Pendekezo: SLAA amrithi SUMARI Arumeru!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru. Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile, kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.
 
Naunga hoja kwamba Dr. Slaa awanie kiti Arumeru. Kwanza, kule ni ukanda wa kwake, so it's unquestionable. Pili, kule ni ngome kubwa ya CDM. Tatu na mhimu sana Dr. Slaa sio tu anasifa stahiki kwa upana wake lkn pia ni kweli anahitajika sana bungeni sasa pengine kuliko wakati mwingine wowote ule.

Sikubaliani na aliyeweka uzi juu ya haja ya Dr. Slaa kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani na kwamba Mh. Mbowe kapwaya ktk nafasi ile. Moja, licha ya kuwa mtoa uzi hajajustify kupwaya kwa Mbowe ktk nafasi hiyo, lkn pia binafsi sioni viashiria vyenye mashiko juu ya udhaifu wa mbowe ktk nafasi hiyo.

Pili, sidhani kama ni maadili na utaratibu wa CDM katika kuimarisha uongozi. Imani yangu ni kuwa kama mtoa uzi anamkubali Dr. Slaa kwa kigezo cha umahiri wake akiwa bungeni, basi asihusishe na nafasi ya uongozi katika kambi rasmi ya upinzani kama mwenyewe alivyothibitisha uwepo wa wabunge wengine mahiri bila kuwa katika nafasi hiyo ya uongozi.
 
​rais atakiwi kugombea ubunge

Nafasi ya Dr Slaa aliyonayo sasa hivi na mchango wake kwa jamii ni mkubwa kuliko angekuwa Mbunge, ni wapuuzi tu ndiyo hawawezi kuona mchango wake...na infact hawapo ndani ya CDM na nadoubt mleta hoja kama ni mwanaCDM.

Mbowe ni kiongozi shupavu sana, haijapata kutokea Tanzania kuwa na kiongozi kama yeye....Kuongoza CDM kwa mafanikio namna hiyo siyo kazi rahisi...kwa wasiolijua hili wamuulize JK atakuambia ugumu wa kuwa mwenyekiti. Kusema amepwaya ni katika lipi?

Ndo sababu nikasema mleta mada ni mmoja wa watumishi wa matumbo. Tunao vijana wengi sana wanaARUMERU wanaoweza kulibeba jimbo lile bila nguvu ya ziada kutumika na mmoja wao ni Joshua Nassari aliyegombea na Summari na kupatiwa kura 19,000+ na NEC ya CCM...na ktk hili tutawafunda CUF maana ya kuwa na mtaji na kuuendeleza.
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru.Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile,kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh. mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.

Wazo zuri ila huna hoja
 
Siungi mkono hoja. Akigombea CCM wanaweza kutumia hata sh trilioni moja ili wamwangushe ambapo sasa atakufa kisiasa. Pili ataonekana ana tamaa. Tatu jimbo lake Karatu sio Arumeru.

Watu wasiojua, hapa mjini kabila lolote anaweza kupata ubunge isipokuwa ilala na temeke pagumu. Ila vijijini kama si mtu wa pale si rahisi kupata. Mimi ni mmeru na nawajua wameru tulivyo wakorofi ukimleta Mmbulu anaweza kukosa.

Kwa swala la ubunge kuna ukabila sana, hata kama angekuwa mmeru lakini si wa jimbo hilo asingepata. Nenda msukukumu ukagombee Kyela, mchagga ukagombee Bukoba vijijini, Mpare ukagombee Hai, huwezi kupata. Nampigia chapuo kijana yule agombee Dr akampigie debe tu
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr. SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru.Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni.

Wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile,kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni, waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa, Lema au Tundu!....

Mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.

Nikuhadharishe ndugu yangu,

kwenye Siasa hakuna cha heavy weight! Nijuavyo mimi hata akigombea hatashinda kwani hakuna atakae kuwakilishwa na wale wenye sifa ya kuwaletea vurugu na maandamano ya kila mara yasiyo na tija. Majimbo yote kwa sasa yanayoongozwa na wenye kupenda vurugu wananchi wamechka na wana waasa wanachi wengine wasiingie kwenye kubahatisha kwa kukichagua chama chenye maslahi na vurugu!
 
Nasikia kuna dogo aliibiwa kura na huyo aliyetwaliwa, nadhani ni mda wake kuwatumikia watu wake. Slaa asiende bungeni, aendelee kufanya kazi za chama, huku akiwajenga wabunge vija kuwa makini kama yeye. Tunamhitaji ashike bendera 2015
 
Joshua Nasari ni kijana machachari anayekubalika pia

Watu wa Arumeru wanahitaji muwakilishi anayeyfahamu vizuri zaidi mahitaji yao. Hawahitaji muwakilishi wa kujaza nafasi.

Joshua Nassari bado anafaa sana kuwawakilisha wanaArumeru na kama kuna mwanaArumeru mwingine anayeweza kubeba majukumu ya kuongoza harakati za maendeleo Arumeru ajitokeze na wanaChadema wa Arumeru watachagua nani apeperushe bendera ya chama.

Having said so, sikubaliani kabisa na wazo lolote la kumtaka Dr. Slaa kugombea ubunge Arumeru, kazi aliyonayo sasa ya kujenga na kuimarisha chama inamtosha.

Kitu cha muhimu ni kujipanga kikamilifu kuhakikisha tunachukua jimbo hilo kwa kuteua mgombea mahiri ili wanaArumeru wampe kura zao.
 
tulisha toa mapendekezo hapa kuwa CDM iisimsimamishe mtu mwingine zaidi ya JOSHUA

Chadema inahitaji mtu huru wa kukisambaza chama zaidi hadi vijijini kama Dr Slaa
........Siiungi mkono hoja kabisa
 
Binafsi napendekeza CHADEMA imsimamishe Dr.SLAA kwenye kinyang'anyiro cha ubunge huko Arumeru.Hii itaipa chadema kwanza nafasi kubwa ya kukinyakua kiti hicho kwa kuwa Slaa kwa sasa ni heavy weight politician na pia watanzania wenye uchungu na nchi hii tumekuwa tukiukosa mchango wa Dr pale bungeni,wengi tunaukumbuka ujasiri wake akiwa anga zile,kiukweli Mboe anapwaya kwenye nafasi ya kiongozi wa upinzani pale bungeni,waziri mkuu Pinda na serikali yake wanahitaji kuchangamshwa na mtu machachari wa aina ya Slaa,Lema au Tundu!....mboe amekua na huruma huruma hivi,sasa slaa kama atafanikiwa kushinda ubunge(nina uhakika atashinda)basi mh.mboe awe muungwana kwa kumpisha bwana Slaa kiti cha kiongozi wa upinzani!hii imekaaje wadau,yote ni katika kuimarisha makali ya bunge.

Ni sawa na kumwambia babako arudi chekechea.
 
Nimekua kimya nikijaribu kufuatilia hoja zenu waungwana,mnaodai ukatibu mkuu wa slaa ni mkubwa kuliko ubunge,hoja yenu dhaifu sana,umaarufu wa slaa hautokani na ukatibu mkuu wake bali ulitokana na ubunge sasa kwa nini asirudi bungeni akamalizie kazi aliyoianzisha?au mnataka asubiri nafasi ya ubunge wa kuteuliwa na rais mwaka 2013 mwishoni kufuatia muafaka wa haya mazungumzo ya upenuni kati ya jk na mbowe?kama hamjui ndio tunakoelekea!

Na nyie mnaodai eti slaa ni rais mnamdanganya pamoja na kujidanganya nyie!na pia mnaosema eti sijui ataibiwa kura na kufirisika kisiasa pia ni uongo!hivi kura huwa zinaibiwaje?ndugu zanguni amkeni msikubali kudanganywa na wanasiasa,tatizo wanasiasa wetu wa africa huwa hawasemi ukweli kwa kuogopa kuwajibika kutokana na kushindwa chaguzi ndio huwa wanakuja na kisingizio cha kuibiwa kura wakishindwa,hivi hamjiulizi kama wizi wa kura upo kwanini cuf inairesa ccm pemba?au kwanini Ndesambura anaitesa kila wakati ccm moshi mjini?au kwanini Mzee Said Arfi makamu mwenyekiti wa cdm amekua kwa muda mrefu hata wakati slaa hajulikani amekua akiitesa ccm huko mpanda kwake?au zitto kwa nini anitesa ccm?Huwezi kuiba kura,huwa mnakua mmeshindwa tu,msidanganyike na watu kujaa kwenye mikutano yenu ya kampeni au hapa jf watu wengi kuonekana wanaipenda chadema,wengi sio wapiga kura!
 
siungi nkono hoja.Nassari apewe haki yake.Slaa ana kazi kubwa ya kuimarisha chadema nchi nzima akijiandaa kukamata dola 2015
 
Nikuhadharishe ndugu yangu,

kwenye Siasa hakuna cha heavy weight! Nijuavyo mimi hata akigombea hatashinda kwani hakuna atakae kuwakilishwa na wale wenye sifa ya kuwaletea vurugu na maandamano ya kila mara yasiyo na tija. Majimbo yote kwa sasa yanayoongozwa na wenye kupenda vurugu wananchi wamechka na wana waasa wanachi wengine wasiingie kwenye kubahatisha kwa kukichagua chama chenye maslahi na vurugu!

Mamatau kumekucha amka! Mbona unaendelea kuota na kijua kishachomoza? Amka!
 
Nilidhani una hoja ya maana hadi kupendekeza Dr. Slaa agombee Arumeru, tumekupa majibu ni kwanini tunapinga.
Lakini nilivyosoma majibu yako nimegundua hata hujui siasa, upo ti ili uonekane ni mwanasiasa lakini siasa imekupiga chenga. Pole kajipange ktk nyanja nyingine kwenye hili hakuna kitu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom