Pengo: Nimesamehe

Pengo: Nimesamehe

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp, Kardinali Pengo amesema amemsamehe Mchungaji Gwajima na wote walioguswa .ameyesema hayo wakati wa ibada ya leo Jumapili katika kanisa la St. Joseph amesema "naomba niseme kutokana na hali iliyopo kuwa kutoka moyoni kabisa nimesamehe yote yaliyosemwa na naomba tumuombee na kuwaombea wote walioguswa sina kinyongo chochote"waumini walilipuka kwa makofi baada ya kusikia kauli ya Mwadhama.My take:Niishauri serikali kuachana na Gwajima madam Mwadhama ametamka tena huku akiwa amekalia kiti cha kiaskofu kwa sisi Wakatoliki nadhani tunajua maana ya tamko linapotolewa huku askofu akiwa amekalia kiti chake maana yake Mungu ameupokea msamahasource Mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye misa
Mkuu JME, nimekusaidia kidogo kwenye maeneo niliko weka red!, jina rasmi la Pengo ni Muadhama Policarp, Kardinali Pengo.Kunapofanyika makosa, tunatumia sheria mbili, jinai, na madai (criminal na civil), criminal mshitaki ni jamhuri, na kwenye civil mshitaki ni aliyeadhirika!. Kwenye hili Pengo hajashitaki popote hivyo hata akisamehe, msamaha wake haizuii jamhuri kuendelea na uchunguzi wake wa kijinai!.Kanisa Katoliki ni moja ya madhehebu ambayo yako very strict kwenye kufuata sheria, taratibu na kanuni, na linapokosema na mtu ambaye sii muumini, huweza kutoa msamaha kama huu kirahisi rahisi tuu kwa maana kwa mujibu wa kanisa, huyo Gwajima ni kama mtu tuu wa mataifa hajui atendalo!. Angekuwa ni Mkatoliki ingempasa kuungama, na kupewa adhabu ya kutimiza malipizi!.Pasco
 
Kasuka ni kasuku tu. Unasema uliyokariri. Ndio maana kukomesha rushwa, ufisadi na sembe ni kazi kubwa Tanzania. Haijalishi ni Kilaini au Gwajima, mtu lazima awe na uwezo wa kueleza kapata wapi pesa zake.

Kama hujui sheria hiyo ipo Tanzania na wamarekani wanashangaa kwa nini haitumiki. Mtu anajenga ghorofa from nowhere lazima aeleze mapato yake na kodi ipi kalipa serikalini. Tunahangaika kutafuta mafaili nani kaiba wakati matunda ya wizi au uuzaji wa sembe yapo dhahiri.

Kama amenunua Chopper kwa hela ya sadaka, athibitishe hilo kwa kuonyesha flow ya mapato yake. Kila week anapata kiasi gani na jinsi anavyo deposit bank.

Sheria tajwa inafumbiwa macho maana itawakumba wakubwa. Sasa wewe umekariri ya kukariri. Akija kiongozi akaitumia hiyo sheria wengi watakimbia nchi nakuhakikishia maana hawawezi kueleza mali wamepata wapi. Lakini kila mtu anajua ni ufisadi au sembe.

kanisa katoliki kama yalivyo makanisa mengine. linamiliki mali nyingi ikiwemo majengo. shule. hospitali . vyuo. ardhi. benki. vyote ni zao la sadaka. swala la mali zake haikua msingi wa yeye kuitwa kutoa maelezo. aliitwa kuzungumzia lugha chafu. kama kuna wasiwasi kuhusiana na mali zake then thats the differen case. inayotakiwa muda wake separately.
 
Gwajima ni wa kumsamehe tu, hana akili nzuri. Kuna clip nimemskia akidai alikuwa anamkemea askofu mwenzake. Yaani Gwajima askofu wa mtaani anataka kujilinganisha na Pengo!!?

Alafu anadai mwenyekiti wa maaskofu wa katoliki ndiye mkuu wa kanisa katoliki Tanzania. Ana uelewa mdogo sana. Sijui anawezaje hata kuwatapeli wafuasi wake kiasi hicho.

Tena akasisitiza sana kwamba Rais wa TEC ndo mkuu wa Kanisa katoliki TZ.
 
Nilisema na Narudia kusema. Hili Sakata Pengo hausiki kwa kinachompata Gwajima. Hawa ni viongozi wa Dini, wanajua wapi pa kukutana wanapokwaruzana. Kuna mtu kajificha nyuma ya Ajenda hii, na ni kwa sababu zenye maslahi mapana kwa Huyo Mtu!
Mungu Akubariki Askofu Pengo, na pia akuongezee Hekima ili uwe na Umoja na Maaskofu wenzako
 
Sasa kwa kuwa mlalamikaji mkuu Pengo amesamehe basi vikosi vya askari havina budi kuondoka haraka hsp kama bado wamemuweka Gwajima chini ya ulinzi.
tafadhali kova toa maelekezo vijana wapo timamu.
 
askofu mkuu wa jimbo la dar es salaam mwadhama pengo amesema amemsamehe mchungaji gwajima na wote walioguswa .
ameyesema hayo wakati wa ibada ya Leo jumapili katika kanisa la st joseph
amesema "naomba niseme kutokana na hali iliyopo kuwa kutoka moyoni kabisa nimesamehe yote yaliyosemwa na naomba tumuombee na kuwaombea wote walioguswa sina kinyongo chochote"
waamini walilipuka kwa makofi baada ya kusikia kauli ya mwadhama

Mytake:niishauri serikali kuachana na gwajima madam mwadhama ametamka tena huku akiwa amekalia kiti cha kiaskofu kwa sisi wakatoliki nadhani tunajua maana ya tamko linapotolewa huku askofu akiwa amekalia kiti chake maana yake Mungu ameupokea msahama
source Mimi mwenyewe nilikuwepo kwenye misa

Ametenda mema pengo kama ni kweli kusamehe ndio nguzo yetu kuu wakristo hatupo kwa ajili ya visasi tupo kwa ajili ya kupendana, kusaidiana, kusameheana pale mwenzako anapokukosea, na kumwombea anayekukwaza Mungu apate kuulegeza moyo wake na kufarijiana hata malaika wa mbinguni hufurahi anapoyaona matendo yetu mema , asiyependa haya ni shetani peke yake.
 
Matusi aliyoyatoa Gwajima kwa Pengo hayakua mazuri tena kwa kiongozi wa kiroho unaongeaje namna ile. Siungi mkono alichokisema Pengo kuhusu mahakama ya kadhi lakini hiyo haimpi mtu yoyote kumtolea matusi kama yake mzee wa watu. Gwajima alikosea na anahitaji kuombewa kweli.
 
kanisa katoliki kama yalivyo makanisa mengine. linamiliki mali nyingi ikiwemo majengo. shule. hospitali . vyuo. ardhi. benki. vyote ni zao la sadaka. swala la mali zake haikua msingi wa yeye kuitwa kutoa maelezo. aliitwa kuzungumzia lugha chafu. kama kuna wasiwasi kuhusiana na mali zake then thats the differen case. inayotakiwa muda wake separately.

Mkuu, nakuelewa lakini hakuna cha kuwazuia polisi kufanya kazi yao. Muda separate upi? Wanaweza kukuita kwa masuala mengi tu na ndio maana mtu anaweza kusomewa mashitaka hata kumi - hakuna limit. Ndio maana wenye akili zao hufanya namna ya kukwepa kufika polisi kwa sababu yoyote.

Fikiria mfano wengi wanaozamia nchi za nje bila hati za kusafiria. Anaweza kuishi hata miaka ishirini bila shida. Lakini siku akiingia polisi kwa sababu yoyote kama wizi au vurugu, lazima aulizwe na hati zake. Huwezi kusema isubiri muda wake.
 
Dhambi ya matusi itamtesa sana Gwajima.
Ni shida nyie fanyieni research hayo makanisa maya Ya kibiashara Ya mambo Ya ajabu ajabu na Aibu tupu yanawakamua walalahoi wa chini Kabisa na wao wanaishia ukwasi wa kufa mtu .unajua watanzania wana matatizo mengi sana internally sasa hao wachungaji kwao ndiko wanapoona nafuu ya kutua matatizo yao nao wakiwaahidi kuwatatulia matatizo yao sugu bila mafanikio .watanzania wanaishia kupata faraja kwa Kuwa wanakutana na wenzao wenye shida zinazofananafanana ila hao maaskofu wa mitaani walishachizika ni Mara nyingi mpaka wana act kufufua watu .hayo nimeyashuhudia na ni balaa sasa mngekuwa mnawajua msingeshughulika nao make hazimo
 
Dhambi ya matusi itamtesa sana Gwajima.

Nataka nikusaidie kitu ndugu yangu usije ukafa na hii dhambi , dhambi zoote ni sawa mbele Mwenyezi Mungu, kuzini, kuiba, kusema uongo, kusengenya, kutamani mali ya jirani yako, kudhulumu wajane, mayatima, na wanyonge, kukopa bila kulipa deni, ulevi, kuwa na kinyongo, kumchukia jirani yako, halafu unajifanya mnafiki ukisujudu na kumpenda Mungu ambaye humwoni lakini jirani yako humpendi hizo zoote ni dhambi na kama wewe msalani unajiona kikombe cha haya umekiepuka na uwe wa kwanza kumshitaki gwajima lakini hata ukijificha Mungu aliye sirini anakuona na anajua yoote uliyoyafanya na unayoyatenda tusipende sana kunyooshea wenzetu vidole kuwa wao sio wakati wewe una mzigo wa dhulma, unafiki, wizi, namengineyo ambayo ni siri yako wewe na nafsi yako.
 
Ni aibu siasa kuingizwa makanisani.

Kamwe huwezi kuliweka Kando Kanisa dhidi ya Siasa. Kanisa ni Kristo, na Kristo ndiye Mfalme, viongozi wa Kisiasa wanalelewa na Kanisa na Misikiti.
Hivyo, dini zote ndizo zinazo determine mustakabali wa Siasa za Nchi.
Ni kwa wasiojua tu Role ya Kanisa katika Siasa za nchi. Ni upunguani kudhani viongozi wa dini wataacha mambo ya Kisiasa yaende hivyo wanavyotaka watawala hata kama ni kutuangamiza. Watarudisha hesabu gani kwa Mungu?
Msichukulie haya mambo kirahisi,eti siasa makanisani! Kanisa lazima likemee Uovu katika Taifa,ndilo jukumu hili. Huwezi kuchunga kondoo na kuwaacha wale majani yenye sumu kisa tu wana Akili!
 
Huyu mjingaaa mmoja anamsamehe nani, si anapaswa kuomba radhi asamehewe, hakuna joka juu ya joka, aliyeanza kukosa aombe radhi sio ngonjera
 
Pengo na CCM ni ndugu moja alisoma darasa moja na mtoto wa mkulima.....so wanafiki utawajua tu kwa vile wanafanana
Uongo mwingine ni wa ajabu. Hata kwa umri wao tu hausimamii ukweli wa kauli yako kwamba kardinali Pengo anaweza kuwa amesoma darasa moja na Waziri Mkuu Pinda!
 
Mkuu JME, nimekusaidia kidogo kwenye maeneo niliko weka red!, jina rasmi la Pengo ni Muadhama Policarp, Kardinali Pengo.Kunapofanyika makosa, tunatumia sheria mbili, jinai, na madai (criminal na civil), criminal mshitaki ni jamhuri, na kwenye civil mshitaki ni aliyeadhirika!. Kwenye hili Pengo hajashitaki popote hivyo hata akisamehe, msamaha wake haizuii jamhuri kuendelea na uchunguzi wake wa kijinai!.Kanisa Katoliki ni moja ya madhehebu ambayo yako very strict kwenye kufuata sheria, taratibu na kanuni, na linapokosema na mtu ambaye sii muumini, huweza kutoa msamaha kama huu kirahisi rahisi tuu kwa maana kwa mujibu wa kanisa, huyo Gwajima ni kama mtu tuu wa mataifa hajui atendalo!. Angekuwa ni Mkatoliki ingempasa kuungama, na kupewa adhabu ya kutimiza malipizi!.Pasco

pasco i appreciate you.
 
Rabuor nahisi uelewa wako ni mdogo sn,sheria za nchi zinajieleza wazi kwa yule atakae toa matusi na lugha chafu kwenye hadhira ya watu hukumu yake ni nn,wwe umeangalia ndege ni kitu cha ajabu sn bila kujua yule jafanya kosa tena kwa makusudi kabisa,usiwe ndondocha la gwajima shtuka acha ujinga wwe
 
Back
Top Bottom