Penzi la Mzee Ngowi na mkewe ni funzo kubwa kwetu

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,720
10,215
Mzee Ngowi na Bi Sikitu ni wapenzi walio pendana toka shuleni wakiwa watoto, mpaka wakaoana. Baada ya kustaafu waliamua kurudi kuishi eneo waliloushi zamani walipokuwa wadogo, na kusoma.

Siku moja walikuwa wanasherehekea miaka 40 ya ndoa yao. Hivyo waliamua kutembelea shule yao waliposomea zamani ili kusherehekea miaka 40 yao ya ndoa.

Wakishikana mikono, walitembea kwenda shuleni kwao. Geti la shule lilikuwa halijafungwa, hivyo wakaingia na kwenda kwenye dawati lao la zamani walilokuwa wanatumia ambalo Mzee Ngowi alikuwa ameandika "Nakupenda, Sikitu."

Baada ya kumaliza kusherekea wakaanza safari ya kurudi nyumbani kwao, lakini njiani wanakuta begi likiwa halina mwenyewe.

Bi Sikitu anaokota begi ilo na kuangalia kuangalia ndani, na kukuta begi limejaa hela. Hakutaka kupoteza muda akalibeba, wakaendelea na safari mpaka nyumbani kwao.

Wakiwa nyumbani Mzee Ngowi akasema, "Tunapaswa kurudisha begi la watu."

Bi Sikitu akasema, "Cha kuokota sio cha kuiba, hata hivyo aliyeokota ni mimi." akafunga begi vizuri na kulihifadhi juu ya paa lao.

Siku inayofuata, maafisa wawili wa polisi walikuwa wakizunguka jirani wakitafuta pesa na wakagonga mlango wao.

"Samahani, je, mmoja wenu aliona begi lililodondoka kutoka kwenye gari la kubeba pesa jana?"

Bi Sikitu akasema, "Hapana."

Mzee Ngowi akasema, "Anawanganya, amelificha juu kwenye paa."

Bi Sikitu akasema, "Msimuamini anaanza kuzeeka."

Maafisa wakageuka kwa Mzee Ngowi na kuanza kumhoji.

Mmoja wao akasema: "Tuambie hadithi kutoka mwanzo ilivyokuwa."

Mzee Ngowi akasema, "Vizuri, wakati Sikitu na mimi tukiwa tunarudi nyumbani kutoka shuleni jana."

Afisa wa polisi wa kwanza akageuka na kumtazama mwenzake na kusema, "Tuondoke hapa tukatafute mahali pengine."

Mwisho 😎🧵...
 
Wakishikana mikono, walitembea kwenda shuleni kwao. Geti la shule lilikuwa halijafungwa, hivyo wakaingia na kwenda kwenye dawati lao la zamani walilokuwa wanatumia ambalo Mzee Ngowi alikuwa ameandika "Nakupenda, Sikitu."
Coincidence ya ajabu, geti halikufungwa na hata mlango wa darasa nao haukufungwa
 
Mzee Ngowi mchaga
Sikitu ni marina ya kimakonde
....... utamalizia mwenyewe
 
Coincidence ya ajabu, geti halikufungwa na hata mlango wa darasa nao haukufungwa
Sio hivyo tu mkuu, pia na kulikuta dawati walilokuwa wakikaa miaka 40 iliyopita alilokuwa ameandika Ngowi kuwa anampemda Sikitu liko palepale😂😂
 
Sio hivyo tu mkuu, pia na kulikuta dawati walilokuwa wakikaa miaka 40 iliyopita alilokuwa ameandika Ngowi kuwa anampemda Sikitu liko palepale😂😂
Darasa halifagiliwi au kudekiwa madawati hayasafishwi wala maandishi kufutika kutokana na dawati kushikwashikwa 😅🤣 Ngowi anatisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom