Philip Mangula vs Dr. Willibrod Slaa

Philip Mangula vs Dr. Willibrod Slaa

Nani mkali kati ya MANGULA na DR. SLAA?

  • MANGULA

    Votes: 7 5.3%
  • DR. SLAA

    Votes: 126 94.7%

  • Total voters
    133
  • Poll closed .
Status
Not open for further replies.
Ni makosa kumfananisha Mangula na Dr.Slaa kwani kwa kuangalia CHADEMA kilikuwaje na kikoje hivi sasa, ndipo utapata jibu la ni nani anaweza kuwa juu ya mwenzie.Ni hoja dhaifu kusema Mangula ameongoza watu 6mln wakati tunajua Watanzania ni zaidi ya hao.Kiongozi mzuri ni yule anayewaongoza hata neutral members na kuwavutia upande wake kitu ambacho kimeonekana kwa Dr.Slaa. Kwa upande mwingine tunapima"leadership supporting hand", kwa upande wa Mangula alikuwa na wakuu wa mikoa na wilaya ambao ni wajumbe wa kamati za siasa wakati Dr.Slaa anategemea wabunge na sehemu ambako hakuna wabunge hutumia juhudi binafsi kuwashawishi watu na kuonesha uhai wa chama. Sababu nyingine ni UCHUMI WA VYAMA: Mangula ameongoza ccm chenye vyanzo vingi vya mapato kama vile majengo na viwanja vya michezo kama Kirumba na ruzuku kubwa hivyo kuwa na mazingira mazuri ya kuwalipa viongozi wa ngazi za chini ili kuwatia hamasa ya kuimarisha chama pamoja na kumudu gharama za uenezi, Lakini Dr.Slaa amefanikiwa bila fedha!
 
vijembe wapi mkùu tupe hoja mangulaàliongoza makatibu wakûu wa vchama kuanzia mikoani mpaka mashinani vp babu?

Mkuu mtz one, hata kama humpendi Dr. Slaa mpe haki yake, anaitwa Dr.Slaa (Phd) na sio babu.
Dr. Slaa ni zaidi ya Mangula tena sana. Dr. Slaa ni katibu wa CDM, kaiongoza ikiwa changa hadi kuwa tishio kwa chama tawala (CCM). CCM sa hivi hawalali sababu ya CDM, wakila chakula inakuwa maji tumboni coz of stress from CDM. Yeye na M/kiti wake wamebuni mikakati mbalimbali ya kuwezesha chama kukuwa na kuwa tumaini la watanzania walio wengi.

Back to Mangula nipe mafanikio yake halisi???? achana na statistics za kubumba (maana ww mwenyewe hujui chochote kuhusu idadi ya wanachama wa CCM). Pili usiongelee uchaguzi-mana unajua fika kuwa CCM tokea mwaka 1995 wanaiba kura (they have been ridging election) na kutumia dola kuwapiga na kuwaumiza wapinzani.

Ukiacha kejeli na kujadili kwa hoja, hata wewe moyoni mwako unamkubali Dr. Slaa, tatizo kubwa ni njaa tu ndugu yangu.
 
japo post si yangu naomba nikwambie tuache ushabiki wa kiroho huwezi kumlinganisha mangula na slaa kwanza mangula aliongoza CCM kama taasisi na wanachama wengi huwez kumlinganisha na slaa anaeongoza kampuni jadili kisomi mkuu

Huwezi mlinganisha Mangula na Dr. Slaa, umemdharau Dr.
 
Duh!!! unamfananisha simba (dr) na mbwa mwitu (magula).
Dont under weight our upcoming pres D.
Wadau kama
tuwajuavyo majembe hayo mawili wote wamepata kuwa na hadhi ya ukatibu
mkuu wa chama ingawaje mpaka sasa dr. slaa bado ni katibu lakini katika
utendaji wao hawa watu kila mtu ana mafanikio yake hasa historia zao za
kutukuka sasa je kati ya hawa unafikiri ni yupi ana mvuto na uwezo zaidi
wa kiuongozi?? piga kura yako
 
mangula nafikiri ni zaidi coz ameongoza CCM taifa zima na kama tujuavyo CCM na CDM ni mlima na kichuguu huwezi kusema slaa anamzidi mangula vinginevyo ni utashi wako binafsi

kiazi we!!unaleta mada tupige kura halafu unaleta ushabiki..ulitakiwa kuwa neutral gamba wewe
 
Tuna mdhalilisha Dkt Slaa kwani haiwezekani kulinganisha mlima na kichuguu. OCTOBA 2007. Wakati Mangula akihojiwa na gazeti la Raia mwema, nyumbani kwake kijiji cha Kinenulo,Iringa baada kubwagwa ktk uchaguzi Mwenyekiti CCM mkoa Iringa alipata kusema " NIKAMWONYESHA KIPEPERUSHI CHENYE MAALEZO YANGU BINAFSI. AKANIKEJELI KUWA WAJUMBE HAWATAKI HAYO SIKU HIZI. WAO HIVI SASA WANASEMA WANATAKA VIPEPE-RUSHWA ,NA SIO VIPEPERUSHI VYA MGOMBEA. HII NDIYO TABIA YA WAPIGA KURA WETU WA SASA. CCM YA SASA SIO KILE CHAMA KILICHO ONGOZWA NA MWALIMU NYERERE ." Nina waomba wakuu murejee kauli hiyo ya Mangula halafu tumutendee haki ipasavyo. Mangula is like a toothless dog to bring changes .
 
uzuri CCM wanacheza kama pele nyie bwatenii habari kamili uwanjani ndani ya dk 90 Ataonekana mshindi nani wenzenu wametulia nyie mnababaika na watoto wanaowajazia mikutano ya hadhara
 
kiazi we!!unaleta mada tupige kura halafu unaleta ushabiki..ulitakiwa kuwa neutral gamba wewe

mtoa uzi kasiz maana hakujua humu dr kapanga safu yake hasa wapiga kura wanaomiliki akaunti kumi kumi
 
Hahahahah jamaa unaota!!! zinduka for God's sake this is Dec 2012....huyo mangula aliiongoza ccmweli kipindi kipi??? na kwann walimweka pembeni??? na kipi kilichowafanya wamrudishe tena??? mangula is history...dr.slaa is the hottest news in town!!!

Respect !
 
tunapojaili vitu jamani tuwe na fikra pana hivi nyie mfano unaweza kusema kwa dhamira yako slaa anamzidi mangulaàliyeongoza chama dola kwa miaka 10? hebu acheni ushabiki maandazi jamani tusijadili mambo kwa kuongozwa na emotions zetu
 
Kuongoza watu wengi sidhani kama ndiyo kigezo pekee. Kuongoza ni kubahatika tu( chance) ya kuwa kiongozi. Ubora wa uongozi ni matokeo ya kazi zako kama kiongozi. Umefanya nini? Ukutana na changamoto ngapi na umekabiliana nazo namna gani. Ubora wa maamuzi yako kama kiongozi. Dr. Slaa ni kweli ameongoza kundi dogo ukilinganisha na Mangula lakini je amekutana na changamoto ngapi na amekabiliana nazo namna gani hii ndiyo hoja. Mangula halikadhalika apimwe kwa kigezo hichohicho. Ikiwa utapima kwa idadi ya watu unaowaongoza, je; Yusu Makamba pia ameongoza CCM chama chenye idadi kubwa ya wanachama je; anamzidi Dr. Slaa. Halikadhalika Joseph Kabila anaongoza DRC, nchi yenye idadi kubwa ya watu Je; anamzidi Kagame?
Hoja hapa nadhani isiwe idadi ya watu unaowaongoza bali iwe matokeo chanya ya uongozi wa mtu.
Mangula aliwahi kutetea makundi ndani ya chama chake, alisema " shughuli ya siasa ni ya makundi hivyo makundi ndani ya chama ni jambo la kawaida" Akaendelea kusema" baada ya uchaguzi ndani ya chama makundi yatakufa" Wote ni mashahidi. Leo makundi yanastawi na hayaelekei kuisha kesho au keshokutwa. Nina hakika alitoa kauli hii baada ya kushindwa kuyakabili makundi. Sielewi anarudishwa kwenye uongozi kufanya nini ikiwa ameshiriki kutoa maamuzi yanayokiangamiza chama chake. Dr. Slaa amekua katibu wa baraza la maaskofu Katoliki, sijapata maamuzi yoyote aliyofanya kwenye taasisi hiyo na wala sijui aliacha kwa sababu zipi hivyo siwezi kujadili. Amekuwa Katibu mkuu wa CHADEMA KWA MIAKA miaka minne sasa. Migogoro ndani ya chama chake ndiyo kwanza inaanza haijaisha. Ni vipi atakabiliana na tuhuma za chama kuwa cha kikanda zaidi, Zito Zuberi Kabwe na harakati zake za kutengeneza kundi ndani ya chama atakabiliana nazo vipi? Sera yake ya kufukuza fukuza wanachama wanaodhani ni wakorofiitakisaidiaje chama chake. Je; ataongeza idadi ya wabunge na madiwani katika uchaguzi ujao, je; atakivusha chama kutoka kuwa chama cha upinzani na kuwa chama tawala? Maamuzi mangapi challenging ameyafanya yanayokiimarisha chama?
mazingira magumu kudidimiza akina ZZK??? MANGULA kaongoza akili za watu 6,000,000 vp huyo babu yenu??
 
ulinganifu gani huu wa kitoto namna hii?
mnaweweseka sana nyie aisee!
Dr. uwe na maisha marefu tuzidi kuona watu wanavyochanganikiwa juu yako...
 
Dr. Slaa ukimwangalia tu usoni utajuwa anayosema siyo ya kinafiki, ndio maana kwa sasa hana mpinzani hasa kutoka ccm, wapo watu wengi wenye madegree yao na uwezo wa kuongoza lakini ni wanafiki na wabinafsi. kwa hali ilivyo sasa tunataka mtu ambaye ni mzalendo wa kweli na siyo mtumikia mafisadi, Tanzania bila "nyinyiem" inawezekana, Just play your part it can be done
 
Mleta thread mbona unataka kumwaibisha huyu mzee Mangula na SSM yake!! Tayari aibu imaeanza na hali ni tete!! Tumaini pekee la hii nchi ni Dr. Wilbroad Slaa tu.. Mungu mlinde Dr. SLaa na vitu vya ncha kali!! Asije akapigwa Risasi ya kichwa na mdono kama yule Paroko Zanzibar. Malaika walinzi muwekeeni himaya ya ulinzi!! Amen.
 
CCM milioni sita (6,000,000) ni sawa na Chadema Sita (6).Maana hata bungeni wabunge wa chedema less than fifty wamewafunika Wabunge wengi wa CCm,ukiacha wale wachache revolutionary kama kina filiku...,
Hivyo bas,DR. ni Kiboko zaidi Mangula.CCM "ndiyo Mzee" wengiiiiiiiii
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom