuna msemo wa kiingereza A JACK OF ALL TRADES AND MASTER OF NONE (yaani kila kitu unajua kidogo ila hakuna unachojua kiukamilifu) Lakini pia kwa kiswahili tuna msemo wa MTAKA YOTE HUKOSA YOTE na ndicho kinachotokea, tunataka mtoto asome ili apate masomo mengi ya kuchezea bahati nasibu ya kufaulu ila tunaishia kuwapoteza jumla.

Wanafunzi wengi sana akisoma masomo 3 atafaulu na ataenda advance akiwa na knowlegde nzuri sana katika nyanja husika. Anakuwa amespecialize hayo masomo muda mrefu na anakuwa mtaalamu kwelikweli.

Hii pia itasaidia kupunguza uhaba wa walimu maana mwalimu mmoja atabaki na wanafunzi wachache ambao wanasoma lile somo kuliko mwalimu kuwa anafundisha watoto 200+ na inaleta shida pia kwa mwalimu huyo kuweza kuwafikia wanafunzi hao mmoja mmoja maana ni wengi sana.

2. WIZARA ITENGENEZE SPORTS AND GAMES SCHOOLS KWA WATOTO KUANZIA SHULE YA MSINGI.
Point hapa ni kwamba mashuleni huku tuna watoto wengi sana wenye vipaji sana kama vingeendelezwa kuanzia utotoni basi wangekuwa wanamichezo wakubwa sana duniani lakini hawana muda wa kuendeleza vipaji.

Mfano wanafunzi wengi wanaweza; MUZIKI, DANCING, KUKIMBIA, KURUKA, MPIRA WA MIGUU, MPIRA WA MIKONO, UCHORAJI, UTUNZI WA NYIMBO NA MASHAIRI na wengi wao huku shuleni tunaona kama hawana akili lakini sio kweli taizo ni kwamba,hawajapewa eneo wanaloliweza maishani.

Kuna msemo ; EVERYBODY IS A GENIUS, BUT IF YOU JUDGE A FISH BY ITS ABILITY TO CLIMB A TREE,IT WILL SPEND ALL ITS LIFE THINKING IT IS STUPID. Na kweli Hawa wanafunzi pia wanajiona hawana akili na jamii inaona hawana akili,lakini ukweli ni kwamba wana akili za kucheza,kuimba ,kuchora nk. ila hawajapata pa kuzifanyia kazi na mara nyingi utakuta hao watoto wengi wanaofaulu sana masomo ya darasani hawana vipaji sana kama wale ambao wanafeli.

Ni kwa kuwa Mungu kamuwezesha kila mtu kuwa productive katika njia yake,ila sisi tumelazimisha kila mtu awe na akili za phyics na history na masomo tu kumbe sio kweli. na Masomo hayawapi muda wa kutrain ipasavo katika vipaji vyao lakini pia miuondombinu ikijumlishwa na walimu wa vipaji hivyo havipo vya kuwawezesha kuendeleza vipaji hivyo.

Kama mtoto ataingia katika shule ambazo ni kwa ajili ya michezo itamsaidia kukuza kipaji na hawa wataweza kujiajiri kupitia vipaji vyao. Wanafunzi hao pia wapewe masomo yasiyozidi 3 pamoja na GENERAL STUDIES; yaani kama ni PCB AU HKL aanze nayo toka form 1 ili wapate muda sana wa kutrain katika maeneo ya vipaji vyao na wapewe walimu wa michezo husika.

Na kwakuwa walimu wa michezo sio wengi basi wale walimu waliopo wa masomo ya darasani wasimamie michezo na wale walimu kabisa wa michezo hiyo wawe wanamove shule moja hadi nyingine kusimamia hizo programs za michezo na kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali.

Tukumbuke pia watoto wetu wanatoka familia zenye changamoto sana,hivo ile kasumba ya kuwafananisha na wanafunzi wa shule private tuiondoe, tujue tunadeal na wanafunzi wanaohitaji njia tofauti kabisa kuweza kuwafikisha kwenye kilele cha elimu chenye mafanikio.

Lakini tukiendelea na mambo ya kusema wanafunzi wote wanaweza bila kuangalia kwamba asilimia kubwa ya watoto wa shule za serikali wanaamka na kuja shule bila kula, anarudi anakuta baba na mama wameshikiana mapanga na hakuna chakula, wazazi wana stress ya vicoba, anarudi pia anaambiwa akauze maandazi au ubuyu ndipo wapate chakula au abebe kabisa akauze shule.

Bado ana masomo 7 na zaidi na anapewa pressure ayafaulu ambapo darasani wapo 80 au zaidi na mwalimu wake ana watoto 200+ wa kuwasaidia wafaulu. Changamoto hii watoto wengi sana private hawana. Hivo tuwafikirie hawa watoto kwa kuzingatia sana mazingira wanayoishi.

3. SERIKALI ITOE CHAKULA CHA MCHANA MASHULENI BILA WAZAZI KUCHANGIA
Wazo la serikali la watoto kula shuleni ni zuri sana na linasaidia kila mtoto apate mlo na kuweza jusoma bila njaa. Lakini tukumbuke kuwa sababu kuu ya kuwapa watoto mlo shuleni ni kwa sababu wengi wao hawawezi kupewa mfano pesa ya kununua chakula , Sasa inapokuja program ya chakula mashuleni halafu tukategemea mzazi yuleyule ambaye alishindwa kumpa mtoto pesa ya kula shule atoe mchango wa kuwezesha kununua chakula inakuwa haiwezekani.

Kuna baadhi ya shule hii program inashindikana kabisa kwa sababu ya wazazi kutokuwa na pesa ya kuchangia chakula lakini pia kutokuwa tayari kutoa huo mchango wa chakula ambapo mwisho watoto wanaendelea kukosa chakula. Ushauri wangu ni kuwa serikali iangalie jinsi ya kusambaza vyakula mashuleni pamoja na kuni /mkaa/gesi halafu wazazi kazi yao iwe kushirikiana na walimu kuangalia jinsi gani wataweza kupika hicho chakula.

Naamini viongozi wa serikali wakianzisha harambee za kuchangia vyakula wakulima wengi na wafanyabiashara watajitolea kuchangia.

Na hatuhitaji michango ya pesa katika hili, watu watoe tu gesi/mchele/Unga/maharage/Mafuta ya kupikia. Then mashule yawe na bustani za mboga mboga. Watoto bora wale ugali na wali maharage wiki nzima,mwezi mzima, mwaka mzima kuliko kukosa chakula kabisa.

Hawatakufa kwa kula hivo vyakula hata sisi tumekula vyakula hivyo na tumekuwa na afya nzuri kabisa. Na ndivyo vyakula ambavyo ni affordable kwa uchumi wetu pia. Pia michango ya pesa inakuwa na shida sana ya watu wengine kutaka kuiba pesa, ila vyakula havitaibiwa sana kama wakichangia pesa.

Baada ya wadau kuchangia basi serikali ikusanye hivyo vyakula na kuvigawa mashuleni labda kila baada ya miezi 3 kwa kulingana na idadi ya wanafunzi wetu. Watoto wengi wazazi hawawezi kuwapa nauli na mahitaji ya shule kila siku. Unakuta mzazi ana watoto 5 na bado hata akisema kila mtoto apewe elf 1 hiyo ni elf 5 kwa siku na bado ana matumizi mengine.

Wengi wao hawawezi kabisa kipato chao kidogo sana.

4. SERIKALI IONGEZE WALIMU ANGALAU WAFIKE RATIO YA 1:100
Katika miaka yangu 15+ya kazi sijawahi kuwa na wanafunzi chini ya 150 ba mara nyingi ni 200 na ninekuwa katika shule 3 za serikali lakini pia maahule mengine hali ni hiyohiyo. Hii pia imechangia sana wanafunzi kushindwa kufuatiliwa na walimu ipasavo.

Utawezaje kuwafatilia watoto 200 mmoja mmoja?ni ngumu sana. Hata madarasani inakuwa ngumu sana kumfikia mwanafunzi mmoja mmoja. Hivo napendekeza pia walimu wawe wengi angalau mwalimu 1 awe na wanafunzi 100 ili kuweza kuwasaidia wanafunzi mmoja mmoja kwa sababu wanafunzi wapo tofauti katika kusoma unahitaji pia kumfikia mmoja mmoja na kumuelekeza kwa kadri ya uelewa wake nje ya kipindi cha darasani.

Sasa imagine una wanafunzi 200 unatajiwa kufundisha,kuandaa somo,kusahihisha kazi zao na bado kutafuta muda wa kuwasaidia individually,kukutana na wazazi wao sometime na kutatua changamoto za haoa na pake katika somo lako. Inakuwa ngumu sana.

Imagine mzazi unakuwa na watoto 2 tu home wanakutoa jasho. Mfikirie mwalimu adeal na wanafunzi 200😀 lazima achanganyikiwe aisee.

5. SERIKALI IKUSANYE SANA MAONI KUHUSU ELIMU KUTOKA KWA WALIMU MASHULENI NA SIO KWA WASOMI TU WASIOJUA REALITY ILIYOPO MASHULENI
Ningeomba serikali wanapotaka kuboresha mitaala basi watembelee mashuleni wasikie maoni ya walimu ambao ndio watendaji wakuu na wenye kujua uhalisia wa nini kipo mashuleni.

Wasomi wanaotoa ushauri pia wasibezwe lakini tukumbuke kuwa mwalimu nfiye anajua practically nini kinatokea na nini kinawezekana ama hakiwezekani katika mazingira yakr na watoto ya kila siku. Lakini kama maamuzi yatakuwa yanafanyika bila kufika mashuleni na kuzungumza na walimu itakuwa inaleta tatizo la kuweka mikakati isiyotekelezeka.

Walimu wanajua sana kuhusu tabia na vipato vxa wazazi wengi kuliko watu wengine. Tusifate tu ushauri wa kwenye vitabu bali tuwafikie walimu mashuleni iwepo mijadala ya wazi ukihusisha walimu wote shule kwa shule ili kujua jinsi ya kusukuma gurudumu la elimu Tanzaniabkwa kutumia mbinu zinazowezekana na zinazoendana na mazingira na wanafunzi na wazazi.

Kwa leo naishia hapa.
Wenu mwalimu.
 
Imagine mzazi unakuwa na watoto 2 tu home wanakutoa jasho. Mfikirie mwalimu adeal na wanafunzi 200 lazima achanganyikiwe aisee.

5. SERIKALI IKUSANYE SANA MAONI KUHUSU ELIMU KUTOKA KWA WALIMU MASHULENI NA SIO KWA WASOMI TU WASIOJUA REALITY ILIYOPO MASHULENI
Ningeomba serikali wanapotaka kuboresha mitaala basi watembelee mashuleni wasikie maoni ya walimu ambao ndio watendaji wakuu na wenye kujua uhalisia wa nini kipo mashuleni.

Wasomi wanaotoa ushauri pia wasibezwe lakini tukumbuke kuwa mwalimu nfiye anajua practically nini kinatokea na nini kinawezekana ama hakiwezekani katika mazingira yakr na watoto ya kila siku. Lakini kama maamuzi yatakuwa yanafanyika bila kufika mashuleni na kuzungumza na walimu itakuwa inaleta tatizo la kuweka mikakati isiyotekelezeka.

Walimu wanajua sana kuhusu tabia na vipato vxa wazazi wengi kuliko watu wengine. Tusifate tu ushauri wa kwenye vitabu bali tuwafikie walimu mashuleni iwepo mijadala ya wazi ukihusisha walimu wote shule kwa shule ili kujua jinsi ya kusukuma gurudumu la elimu Tanzaniabkwa kutumia mbinu zinazowezekana na zinazoendana na mazingira na wanafunzi na wazazi.

Kwa leo naishia hapa.
Wenu mwalimu.
Nafatilia
 
  • Thanks
Reactions: Cyn
Mada ina masaa 4 Tena inahusu mustakabali wa taifa letu kwa vijana lakn ajabu Haina wachangiaji

N watanzania sisi tukikaa kwenye vijiwe vyetu Kaz ikuikosoa serikali bila kutoa ushauri

Mwenzetu kaleta wazo tuchangie na kurekebisha pale tunapoona inafaa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Umenena vema kaka. Hili ni tatizo pia nadhani sometime watu wanafurahi kukosoa tu ila hawataki solution. Ila tutafika tu taratibu😊
 
Serikali iheshimu Sana taaluma za watu. Usimuone madam mwalimu ana certificate ya Mwaka 1985 au 90 ukamfafanisha na mwenye certificate ya miaka ya 2020. Ni watu wawili tofauti.

Kuna mabadiliko wameyatoa lkn hawaheshimu walimu wenye diploma. Wanadhani wanafanana na wenye degree za miaka 2020. Hawa Wana utofauti mkubwa sana
 
Back
Top Bottom