Pesa taslimu za kununua ndege anazipata wapi?

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Heri ya Krismas wakuu.

Naomba kufahamishwa. Pesa taslimu za kununua haya madege anazipata wapi? kuna mtu alinitonya kuwa mzeebaba amesanya pesa zote kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hadi kuifilisi na alipoona hivyo akaja na spin za kuiunganisha kubaki na mfuko mmoja na baada ya hiyo spin akaja na twisti nyingine ya wenye pesa zao kupewa 25%. je haya ni ya kweli?

kama siyo ya kweli pesa taslimu kununua madege mapya anazipata wapi?
 
Heri ya Krismas wakuu.

Naomba kufahamishwa. Pesa taslimu za kununua haya madege anazipata wapi? kuna mtu alinitonya kuwa mzeebaba amesanya pesa zote kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii hadi kuifilisi na alipoona hivyo akaja na spin za kuiunganisha kubaki na mfuko mmoja na baada ya hiyo spin akaja na twisti nyingine ya wenye pesa zao kupewa 25%. je haya ni ya kweli?

kama siyo ya kweli pesa taslimu kununua madege mapya anazipata wapi?
Sisi ni nchi tajiri tunaweza kua ata donnor country......hii nchi ilikua inachezewa sana nawapiga dili wafanya biashara walikua hawalipi kodi.....na kulikua na wafanya kazi hewa kila sehemu......
 
Mkuu Si ulishaambiwa ni pesa za ndani? Unataka jibu gani tena?ili baba anunue bajaji pale nyumbani kwa kutumia pesa za biashara ya mayai ambayo watoto ndo mnafuga hao kuku, kutakuwa na haja ya kuwaeleza kilichotokea? Si mtaiona bajaji na pesa za mauzo ya mayai hamtaziona wala yale mayai mlikuwa mnaacha mle asubuhi na chai hamtayaona? Kuna haja ya kuambiwa tumeuza mayai yote na Ile pesa ya kuuza mayai tumenunua bajaji wakati wote tulienda ipokea bajaji wakati inaletwa? Pesa za ndege zinatoka ndani, ndani ya nchi, haya haya makusanyo ya ndani ya nchi. Acha maswali.
 
Naona kama unongeza utata vile ..Haya twambie kapata wapi hizo za kulipia hiyo mifuko ukimaliza twambie hiyo ya ndege.
Aisee. Kwann mnauliza maswali ya uelewa wa kiwango hiki kipindi cha sikukuu lakini? Haya Ngoja tusubiri majibu kama yapo.
 
Kwani hela za:
Elimu bure
Afya
Mishahara
SGR
Stiglers
Hizi zote anazipata wapi?
Ina maana hadi umri huu hujui vyanzo vya mapato ya serikali?
Au unataka majibu ya kukufariji kwamba anaziiba?
Nimegundua hakuna kitu kinawapa tabu kama ununuzi wa ndege.
Badala ya kuhoji trillion 7 za kujenga SGR anazipata wapi wewe unaulizia bilioni 700 za kununua ndege?
January Airbus nyingine inaingia.
KAA DAWATI LA MBELE USOME NAMBA VIZURI.
 
Watanzania sjui baadhi yenu mnaakili gani.
Angeshindwa kulifufua mngemcheka saana
2015 si aliwaambia mkimchagua atazinunua
Mpaka hapo kashafanikiwa, watendaji sasa washindwe tu tuwapige kitanzi. Watu wanalalamika arafu wao walete upumbavu. Wafanye kazi ikiwezekana usiku na mchana mpka tu break even.
 
Muwe mnaumiza vichwa kabla ya kuweka uzi jukwaani. Mnasahau kuwa awamu zilizopita pesa ya chai maofisini ilikuwa ni mabilioni ya shilingi?.

Mnasahau kuwa mikutano ya wizara na taasisi za kiserikali siku hizi haifanyiki tena bagamoyo na kule kwenye mahoteli ya baharini?.

Mnasahau kuwa vitu kama drones vilikuwa havitozwi kodi lakini kwa sasa ndio chanzo cha mabilioni ya mamlaka ya anga kimapato?.

Mnasahau kuwa yeye mwenyewe Ngosha hajatoka nje ya afrika tangu aingie magogoni?. Mnasahau ile misafara ya kwend New York yenye watu zaidi ya 40 wanaolipwa posho ya kila dakika wakiwa kule?.

Ngosha kabana matumizi yasiyo na ulazima, matokeo yake pesa zinaenda kufanya mambo yenye tija kwa taifa.
 
Back
Top Bottom