Mkuu JME, nimekusaidia kidogo kwenye maeneo niliko weka red!, jina rasmi la Pengo ni Muadhama Policarp, Kardinali Pengo.Kunapofanyika makosa, tunatumia sheria mbili, jinai, na madai (criminal na civil), criminal mshitaki ni jamhuri, na kwenye civil mshitaki ni aliyeadhirika!. Kwenye hili Pengo hajashitaki popote hivyo hata akisamehe, msamaha wake haizuii jamhuri kuendelea na uchunguzi wake wa kijinai!.Kanisa Katoliki ni moja ya madhehebu ambayo yako very strict kwenye kufuata sheria, taratibu na kanuni, na linapokosema na mtu ambaye sii muumini, huweza kutoa msamaha kama huu kirahisi rahisi tuu kwa maana kwa mujibu wa kanisa, huyo Gwajima ni kama mtu tuu wa mataifa hajui atendalo!. Angekuwa ni Mkatoliki ingempasa kuungama, na kupewa adhabu ya kutimiza malipizi!.Pasco