Cynic
JF-Expert Member
- Jan 5, 2009
- 5,144
- 1,655
Nyaraka kaama hizo si ngeni kutoka toka kuanza chaguzi za vyama vingi. Lakini hii yaonekana yaonekana kukilenga chama tawala kwa muono wa Serikali ambayo i sawa na kusema CCM kwa sasa hivi. Kwa baadhi wameenda mbali zaidi na kuona kuwa, waraka huo si tu unailenga CCM, bali ni Rais Kikwete na washabiki wake serikalini kwa kuonekana kutolisikiliza kanisa katoliki kama ilivyokuwepo kwa akina Nyerere na Mkapa.
Wataalamu wa mambo ya siasa, wameeleza kuwa nguvu au ushawishi wa kanisa katoliki ndani ya serikali umepungua sana. Na hii imetokana na Kikwete kutaka kutenganisha kabisa dini na serikali kwa vitendo kitu ambacho kitakuwa kipya kabisa toka tukiwa Tanganyika na hatimaye Tanzania. Kwa maana hali hiyo ilirithiwa toka kwa wakoloni na kupewa baraka zote na mataifa ya magharibi.
Kikwete aliweza kuwashinda kidiplomasia akina Pengo na wafuasi wake, na ndio maana wakathubutu kutamka kuwa Kikwete ni chaguo la Mungu. Rais Kikwete alijua wazi kuwa kuna gharama kubwa ya kulipa kwa kuungwa mkono na makanisa yote. Ni vipi alijiandaa na hilo, hakuna ajuaye isipokuwa waliyekaribu naye tu. Kwa vile yeye ni mkongwe wa siasa wa muda mrefu, ninahakika kabisa anaelewa Nguvu na ushawishi wa kanisa Katoliki duniani. Tena liko tayari hata kuleta vita pale ambapo linaona kuwa linapoteza umaarufu, kwa nia ya kujipanga upya.
Waraka wa Katoliki ni mzuri, lakini inaonekana tunadandia dandia bila kujua undani wake. Inaonekana hata Waislam wamedandia dandia kwa kufuata mkumbo tu bila kujua undani. Angalieni ya Uganda! Mbuyu ulianza kama mchicha jamani.