Pengo amtolea uvivu Kikwete

Pengo amtolea uvivu Kikwete

Sijawa huko na sitaruhusu kujirahisisha kujadili udini, hapa nilikuwa najaribu tu kumwambia tunaja mengi na historia kuliko wanavyofahamu ila hatuko tayari kwani tukifanya hivyo wenye moyo mchache wa kujadili ukweli watakimbilia majambia.

Ndio maana nasisitiza tujadili hoja iliyoletwa hapa na kama hoja ya dini aanzishe anayetaka thread yake na kama mod ataruhusu ndipo tuijadili. Kwa hapa tunajadili Cardinal pengo anapoonya maovu na udhaifu wa serikali kwa manufaa ya watanzania wote.

Tunaoonja makali ya maisha ni sote, na tukiendekeza ushabiki kwa misingi ambayo wengine wanaendekeza hapa tutaishia umaskini wa kutupwa na kuona tatizo ni yule unayemwona mbele yako badala ya kuelewa ukweli wa nini viongozi wetu wafunguke mioyo na akili zao kuona, kusikia na kufanya tunayowaambia, maana kujitetea kwa viongozi na kutafuta visingizio vya hapa na pale si hoja ya kuondoa matatizo yaliyopo.
Mkuu wangu kama kweli ungekuwa huna udini usingeandika hivi hata iwe kwa kutolea mfano tu, kwa kufanya hivi unachochea moto zaidi badala ya wewe pia kujadili mada yenyewe..
Katika Udini huo huo tunaoupiga vita umemjibu huyo jamaa hivi:-
Kaanzishe thread ya kujadili udini, hapa tunajadili thread ya Kikwete mbele ya maaskofu katoliko wote Tanzania kwamba viongozi wa dini ni wauza unga. Kaambiwa ataje majina ya wauza unga hadi leo kimya. Hii ya kujadili udini si mahali pake maana nikikuambia Mtume muhamad alifukuwa dini ya ukristo na kwenda kinyume cha maadili ndipo akaenda kuanzisha uislamu utaenda kutafuta jambia kunikata kichwa, Hahahaha wajameni tujadili yanayojilia tusiingize udini hapa si mahali pake.
 
Shukran sana tena hapa ndio mfano wako unaleta maana kabisa.. Kama Pinda au Mkapa angekuwa ktk sherehe ya kiislaam kisha akawaambia Masheikh waache kujihusisha na biashara za madawa ya kulevya.. mkuu wangu, Usingesikia Muislaam hata mmoja akipiga kelele kwa sababu sisi waislaam hatuna daraja la ubora wa mtu (binadamu) mbele ya Mungu isipokuwa mitume. Sheikh na mimi hatuna tofauti yoyote ya kimatendo isipokuwa tofauti ni kwamba yeye kasoma dini na kakabidhiwa mamlaka ya kuongoza zaidi ya hapo kila mmoja anabeba msalaba wake..

Na ndio maana mimi naweza kabisa kuandika hapa kwamba Sheikh Mkuu Simba ni fisadi na fisadi kweli kwa sababu najuua fika anauza mali za waislaam kwa kupitia bakwata. bakwata ni kundi la Mafisadi kitu ambacho wewe ktk Ukristu huwezi kusema hivyo kumshutumu Pengo. Na ndio maana kesi zozote zinazohusiana na kanisa huwa hazifiki mahakamani kwa sababu kanisa linachukua dhamana ya makosa ya watu hao..

Umeniuliza kazi ya Pengo, yeye ni kiongozi wa dini tena basi ni balozi wa Vatican... kazi yake ni dini na amepewa Immunity kwa sababu ya kazi yake. Alichotakiwa kufanya angemfuata JK na kuomba majina ya wauza unga kutoka kanisa lake ama angetazama list ya watuhumiwa walioko mahakamani tayari na kufuatilia kesi zao kuhakikisha kwamba kanisa lake halihusiki kabisa na vitendo hivyo. Lakini badala ya yeye kuchukua njia na taratibu zinazotakiwa karukia kwenda jukwaani na kudai yeye Pengo sijui apewe majina ya wauza Unga na rais wetu wa jamhuri ya Muungano, ILI IWEJE..Unaleta kusutana na rais wetu ati awataje wauza unga wakati hujawahi kumfuata ukaomba majina kama utaratibu wa kawaida tu..Haya nambie Pengo akipewa hayo majina ya wauza unga unategemea atayafanyia nini - Kuyaombea au?

Hili ndilo swali langu ambalo pia ktk maandamano ya Washington nimeuliza wanaandamana Marekani ili IWEJE... Tunachotafuta hapa sio ubishi na kunyoosheana vidole bali ni kupata suluhisho la matatizo sugu tuiliyokuwa nayo..Unga ni moja ya mchango mkubwa wa fedha za madafu nchini. Leo hii maisha yamepanda sana Tanzania kwa sababu ya mchango mkubwa wa unga na money laundry ndio maana nyumba za Kariakoo zimefika hadi billioni moja na baadhi ya watu wanalipa cash.. Haitokea watu kujiuliza hii purchasing power inatoka wapi ktk nchi maskini ambayo haina umeme, maji, usafiri na hata ku abuse maliasili na rasilimali zake..

Sasa kama mnataka tuhalalishe biahssra za Unga na Bangi semeni na itakuwa jambo bora zaidi iwe kama Afghanstan kila mtu atajirike kwa biashara haramu kuliko kupiga marufuku biashara za madawa ya kulevya kumbe viongozi wa dini zetu ndio wako mstari wa mbele kabisa kuziendesha na sisi wananchi tunawawekea kifua..I would careless kujua kama viongozi hao ni waislaam au wakristu kwa sababu tamaa ya kufanya biashara haramu haitokani na dini ya mtu..

Mkuu ningependa kujua kama ume reside tanzania au nje ya nchi!! kwa sababu kwa hali halisi iliyopo Tanzania sidhani kama maneno " sisi waislaam hatuna daraja la ubora wa mtu mbele ya Mungu isipokuwa mitume. " yana apply. Kama kauli za maaskofu za kutaka serikali kutenda haki , kupambana na ufisadi nk zinatafsiriwa vibaya na mshehe kwamba maaskofu wanasema hivyo kwa sababu rais ni mwislam ,unategemea kauli kama aliyoitoa kikwete ingeamsha nini kama ingetolewa na kiongozi wa kikristo mbele ya mhadhara wa waislam?
Mkuu hapa hali ni tete na sielewi ni kwanini viongozi wa serikali na wa dini hawataki ku address hii issue..!

Mkuu ni sawa unaweza kubandika hapa kama sheikh mkuu Simba ni visadi...hii inatokana na kwamba una proof za huo ufisadi..mathalan ameuza viwanja vya waislam..! Na mimi naweza kumshutumu Pengo kama kuna proof za ufisadi wake. Kwanini unasema kesi zote zinazohusiana na kanisa hazifiki mahakamani? Kuna kesi moja ya padre kumlawiti kijana mmoja aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani kama sikosei...hiyo kesi ipo mahakamani! Hiyo kitu ya kanisa kuchukua dhamana ya makosa yao sijaielewa ,ina bidi labda unitolee mfano!

Sioni ni kwanini Pengo alitakiwa amfuate JK kutafuta majina ya wachungaji wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya. Kikwete mwenyewe siyo kazi yake kusema kile alichokisema. Hiyo ni kazi ya mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya..Mr Godfrey Nzowa...! Nzowa angetoa taarifa kwenye vyombo vya habari kama kawaida..watu x na y wamekamatwa kwa kujihusisha na _ _ ! kwa hiyo tunarudi kule kule ..kikwete hakutakiwa atoe ile kauli pale ndiyo maana inaonekana kama uchokozi!

Hujaniambia kama Pengo ana wajibu au la wa kukemea ,kuomba watuhumiwa wa ufisadi/madawa ya kulevya watajwe , washtakiwe ili haki itendeke!

mkuu kwa mtazamo wangu nimeona hii issue kila pande unaichukulia kivyake..tunaweza tukabishana sana hapa....! kwa upande wangu mimi kama mkatoliki naona kidogo nimekuwa offended na kauli ya kikwete!
 
Mkandala, Kikwete alitoa tuhuma za viongozi wa dini kujihusisha na biashara ya unga jukwaani, tena ndani ya Ibada ya kumsimika Askofu Ndimbo wa Jimbo la Mbinga. Kikwete angetumia busara sana kuwaeleza viongozi wenzake kwa ustaarabu wa kiofisi na kuwakabidhi majina ya hao wauza unga. Sasa hili la Kikwete kwenda kwenye mimbari (stand ya kusomea neno la Mungu) na kuwatangazia maaskofu katolikI wote waliokusanyika pale toka nchi zima na kutoa tuhuma kwamba wanajihusisha na uuzaji wa unga bila vielelezo na bila kuwataja wahusika, ni shutuma za jumla zisizohakikiwa na leo anashindwa kutoa uthibitisho. Busara hapo ndio imejionyesha kwa rais wetu ama kutumia vionjo, jazba, wivu au upeo mdogo na kuchagua nafasi gani na kwa namna gani atoe tamko rasmi.

Hawa Maaskofu wakatoliki wako makini sana na hawakurupuki katika kujibu hoja, huzifanyia kazi kwanza na baada ya utafiti na kujiridhisha ndipo wanapotoa tamko. Kwa mtazamo wangu Muadhama Policarp Cardinal Pengo anapochukua hatua ya kujibu tuhuma baada ya mwezi mmoja amejihakikishia katika utafiti wake ndani ya watumshi wake hajaona dalili ya dalali wa madawa hayo zaidi ya udalali wao wa kutangaza Neno la Mungu. Ndio maana anaomba Rais amsaidie kwa mwono wake atangaze majina ya viongozi wa dini wauza unga maana shutuma bila uthibitisho ni kujidhalilisha. Na ametumia njia ile ile ambayo Rais Kikwete alitumia kuwadhalilisha viongozi wa dini.

Kwa vyo vyote Rais Kikwete kwenda kuongelea hayo mbele ya Maaskofu katoliki wakiwa katika shughuli maalum ya kikanisa na kutoa shutuma bila uthibitisho na hata baada ya kuombwa kushindwa kuthibitisha kauli yake ni dhahiri Rais Kikwete amejidhalilisha mbele ya watu. Ndio maana uongozi si shauri ya kukalia kiti tu na kuropoto, busara na hekima licha ya kanuni na wajibu ni vipa umbele, vinginevyo kwa mtazamo huu Rais Kikwete katika uongozi wake anajidhihirisha AMEPWAYA MNO.
 
Mwadhama Policarp Cardinal Pengo kasema tu, lakini kila mwenye akili timamu anajua kuwa rais Kikwete ni hopeless kabisa
 
<br />
<br />
Kaka fungua google search....type (the secret terrorists) ikifunguka download web namba mbili yenye PDF by Bill Hughes

Jana ulisema unamfahamu sana Muadhama Policarp Cardinal Pengo, sidhani. Kwa kumbukumbu zangu huyu ni mkimya sana, mtaratibu sana, hana makuu kabisa. Lakini ni mkweli, mpenda watu, mpenda maendeleo na mtetezi mkubwa wa wanyonge.

Nilimwona kwa mara ya kwanza Mwadhama Pengo mwanzoni mwa miaka ya 80 akiwa padre akitokea Rome masomoni huko Sumbawanga katika kijiji cha Ntuchi wilayani Namanyere akielekea Kate, akitembezwa na mzee wake Marehemu Askofu Carolo Msakila. Kwa vile nilimwona mara ya kwanza hakuonyesha upekee na nilishangaa kama ametoka Rome masomoni. Punde nikaambiwa kapangiwa kazi ya kuanzisha Seminari kuu ya Segerea hapa Dar es Salaam. Baada ya miaka michache Pope akamteua kuwa Askofu wa Kwanza wa jimbo jipya katoliki la Tunduru-Masasi. Baada ya miaka michache tu Pope akamteua kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam lilikokuwa likiongozwa na hayati Muadhama Laureano Cardinal Rugambwa. Kwa mtazamo finyu ingeweza tafsiriwa kwamba kateremshwa cheo kutoka askofu mwenye jimbo na kuja dar kuwa askofu msaidizi. Lakini ilikuwa demotion for promotion, na maana yake Pope kumwandaa kwa kazi nzito aliyo nayo sasa.

Mwadhama Policarp, hakurupuki katika kuongelea kitu, si mwoga, ni mkweli, mtetezi mwenye unyofu wa moyo. Wengi hapa tunaongelea kwa mitazamo tofauti lakini si kile kilichoko ndani ya moyo wake. Tukumbuke hawa ni manabii kama akina Eliya walipowatahadharisha watawala wakakaidi na madhara yaliyotokea kwa wanahistoria ya taifa la Israel tunayajua.

Tuweke kando itikadi za kisiasa na tuangalie anachoongelea Muadhama. Kuna mengi kama hayo ambayo wengi wetu tunajua lakini hakuna hatua zinazochukuliwa zaidi ya kulalamika majukwaani kama hawana mamlaka za kutolea uvivu. Hao wavuja pesa yanayoendelea ni kitendawili tega. Hii ya funika kombe mwanaharamu apite inazidi kutupeleka pabaya. Kiongozi asipokuwa tayari kukosolewa maana yake yupo huru kujifanyia atakavyo na kujikuta yuko juu ya sheria. Hakuna chombo cha kumwajibisha. Na dhana ya mapokea kwa viongozi wetu hata wanapopotoka kuendelea kuwaimbia nyimbo za kuwasifu imetufikisha hapa, na wanufaika na mwenendo huu mbovu ndio watetezi wa wakuu na wanyonge kuendelea kunyongeka.

Tunapaswa kumpongeza Muadhama Policarp kwa ujasiri wa kuonya, kukemea na kushauri bila woga, maana viongozi waandamizi wa serikali hawaku tayari kufanya hivyo kwa sababu ya kutetea maslahi yao na nafasi zao katika uongozi.

Yana mwisho na ukingo unakaribia zinakoishia mbio hizi.

Mkuu ningependa kujua kama ume reside tanzania au nje ya nchi!! kwa sababu kwa hali halisi iliyopo Tanzania sidhani kama maneno " sisi waislaam hatuna daraja la ubora wa mtu mbele ya Mungu isipokuwa mitume. " yana apply. Kama kauli za maaskofu za kutaka serikali kutenda haki , kupambana na ufisadi nk zinatafsiriwa vibaya na mshehe kwamba maaskofu wanasema hivyo kwa sababu rais ni mwislam ,unategemea kauli kama aliyoitoa kikwete ingeamsha nini kama ingetolewa na kiongozi wa kikristo mbele ya mhadhara wa waislam?
Mkuu hapa hali ni tete na sielewi ni kwanini viongozi wa serikali na wa dini hawataki ku address hii issue..!
Mkuu ni sawa unaweza kubandika hapa kama sheikh mkuu Simba ni visadi...hii inatokana na kwamba una proof za huo ufisadi..mathalan ameuza viwanja vya waislam..! Na mimi naweza kumshutumu Pengo kama kuna proof za ufisadi wake. Kwanini unasema kesi zote zinazohusiana na kanisa hazifiki mahakamani? Kuna kesi moja ya padre kumlawiti kijana mmoja aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani kama sikosei...hiyo kesi ipo mahakamani! Hiyo kitu ya kanisa kuchukua dhamana ya makosa yao sijaielewa ,ina bidi labda unitolee mfano!

Sioni ni kwanini Pengo alitakiwa amfuate JK kutafuta majina ya wachungaji wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya. Kikwete mwenyewe siyo kazi yake kusema kile alichokisema. Hiyo ni kazi ya mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya..Mr Godfrey Nzowa...! Nzowa angetoa taarifa kwenye vyombo vya habari kama kawaida..watu x na y wamekamatwa kwa kujihusisha na _ _ ! kwa hiyo tunarudi kule kule ..kikwete hakutakiwa atoe ile kauli pale ndiyo maana inaonekana kama uchokozi!

Hujaniambia kama Pengo ana wajibu au la wa kukemea ,kuomba watuhumiwa wa ufisadi/madawa ya kulevya watajwe , washtakiwe ili haki itendeke!
mkuu kwa mtazamo wangu nimeona hii issue kila pande unaichukulia kivyake..tunaweza tukabishana sana hapa....! kwa upande wangu mimi kama mkatoliki naona kidogo nimekuwa offended na kauli ya kikwete!
Mkuu wangu Uislaam hauna Tanzania wala nje sisi wote tunasali sawa dunia nzima na tunafuata kitabu dunia nzima tofauti zetu zipo ktk baadhi ya mila na tamaduni za makabila na watawala ktk madhehebu ya Shia lakini sio kwetu Sunni. hakuna mtu mbora mbele ya mwenyezi Mungu isipokuwa yule mwenye kufanya Ibada hivyo kwetu waislaam kila mmoja wetu ana equal opportunity ya kuwa mtukufu mbele ya bwana kutokana na matendo yake.. Mimi naweza kuwa mbora mbele ya Mungu kuliko Mufti Sheikh Mkuu.. Hii haina maelezo zaidi na kama umeona tofauti basi ni sawa na kumuona Mkristu anakunywa pombe ukasema ndio Ukristu huo..

Pili, Namshutumu Sheikh Mkuuu kwa Ufisadi sio nina Ushahidi hapana sina ushahidi lakini kesi zake ni sawa na za Mkapa kuuza nyumba za serikali.. sina ushahidi zaidi ya kuona kwa macho au Mkataba wa Barricks/Richmond na kadhalika. Binafsi sina ushahidi isipokuwa naamini vitu hivi vimetokea kulinagana na ushahidi ulotolewa. Na hakika sidhani kama Pengo au Simba wakifanya biashara ya Unga, wewe na mimi tunaweza kukusanya ushahidi dhidi yao..

Tatu, umesema huoni sababu ya Pengo kwenda kuchukua majina ya wauza unga..Sasa kama haikuwa na haja huyo Pengo kataka JK awataje ili iweje?.Nijibu hapo tu tumalize mjadala na malumbano..

Na kama kazi hii sio ya rais imekuwaje Pengo asiende kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya kupata majibu yake..Na kwa nini unafikiri ..Mr Godfrey Nzowa alitakiwa kutangaza majina ya wahusika.WHY?.. unafikiri ingekuwa bora zaidi viongozi hao kuanikwa ktk vyombo habari kukamatwa kwao kuliko kuwakanya waumini wote wasijihusishe na biashara hizo baada ya kuonekana baadhi wameisha kamatwa..

Lengo la JK ni kuwaonya wale ambao hawajakamatwa au hawajajihusisha wasifanye vitendo hivyo.. Ushahidi tayari umesha jitokeza kwa kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa dini kwa hivyo humshutumu mtu ktk mkutano huo laa ila unawaonya wengine wasifanye vitendo vile vya kiovu baada ya baadhi yao kukamatwa. Hii haifanyi kanisa zima kuhusika..
 
Alianza na orodha ya wauza unga ya merehemu Amina Chifupa...hamna kitu!
Akaja na orodha ya wabadhirifu.....kimya!!
Sasa amekuja na orodha ya maaskofu wauza unga....kimya!!
Bado mnaendelea kumtetea?
Ama kweli kipendacho roho....
 
Mkuu wangu Uislaam hauna Tanzania wala nje sisi wote tunasali sawa dunia nzima na tunafuata kitabu dunia nzima tofauti zetu zipo ktk baadhi ya mila na tamaduni za makabila na watawala ktk madhehebu ya Shia lakini sio kwetu Sunni. hakuna mtu mbora mbele ya mwenyezi Mungu isipokuwa yule mwenye kufanya Ibada hivyo kwetu waislaam kila mmoja wetu ana equal opportunity ya kuwa mtukufu mbele ya bwana kutokana na matendo yake.. Mimi naweza kuwa mbora mbele ya Mungu kuliko Mufti Sheikh Mkuu.. Hii haina maelezo zaidi na kama umeona tofauti basi ni sawa na kumuona Mkristu anakunywa pombe ukasema ndio Ukristu huo..

Pili, Namshutumu Sheikh Mkuuu kwa Ufisadi sio nina Ushahidi hapana sina ushahidi lakini kesi zake ni sawa na za Mkapa kuuza nyumba za serikali.. sina ushahidi zaidi ya kuona kwa macho au Mkataba wa Barricks/Richmond na kadhalika. Binafsi sina ushahidi isipokuwa naamini vitu hivi vimetokea kulinagana na ushahidi ulotolewa. Na hakika sidhani kama Pengo au Simba wakifanya biashara ya Unga, wewe na mimi tunaweza kukusanya ushahidi dhidi yao..

Tatu, umesema huoni sababu ya Pengo kwenda kuchukua majina ya wauza unga..Sasa kama haikuwa na haja huyo Pengo kataka JK awataje ili iweje?.Nijibu hapo tu tumalize mjadala na malumbano..

Na kama kazi hii sio ya rais imekuwaje Pengo asiende kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya kupata majibu yake..Na kwa nini unafikiri ..Mr Godfrey Nzowa alitakiwa kutangaza majina ya wahusika.WHY?.. unafikiri ingekuwa bora zaidi viongozi hao kuanikwa ktk vyombo habari kukamatwa kwao kuliko kuwakanya waumini wote wasijihusishe na biashara hizo baada ya kuonekana baadhi wameisha kamatwa..

Lengo la JK ni kuwaonya wale ambao hawajakamatwa au hawajajihusisha wasifanye vitendo hivyo.. Ushahidi tayari umesha jitokeza kwa kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa dini kwa hivyo humshutumu mtu ktk mkutano huo laa ila unawaonya wengine wasifanye vitendo vile vya kiovu baada ya baadhi yao kukamatwa. Hii haifanyi kanisa zima kuhusika..
kweli mkuu hapa tunaweza kulumbana mpaka asubuhi...! Nilichosema mimi ...hiyo ni kazi ya mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya. Yaani kilichotakiwa kufanyika ni kama kawaida..wakikamatwa watu iwe airport au majumbani mwao huwa zinatolewa taarifa kwa vyombo vya habari. kuna wakati mwingine huwa hawatoi habari mpaka wawakamate wahusika wote ....! hiyo ni kazi ya Nzowa! Kama kikwete asingetoa kauli yake kulikuwa hakuna sababu ya Pengo kutaka awataje majina...!. Instigator wa malumbano haya yote ni Kikwete.
Sidhani kwenye utawala wa sheria kuna haja ya kutoa onyo! kama wahalifu/mafisadi wanakamatwa na kushtakiwa nadhani hilo ni onyo tosha kabisa lenye kufanya kazi kuliko maneno matupu!
Mkuu, kikatiba Kikwete ana madaraka makubwa sana ..probably kwa tanzania baada ya Mungu anafuata Kikwete kwa kuwa na nguvu.
Hayo majina ya mafisadi serikalini/ndani ya chama chake, wauaza madawa nk anayo mda mrefu tu lakini amekuwa mtu wa kutoa maonyo na kutabasamu tu badala ya kushinikiza wakamatwe, washtakiwe ..ili .haki itendeke!

Thread hapo chini nadhani umeiona!
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/257-majina-ya-wauza-madawa-ya-kulevya-jk-anayo.html
 
Wakati mwingine lazima tuweke itikadi za kidini na kichama pembeni kwa maslai ya taifa, tusiwe malimbukeni wa mambo, kila mtu anajua kuwa uongozi uliopo ni lelemama, kila aliye na nafasi anafanya atakalo kwa nafasi yake bila ya kuangalia wenzake. Kama kweli Utukufu unakuja kinafki basi na tuusubiri ila kama unakuja kwa kutenda haki na yalo mema na tuisubiri hasira ya Mungu.

Tusitetee ujinga kwa sababu ya Dini, hao wanaotetea dini zao wala hawajui chimbuko la dini zao wanafuata upepo, Tanzania kuna watu wanaishi kama peponi kwa jasho la wananchi ili hali malimbukeni wa kutetea ujinga na uozo uliokithiri wanakosa ata ada za watoto wao.

Amkeni acheni hoja za kimwambao la sivyo mtaendelea kudharauliwa daima ata mkibebwa.
 
KWA mara nyingine, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ameonyesha kukerwa na kauli ya kufumbafumba aliyoitoa Rais Kikwete akiwahusisha viongozi wa dini na biashara ya dawa za kulevya.

Baada ya kufanya hivyo katika kipindi kisichozidi wiki mbili, Kardinali Pengo alirejea tena wito wake jana, akimtaka Rais Kikwete kuwataja hadharani viongozi wa dini ambao aliwatuhumu kujihusisha na biashara hiyo.

Tofauti na ilivyokuwa wakati alipozungumza kwa mara ya kwanza, katika kauli yake ya jana, Pengo alikifananisha kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kuwataja kwa majina viongozi wa kiimani anaowashutumu na usaliti.

“Kiongozi mwenye uchungu na mzalendo kwa taifa hana budi kutaja majina ya watu wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali kwa masilahi ya taifa na wananchi kwa ujumla… yeye kushindwa kufanya hivyo ni msaliti wa nchi,” alisema.

Kiongozi wa nchi wa kweli haoni haya kutaja mafisadi, au wala rushwa hadharani. Endapo anaona haya kuwataja ni msaliti ndani ya nchi yake,” alisema Pengo.

Pengo alikwenda mbali zaidi na akamfananisha kiongozi mwenye uzalendo na nchi kuwa sawa na mwanamke mjamzito anayeshikwa na uchungu wa kuzaa wakati akiwa mbele ya nyoka mwekundu.

Alisema kuwa mwanamke wa namna hiyo huendelea na uzazi pasipo kujali au kuhofia hatari ya nyoka aliyeko mbele yake.

Pengo alitoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza katika ibada maalumu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Kristo Mfalme, Tabata jijini Dar es Salaam jana.

Kardinali Pengo, mmoja wa viongozi wa dini wanaoheshimika, alisema kitendo cha Kikwete kutoa tuhuma hizo nzito wakati akiwa katika shughuli ya Wakatoliki kinaweza kutafsiriwa kuwa alikuwa akiwalenga wao ambao walikuwapo katika hafla hiyo.

Rais Kikwete alitoa tuhuma hizo ambazo zimeibua manung’uniko ya wazi kutoka kwa viongozi wa Kikristo wakati wa ibada maalumu ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu wa Jimbo la Mbinga, Mhashamu John Ndimbo.

“Rais Kikwete hakupaswa kutumia jukwaa la Wakatoliki kutoa kauli hiyo. Angeweza kutumia sehemu nyingine ili tuliokuwepo tusijione kuwa walengwa wa ujumbe,” alisema Kardinali Pengo.

Pengo anakuwa ni kiongozi wa pili wa juu wa Kikristo kutoa kauli hiyo kali, baada ya Umoja wa Maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania, (CCT) kumpa Rais Kikwete saa 48 za kuwataja kwa majina viongozi wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya.

Tamko hilo la maaskofu wa CCT ambalo hata hivyo halikujibiwa na Kikwete hadharani zaidi ya majibu yasiyo na majina kutolewa na viongozi wengine, lilisomwa mbele ya wanahabari mwanzoni mwa mwezi Julai na Mwenyekiti wao, Askofu Peter Kitula.

“Tunampa saa 48 rais awataje kwa majina viongozi hao ambao yeye anadai wanajihusisha kuuza dawa za kulevya na kama atashindwa kufanya hivyo tutatafsiri kuwa ni kiongozi mwongo na mzushi.

[TD="bgcolor: #ffffff"]

• ATAKA AWE NA UJASIRI WA MWANAMKE MJAMZITO

na Datus Boniface

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
[/TD]
 
kweli mkuu hapa tunaweza kulumbana mpaka asubuhi...! Nilichosema mimi ...hiyo ni kazi ya mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya. Yaani kilichotakiwa kufanyika ni kama kawaida..wakikamatwa watu iwe airport au majumbani mwao huwa zinatolewa taarifa kwa vyombo vya habari. kuna wakati mwingine huwa hawatoi habari mpaka wawakamate wahusika wote ....! hiyo ni kazi ya Nzowa! Kama kikwete asingetoa kauli yake kulikuwa hakuna sababu ya Pengo kutaka awataje majina...!. Instigator wa malumbano haya yote ni Kikwete.
Sidhani kwenye utawala wa sheria kuna haja ya kutoa onyo! kama wahalifu/mafisadi wanakamatwa na kushtakiwa nadhani hilo ni onyo tosha kabisa lenye kufanya kazi kuliko maneno matupu!
Mkuu, kikatiba Kikwete ana madaraka makubwa sana ..probably kwa tanzania baada ya Mungu anafuata Kikwete kwa kuwa na nguvu.
Hayo majina ya mafisadi serikalini/ndani ya chama chake, wauaza madawa nk anayo mda mrefu tu lakini amekuwa mtu wa kutoa maonyo na kutabasamu tu badala ya kushinikiza wakamatwe, washtakiwe ..ili .haki itendeke!

Thread hapo chini nadhani umeiona!
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/257-majina-ya-wauza-madawa-ya-kulevya-jk-anayo.html
Bado unashindwa kuelewa.. List ya wauza Unga alopewa JK na marehemu Amina Chifupa sio swala tunalozungumzia hapa wala sio ombi la Pengo kutaka majina hayo...

Narudia tena kusema upya. Watu walikamatwa wakijihusisha na biashara ya madawa na kufunguliwa mashataka. Watu hao ni viongozi wa dini iwe (yeyote ile) ingawa ktk kesi hii nitasema walikuwa wakristu...Hilo moja lililotangulia na tuliweke pembeni.

Kisha JK anakaribishwa ktk sherehe ya Wakristu kama rais na kupewa jukwa la kuzungumza.. Je, kuna ubaya gani kwa rais kusema viongozi wa dini wanaojihusisha na biashara za madawa waache?(ushahidi ni wale waliokamatwa! ila unataka iwe kazi ya kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya ambao hawakualikwa na wala hapakuwa na kazi ya kukamata watu pale kwenye sherehe.

Na ndio nimekupa mifano kibao kwamba inaruhusiwa kwa kiongozi kuwakanya wengine kutoshiriki ktk vitendo vibaya na isiwe na maana kwamba anawashutumu wao.. Bado wewe unashikilia kwamba JK anawatuhumu viongozi wa dini ( mawazo ya Pengo) hali wapo watu waliokamatwa na kilichofuatia ni kuwasihi wengine wasishiriki ktk biashara hiyo...Unless wewe unachukulia nadharia ya samaki mmoja akioza basi ndio kapu zima limeoza!

OK lets say JK alikuwa na list au wafanya biashara ya kuuza unga, kulikuwa na sababu gani yeye Pengo kusimama na kulizungumzia hili kama unavyoshindwa kuelewa kwa nini JK kalizungumza!..Kwani ni kazi yake? kwa nini isiwe tena Kikosi cha kupambana na wauza unga ndio waiombe list hiyo ili waisfanyie kazi.. Kuitaja itatusaidia kitu gani au ndio kanisa llipate muda wa kuunda utetezi upande wake.. Nachoshindwa kuelewa mimi ni kwamba iweje ni haramu kwa JK kusema jambo fulani lakini halali kwa Pengo kusema atakavyo hali naye sii kazi yake na hawezi kufanya lolote hata akipewa orodha hiyo.

Binafsi mkuu wangu nitakwambia kitu kimoja na cha mwisho, Ugaidi unafanywa na waislaam wenye siasa kali na kila siku tukifungua TV ni maelezo yanayotuasa tuache Ugaidi pamoja na kwamba wanadai majina ya magaidi wanayo....Hakuna hata siku moja nitawataka au kuitaka serikali ya Marekani wayatoe majina hayo hadharani kwa sababu sio kazi yangu na hata wakiyatoa kwangu nitayafanyia nini. Sioni kosa akizungumza Obama, JK, Papa au hata Kardinali Pengo sintaona ubaya wowote..Ila nitaendelea kuamini kwamba wapo waislaam magaidi na wanafanya vitendo viovu na mimi nimekanywa kutojihusisha na vitendo hivyo. Sikudhalilishwa wala kunyooshewa kidole.
- Nilikuwepo.
 
Kwanini Pengo ilimuuma ile kauli ya Kikwete? au ni mmoja wa washukiwa.

lakini siku hizo hana uzito wowote kulinganisha na Wakati za Nyerere.

Kwa sababu rais mzima anaendekeza kauli za jumlajumla, za kizushizushi, kimbeambea.

Ukishasema viongozi wa dini wanahusika katika kuuza madawa ya kulevya, inabidi uwataje.

Kwanza kama Kikwete anaelewa utawala wa sheria, yeye wala si mtu wa kusema kitu ambacho hakijaamuliwa na mahakama, angeacha wakamatwe, wahukumiwe na mahakama, halafu ndipo angesema. Vinginevyo anaweza kuonekana anaweka pressure isiyofuata utawala wa sheria bure. Anachukua jukumu la mahakama kuamua nani muuza madawa na nani safi.

Ukishasema viongozi wa dini wanauza madawa, bila kuwataja, inaonekana kama unawaogopa, au hata kama huwaopgopi, unawapaka matope wooote, kila mmoja anakuwa suspect.

Kitu ambacho mtu makini hawezi kufanya.

By the way alisema pia wala rushwa pale bandarini anawajua lakini hajafanya kitu mpaka leo. Ina maana anawalea au rafiki zake anakula nao?
 
Pengo amnyoshee kidole Mkapa kwanza; then sisi wengine tutamchukulia serious.

Kwa hiyo unataka kusema Pengo mdini? Anamuandama Kikwete kwa sababu Kikwete muislam na hajamuandama Mkapa kwa sababu Mkapa Mkatoliki?

Au una maana gani?

Maana watu wawili wakifanya vibaya sina haki ya kumyooshea kidole mmoja? Mpaka niwanyooshee wote wawili? Nitanyooshea wangapi? Na nikinyooshea wawili napo kweli hutaniambia kwamba hutanichukulia serious mpaka ninyooshee watatu, ad infinitum ?
 
Kiranja,
Kardilnali Pengo anacheza karata moja mbaya sana ambayo inaweza kutafsriwa kama Udini kutokana na dhana yake kwa nini JK amesema viongozi wa dini waache kujishughulisha na biashara za Unga. Na yawezekana kweli JK hakupaswa kulitumia jukwaa lile kulingana na taratibu za Kikristu lakini alipaswa kusamehewa kwa sababu hajui tofauti na Mwinyi alokwenda ktk jukwaa la Kiiislaam siku ya maulidi na kuanza kuzungumzia ngono na matumizi ya Condom. Akatokea kijana na kumpa kofi la Kerbu mzee Ruksa! yamekwisha siku hiyo hiyo. Kisha tuliokuwa tumetulia kidogo na hizi habari za Masheikh na Mapadre ktk siasa za Bongo, mara Pengo analiibua jambo ambalo limepita toka Easter..

Tatizo ambalo linanikera mimi ni pale Kardinali Pengo anapotumia majukwaa ya dini akiwa makanisani au sikukuu za Kikristu kumzungumzia utawala wa JK jambo ambalo halijawahi kutokea nchini kwa kanisa kujiingiza ktk siasa kiasi hiki..Kama ni umaskini na Ufisadi ulikuwepo toka enzi za mwinyi, na Mkapa lakini inaonyesha wakati huu kanisa limechukua muda mwingi kujihusisha na siasa bila sababu za Kiimani..JK ambaye anakemea swala la kiimani watu kujihusisha na Unga anaonekana sii kiongozi mzuri kwa sababu tu hakuwataja na limewagusa viongozi wa kanisa na sio Biblia wala mafundisho ya YESU na mitume..

Yeye Kardinali anajua fika wapo viongozi wa dini wanaojihusisha na biashara hizi na kama hajui angejaribu kufanya uchunguzi hata kidogo kabla hajachukua maelezo ya JK kama ni kashfa ya kanisa lake. Yeye Kardinali anajua fika acha unga wapo viongozi wa dini wanaotumia msamaha wa kodi kwa kuingiza mali za watu na kukatiwa kitu pembeni kinyume kabisa cha sheria kwa sababu lazima wanaweka hesabu ya matumizi ya hizo misamaha ilotumika. Kupitisha mali kwa kutumia kanisa/Bakwata ndio mission town vijana wa mjini wanapatia panga lao..

Watu mjini wanacheza na makanisa kupata visa za nchi za kigeni ambazo hazipatikani kirahisi ili kwenda fanya biashara na kadhalika.. Haya yote ni matatizo yatokanayo na Umaskini kanisa linawasaidiwa watu kiasi kwamba linakiuka hadi kanuni na taratibu zake.. na kama navyosema siku zote pale penye Mapungufu basi Rushwa hupenyeza!..Hii haina cha kanisa wala msikiti binadamu wote tumeumbwa na tamaa na sii vizuri kumwekea dhamana binadamu mwenzako kwa sababu hujui yaliyomo rohoni mwake. Wale waliokamatwa ni viongozi wa dini na mfano tosha kabisa kutuelewesha kwamba wapo Unga umeingia hadi sehemu za ibada.
 
Kwa hiyo unataka kusema Pengo mdini? Anamuandama Kikwete kwa sababu Kikwete muislam na hajamuandama Mkapa kwa sababu Mkapa Mkatoliki?

Au una maana gani?

Maana watu wawili wakifanya vibaya sina haki ya kumyooshea kidole mmoja? Mpaka niwanyooshee wote wawili? Nitanyooshea wangapi? Na nikinyooshea wawili napo kweli hutaniambia kwamba hutanichukulia serious mpaka ninyooshee watatu, ad infinitum ?

Nimesema angemnyoshea kidole na Mkapa "Kwanza".. kwa sababu Mkapa anahusika kwa madudu mengine mengi tuliyonayo sasa na binafsi naamini anastahili kujibu. Ningependa mtu kame Pengo amlaumu Kikwete kwa kutomchukulia hatua Mkapa! Haya ya udini na waachie wengine wanaobishania hayo.
 
Jana ulisema unamfahamu sana Muadhama Policarp Cardinal Pengo, sidhani. Kwa kumbukumbu zangu huyu ni mkimya sana, mtaratibu sana, hana makuu kabisa. Lakini ni mkweli, mpenda watu, mpenda maendeleo na mtetezi mkubwa wa wanyonge.

Nilimwona kwa mara ya kwanza Mwadhama Pengo mwanzoni mwa miaka ya 80 akiwa padre akitokea Rome masomoni huko Sumbawanga katika kijiji cha Ntuchi wilayani Namanyere akielekea Kate, akitembezwa na mzee wake Marehemu Askofu Carolo Msakila. Kwa vile nilimwona mara ya kwanza hakuonyesha upekee na nilishangaa kama ametoka Rome masomoni.

Punde nikaambiwa kapangiwa kazi ya kuanzisha Seminari kuu ya Segerea hapa Dar es Salaam. Baada ya miaka michache Pope akamteua kuwa Askofu wa Kwanza wa jimbo jipya katoliki la Tunduru-Masasi. Baada ya miaka michache tu Pope akamteua kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam lilikokuwa likiongozwa na hayati Muadhama Laureano Cardinal Rugambwa.

Kwa mtazamo finyu ingeweza tafsiriwa kwamba kateremshwa cheo kutoka askofu mwenye jimbo na kuja dar kuwa askofu msaidizi. Lakini ilikuwa demotion for promotion, na maana yake Pope kumwandaa kwa kazi nzito aliyo nayo sasa.

Mwadhama Policarp, hakurupuki katika kuongelea kitu, si mwoga, ni mkweli, mtetezi mwenye unyofu wa moyo. Wengi hapa tunaongelea kwa mitazamo tofauti lakini si kile kilichoko ndani ya moyo wake. Tukumbuke hawa ni manabii kama akina Eliya walipowatahadharisha watawala wakakaidi na madhara yaliyotokea kwa wanahistoria ya taifa la Israel tunayajua.

Tuweke kando itikadi za kisiasa na tuangalie anachoongelea Muadhama. Kuna mengi kama hayo ambayo wengi wetu tunajua lakini hakuna hatua zinazochukuliwa zaidi ya kulalamika majukwaani kama hawana mamlaka za kutolea uvivu.

Hao wavuja pesa yanayoendelea ni kitendawili tega. Hii ya funika kombe mwanaharamu apite inazidi kutupeleka pabaya. Kiongozi asipokuwa tayari kukosolewa maana yake yupo huru kujifanyia atakavyo na kujikuta yuko juu ya sheria.

Hakuna chombo cha kumwajibisha. Na dhana ya mapokea kwa viongozi wetu hata wanapopotoka kuendelea kuwaimbia nyimbo za kuwasifu imetufikisha hapa, na wanufaika na mwenendo huu mbovu ndio watetezi wa wakuu na wanyonge kuendelea kunyongeka.

Tunapaswa kumpongeza Muadhama Policarp kwa ujasiri wa kuonya, kukemea na kushauri bila woga, maana viongozi waandamizi wa serikali hawaku tayari kufanya hivyo kwa sababu ya kutetea maslahi yao na nafasi zao katika uongozi.

Yana mwisho na ukingo unakaribia zinakoishia mbio hizi.

NDUGU WAKALA WA PENGO AMA PENGO MWENYEWE KWA KIFICHO...TUMSIFU YESU KRISTU WA NAZARETH. Ungekuwa unaongea kwa upole uliotukuka kama ulivyofanya hapa tungekuwa pamoja na tusingetiliana mashaka wala kukashifiana...maana iwapo lengo ni kulinda na kujenga nchi, malumbano hayafai.

Nilichokulaumu ni kumdhalilisha kiongozi mkuu wa nchi hata kama ana mapungufu si busara kwa Taifa na hata kwa mataifa ya nje. Mimi nina imani kuwa uko kwenye nafasi nzuri kabisa kama Mkuu wa Kanisa lenye waumini wengi watanzania...kuzungumza na Rais ukamshauri uso kwa uso juu ya mambo ambayo umeyatoa hadharani.

Yeye hakukuita kwa kuwa mlengwa hukuwa wewe ktk saga la madawa. Hakuwa ana undermine kanisa kwa uislamu wake...bali alizungunza kama Kiongozi wa nchi mwenye dhamana ya watanzania wote. Wewe na yeye ni watu wazima tena Viongozi...mnapolumbana through media isn't fair kwetu sisi watoto wenu.

Ukimwona pengine si wa imani yako..basi ungepitia hata kwa PM pengine ambapo protokali lazima ingezingatiwa. Jitahidi kama Kiongozi Mkuu wa kidini usiiteteleshe serikali ambayo ipo madarakani kisheria na hujazuiwa kuikosoa ama kuishauri muda wote. Najua jinsi imani ya dini ilivyo na nguvu na kiongozi kama wewe ukiitumia kama shield au spear utaigawa nchi mjomba.....mtu mzima akikosea mwite faragha...sema naye..ni binadamu yule anaelewa...

Ukitumia imani kulumbana naye itakuwa kama Bin Laden Osama kutumia dini kama kivuli lkn finally ameuwawa na anaowaita infidels. Mumi nadhani kama JK angekuwa ana utawala wa kiimla...hata jamii forums isingekuwepo na kungekuwa na msako mkali dhidi ya wabaya wake just like Libya...etc.

TUFIKE MAHALI TUJENGE KISIWA CHA AMANI JAMANI TUACHE TOFAUTI ZA KIDINI NA KISIASA. IN WAR THERE IS NO WINNER...ALL ARE LOOSERS...alisema British Premier Chamberlain in WW2 akiwatahadharisha waingereza juu ya athari za kupigana na Hitler. Alujiuzulu kwa shinikizo na akarithiwa na Winston Churchill aluyeingia kwa kutangaza "There is nothing to offer except blood....sweat and tears" Ilikuwa patashika nguo kuungua.

Sasa twaweza furahi Rais akijiuzuru lakini je unaye mtu unayependekeza awe badala yake? Na je unadhani mtu huyo unayempendekeza anakubalika na majeshi yote ya ulinzi na usalama na wananchi? Yasije yakawa ya Kabila or JF Kennedy or A. Lincolin or unawajua bwana. Ushabiki wa kiimani ya dini na kuyasahau hayo itakuja tokea mambo ya Ariel Sharon btn Likurd na Kaduma yake...or ya Bingu wa Mutharika na chama chake.

Tumpe pumzi Rais ya kuongoza nchi huku tukimshauri kupitia majukwaa kama hivi ili nini afanye juu ya kipi tutakacho. Kumtukana Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vyote vya ulinzi na usalama na ambaye ni Rais kidemokrasia anayeachia demokrasia ya habari nchini....KWANGU MIMI NI UHUNI.

NA INGELIKUWA MMENICHAGUA MIMI NDO RAIS...HAKI YA MAMA YANGU MZANAKI...UNAOKOTWA UNA MSUMARI WA INCH SITA UTOSINI..POTELEA KWA MBALI ILI NCHI ITAWALIKE BILA USWAHILI.
 
Kiranja,
Kardilnali Pengo anacheza karata moja mbaya sana ambayo inaweza kutafsriwa kama Udini kutokana na dhana yake kwa nini JK amesema viongozi wa dini waache kujishughulisha na biashara za Unga. Na yawezekana kweli JK hakupaswa kulitumia jukwaa lile kulingana na taratibu za Kikristu lakini alipaswa kusamehewa kwa sababu hajui tofauti na Mwinyi alokwenda ktk jukwaa la Kiiislaam siku ya maulidi na kuanza kuzungumzia ngono na matumizi ya Condom. Akatokea kijana na kumpa kofi la Kerbu mzee Ruksa! yamekwisha siku hiyo hiyo. Kisha tuliokuwa tumetulia kidogo na hizi habari za Masheikh na Mapadre ktk siasa za Bongo, mara Pengo analiibua jambo ambalo limepita toka Easter..

Ukiogopa kusema kweli kwa sababu unaogopa watu watakavyokutafsiri utakuwa huwezi kusema chochote maishani mwako, maana kila mtu anaweza kukutafisiri anavyotaka.

Tatizo ambalo linanikera mimi ni pale Kardinali Pengo anapotumia majukwaa ya dini akiwa makanisani au sikukuu za Kikristu kumzungumzia utawala wa JK jambo ambalo halijawahi kutokea nchini kwa kanisa kujiingiza ktk siasa kiasi hiki..Kama ni umaskini na Ufisadi ulikuwepo toka enzi za mwinyi, na Mkapa lakini inaonyesha wakati huu kanisa limechukua muda mwingi kujihusisha na siasa bila sababu za Kiimani..JK ambaye anakemea swala la kiimani watu kujihusisha na Unga anaonekana sii kiongozi mzuri kwa sababu tu hakuwataja na limewagusa viongozi wa kanisa na sio Biblia wala mafundisho ya YESU na mitume..

Kaka hiki anachofanya Kardinali Pengo hakikuanza leo wala jana. Hii ni "Liberation Theology", kanisa linapowapigania watu masikini kama sehemu ya mafundisho ya Yesu Kristo. Kaangalie hata Papa John Paul aliingia katika siasa za Poland kumsaidia Lech Walesa kuwaondoa Wakomunisti, kuna maaskofu mpaka wameuawa huko kipande cha Latin America kwa kuwasemea mbovu ma dikteta wa kijeshi. Kwa hiyo ni vile tu siasa zetu hazijakomaa ndiyo maaana tunaona kitu kigeni. Lakini huko kipande cha Costa Rica na Nicaragua Askofu kumbwatia Commandante si kitu cha ajabu wala nini.

Hebu angalia kipande hiki hapa wanaongelea hii "Liberation Theology" Liberation theology - Wikipedia, the free encyclopedia

Yeye Kardinali anajua fika wapo viongozi wa dini wanaojihusisha na biashara hizi na kama hajui angejaribu kufanya uchunguzi hata kidogo kabla hajachukua maelezo ya JK kama ni kashfa ya kanisa lake.

Kwa nini unafikiri Kardinali anafikiri kanisa lake limesemwa wakati Kikwete kashasema si kanisa lake? Tatizo hapa ni ukweli kwamba Kikwete hawi muwazi, na kama kiongozi wa nchi kutokuwa muwazi ni noma. Sasa kasema si makanisa makubwa, ni madogo, madogo yako mangapi? Kashawapaka matope viongozi wa makanisa madogo wote tu.

Yeye Kardinali anajua fika acha unga wapo viongozi wa dini wanaotumia msamaha wa kodi kwa kuingiza mali za watu na kukatiwa kitu pembeni kinyume kabisa cha sheria kwa sababu lazima wanaweka hesabu ya matumizi ya hizo misamaha ilotumika. Kupitisha mali kwa kutumia kanisa/Bakwata ndio mission town vijana wa mjini wanapatia panga lao..

Sasa Kardinali akimpaka rais kwa kuachia viongozi wa dini kufanya hivyo na kupiga soga badala ya kuchukua hatua utamshangaa?

Watu mjini wanacheza na makanisa kupata visa za nchi za kigeni ambazo hazipatikani kirahisi ili kwenda fanya biashara na kadhalika.. Haya yote ni matatizo yatokanayo na Umaskini kanisa linawasaidiwa watu kiasi kwamba linakiuka hadi kanuni na taratibu zake.. na kama navyosema siku zote pale penye Mapungufu basi Rushwa hupenyeza!..Hii haina cha kanisa wala msikiti binadamu wote tumeumbwa na tamaa na sii vizuri kumwekea dhamana binadamu mwenzako kwa sababu hujui yaliyomo rohoni mwake. Wale waliokamatwa ni viongozi wa dini na mfano tosha kabisa kutuelewesha kwamba wapo Unga umeingia hadi sehemu za ibada.

Sasa kwa nini rais asihimize mkondo wa sheria ufuatwe na kuja kutoa taarifa kwa wananchi kuna viongozi hawa na hawa wa dini walijihusisha katika biashara haramu, serikali yangu haitaki mchezo? Kikwete ni joker, hilo ndilo tatizo, kasema anawajua wala rushwa bandarini, sasa kafanya nini mpaka leo?

Kwa nini hajasema kuna mabalozi wanatumia vyeo vyao kuuza silaha kwa waasi wa Congo? Kwa nini kamtoa yule balozi wa Tanzania Burundi kimyakimya? Si anajua kusema sana yeye?

Unafiki tu!
 
Son of Africa
NA INGELIKUWA MMENICHAGUA MIMI NDO RAIS...HAKI YA MAMA YANGU MZANAKI...UNAOKOTWA UNA MSUMARI WA INCH SITA UTOSINI..POTELEA KWA MBALI ILI NCHI ITAWALIKE BILA USWAHILI.
Umenichekesha sina mbavu duuuh! ama kweli wewe Mzanaki!
 
Back
Top Bottom