Peter Msigwa kurudi CHADEMA Machi 23, 2025?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,921
Reaction score
63,641
Kuna kila dalili za aliyekuwa Mbuge wa Iringa, Mwenyekiti Kanda ya Nyasa na Mjumbe wa Kamati kuu na Mkutano Mkuu Mchungaji Peter Msigwa kurudi CHADEMA 23/03/2025.

Kashajitenga na CCM.

Je, Urafiki wake na Tundu Lissu Mwenyekiti wa CHADEMA ndo unamfanya alambe matapishi yake?

Mwingine anayepokelewa CHADEMA ni Dr. Slaa.

Kama ikiwa hivyo, CHADEMA itakuwa imezaliwa mara ya pili. Kila la heri

Msigwa alitambulishwa kuwa mwanachama mpya wa CCM baada ya kutimka kutoka CHADEMA Siku ya Jumapili, Juni 30, 2024, mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho (NEC), katika kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wake, Rais Samia Suluhu Hassan. Kama atarudi CHADEMA, atakuwa hajaa huko hata mwaka mmoja.

Mchungaji Peter Simon Msigwa

Msigwa aliikimbia CHADEMA baada ya kushindwa na Joseph Mbilinyi (Sugu) kwa tofauti ya kura mbili tu, katika uchaguzi wa ndani wa CHADEMA uliofanyika Mei 29, 2024 huku akimshtumu aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, kwa kutumia mamlaka yake kuingilia mchakato wa demokrasia ndani ya chama kulazimisha watu anaowataka yeye ndo wawe washindi.
 
Huyo alishindwa kabisa kuhama CHADEMA, alikuwa akili na roho yake iko CHADEMA ila mwili CCM aweze kula. Nadhani unachosema ni sahihi lazima atarudi. CCM wamemkaushia hana dili.
 
Uzuri msigwa alishaweka wazi hana ugomvi na chadema ila hakubaliani na mfumo wa uongozi wa Mbowe the Autocratic, anaeendesha chama kama sultan kwa zaidi ya miaka 20, huku akiwa hakubaliani na mawazo mbadala.
 
Kwa hiyo joseph mbilinyi kaondoka chadema!
 
Huyo ameshaitukana sana Chadema asirudi akae huko huko kwa wauaji, kwanza alichangia mauaji ya kikatili ya Mzee wetu Ali Kibao
Mtaji wa Chama cha siasa ni Watu. Kama hakitaki watu kitajiitaje chama cha siasa. Pia kuwa majini na mihemko yako, acha kutukana watu hata kama hukubaliani na maamuzi yao.

Alichangiaje mauaji ya Ali Kibao? Wenzio hatujui
 
Si vibaya kashakula Mamilioni ya ccm.

Mjini akili.
 
Mtaji wa Chama cha siasa ni Watu. Kama hakitaki watu kitajiitaje chama cha siasa. Pia kuwa majini na mihemko yako, acha kutukana watu hata kama hukubaliani na maamuzi yao.

Alichangiaje mauaji ya Ali Kibao? Wenzio hatujui
Wapi nimetukana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…