Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,952
- 146,223
NDUGU WAKALA WA PENGO AMA PENGO MWENYEWE KWA KIFICHO...TUMSIFU YESU KRISTU WA NAZARETH. Ungekuwa unaongea kwa upole uliotukuka kama ulivyofanya hapa tungekuwa pamoja na tusingetiliana mashaka wala kukashifiana...maana iwapo lengo ni kulinda na kujenga nchi, malumbano hayafai.
Nilichokulaumu ni kumdhalilisha kiongozi mkuu wa nchi hata kama ana mapungufu si busara kwa Taifa na hata kwa mataifa ya nje. Mimi nina imani kuwa uko kwenye nafasi nzuri kabisa kama Mkuu wa Kanisa lenye waumini wengi watanzania...kuzungumza na Rais ukamshauri uso kwa uso juu ya mambo ambayo umeyatoa hadharani.
Yeye hakukuita kwa kuwa mlengwa hukuwa wewe ktk saga la madawa. Hakuwa ana undermine kanisa kwa uislamu wake...bali alizungunza kama Kiongozi wa nchi mwenye dhamana ya watanzania wote. Wewe na yeye ni watu wazima tena Viongozi...mnapolumbana through media isn't fair kwetu sisi watoto wenu.
Ukimwona pengine si wa imani yako..basi ungepitia hata kwa PM pengine ambapo protokali lazima ingezingatiwa. Jitahidi kama Kiongozi Mkuu wa kidini usiiteteleshe serikali ambayo ipo madarakani kisheria na hujazuiwa kuikosoa ama kuishauri muda wote. Najua jinsi imani ya dini ilivyo na nguvu na kiongozi kama wewe ukiitumia kama shield au spear utaigawa nchi mjomba.....mtu mzima akikosea mwite faragha...sema naye..ni binadamu yule anaelewa...
Ukitumia imani kulumbana naye itakuwa kama Bin Laden Osama kutumia dini kama kivuli lkn finally ameuwawa na anaowaita infidels. Mumi nadhani kama JK angekuwa ana utawala wa kiimla...hata jamii forums isingekuwepo na kungekuwa na msako mkali dhidi ya wabaya wake just like Libya...etc. TUFIKE MAHALI TUJENGE KISIWA CHA AMANI JAMANI TUACHE TOFAUTI ZA KIDINI NA KISIASA.
IN WAR THERE IS NO WINNER...ALL ARE LOOSERS...alisema British Premier Chamberlain in WW2 akiwatahadharisha waingereza juu ya athari za kupigana na Hitler. Alujiuzulu kwa shinikizo na akarithiwa na Winston Churchill aluyeingia kwa kutangaza "There is nothing to offer except blood....sweat and tears" Ilikuwa patashika nguo kuungua.
Sasa twaweza furahi Rais akijiuzuru lakini je unaye mtu unayependekeza awe badala yake? Na je unadhani mtu huyo unayempendekeza anakubalika na majeshi yote ya ulinzi na usalama na wananchi? Yasije yakawa ya Kabila or JF Kennedy or A. Lincolin or unawajua bwana. Ushabiki wa kiimani ya dini na kuyasahau hayo itakuja tokea mambo ya Ariel Sharon btn Likurd na Kaduma yake...or ya Bingu wa Mutharika na chama chake.
Tumpe pumzi Rais ya kuongoza nchi huku tukimshauri kupitia majukwaa kama hivi ili nini afanye juu ya kipi tutakacho. Kumtukana Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vyote vya ulinzi na usalama na ambaye ni Rais kidemokrasia anayeachia demokrasia ya habari nchini....KWANGU MIMI NI UHAINI. NA INGELIKUWA MMENICHAGUA MIMI NDO RAIS...HAKI YA MAMA YANGU MZANAKI...UNAOKOTWA UNA MSUMARI WA INCH SITA UTOSINI..POTELEA KWA MBALI ILI NCHI ITAWALIKE BILA USWAHILI.
Kardinali kama kiongozi wa kidini, kaona kwamba ana uwezo wa kuingia Ikulu na kuteta na Kikwete, lakini baba hateti kwake katika kurekebisha mambo.
Wengi tunaona hili kama tatizo la Kikwete. Lakini Kikwete ni nani jamani? Si Mtanzania mwenzetu yule? Hizo tabia za kuteta teta, vineno nusu nusu, vijembe vijembe bila sababu siku hizi inaota sugu. Sasa basi, katika kumsema Kikwete, kuna ujumbe kwa wengi sana. Tuwe wakweli, tuwe wawazi, tuwe direct. Hizi habari za mafumbo fumbo hazifai, especially kwa mtu mwenye dhamana ya heshima kama rais.
Kwa hivyo ile ilikuwa broadcast maalum kwa Kikwete, lakini ujumbe utanufaisha wabongo wote wenye tabia kama hizo.