Pengo: Nchi imeoza!

Pengo: Nchi imeoza!

Hawa jamaa wao mgomvi wao ni Pengo kama mtu na si issues.Nchi kuoza haijasemwa na Pengo pekee hata Sitta anasema ina way kwamba Nchi imeoza ila wao wanakuja mahubiri ya nabii muongo hapa .Chuki zenu bure kabisa

Kama ungejibu hoja badala ya kuleta unsubstantiated allegations pengine ingesaidia kuona hoja yako.
Hapa Padri Privatus Kagurendo amejenga hoja kwa kutumia Biblia kwamba 'mipaka imevukwa'. Anasema wazi scope of the mission of Jesus did not cover worldly affairs.

Je, na wewe unaweza kutumia Biblia kujenga hoja y.a.ko?. Ndio maana nilisema nipatie ushahidi kwamba Biblia imeamrisha kukataza maovu na hadi dakika hii ya 90 hakuna aliyeleta ushahidi.

Nimeuliza scope ya anayoyasema yanadhibitiwa na nini, pia sikupata jibu.

Soma hoja ya Padri Privatus hapo chini.

Asanteni.

http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1668
 
Last edited:
Swali from MZINGANYIKA! ""Angekuwa Rais tungesema katiba inamdhibiti. Kama Kiongozi wa Kanisa ni kipi kinachodhibiti matamshi yake?"

JIBU LANGU: Mi nadhani wewe unamchukia Kardinali Pengo. Nasema hivi kwa sababu waraka huu si wa Pengo bali ni wa wakatoliki! Pengo naye ni mkatoliki, ila kwa bahati mbaya au nzuri ametokea kuwa kardinali!

Kazi ya kiongozi wa dini ni kulinda kondoo zake, Pengo na maaskofu wote wanalinda kondoo zao, yaani waumini. Sasa kuna shida gani kwa kiongozi wa dini kukemea ufisadi? Yesu aliwaambia wanafunzi wake "nendeni duniani kote mkatangaze habari njema". Ufisadi ni habari njema? Hapana! Tena hata waraka wa waislamu unasema tusichague mafisadi. Sasa mbona Waislamu hujawapinga? Ila wewe mtu unayemchukia ni Pengo tu!

Halafu nadhani kwa wakatoliki, Pengo ni kiongozi wao, so yes kwa madaraka aliyopewa na wakatoliki, ana official say kwao na si kwako kama wewe sio mkatoliki. Amechaguliwa na wakatoliki. Ukatoliki hauna nchi, ila wakatoliki wana uraia wa nchi zao, naomba hilo ulielewe. Naamini vile vile kuwa uislamu hauna nchi ila waumini wa kiislamu wana nchi zao, ndio maana lugha ya kiarabu inakubalika kwenye uislamu na Vatikani inakubalika kwenye masuala ya kikatoliki. Nadhani umenipata vizuri tu!
Ili uweze kuuelewa waraka wa wakatoliki, nakushauri ondoa chuki zako dhidi ya Pengo. Usome na uuelewe, ndipo hapo utakapoelewa Pengo anasema nini. Tafadhali jaribu kufanya hivyo. Haina maana kumchafulia jina Kardinali Pengo kwani hajasema kitu chochote kibaya. Nathani hilo unalielewa.

Mimi naona, waraka ni mzuri tu ila watu wanajaribu kutumia siasa kuuzika. Na nadhani hawatafanikiwa kwa hilo, kwa sababu sauti ya Mungu hupitia kwa viongozi wa dini. Hata kama mtapinga vipi, kama Mungu ametumia viongozi hawa kurekebisha jamii ya watanzania, hata kama mtatumia mbinu gani kupinga, mtashindwa tu. Hakuna anayeweza kupingana na Mwenyezi Mungu. Kama kamtumia Kardinali Pengo basi sauti yake itasikika tu, kama hakumtumia basi sauti ile haitazaa matunda. Ushauri wangu ni kuwa, tusubiri tuone! Au unasemaje ndugu yangu Mtanzania? Naomba vile vile kuuliza je wewe ni muumini wa dini gani?
 
Last edited:
Kama ungejibu hoja badala ya kuleta unsubstantiated allegations pengine ingesaidia kuona hoja yako.
Hapa Padri Privatus Kagurendo amejenga hoja kwa kutumia Biblia kwamba 'mipaka imevukwa'. Anasema wazi scope of the mission of Jesus did not cover worldly affairs.

Je, na wewe unaweza kutumia Biblia kujenga hoja y.a.ko?. Ndio maana nilisema nipatie ushahidi kwamba Biblia imeamrisha kukataza maovu na hadi dakika hii ya 90 hakuna aliyeleta ushahidi.

Nimeuliza scope ya anayoyasema yanadhibitiwa na nini, pia sikupata jibu.

Soma hoja ya Padri Privatus hapo chini.

Asanteni.

http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=1668

Mara ngapi Makamba amenukuu mistari ya Biblia? Mara ngapi makamaba amenukuu aya za Ku'ran tukufu. Kwanini hukusema kuwa anachangaya siasa na dini?
Wapi unapochorwa msitari unaotenganisha dini na siasa?

Mkuu nauliza maswali haya kujaribu kuonesha kuwa issue hii ni complicated kuliko tunavyojaribu kuifanya. Ni sawa na kumwambia mkulima asichangaye kilimo na siasa, au mfanyabiashara asichangaye biashara na siasa.
Pamoja na kuwa tuna katiba inayotengenisha mambo hayo mawili, katiba imeshindwa kuonesha wapi ni mwisho wa siasa na wapi ni mwanzo wa dini. Kama tunaona katiba iko wazi basi itakuwa buasara kama Pengo akifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kukiuka katiba ya nchi.
Kama ikishindikana basi ujue kuwa hajakiuka sheria.
 
MZANGANYIKA umeandika: "
Na aya nilizoleta zinazosema kwamba righteousness does not count hazipo ndani ya Biblia ama nimetafsiri vibaya?

Nimeshasema niko tayari kuleta ushahidi wa tafsiri ninayoilelewa mimi na tafsiri hiyo imeandikwa na wahubiri wenyewe. Ukitaka nilete ushahidi unaweza kusema."

JIBU langu:

"Naomba ulete ushahidi huo kutoka kwa wahubiri wa kikatoliki". Unaweza kufanya hili? Ukifanya hivi utakuwa umenisaidia sana.
 
Munapomfananisha na wanasiasa hapo munamjenga ama munambomoa?

Hapa tulipofikia hatukufikishwa na wanasiasa?
 
MZANGANYIKA umeandika: "
Na aya nilizoleta zinazosema kwamba righteousness does not count hazipo
JIBU langu:

"Naomba ulete ushahidi huo kutoka kwa wahubiri wa kikatoliki". Unaweza kufanya hili? Ukifanya hivi utakuwa umenisaidia sana.

I hope you know that Catholics follow St. Paul and I have cited various verses in Romans by Paul where he explicitly said numerous times that from now on righteousness does not count. MIfano ya maneno ya Paul ni haya hapa.

Romans 4:15

15for (A)the Law brings about wrath, but (B)where there is no law, there also is no violation.

Galantians 5:4
"You who want to be justified by the Law have cut tour self off from Christ, you have fallen from grace.

Romans 10:4
"For Christ is the end of the Law of righteousness to every one who believes.

Ndio maana nimeomba niletewe verses zinamtaka muumini apige vita maovu.

Ile makala ya Padri niliileta pia anasema wazi kwamba scope ya mission of Jesus iliishia katika kiroho.

Natumai hapo unajionea mwenyewe.
 
Munapomfananisha na wanasiasa hapo munamjenga ama munambomoa?

Hapa tulipofikia hatukufikishwa na wanasiasa?
Ukitaka ujadili vizuri point zako inabidi kwanza uelewe unachoongea. What is politics in first place? Maana wewe unatenganisha kabisa politics na maisha ya kila siku. Lazima ujue kuwa Siasa ndiyo tunaishi nayo kila siku, na ndiyo ina-shape our lives. Please go back to learn and come to discuss. Pengo, Kikwete, Myself and yourself are ruled by politics and our destiny detrermined by political affiliation a country moulds itself to. Kwa mfano Siasa ya ujamaa ili-affect vipi maisha yetu. Je sasa, maisha yetu yote yako impacted na hisi siasa. Hata dini inashape vile vile kwa sababu wale watu nao wanaomini hizo dini wako shaped na hizi political za uchwara! Wakeup please!!
 
JIBU LANGU: Mi nadhani wewe unamchukia Kardinali Pengo. Nasema hivi kwa sababu waraka huu si wa Pengo bali ni wa wakatoliki! Pengo naye ni mkatoliki, ila kwa bahati mbaya au nzuri ametokea kuwa kardinali!
Sio kila anayepinga Waraka ama Muongozo anamchukia Pengo ama Ponda. Ni wazi ana muono tofauti na wewe unayeona kuwa waraka huo na hao wanao ona Muungozo ni muafaka.

Ilani ya Kanisa la Katoliki ama Waraka kama tulivyozeshwa kuita sio wa wakatoliki kwa mantiki ya kuwa ni wao waliotengeneza kama ilivyo muongozo sio wa Waislamu. Ni watu wachache wenye ama uhalali au wanaolazimisha uhalali wa uongozi wa kujenga maoni (influence process) ambao wanawataka Waislamu na Wakristo kufuata maoni yao wanayoamini ni makini hata kama wapo miongoni mwa waumini ama wafuasi wao wasio afiki kama ilivyo katika mengi yahusianayo na imani zao.

Kardinali Pengo ameubariki na hivyo kama ambavyo RAIS KIKWETE anavyolaumiwa na kushutumiwa kwa mambo yanayotokea ama yasiyotokea ambayo yeye hakuyafanya ama hakupaswa kufanya ila ndiye mwenye dhamana basi tuhuma na shutuma kwa Kardinali Pengo ni halali ingawa zaweza zisiwe za ukweli kama ambavyo ipo kwa RAIS KIKWETE

Sasa kuna shida gani kwa kiongozi wa dini kukemea ufisadi? Yesu aliwaambia wanafunzi wake "nendeni duniani kote mkatangaze habari njema". Ufisadi ni habari njema? Hapana! Tena hata waraka wa waislamu unasema tusichague mafisadi. Sasa mbona Waislamu hujawapinga? Ila wewe mtu unayemchukia ni Pengo tu!
Hakuna anayelalama kukemea ufisadi bali kutoa ILANI zenye kulenga zoezi la kisiasa kama uchaguzi ktika nchi ambayo misingi na vision yake ambayo sio kwa kupenda bali kwa ulazima wa mazingira tunapaswa kuepuka kufanya siasa katika religious or tribal realms.

Labda yeye imani yake inamwambia kuwa Muongozo unaotoka na wale anaoamini kuwa wana mahusiano mahususi na muumba wake hauwezi kuwa na matatizo kama ambavyo inawezekana ndivyo wewe unavyo ona. Lakini tupo wengi tunaopinga vyote vilivyotokea na vingine vinavyoendelea kutokea ambavyo ni kinyume cha misingi na ndoto zetu kama watanzania.

Halafu nadhani kwa wakatoliki, Pengo ni kiongozi wao, so yes kwa madaraka aliyopewa na wakatoliki, ana official say kwao na si kwako kama wewe sio mkatoliki. Amechaguliwa na wakatoliki. Ukatoliki hauna nchi, ila wakatoliki wana uraia wa nchi zao, naomba hilo ulielewe. Naamini vile vile kuwa uislamu hauna nchi ila waumini wa kiislamu wana nchi zao, ndio maana lugha ya kiarabu inakubalika kwenye uislamu na Vatikani inakubalika kwenye masuala ya kikatoliki. Nadhani umenipata vizuri tu!
Kuhus kuchaguliwa na wakatoliki sidhani kama ni sawa na hili ni suala muhimu pia kwa upande wa hao wanaoitwa viongozi wa waislamu. Hivyo kuchaguliwa sio sehemu inayowapa uhalali bali imani ya wafuasi wao ambayo mara nyingi haihusishi nafasi ya LOGIC kufikia maamuzi ya kipi kitokanacho na hao viongozi wao wa kiimani ni cha kufuata na kipi cha kutofuata. Na pia hakuna lugha inayoitwa Vatikan. Labda tuelimishane zaidi

Ili uweze kuuelewa waraka wa wakatoliki, nakushauri ondoa chuki zako dhidi ya Pengo. Usome na uuelewe, ndipo hapo utakapoelewa Pengo anasema nini. Tafadhali jaribu kufanya hivyo. Haina maana kumchafulia jina Kardinali Pengo kwani hajasema kitu chochote kibaya. Nathani hilo unalielewa.
Kama ni waraka suala hapa sio Pengo bali ni Kardinali Pengo aliyehalalisha WARAKA wenye malengo ya kisiasa ambao ni kinyume cha misingi, maadili na vision ya nchi yetu. Kama ambavyo RAIS Kikwete anavyobeba kila lawama ya matatizo, maovu na mapungufu ya nchi yetu ndivyo ambavyo Kardinali Pengo anavyobeba lawama, shutuma na hata kebehi zihusianazo na WARAKA uliobarikiwa na kanisa lake.

Mimi naona, waraka ni mzuri tu ila watu wanajaribu kutumia siasa kuuzika. Na nadhani hawatafanikiwa kwa hilo, kwa sababu sauti ya Mungu hupitia kwa viongozi wa dini. Hata kama mtapinga vipi, kama Mungu ametumia viongozi hawa kurekebisha jamii ya watanzania, hata kama mtatumia mbinu gani kupinga, mtashindwa tu. Hakuna anayeweza kupingana na Mwenyezi Mungu. Kama kamtumia Kardinali Pengo basi sauti yake itasikika tu, kama hakumtumia basi sauti ile haitazaa matunda. Ushauri wangu ni kuwa, tusubiri tuone! Au unasemaje ndugu yangu Mtanzania? Naomba vile vile kuuliza je wewe ni muumini wa dini gani?
Kusubiri is not an option katika kulinda mustakabali wa nchi na haswa maelewano ya kijamii katika nchi yenye mifumo legelege ya kiutawala kama yetu.

Pia ILANI ama Waraka sio matamshi ya kidini bali maagizo yao utekelezaji wa kisiasa yenye vibwagizo vya kidini hivyo watu kuufanyia siasa ni sawa tu.

Na haya ya kumsingizia Mwenyezimungu kuhalalisha maoni na mitizamo yetu ndio yaleyale yaliotuletea huyo mnayemshutumu kupelekea nchi kuoza wakati tunajua kuwa yeye ni mrithi tu wa shamba la babu lilikuwa limejaa magugu na vichaka. Kosa lake ni kuacha kuchoma moto na kuamua kutumia mbinu ya kupalilia ili kuhakikisha kuwa ana acha mboji ya kulinda rutuba (usalama) wa shamba (nchi) letu.

Na pia lazima utambue kama ambavyo Mkristo Mkapa alipotoa majengo ya serikali kuwapa Waislamu wafanye chuo kikuu ama hivi karibuni Mkatoliki Pinda alipotoa msimamo rasmi wa serikali kuhusu waraka kule bungeni hakujatokea upinzania mkali, mantiki hiyo pia inaweza kuwa tofauti pale Mkrsito Pengo anapomkosoa Rais ama Urais/Uongozi wa Muislamu/Mswahili Mrisho Kikwete.

Uongozi bora ni pamoja na kuwa makini (sensitive) na hali na mazingira kama hayo katika kushughulikia matatizo hata yawe ni yale makubwa kama lilivyo suala la UFISADI.

Pia ni lazima tukubali kuwa kitendo cha Kardinali Pengo kumfanyia sala/maombi maalumu Benjamin Mkapa mara baada ya shutuma za UFISADI kuanza kumgubika na baadae "kubariki" Kitabu cha Mke wa LOWASA ambaye ni siku chache amelazimika kujiuzulu kwa shutuma za Ufisadi, kunapunguza ama hata kuondoa uhalali wake katika kukemea UFISADI miongoni mwa wengi, haswa wale wasio wafuasi wake kiimani. Kwa hiyo kama ambavyo Kikwete anavyokosa uhalali wa kuwa na nia ya dhati kupiga vita ufisadi kutokana na kuwa ni RAFIKI zake wakubwa ambao bado yuko/inasemekana yuko nao ndio wanaoshutumiwa kuwa ni wahusika wakuu wa UFISADI mkubwa unaotumika kama mfano wa kuoza kwa nchi yetu, ndivyo ilivyo kwa upande wa Pengo.

omarilyas
 
Last edited:
kama kuna separation ya dini na siasa ina maana kama kuna maovu katika siasa wanaotakiwa kupiga kelele ni wanasiasa tu hata wananchi hawatakiwi kulalamika ?nadhani mtu yoyote mwenye uchungu na rasilimali za nchi hii ana haki ya kujumuika katika harakati za ukombozi regardless wa yeye kuwa mtu baki,mchungaji,sheikh,profesa,mwanasheria,nk .tuangalie nini kinalalamikiwa sio nani au anatoka wapi analalamika.Aim ni kuokoa rasilimali za nchi.ni wakati wa kusahau tofauti za dini,kabila,jinsia ,nk na kufocus towards a common goal-kupigana na ufisadi
ndugu yangu mdudu ya kanisani ni ya kanisani na ya siasa ni ya siasa,kumbuka hata enzi za yesu selikali ya kiyahudi ilikuwa ni ya kikatili mno hata ikataka kumwua yesu wakati mdogo,lakini je?uliona yesu akishughulika na mambo ya selikali?
 
Hili kanisa katoliki na kiongozi wao Pengo hivi hawaoni haya? kanisa lao linamatatizo chungu nzima yanayotakiwa kushughulikiwa lakini wao wameyaacha na kuanza kuhubiri siasa hivi kweli wanaakili? bado ule mgogolo wa mapadre kuoa au kutokuoa haujaisha bado kanisa linagubikwa na mambo ya ushirikina,masista wao wamekuwa vicheche,mahudhulio ya vijana kanisani yanapungua wao hawajiulizi hata! mapadre wanapungua kwa sababu vijana hawataki wito bado kanisa halijiulizi kwahili? matokeo yake wameona bora waanze siasa kwa sababu dini shetani kawazidi nguvu,kanisa limepoteza mwelekeo, linataka kuwa na sauti mbele ya selikali badala ya kuwa na sauti mbele ya shetani,hata ukienda makanisani kwao siku hizi hawana lolote! wanahubiri ya kaisali zaidi kuliko ya MUNGU,wako kibiashara zaidi siku hizi.
Mi nafikiri muda umefika kuelezana ukweli tu,muda wa kanisa kutuibia dhahabu zikaijenge roma umekwisha sasa nashangaa sana hata ule mswada wa madhebu ya dini kutokulipa kodi ulipoondolewa, kwanini wasilipe kodi? mbona wanafanya biashara? kipi cha msaada wanachokifanya sasa? hata zamani walipofanya hivyo walikuwa na kusudi lao, hawa wakatoliki wasituchanganye kabisa! mambo hayo wakayafanye ROMA kwenye selikali yao.
 
Last edited:
Serekali inaweza ikafikiri inapambana na kanisa katoliki pekee lakini ukweli wa mambo itakuwa ikipambana na wakristo wa madhehebu yote na pengine inaweza kuitumbukiza Tanzania katika mgogoro mkubwa kuliko tunavyofikiri.Kikwete anajua hili ndiyo maana hawezi kumwona Pengo mwenyewe kwa kuwa anajua dhambi na hila za serekali yake dhidi ya kanisa.Kikwete alilitumia kanisa kufika hapo alipo,ni huyu huyu Pengo na maaskofu wa madhehebu karibu yote walikuwa wakituambia muungwana ni chaguo la Mungu.

Kikwete kwa maoni yangu anayo karata moja ya kucheza nayo ni kumtumia Mizengo Pinda ambaye ni mkatoliki safi kutuliza mambo kabla hayajaaribika kabisa.Tatizo hapa je Pinda atakubali kutumika kama daraja au naye atataka kutumia fursa hii adimu kama mtaji wake wa siasa hasa kupewa nafasi na chama kugombea urais baada ya muungwana mwaka 2015.
.

Hivi kanisa katoliki huko Tanzania linawakilisha wakristo wote?

Mbona hatujasikia Askofu Malasusa amehusishwa katika waraka? Mbona kakobe anaupinga? mbona Anglican na Pentekoste na wasabato haajachangia chochote.

Mimi nakubali kabisa kuwa Yale ya Kabaka kule Uganda, sasa yanataka kuwa huko Tanganyika yaani Pengo na Kikwete nani zaidi.

Tuiombee Amani Tanganyika na balaa linalotaka letwa na wakatoliki
 
Ukiliona tatizo hili utakubaliana nami kuwa jukumu la kuwaelimisha wananchi kuwachagua wagombea waadilifu ni la serikali. Lazima tukumbuke kuwa hili ni jambo la kudumu na inabidi liwafikie wananchi wote kwa fedha ya walipa kodi.

Pamoja tuaendelea, tusikimbilie utatuzi wa harakaharaka. Dalili ya mvua ni mawingu.

Inaonekana hujabaini tatizo. Serikali ipi? Serikali ambayo tayari imetekwa naMafisadi ndiyo unategemea itoe elimu kwa wapiga kura kuwaasa wachague watu safi. Hii itakuwa sawa na kujiua weneywe ( commit suicide)!!!!!!!!!!!!!!!
 
Si serikali bali vyama vya siasa na asasi za kiraia zisizoegemea upande wowote wa kisiasa na wala makundi ya kijamii, iwe makabila, dini, n.k

Omarilyas
 
Ndugu yangu MZINGANYIKA, naona umeshindwa kabisa kujibu swali langu? Nilikuuliza wewe ni muumini wa dini gani? Na kwamba utoe ushaidi kuhusu yale uliyoyasema kuwa kanisa halitakiwi kupinga ufisadi. Umeshindwa kujieleza. Umebakia tu kunukuu aya za biblia bila ya kuzielewa na hata unakosea unaposema wakatoliki wanamfuata Mtume Paolo. Ukweli ni kwamba wakatoliki wanamfuata Yesu kama waislamu wanavyomfuata Mtume wao. Paolo alikuwa ni mtume wa Yesu na alifundisha mafundisho ya Yesu. Hivyo naomba niweke wazi kuwa Paolo na wakatoliki wanamfuata Yesu. Naomba nikusahihishe kwa sababu hoja zako zinalenga kupotosha ukweli wa mambo na kuwapinga tu wakatoliki kwa kutaka kuwapinga bila sababu ya kimsingi. Naomba ndugu yangu uondoe chuki dhidi ya wakatoliki ili tuweze kueleweshana kuhusu waraka huu. Bila ya wewe kuondoa chuki yako kwa wakatoliki tutaishia tu kubishana bila ya kufanya mazungumzo yanayojenga hoja za maana. Naomba uzingatie ushauri wangu ili mimi na wewe tuweze kujadili pointi za waraka na sio mawazo yaliyo nje ya waraka ambayo kimsingi hayakulengwa na waraka ule!
 
Ndugu yangu MNYIKUNGU, nadhani hii unaonyesha kabisa kuwa wewe una chuki binafsi na wakatoliki. Hivi kama una elimu ya kutosha na kama wewe ni muungwana unawezaje kushusha matusi mazito ya namna hii kwa wakatoliki kwa kuwaita wapuuzi? Sasa kutokana na maneno uliyoyasema, je prove kwamba wewe sio mpuuzi na maskini wa hoja! Nakuomba ujifunze kutumia lugha safi kwenye blog yetu ya jamii. Mimi sina ugomvi na wewe ila nakupa tu ushauri. Kama una hoja ilete tuijadili lakini matusi hatuyaki hapa. Nadhani uliteleza tu, na kuteleza sio kuanguka.
 
Ndugu ya OMARILYAS umeandika "Kardinali Pengo ameubariki na hivyo kama ambavyo RAIS KIKWETE anavyolaumiwa na kushutumiwa kwa mambo yanayotokea ama yasiyotokea ambayo yeye hakuyafanya ama hakupaswa kufanya ila ndiye mwenye dhamana basi tuhuma na shutuma kwa Kardinali Pengo ni halali ingawa zaweza zisiwe za ukweli kama ambavyo ipo kwa RAIS KIKWETE"

JIBU LANGU: mi naona kuwa unachanganya mambo. Kardinale na maaskofu walibariki waraka wa dini yao na si wa serikali. Naomba hili ulielewe. Waraka ule si wa waislamu wala wapagani. Ni waraka wa wakatoliki, sasa kama wewe si Mkatoliki waraka ule unakuhusuje? Mbona wakatoliki hawaujadili ila watu wasio wakatoliki wanauvalia njuga kama wao? Ahaaa! UFISADI! Je wewe unapenda Mafisadi? Kama unawapenda basi naona una kila sababu ya kuupinga waraka ule maana umegusa mioyo ya mafisadi zaidi. Kama si fisadi, naomba vilete vipengele vya waraka unavyovipinga ili tuvijadili!
 
Ndugu yangu OMARILYAS UMEANDIKA: "Na pia lazima utambue kama ambavyo Mkristo Mkapa alipotoa majengo ya serikali kuwapa Waislamu wafanye chuo kikuu ama hivi karibuni Mkatoliki Pinda alipotoa msimamo rasmi wa serikali kuhusu waraka kule bungeni hakujatokea upinzania mkali, mantiki hiyo pia inaweza kuwa tofauti pale Mkrsito Pengo anapomkosoa Rais ama Urais/Uongozi wa Muislamu/Mswahili Mrisho Kikwete."

HOJA YANGU:
Naomba hoja yako kuhusu waraka wa Waislamu.

Naomba uelewe kuwa waraka wa wakatoliki haujampinga Rais Kikwete. Kama kuna sehemu iliyompinga Mheshimiwa Rais wetu naomba uilete hapa tuijadili! Si lengo la wakatoliki kupambana na Rais Kikwete na serikali yake. Kama ulikuwa ukifikiri hivi nadhani umekosea. Halafu kardinale kama kiongozi yeyote yule wa dini yeyote anaweza kumshauri mheshimiwa Rais. Zaidi ya hayo kardinale ni mtanzania vile vile.

Waraka unaipa changamoto ya serikali kupambana na mafisadi. Ila haupingi serikali. Ila kwa bahati mbaya, baadhi ya viongozi wa serikali ni mafisadi. Ndio maana wanasema waraka una malengo ya kisiasa zaidi ya kutoa elimu ya uchaguzi kwa wakatoliki. Mi nadhani tuusome waraka ili tuuelewe. Wadau mbona mmekaa kimya kuhusu waraka wa Waislamu?
 
Waraka wenyewe naona jamaa wameamua kuuficha. Kwa hakika tuna usongo sana na mwongozo huo. Lakini kwa bahati mbaya hakuna hata mmoja aliyeuleta. Tunawaomba maustadhi mliomo humu mtuletee huo mwongozo.
 
Back
Top Bottom