Wadau kama tuwajuavyo majembe hayo mawili wote wamepata kuwa na hadhi ya ukatibu mkuu wa chama ingawaje mpaka sasa dr. slaa bado ni katibu lakini katika utendaji wao hawa watu kila mtu ana mafanikio yake hasa historia zao za kutukuka sasa je kati ya hawa unafikiri ni yupi ana mvuto na uwezo zaidi wa kiuongozi?? piga kura yako
Rob
Umeleta uzi ambao ni skeleton and to that effect umeacha wachangiaji wajaribu ku-stuff it with flesh no matter it's fresh or stinking or filth. Ndio maana hapa baada ya kujadili issues watu wanachangia matusi. Ulipashwa utupatie vigezo vya kuwapima na hapo tupate kupiga kura. Magula kama katibu mkuu wa CCM wa wakati ule na Slaa katibu mkuu wa sasa these are two characters diametrically opposed. CCM kimekuwa ni chama dola na baadae chama kinachosaidiwa na dola kwa namna yoyote ile iwe kwa lazima au kwa wahusika wanaotegeneza dola kujikomba. Magula amekuwa katibu mkuu kwa wakati ule na kiongoza wananachama ambao wachangiaji wanasema 6million. Great, let us put ourselves in their shoes. Lakini wakumbuke kuwa sio Mangula aliyewatafuta weingi waliingia kwa mapenzi yao na wengine ikiwa ni kwa ajali ya kihistoria ili wapate kusoma au wapate passports.
Dr.Slaa anaongoza chama ambacho kimestruggle desperately from the scratch. Unapata wanachama wengine si kwa mapenzi ya dhati ya hitikadi yako bali kwa sababu wameshindwa kupata upenyo CCM. Wanakuja CDM kwa sababu lazima wawe na chama tena kinachokua ili wapate kwenda point B. Wengine ni mamluki. Panahitajika mtu wa kuweza kuwatambua hawa wote na kuweza kutoa uongozi na sanctions. Je, Dr.Slaa ameweza kuwatambua hawa na kuweza kutoa reliable leadership and sanctions when needed. Hapa huwezi kumlinganisha na Mangula. Sote ni mashuhuda na tunaona anavyojitahidi bila kuchoka.
CDM ina hitikadi yake na haioni aibu kujitambulisha kwayo. CCM hatujui mpaka kesho wana hitikadi ipi. Wanasema ujamaa na kujitegemea. Hivi ni kweli? Mwasisi wake Mwalimu Nyerere alisema walipokutana Zanzibar wakalivunja Azimio la Arusha ahalafu wakarudi kimyakimya. Waliua blue print halafu wakaanza kuendesha mambo kivyao vyao na wala sio kibepari maana kusema kibepari ni kuwatukana wanaofuata siasa ya kibepari ambayo ni sociala market economy ambapo soko linawajibika kwa watu. Sisi hapa tunawajibika kwa soko ambapo kuna wanaogelea kwenye utajiri wakati kuna wengi jirani ambao wako katika umasikini wa kupindukia.
Rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma imekuwa ni kama sera ndani ya CCM. Rejea EPA na jinsi pesa hiyo ilivyotumika katika uchaguzi wa 2005. Ni kipindi ambacho CCM ilishindwa kuisimamia serikali na matokeo yake viongozi wa serikali wakashiriki uporaji rejea ubinafsishaji wa mashirika ya umma usiokuwa na maslahi, mikataba laghai ya madini na viongozi kufanya biashara wakiwa madarakani (Kiwira na Mkapa).
Nisaidie kwa kusema labda tuweke vigezo tuwapime kwa yafuatayo:-
1.kusimamia sera
2.kubuni na kutekeleza mikakati endelevu
3.kuchukia, kukemea na kuzuia rushwa na mianya ya rushwa
3.kutekeleza kwa vitendo hitikadi ya chama
4.kufanya maamuzi kwa mujibu wa katiba ya chama
5. kuzuia na kukemea aina yoyote yamakundi
Nawasilisha