Mkuu KIM KARDASH
Kwajuu juu mtu akiangalia hoja yako anaweza kudhani ina mantiki ila kiukweli ukiiangalia kwa jicho la tatu ina mdhaifu mengi na ina impact kubwa kwa siasa zetu za Kibongo.
Unajua siasa ni mchezo wa kutumia ujanja sana katika kummaliza mwenzako kisaikolojia na kuondoa ile nguvu yake na imani yake kwa wananchi, kwenda kwenye chaguzi ndogo ni tofauti sana na uchaguzi mkuu, Amini nakwambia ikitokea unavyotaka wewe kwa Dr kugombea Arumeru mashariki CCM watafanya kila linalo wezekena ilimradi tu kuhakikisha Dr Slaa anashindwa ili kumbomoa kisiasa.
Hoja nyingine dhaifu ni kusema eti Mbowe amepwaya sana kwenye uongozi wa kambi ya upinzani bungeni, hapa unajaribu kutuambia nini? kuwa Hamadi Rashid alikua bora zaidi ya Mbowa alivyo sasa?....... you must be kidding
Umetumia vigezo gani kusema eti Dr Slaa akishanda ubunge basi Mh Mbowe ampishe kiti hicho cha kiongozi kambi ya upinzani Dr Slaa, kwangu mimi hizi ni dharau kubwa kwa kutokutambua anachofanya Mh Mbowe Bungeni,
Kumbuka pia hicho kipindi unachosema Dr Slaa alikuwa anawasha moto wa uhakika bungeni hakuwa mkuu wa kambi ya upinzani bungeni hivyo hoja yako haina nguvu tena
Nilazima tutambue kuwa Dr Slaa hajaukosa ubunge kwa bahati mbaya, hapana yupo pale kama katibu mkuu kujenga chama kwa talanta alioionyesha ya uongozi wa kiwango kizuri, wananchi wa Arumeru tayari walikuwa na kijana wao anayeonekana kukubalika tayari, hivyo ingekuwa vyema akaachwa aendelee na mbio zake kuliko kuwalazimishia mtu ambaye hawakuwa wakimfikiria kabla eti tu kwa kigezo cha kwenda kuimarisha makali ya bunge kama ulivyo jenga hoja yako.
Pia kuna tathmini ya kina ulipaswa kujiuliza nini nafasi ya kushinda iwapo atagombea Arumeru mashariki na nini hatari yake iwapo atagombea kwenye jimbo ambalo sio lake.
Kwa mtazamo wako siri ya ushindi umeikita kwenye u heavy weight politician kitu ambacho hakijitoshelezi kabisa
Kwanza,Risk kubwa ninayo iona mimi ni kuwa chaguzi ndogo ni rahisi sana kufanya ujanja wa matokeo kwa CCM, hivyo basi kama nilivyoainisha hapo juu itatumika nguvu kubwa na gharama yoyote kuhakikisha Dr Slaa hashindi na hili litakuwa baya sana kisiasa kwa Dr Slaa na chama chake kuliko unavyoweza kufikiri
Pili historia na uzoefu inaonyesha ni mara chache sana mtu wa oneo fulani kwenda kugombea eneo jingine, hii ni risk, watu wa ukanda huo ni nadra sana kumkubali mtu zaidi ya "mwenzao", swali ni je tuna hakika watu wa Arumeru watakuwa tayari kuchagua mtu yoyote kwa maslahi ya chama au watataka kuchagua mwakilishi wao kwa matakwa yao? think about it
Tatu, moja ya madai ya CCM kufanya vibaya uchaguzi uliopita ni kitendo cha kupitisha wagombea kwa matakwa ya chama badala ya matakwa ya wananchi, Swali la kujiuliza hapa ni kuwa unategemea yule kijana Joshua na wafuasi wake watakuwa tayari kuona wanapelekewa mtu mwingine kugombea badala ya mtu wao wanae amini anajuwa vizuri matatizo yao, je itamfurahisha Joshua mwenyewe na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wafuasi wake.
Naamini Joshua akipewa sapoti kubwa na chama chake atafanya vizuri zaidi na atakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda kuliko Dr Slaa "kupelekwa" akagombee Arumeru mashariki