Lu-ma-ga
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 4,780
- 3,228
Walizoea kusikia trilion kadhaa zimeibiwa .Kusikia reliable imejengwa, viwanja vya ndege kukarabariwa, zahanati 350 kujengwa au wanafunzi kusoma bure. Kwa ni miujiza kama kufufuka bwana Yesu.
Muwe mnaumiza vichwa kabla ya kuweka uzi jukwaani. Mnasahau kuwa awamu zilizopita pesa ya chai maofisini ilikuwa ni mabilioni ya shilingi?.
Mnasahau kuwa mikutano ya wizara na taasisi za kiserikali siku hizi haifanyiki tena bagamoyo na kule kwenye mahoteli ya baharini?.
Mnasahau kuwa vitu kama drones vilikuwa havitozwi kodi lakini kwa sasa ndio chanzo cha mabilioni ya mamlaka ya anga kimapato?.
Mnasahau kuwa yeye mwenyewe Ngosha hajatoka nje ya afrika tangu aingie magogoni?. Mnasahau ile misafara ya kwend New York yenye watu zaidi ya 40 wanaolipwa posho ya kila dakika wakiwa kule?.
Ngosha kabana matumizi yasiyo na ulazima, matokeo yake pesa zinaenda kufanya mambo yenye tija kwa taifa.