Yeah, may be...
But can you calculate how much has been saved from those angles of expenditures?
And are sure kweli kweli hakuna safari za kiserikali outside Africa? Hakuna semina? Kweli kabisa?
Hivi unajua ni gharama kiasi gani zimetumika kwa kununua wanasiasa wa upinzani (wenyeviti wa vijiji/mitaa, madiwani na wabunge?
Unajua ni gharama kiasi gani zimetumika kufanya chaguzi za marudio kuziba mapengo ya walionunuliwa?
Unajua mpaka sasa serikali inadaiwa kiasi gani na watoa huduma mbalimbali kwenye idara na taasisi za serikali?
Unajua serikali inadaiwa kiasi gani na wafanyakazi wake (watumishi wa umma) kama madeni halali kwa mishahara mipya na malinbikizo?
Najua hili la mwisho unaweza ukasema "hakuna kitu kama hicho kwa sababu serikali imelipa na haidaiwi chochote"
Ni kujidanganya na kumbuka deni haliozi. Hata kama yeye atakayakana leo, lakini yatafufuliwa kwa kiongozi ajaye. Huyu yeye si ni mbabe bwana wa kudhulumu haki za watu?
Kwa hiyo hili ninaweza kulisema kirahisi kwa namna hii:
Anapora haki na stahili mbalimbali halali za kisheria za watumishi wake wanaosota usiku na mchana wakifanya kazi, badala fedha hizo zinazikwa kwenye kununua eti ndege na ninyi ku - shout eti amebana matumizi, aka - save na kisha kununulia ndege, kujenga SGR nk!!
Ni uongo, siyo kweli kwa 100%!!